Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 29, 2016

UN kuimarisha misaada Syria

Umoja wa Mataifa unapanga kutoa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Syria laki moja unusu ambao wamekua kwenye maeneo ya vita, kufuatia muafaka wa kusitisha mashambulizi. Umoja huo unasema unatarajiwa kuwafikia raia milioni 1.7 ifikapo mwisho wa mwezi Machi.Muafaka wa kusitisha mapigano uliafikiwa Jumamosi japo kumekua na madai ya maafikiano yao kukiukwa. Misaada ya kibinadamu ni pamoja na chakula, maji na dawa ambayo itapelekwa katika miji kama ule wa Madaya ambapo wakaazi wake wameripotiwa kufa njaa.Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba karibu watu nusu milioni wamekwama katika maeneo ya vita nchini Syria. Muafaka wa kusitisha mashambulizi ulifanikishwa kufuatia makubaliano kati ya Marekani na Urusi ambao wanaunga mkono makundi hasimu katika vita vya Syria. Hata hivyo mashambulizi dhidi ya makundi ya Islamic State na Nusra Front yanaendelea.

Leonardo DiCaprio ajishindia tuzo ya Oscar

Brie Larson ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike naye DiCaprio mwigizaji bora wa kiume Mwigizaji nyota Leonardo DiCaprio hatimaye amejishindia tuzo yake ya kwanza ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu ya The Revenant, baada ya kushindania tuzo hizo mara sita. Ametawazwa mwigizaji bora kwenye makala ya 88 ya tuzo hiyo. Tuzo ya mwigizaji bora wa kike imemwendea Brie Larson kwa uigizaji wake katika filamu ya Room. Spotlight ndiyo iliyozoa tuzo ya filamu bora zaidi Oscar ingawa filamu Mad Max: Fury Road ndiyo imezoa tuzo nyingi, ikichota tuzo sita. Mark Rylance ameshinda tuzo ya mwigizaji bora msaidizi katika tuzo hizo za Oscars, huku Miwngereza mwenzake Sam Smith akishinda tuzo ya wimbo bora asilia original song. Miongoni mwa walioshindia Mad Max: Fury Road, iliyokuwa imeteuliwa kushinda tuzo kumi, ni mbunifu Mwingereza Jenny Beavan, aliyeshinda tuzo ya ubunifu wa mavazi bora zaidi. Filamu ya The Revenant imeshinda tuzo tatu kati ya 12 ilizoteuliwa kupigania. Orodha ya washindi wa Tuzo za Oscars 2016 Alejandro Inarritu amezoa tuzo ya mwelekezi bora naye Emmanuel Lubezki akajishindia tuzo yake ya tatu mtawalia ya Oscar katika kuandaa sinema bora, baada ya kushinda kwa filamu ya Birdman 2015 na Gravity 2014. DiCaprio ameshangiliwa sana akienda kupokea tuzo yake. Alikuwa ameteuliwa kupigania tuzo hiyo mara sita awali, tano kama mwigizaji bora na moja kama produsa wa filamu ya Wolf of Wall Street lakini hakufanikiwa kushinda. Alisema filamu ya The Revenant ilikuwa "kuhusu uhusiano wa binadamu maumbile asilia.” "Mabadiliko ya tabia nchi ni jambo la kweli, mabadiliko haya yanafanyika,” amesema. "Ndilo tishio kubwa zaidi kwa sasa kwa viumbe wote na tunahitaji kuchukua hatua sasa.”

Clinton asomba kura South Carolina

Mgombea Urais wa Marekani Hilary Clinton amepata ushindi mkubwa dhidi ya Bernie Sanders katika uchaguzi wa mchujo wa chama cha Democratic katika jimbo la Carolina Kusini kuwania uteuzi wa mgombea urais wa chama hicho. Ushindi huo wa Jumamosi (27.02.2016) unampa Clinton msukumo kabla ya siku muhimu kabisa ya uchaguzi huo wa mchujo : yaani mpambano wa "Jumanne Kabambe" ambapo majimbo 11 yatapiga kura kuchaguwa wagombea wa kupeperusha bendera za vyama katika uchaguzi wa rais wa Marekani baadae mwaka huu. Baada ya wiki nne za uchaguzi wa mchujo kuwania kuingia Ikulu ya Marekani Clinton waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje amejipatia ushindi wake wa kwanza muhimu katika kampeni yake baada ya ule wa kibaruwa kigumu wa Iowa na kushindwa na Sanders huko Hampshire na halafu ushindi wa pointi nne wa Nevada. South Carolina ni jimbo la kwanza la kusini kupiga kura kuteuwa mgombea wa kukiwakilisha chama cha Demokratik katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 kabla ya uchaguzi huo wa mchujo kuingia katika majimbo mengine 11 nchini kote. Clinton amesema huku akishangiliwa na umati kwamba "Kesho kampeni hii inaingia ngazi ya taifa " akiwashukuru wafuasi wake huko Columbia South Carolina ambapo ameibuka na ushindi unaomfungulia njia ya kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama hicho amesema " Tataigombania kila kura katika kila jimbo.Hatukichukulii kitu chochote, wala mtu yeyote kwa mzaha". Clinton pia alimdhihaki mtu ambaye wengi wanamuona kuwa yumkini akawa mgombea wa urais wa chama cha Republican : Donald Trump ambaye kauli mbiu ya kampeni yake ni "Ifanye Amerika Adhimu". Clinton amesema "Licha ya kile mnachokisikia, hatuna haja ya kuifanya Marekani iwe adhimu tena. Marekani katu haikuwahi kuacha kuwa adhimu." Ameongeza kile wanachotakiwa wafanye ni "kuifanya tena Marekani iwe kitu moja " ikiwa ni hoja dhidi ya kauli za majigambo zinozopendelewa na Trump zenye kugawa watu ambazo zinachochea chuki dhidi ya wahamiaji, Waislamu na wapinzani wake. Wakati asimia 99 ya maeneo yaliyopiga kura matokeo yake yakiwa yamepatikana Clinton alijizolea asilimia 73.5 dhidi ya asilimia 26 alizopata Sanders. Ushindi huo kabambe umemkombowa Clinton ambaye mwaka 2008 alishindwa vibaya katika jimbo hilo na Barack Obama ambaye ushindi wake hapo ulikuwa nukta muhimu kwa kampeni yake ya mafanikio na kuja kuchaguliwa kuwa rais. Kura za awali katika jimbo hilo la South Carolina zinaonyesha Wamarekani wenye asili ya Kiafrika ambao wanawakilisha asilimia 61 wa chama cha Demokratic katika uchaguzi huo wa mchujo walimuunga mkono Clinton kwa asilimia 86 kuliko vile walivyomuunga mkono Obama miaka minane iliopita. Kwa uangalifu Clinton amewashawishi wapiga kura weusi kwa kiasi fulani kwa kumpongeza Obama na kwa kuahidi kuendeleza haiba yake. Pia amekuwa akiendesha kampeni yake hiyo bega kwa bega na maskofu weusi na kuzuru makanisa ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika na vyuo vya weusi vya kihistoria. Bernie Sanders anawania ateuliwe awe mgombea wa urais wa chama cha Demokratik nchini Marekani. Bernie Sanders anawania ateuliwe awe mgombea wa urais wa chama cha Demokratik nchini Marekani. Sanders ambaye anajieleza kuwa yeye ni mjamaa wa chama cha Democratic anayetaka kuanzisha mapinduzi ya kisiasa nchini Marekani tayari anaangalia mbele baada ya kushindwa South Carolina. Mapema Jumamosi ameelekea Texas na baadae Minnesota majimbo mawili ambayo yatapiga kura hapo Jumanne wakati seneta huyo wa Vermont anapohitaji kuendelea kuonyesha ari yake iwapo anataka kuzidi kumpa changamoto Clinton katika uchaguzi huo wa mchujo. Sanders alimpongeza Clinton lakini amesisitiza kwamba yuko tayari kwa mpambano wa muda mrefu wa kampeni. Amesema katika taarifa baada ya kutolewa kwa matokeo kwamba "Nataka ifahamike wazi kwa kitu kimoja usiku huu.Kampeni hii ndio kwanza imeanza."

Mkataba wa kusitisha vita Syria wavunjwa

Watoto walipata fursa ya kucheza nje baada ya mkataba wa kusitisha mapigano kutekelezwa Ndege za jeshi zimeshambulia maeneo kadha ya kaskazini mwa Syria, siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kutekelezwa nchini humo. Wanaharakati wa huko wanafikiri mashambulio hayo yamefanywa na Urusi, ambayo inasaidia majeshi ya Rais Bashar al-Assad kukabiliana na waasi. Upinzani umelalamika kuwa makubaliano yamevunjwa mara 15 na upande wa serikali. Warusi pia wanasema, wameona visa kadha kinyume na mkataba, lakini kwa jumla, usitishwaji wa mapigano unaendelea. Awali Mawaziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani na Urusi, John Kerry na Sergei Lavrov, wamekaribisha mwanzo wa usitishaji mapigano nchini Syria. Wanaharakati wa huko wanafikiri mashambulio hayo yamefanywa na Urusi, ambayo inasaidia majeshi ya Rais Bashar al-Assad Ingawa kumekuwa na ripoti za wapiganaji kukiuka mapatano hayo ya usitishaji mapigano lakini kwa ujuma hali imetulia. Maeneo yaliyokuwa na mapigano makali ya Aleppo yametajwa kuwa tulivu. Bwana Kerry na Bwana Lavrov walizungumzia uwezekano wa kuanzisha mashauriano ya amani, ambayo Umoja wa Mataifa unatarajia yataanza juma lijalo. Wapiganaji wa Islamic State ambao hawashirikishwi katika usitishaji huo wa mapigano, walifanya mashambulizi dhidi ya mji wa Tal Abyad, Kaskazini mwa Syria. Wapiganaji Wakurdi walisema kuwa mashambulizi hayo yalizimwa.

Nigeria ina wafanyikazi hewa 24,000

Serikali ya Nigeria imeondoa karibu wafanyikazi 24,000 kutoka kwa orodha ya malipo ya wafanyikazi wa umma baada ya uchunguzi kugundua kwamba majina hayo yalikua gushi. Wizara ya fedha imesema hatua hii imesaidia kuokoa kima cha dola bilioni 11.5. Hii ni moja wapo ya kampeini ya kupambana na ufisadi aliyo ahidi Rais Muhammadu Buhari alipochukua mamlaka mwaka uliopita. Ufisadi na usimamizi mbaya wa fedha za umma zimetajwa kama vizingiti vikubwa dhidi ya ukuaji wa Nigeria, ambapo serikali imelazimika kubana matumizi kutokana na tisho la mdororo wa uchumi. Nigeria ndiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Barani Afrika na pia inaongoza katika uzalishaji wa mafuta imekumbwa na matatizo ya kifedha hususan kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Nchi hiyo pia inakumbwa na mfumuko wa bei, kuanguka kwa soko la hisa huku uchumi huo ukiwa na ukuaji wa chini zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja.

KKK lawashambulia weusi kwa visu California

Watu watatu wamedungwa visu katika mapigano kati ya kundi linalowachukia watu weusi la Ku Klux Klan (KKK) na waandamanaji wanaowapinga katika jimbo la California. Tukio hilo lilitokea karibu na eneo kulikopangwa mkutano wa hadhara wa wazungu wao wanachama wa KKK. Watu wanne walitiwa mbaroni katika makabiliano hayo, akiwemo mwanachama mmoja wa KKK aliyemdunga mweusi kisu. Msemaji wa polisi alieleza kuwa shida ilianza wakati wanachama wa KKK waliwasili katika uwanja wa Anaheim, karibu kilomita 50 Kusini Mashariki mwa Los Angeles, karibu na Disneyland. Msemaji wa polisi alisema kuwa wanachama hao wa KKK walishambuliwa weusi walipokuwa wanatoka kwenye gari. Mmoja aliangushwa chini. Waandamanaji watatu wanaopinga KKK walidungwa visu katika makabiliano hayo. Mtu mmoja aliyeshuhudia matukio hayo alisema kuwa wanachama wa KKK walikuwa wamelemewa. Mmoja wa waliodungwa visu anaugua na amelazwa hospitalini.

Sunday, February 28, 2016

Mahubiri ya Siku ya mazingira Kikanisa toka Kitabu cha Mwanzo 1:29-31

Wapendwa Washarika kitabu hiki cha Mwanzo ni cha mwanzo kweli, tofauti na Agano Jipya ambalo linasadikiwa kuchukuwa takribani nusu karne ambayo ni kuanza kuandikwa kati ya mwaka 50-100 Baada ya Kristo (AD) ili kukamilika kuandikwa kwake si hivyo kwa Agano la Kale ambalo linaaminika kuchukuwa milenia nzima yaani mwaka wa 1400-400 Kabla ya Kristo (BC) . Tunaona katika Agano la Kale kuwapo na Vitabu vya Kihistoria, Kinabii na Mashairi. Huku Lugha rasmi inayotumika ni Kiebrania (Hebrew) na Kiaramaiki (Aramaic)kwa baadhi ya vitabu. Wapendwa watu wa Mungu leo tunapewa kitabu hiki cha Kihistoria (Pentateuch) ili kituwezeshe kutafakari jsiku hii ya mazingira. Kitabu hiki cha Mwanzo kimeandikwa na Musa kama ilivyo dhamira ya historian a kwa kuwa ni cha kwanza ndicho kinabeba historia nzima ya kuanza kwa ulimwengu na maisha ya mwanadamu kwa ujumla. Mlamgo tuliopewa kuusoma ni eneo muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu awaye yeyote, ni Uumbaji wa kila kitu. Na hapa leo ni namna ambavyo Mungu anaviweka wakfu na kumkabidhi huyu mwanadamu (Adamu). Ili aweze uvitunza na kuvitiisha. Kikanisa na kwa mujibu wa Kalenda yetu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania toleo la mwaka 2016, leo ni Jumapili ya nne Kabla ya Pasaka na tunapaswa kutafakari zaidi juu ya Mazingira. MAZINGIRA NI NINI? Wapendwa Washarika Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni jua hewa, ardhi na maji. Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu namazingira. KWA NINI TUTUNZE MAZINGIRA? Wapendwa wangu shughuli za wanadamu zinaidhuru sayari yetu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Matatizo kama vile kuongezeka kwa joto duniani yanapozidi kuwa mabaya, wanasayansi, serikali, na viwanda vinazidisha jitihada za kukabiliana na hali hiyo. Je, sisi mmoja-mmoja tuna wajibu wa kusaidia kutunza mazingira? Ikiwa ndivyo, tunaweza kusaidia kwa kadiri gani? Biblia inatoa sababu nzuri kwa nini tunapaswa kufanya mambo yenye manufaa kwa dunia. Pia inatusaidia tuwe na usawaziko katika jitihada zetu. Tukumbuke kuwa "sisi ni nchi ya pili duniani nyuma ya Brazil kwa ubora wa uoto wa asili". Prof Maghembe TBC Radio 28.02.2016 saa 12:06 Asubuhi KUTENDA KUPATANA NA KUSUDI LA MUNGU. Mungu aliumba dunia iwe makao ya bustani kwa ajili ya wanadamu. Alisema kwamba kila kitu alichokuwa amefanya kilikuwa “chema sana” na akampa mwanadamu mgawo wa ‘kuilima na kuitunza dunia.’ (Mwanzo 1:28, 31; 2:15) Mungu anahisije kuhusu hali ya sasa ya dunia? Kwa wazi, yeye anachukizwa sana mwanadamu anapokosa kuitunza dunia, kwa kuwa Ufunuo 11:18 inatabiri kwamba ‘atawaharibu wale wanaoiharibu dunia.’ Kwa hiyo, hatupaswi kupuuza hali ya dunia. KUSAIDIA KUISAFISHA DUNIA Shughuli za kawaida za wanadamu hutokeza kiasi fulani cha takataka. Mungu ametupa zawadi ya majira yaani mizunguko ya asili ya dunia ili kuondoa takataka hizo, kusafisha hewa, maji, na ardhi. (Methali 3:19) Mambo tunayofanya yanapaswa kupatana na mizunguko hiyo. Hivyo, tunapaswa kuwa waangalifu tusishiriki katika kuharibu zaidi mazingira ya dunia. Utunzaji kama huo unaonyesha kwamba tunawapenda majirani zetu kama sisi wenyewe. (Marko 12:31) Fikiria mfano katika nyakati za Biblia. Mungu aliagiza taifa la Israeli lizike kinyesi cha wanadamu “nje ya kambi.” (Kumbukumbu la Torati 23:12, 13) Hilo lilifanya kambi iwe safi na uchafu ulioza haraka. Vivyo hivyo, leo Wakristo hujitahidi kutupa takataka upesi na kwa njia inayofaa. Tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa tunapotupa vifaa vyenye sumu. Takataka nyingi zinaweza kuboreshwa ili zitumiwe tena. Ikiwa sheria inasema kwamba takataka zitumiwe tena basi kutii sheria kama hizo ni sehemu ya kumlipa “Kaisari vitu vya Kaisari.” (Mathayo 22:21) Huenda jitihada nyingi zaidi zikahitajika ili kutumia tena takataka, lakini kufanya hivyo kunaonyesha kuwa mtu anatamani kuona dunia ikiwa safi. KUHIFADHI MALIASILI ZA DUNIA Wapendwa Washarika ili kutimiza mahitaji yetu ya chakula, makao, na mafuta, na hivyo kuendeleza uhai wetu, lazima tutumie maliasili za dunia. Kutambua kwetu kwamba mali hizo ni zawadi kutoka kwa Mungu kutaonekana tunapotumia mali hizo. Waisraeli walipotamani nyama jangwani, Yehova aliwapa kware wengi sana. Pupa iliwafanya watumie vibaya na kwa ubinafsi zawadi hiyo, nao wakamkasirisha sana Yehova Mungu. (Hesabu 11:31-33) Mungu hajabadilika tangu wakati huo. Kwa sababu hiyo, Wakristo wenye dhamiri nzuri huepuka kutumia maliasili vibaya kwani kufanya hivyo kunaweza kuwa ishara ya pupa. Huenda wengine wakaona kuwa wana haki ya kutumia nishati au mali nyingine za asili kupita kiasi. Lakini, maliasili hazipaswi kutumiwa vibaya eti kwa sababu tunaweza kuzigharimia au ziko kwa wingi. Baada ya Yesu kulisha umati mkubwa, alielekeza kwamba samaki na mikate iliyosalia ikusanywe. (Yohana 6:12) Alijitahidi asipoteze kile ambacho Baba yake alikuwa ameandaa. KUWA NA USAWAZIKO Ndugu zangu kila siku sisi hufanya maamuzi yanayoathiri mazingira. Je, tuchukue hatua za kupita kiasi kama vile kujitenga na jamii ya wanadamu ili kuepuka kuidhuru dunia? Biblia haipendekezi mahali popote jambo kama hilo. Fikiria mfano wa Yesu. Alipokuwa duniani, aliishi maisha ya kawaida ambayo yalimwezesha kutimiza kazi aliyopewa na Mungu ya kuhubiri. (Luka 4:43) Isitoshe, Yesu alikataa kujihusisha katika siasa ili kutatua shida za jamii ya wakati huo. Alisema hivi waziwazi: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu.”—Yohana 18:36. Hata hivyo, ni muhimu kwetu kufikiria jinsi tunavyodhuru mazingira tunapofanya maamuzi fulani kama vile kununua vifaa vya nyumbani, kusafiri, na kujihusisha na tafrija. Kwa mfano, wengine huamua kununua vitu ambavyo vimeundwa au vinavyotumika katika njia ambayo haiharibu sana mazingira. Wengine hujitahidi kupunguza muda wanaotumia katika utendaji unaochangia uchafuzi au unaotumia vibaya maliasili. Hakuna haja kwa mtu yeyote kuwalazimisha wengine wafuate maamuzi yake kuhusu kutunza mazingira. Hali hutofautiana ikitegemea mtu binafsi na eneo analoishi. Lakini sisi sote tunawajibika kibinafsi kwa sababu ya maamuzi tunayofanya. Kama Biblia inavyosema, “kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe.”Wagalatia 6:5. Muumba aliwapa wanadamu madaraka la kutunza dunia. Kuthamini mgawo wetu na kumheshimu Mungu na kazi zake za uumbaji kwa unyenyekevu kunapaswa kutuchochea tufanye maamuzi ya akili na ya kudhamiria kuhusu jinsi tunavyoitunza dunia. “Environmental justice is based on the principle that all members of a society have the right to clean air, water, and soil, as well as a right to live in communities where they can raise their families and send their kids out to play in healthy and nurturing natural environments. Further, it embraces the notion that no one possesses the right to degrade and destroy the environment, whether the government at all levels, private industry, or individual citizens. Finally, environmental justice includes a guarantee of equal access to relief and the possibility of meaningful community participation in the decisions of government and industry”.Hii imewasiliswa katika maadhimisho ya 20 ya Kuheshimu mchango wa Dr Martin Luther King katika utunzaji wa mazingira iliyotolewa katika chuo Kikuu Yale chini ya Yale Peabody Museum of Natural History Sunday, Jan 17- 18, 2016 UHUSIANO WA MAISHA NA MAZINGIRA YETU Ni wazi kuwa maisha katika uso wa Dunia hutegemea huduma ubora wa huduma zitolewazo na mazingira husika. Ukiangalia mfumo wa ikolojia wa misitu, bahari, mbugani na kwenye udongo utaona uwepo wa maji, hewa nzuri na rutuba ya udongo ndivyo vinavyopelekea wanyama na mimea kuwepo na kupendezesha mazingira. HEWA – ni sehemu muhimu ya mazingira kwani viumbe hai vyote hupumua ili kumudu maisha. Wakati wanyama wanavuta hewa ya oksijeni mimea huvuta hewa ya Kaboni dayoksaidi wakati wa mchanga ili kutengeneza chakula, hewa ambayo wanyama huitoa kama hewa chafu. Hapa tulijifunza uhusiano kati ya wanyama na mimea katika kuishi na pia katika kuweka usawa wa hewa safi angani. UDONGO – ni maada ambamo mimea hupandwa na kukulia pia wanyama hupata mahitaji yao kama Chakula kutoka kwenye udongo na pia udongo hufanya nchi kavu ambapo binadamu na Wanyama wengi huishi. Lakini pia udongo unahifadhi wadudu wadogo wadogo wengi tusioweza kuwaona kwa macho ambao husaidia kurutubisha udongo na kuifanya mimea iweze kustawi na pia mizizi iweze kupata maji na hewa. Hapa tunaona umuhimu wa udongo katika kuboresha maisha kwa kuifanya mimea iweze kukua.aa JUA – ni chanzo kikubwa asilia cha nishati ya mwanga na joto. Nishati ya mwanga kutoka katika Jua mbali na kutupatia joto na kusaidia kufanyika kwa mvua na kupunguza baridi katika uso wa Dunia, bado ni muhimu sana katika kuisaidia mimea kuweza kutengeneza chakula chake chenyewe. Bila kuwepo kwa mwanga wa Jua mimea itashindwa kutengeneza chakula na kupelekea kufa, hivyo kuwafanya wanyama wanaotegemea mimea kufa, ambao nao watawafanya wanyama wala nyama kufa akiwamo binadamu anayekula nyama na mimea. MAJI – yamechukua sehemu kubwa ya Dunia yetu, ni sehemu kubwa ya miili yetu na maisha ya viumbe wengi hutegemea maji kwa ajili ya kuwa hai. Maji hupatikana katika maeneo mbali mbali kama kupitia mvua na hupatikana kwa wingi katika mito, maziwa, visima, bahari, barafu ,unyevu na Umande na pia chini ya ardhi. Maji huzunguka kwa kuvukizwa kutokana kwenye uso wa Dunia na kupanda juu na kutengeneza mawingu ambayo baadae hurudi Duniani kama mvua au theluji na kufanya maisha yaendelee Duniani. Mvua inaponyesha kiasi kikubwa cha maji yake huanguka ardhini na kisha kuzama chini na kufanya Chemchem, maji yanayotiririka hufanya Mito nayo mito hutiririka hadi katika maziwa au Bahari kisha maji ya bahari yanapopata joto mtiririko hujirudia. KUTEGEMEANA KATIKA MAZINGIRA (IKOLOJIA) – Wapendwa Washarika viumbe hai vimegawanyika katika makundi mawili nayo ni Mimea na Wanyama. MIMEA hutegemea mazingira ufu na ndilo kundi pekee lenye kujitengenezea chakula chake chenyewe kwa kutumia chumvichumvi za ardhini, maji,gesi ya kabon dayoksaid na mwanga wa jua na kufanya mimea kukua katika udongo au maji. Mimea bado hutegemea wanyama kuweza kustawi kutokana na samadi inayotokana na wanyama kisha huoza na kufanyika mbolea inayorutubisha udongo. WANYAMA hutegemea kupata hewa safi ya oksijeni iliyotengenezwa na mimea, ambayo hutumika kutengenezea nishati kutokana na chakula kilichosharabiwa katika mwili. MZUNGUKO WA KABONI – hutokana na kutegemeana kwa viumbe hai kwa ni Kabonidoiksaidi iliyoko hewani ambayo hutumika na mimea kutengeneza chakula. Mimea huliwa na baadhi ya wanyama kisha wanyama hao huliwa na wanyama wanaokula nyama.kisha mizoga ya wanyama na mimea huoza na kutoa kaboni inayorudi angani. Hapa kwetu Tanzania sisi huungana na wenzetu duniani kote kila mwaka, tarehe tano Juni ni siku ya mazingira duniani. Watu katika nchi mbali mbali hapa ulimwenguni huadhimisha siku hii kwa namna mbali mbali, wengi aghalabu hufanya shughuli mbali mbali za utunzaji wa mazingira. Kwa hapa kwetu nchini, sherehe hizi huambatana na kufanya kazi za utunzaji mazingira, kama vile uokotaji wa taka mahali mbali mbali, upandaji wa miti sehemu za wazi na kadhalika. Lakini kwa upande mwingine, hapa nchini kwetu upandaji wa ,miti kitaifa hufanyika kila mwaka siku ya Januari mosi, yaani siku ya mwaka mpya. Nadhani hii tarehe imewekwa makusudi kwa sababu kwa maeneo mengi (kama si yote) hapa nchini huwa ni msimu wa mvua. Kwa hiyo ili miti iliyopandwa iote vizuri, ni lazima ipate maji ya kutosha, kutokana na mvua hizi. Wapendwa Washarika dunia imeanza kuonja machungu ya kutotunza mazingira (Global Warming) na kupelekea kujaribu kuzisaidia na kuanzisha mradi wa malipo kwa wote wanao miliki misitu maarufu Carbon yote hii ni kujaribu kuhamisisha upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira. Kanisa letu limeanza kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kuanzisha Programu maalum ya Uhai na Mazingira chini Bibi Patricia Mwaikenda. Programu hii mpaka sasa imeshaandaa Sera ya Mazingira ya Kanisa, kuanzisha miradi ya mitambo wa kuzalisha nishati mbadala ya kinyesi (Biogasi) na kuanzisha miradi ya upandaji wa miti kwa ushirikiano wa kanisa na wenzetu wa Ushirikiano wa Makanisa ya Ulaya (Lutheran Mission Cooperation)- LMC). Na mwaka jana 9Disemba,2015 ilikuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa na tumeona jana kwetu hapa Dar Es Saalam na mikoa mingine kuwa ilikuwa ni siku maalum usafi wa mazingira ambayo kwa sasa inaonekana kuwa itakuwa hivyo kwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Kwa kuwa Kanisa lipo katikati ya jamii na wanajamii ndiyo washarika na ndiyo wafuasi wa Yesu basi tushirikiane kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu na kuacha kulalamika tu. Tukumbuke hii ni kwa ajili ya ustawi wa afya zetu na vizazi vinavyokuja. Tukumbuke kuwa kulingana na tafiti inaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2,050 watu bilioni sita duniani hawatakuwa kabisa na huduma ya maji, kwa nini sisi tujione tu salama? Na tujuwe kuwa vita ijayo ni ya kugombea zrdhi na maji na hapa kwetu Tanzania tayari viashiria vimeanza baina ya mapigano ya wakulima na wafugaji katika maeneo yetu. “Our lives begin to end the day we become silent about things that matter.” — Dr. Martin Luther King, Jr. Tumsifu Yesu Kristo .

Waitaliano kuifumua Manzese

ENEO la Manzese lililopo jijini Dar es Salaam linatarajiwa kufumuliwa na kujengwa majengo ya kisasa kutokana na ramani ya mipango miji inayofanywa na wataalamu. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipogawa ramani 104 kati ya 329 kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Dar es Salaam ili kumaliza migogoro ya ardhi. Lukuvi alisema hadi kufikia Julai, mwaka huu, Dar es Salaam itakuwa na mipango miji yake ambayo kazi hiyo inafanywa na wataalamu kutoka nchini Italia. “Dar imejaa lakini lazima tujenge, Manzese ihame lazima ije Manzese mpya, iende juu. Hatufukuzi watu pale lakini watatafutiwa namna,” alisema Lukuvi. Alilitaja eneo jingine litakalojengwa nyumba za kisasa, hoteli pamoja na kumbi za mikutano ni kando ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). “Eneo hilo lazima liwe transformed (libadilike) ili kuendana na uwanja wa ndege wa kisasa ambao unajengwa. Hatuna haja ya watu wamekuja kwa ajili ya mikutano kuja hadi katikati ya mji,” alisema Lukuvi. Alitaja miji mingine ambayo inatengenezewa mipango miji ni Arusha ambayo itakwenda hadi Meru na Mwanza ambako wataalamu wanaohusika kuutengeneza wanatoka nchini Singapore. “Hao Singapore ni watu wenye uwezo mkubwa, master plan ya Mwanza na Arusha tumeshawalipa fedha nyingi za wizara hivyo itakuwa tayari. Awali ya Dar ilivyoletwa niliikataa kwa kuwa ilikuwa na upungufu na haikuwa na basement wala data za sasa,” alisema Lukuvi. Alisema ramani hizo zitawasaidia wenyeviti hao wa vijiji kujua ni yapi maeneo ya wazi na wapi panapaswa kujengwa nini pindi watendaji wa miji wanapokwenda kwa lengo la kufanya kazi. “Hii ya kuvunja vunja nyumba za masikini kama mwenyekiti wa mtaa hana ramani anashindwa kumtetea mnyonge anayebomolewa. Leo hii mama masikini akivamiwa ardhi yake mwenyekiti anaweza kuingilia, leo hii wenyeviti 104 tunawapa ramani,” alisema Lukuvi. Alisema hilo litasaidia kuwaondoa wote waliojenga katika maeneo ya wazi pamoja na maeneo ya huduma za kijamii. Lukuvi alisema kuna watu waliuziwa viwanja tofauti na matumizi yanayofanyika ambapo ni lazima virudishwe. “Nitaanza na Mbezi eneo ninakoishi, eneo la Shule ya Msingi ya Kata watu wamevamia, jamani mkiona uvunjifu toeni taarifa wilayani kuweni wa kwanza kuwa askari. “Mfano kati ya majengo 48 yaliyobomolewa Kinondoni, 12 yalimaliziwa na matapeli, kuna waliokuwa wameanza msingi matapeli wakaja kumalizia hao wameshindwa hata kutufikisha mahakamani, lengo letu ni kuzuia uendelezaji holela wa majengo,” alisema Lukuvi. Alisema Dar es Salaam haina haja ya kuwa na mabwana shamba au nyuki badala yake waongezwe wataalamu wa mipango miji. Katika hatua nyingine, alisema awamu ya pili itafanya urasimishaji na nyumba zitakazokutwa zimejengwa maeneo mazuri hazitabomolewa. “Mtaa ulio tayari kurasimishwa watuambie. Kwa uzembe wetu Serikali au kuchelewa, wananchi walituwahi kujenga sasa kama wako pazuri wasibomolewe, nyumba za masikini zitakazorasimishwa zipewe namba na hati,” alisema Lukuvi. Aliwataka viongozi wa ardhi kwenda maeneo ya matukio wakiwa tayari wametoa taarifa kwa wenyeviti wa mitaa. Pia aliwataka watendaji waliohudhuria hapo kumfikishia salamu mtu aliyemtaja kwa jina la Mahinga kuwa ndiye kinara wa kutoa vibali vya ujenzi hadi barabarani katika eneo la Kibaha. Alisema mipango miji itaondoa uvunjifu wa maadili kwa kuweka shughuli moja katika eneo husika. “Watu wanapiga muziki hadi asubuhi huku grocery wanauza kitimoto hatua mbili ya msikiti, eneo jingine wanauza pombe hatua mbili kanisa. Zipo nyingi lakini zinapaswa kuendeshwa kwa maadili, lazima kurudisha nidhamu, mwenyekiti aanze kurudisha nidhamu,” alisema Lukuvi. Alisema watu wanaokuja kuomba kujenga wasiangaliwe sura bali waambiwe utaratibu ulivyo na kama ni eneo la kujenga ghorofa moja lijengwe hivyo na si vinginevyo. “Nyie msivunje lakini mtoe taarifa hata kama ni ujenzi wa choo ambao hauna kibali toeni taarifa lengo ni kuwapa silaha ili tuijenge Dar es Salaam ambayo ndio kioo cha nchi. Jiji limejaa lakini hadi Julai utaona mabadiliko hakutakuwa na uvamizi,” alisema Lukuvi. Aliwataka wenyeviti hao ambao wana matatizo katika maeneo yao na walikwishatoa taarifa wilayani lakini hazifanyiwi kazi kwenda moja kwa moja ofisini kwake au kutuma ujumbe mfupi kupitia namba ya simu aliyowapatia. Alisema ili kuboresha waliitoa Pwani katika Kanda ya Dar es Salaam ambako kwa sasa wana uwezo wa kumpatia mtu hati ya nyumba ndani ya mwezi mmoja. Alisema hadi sasa kuna hati 3,000 za nyumba ambazo wananchi hawajakwenda kuzichukua huku wizara hiyo ikijitahidi kuboresha ili kuingia katika mfumo wa elektroniki ambako hati inaweza kupatikana kwa siku moja. Awali, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mikoa, Profesa John Lupala, alisema michoro ya mitaa 104 ilikamilika kati ya mitaa 329 huku iliyobaki ikisubiri urasimishaji. Alisema katika michoro hiyo, Wilaya ya Kinondoni ilipata 33, Temeke 10 na Ilala 61. Profesa Lupala alisema katika sensa iliyofanyika ilionyesha Kinondoni ina kata 35 na mitaa 113, Temeke kata 36 na mitaa 105 huku Ilala ikiwa na kata 35 na mitaa 111. “Kwa maeneo ambayo hayana utata, Machi 30 itakuwa tayari lakini yenye urasimishwaji Juni yatakamilika,” alisema Profesa Lupala.

Wafanyabiashara wa sukari wapambana na Magufuli

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam*Mwenyekiti wa Bodi aibuka asema wemelenga kumkomoa NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM SASA ni wazi kwamba wafanyabiashara wa sukari nchini wameamua kuanzisha vita na Rais John Magufuli, kwa kuamua kuficha bidhaa hiyo na hivyo kuadimika katika soko na kupanda bei. Hatua hiyo ya wafanyabiashara imekuja baada ya Rais Magufuli kutangaza utaratibu mpya hivi karibuni wa kutaka uagizwaji wa sukari kutoka nje ufanywe na wazalishaji wa bidhaa hiyo hatua ambayo inakata mrija wao wa ulaji. Jana Bodi ya Sukari ililazimika kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kile walichokibaini baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa bidhaa hiyo imeadimika. Akitoa tamko kwa niaba ya Bodi ya Sukari na wazalishaji bidhaa hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Ami Mpungwe, alisema tangu Rais Magufuli alipotangaza utaratibu mpya wa kuwatumia wazalishaji kuagiza sukari wamebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kufanya mipango ya kuhujumu taratibu hizo. Alisema wafanyabiashara hao wameamua kuficha bidhaa hiyo ili kuwaaminisha wananchi kwamba sababu kubwa ya kuadimika kwa sukari inachangiwa na uamuzi huo wa rais. Kabla ya uamuzi huo haujafikiwa na Rais Magufuli, wafanyabiashara wengi wa bidhaa hiyo walikuwa hawalipi kodi hali iliyochangia kufanya biashara hiyo kiholela huku wakipata faida nyingi na kuinyima mapato Serikali. Hili linathibitishwa na kauli iliyotolewa na Mpungwe jana ambaye aliwanyooshea vidole waziwazi wafanyabiashara hao kwamba walikuwa wakinufaika na uingizaji holela wa sukari bila kulipia kodi na kwamba hata wanachokifanya sasa cha kupandisha bei ya sukari ni mbinu chafu ili kudhoofisha juhudi za Serikali za kuendeleza viwanda vya ndani kwa nia ya kujinufaisha wao binafsi. “Wameanzisha kampeni za kuwatia hofu wananchi wakiwaonyesha sukari imeadimika kutokana na agizo lililotolewa na Serikali la kudhibiti uingizaji sukari nchini,” alisema Mpungwe. “Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuficha maghalani na kuendesha propaganda kwamba bei ya sukari imepanda na wapo waliopandisha kwa ghafla bei ya sukari kwa madai kwamba kuna upungufu viwandani na wengine wakiwalaghai watu kwamba bei wanayonunulia viwandani imepanda,” alisema Mpungwe na kusisitiza kuwa wanaofanya hujuma hiyo watachukuliwa hatua za kisheria. Akizungumzia utaratibu huu mpya alisema unafanyika kwa kuzingatia ulipaji kodi kwa sukari ya nje inayoingizwa nchini lakini pia umelenga kulinda viwanda vya sukari kwa kuimarisha soko la ndani. Mwenyekiti huyo wa Bodi ya sukari nchini, alisema wazalishaji nchini wanatambua kwamba viwanda vyote vya wasambazaji vinauza sukari kati ya shilingi 1,700 na 1,800 kwa kilo na hakuna kilichopandisha bei tangu tamko la Rais lilipotoka. “Hali ya uzalishaji sukari msimu huu 2015/2016 ni nzuri na msimu utafungwa Aprili kupisha matayarisho ya msimu mpya 2016/2017 Mei na Juni 2016 kama ilivyo taratibu kwa kila mwaka na viwanda vina akiba ya tani 32,000 za sukari inayoendelea kuuzwa,” alisema na kuongeza: “Kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo Moshi na kile cha Kagera vinaendelea kuzalisha sukari hadi Aprili 2016 na Serikali imeshatangaza utaratibu wa uagizaji wa sukari ambao utahakikisha sukari inayoruhusiwa kuingizwa nchini na kiasi kinachohitajika kuziba mahitaji ya wakati viwanda vinapokuwa vimefunga uzalishaji.” Aliongeza kuwa kutokana na utaratibu huu mpya wa kuweka uwazi katika usimamizi wa bidhaa ya sukari, utasaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti sukari ya magendo na kuhakikisha inayoingia ni ile iliyoruhusiwa kwa kulipiwa kodi. Mwenyekiti huyo alisema Bodi ya sukari na wazalishaji wanawahakikishia Watanzania kwamba hali ya upatikanaji wa sukari nchini ni nzuri na wao kwa kushirikiana na vyombo husika vya Serikali watahakikisha wanaendelea kuwa na sukari ya kutosha kwa muda wote. KAULI YA RAIS MAGUFULI Hivi karibuni Rais Magufuli alitoa kauli ya kupiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka mataifa ya kigeni ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini ambavyo vimeathiriwa na uingizaji wa sukari ya bei rahisi kutoka nje. Rais huyo alisema Taifa haliwezi kufikia malengo yake ya kuimarisha viwanda vya ndani iwapo viwanda vya sukari nchini havitalindwa na kuwezeshwa dhidi ya uingizaji huo. Rais Magufuli alielezea kuwepo kwa viwanda nchini ambavyo hununua miwa kutoka kwa wakulima wadogo wadogo na viwanda hivyo huzalisha sukari, lakini pia ajira ni chanzo cha mapato ya Serikali. Alisema ingawa ipo hifadhi ya kutosha ya sukari lakini wapo watu serikalini wanaotoa vibali vya kuingiza sukari kutoka nje. Aliwaelezea watu hao kama ni sehemu ya kukandamiza juhudi za Serikali hali iliyosababisha kuchukua hatua ya kuzuia utolewaji wa vibali kuruhusu uingizaji wa sukari, hadi itakapotokea mahitaji maalumu. Alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu ambao wamekuwa wakiingiza sukari nchini iliyoisha muda wake wa matumizi na haifai kutumiwa na binadamu. Mahitaji ya sukari nchini ni tani 420,000 ambako tani 170,000 zinatumiwa kwa mahitaji ya nyumbani na nyingine iliyobaki hutumiwa viwandani. Alisema viwanda vya hapa nchini vimekuwa vikizalisha tani 300,000 hali inayosababisha kuwepo kwa upungufu wa tani 290,000 kila mwaka kwa matumizi ya nyumbani na yale ya viwandani. Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Saturday, February 27, 2016

Tanzania na Kenya zazindua kituo cha mpakani

Tanzania na Kenya zimezindua huduma ya kituo cha pamoja mpakani yaani One Border Post katika mpaka wa Holili (Tanzania)-Taveta (Kenya). Wakizindua huduma hiyo na majengo ya kisasa Waziri wa Tanzania anayeshughulikia Nchi za nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na ushirikiano wa kimataifa Balozi Agustin Mahiga na Phyillis Kandie ambaye ni Waziri wa Kazi na Afrika Mashariki upande wa Kenya wamesema huduma hii iliyozinduliwa ni msingi muhimu katika kuelekea kwenye Ushirikiano imara wa Afrika Mashariki. Waziri Kandie amesema kuweka huduma za Mpaka wa Nchi mbili katika eneo moja kutakuza uchumi wa nchi zote mbili kwa haraka. Balozi Mahiga wa Tanzania amesema hii ni moja ya hatua mojawapo za kuelekea katika matumizi ya sarafu moja. "Mfano wa faida za mradi kama huu ni unaona itapunguza takribani 400 (barabara ikikamilika kutoka Mombasa kwenda Burundi) japo Gharama ni kufikia milioni 12 dola za kimarekani lakini Afrika Mashariki tutafaidika" Ameongeza Katibu Mkuu wa Mtangamano wa Afrika Mashariki Richard Sezibera aliyekuwepo kushuhudia ufunguzi huu. Mradi huu ambao umechangiwa na Nchi wahisani pamoja na Kenya na Tanzania umesimamiwa na Trade Mark East Africa.

Wana mabadiliko waeleka kushinda Iran

Ripoti kutoka Iran zinasema kuwa matokea ya awali ya uchaguzi wa wabunge, yanaonesha kuwa wagombea wanaopendelea mabadiliko, wanaelekea kushinda kwa wingi mkubwa kabisa katika mwongo mzima. Matokeo rasmi bado hayajatolewa, lakini ripoti zinasema, inaonyesha wagombea wasiopenda mabadiliko wamepoteza kura. Ikiwa wabunge wanaopenda mabadiliko, na wanaotaka kuimarisha uhusiano na mataifa ya Magharibi, wakiongezeka, watampa nguvu Rais Hassan Rouhani. Uchaguzi huo ndio wa kwanza, tangu Iran kutia saini makubaliano na mataifa makuu kuhusu mradi wake wa nuklia,mkataba uliopelekea karibu vikwazo vyote vya kiuchumi vya kimataifa dhidi ya Iran, kuondoshwa.

Wanajeshi 100 kupelekwa nchini Burundi

Umoja wa Afrika umetangaza kwamba utawapeleka waangalizi 100 wa haki za kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100 wa kijeshi nchini Burundi. Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza ameunga mkono mpango huo. Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika ziara ya siku mbili wiki hii. Walikutana na bwana Nkurunziza na viongozi wawili wa upinzani ambao wamesalia nchini humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi Aprili baada ya Nkurunziza kutangaza kuwa atawania muhula wa tatu. Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo hivi karibuni.

Shambulio la angani lawauwa watu 30 Yemen

Takriban watu 30 wameuawa katika shambulio la angani ndani ya soko moja karibu na mji mkuu wa Yemen Sanaa,kulingana na mashahidi. Wakaazi walinukuliwa na shirika la habari la Reuters wakisema kuwa takriban watu 30 wamejeruhiwa wengi wakiwa raia . Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulio hilo. Takriban watu 6000 wameuawa tangu muungano wa kijeshi unaoongozwa na taifa la Saudia kuanza kuwashambulia waasi mwezi Machi. Mashambulio hayo yanalenga kuirejesha mamlakani serikali na kuwafurusha waasi wa Houthi wanaomuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Ali Abdullah Saleh.

Ukawa waweka msimamo ushindi meya Dar leo

WAKATI uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ukitarajiwa kufanyika leo, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeweka msimamo wa ushindi, huku ukikitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutotumia vyombo vya dola kuuvuruga. Umoja huo unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD, ulifanikiwa kupata mameya wa manispaa za Kinondoni na Ilala, huku CCM wakipata meya wa Manispaa ya Temeke. Awali katika chaguzi hizo, CCM, yenye idadi ndogo ya madiwani, ililaumiwa kwa kutumia wabunge wa viti maalumu kutoka Zanzibar na mikoa mingine na wabunge wa kuteuliwa ili kuongeza idadi ya wapiga kura, jambo lililofanya uchaguzi wa meya wa jiji kuahirishwa mara kadhaa na kukwamisha shughuli nyingi. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, alisema idadi ya wapiga kura inawabeba kushinda uchaguzi huo. “Tunakwenda kesho kupiga kura tukiwa na wapiga kura halali 58 wa Kinondoni na kati ya hao, vyama vya Ukawa kwa maana ya Chadema na CUF ni 38 na CCM 20. Wajumbe 54 kutoka Ilala, kati yao 31 ni wa Ukawa na 23 ni wa CCM. Wapiga kura kutoka Manispaa ya Temeke wakiwa 49, Ukawa wakiwa 18 na CCM 21. Jumla ya wajumbe ni 161,” alisema Mwalimu. Akizungumzia msuguano uliosababisha uchaguzi huo kucheleweshwa, Mwalimu alisema ulisababishwa na CCM na mamlaka zinazosimamia uchaguzi huo. Hata hivyo, alisema kutokana na vikao vya usuluhishi vilivyohusisha vyama vya siasa vyenye madiwani, yaani Chadema, CUF na CCM, majina maalumu ya wapiga kura yameshapitishwa. “Mpaka tumefikia hapa, tayari vimeshafanyika vikao vya kupitisha na kuthibitisha majina ya wapiga kura. Wamekubaliana kuwa walioshiriki kupiga kura kumchagua Meya wa Temeke, Ilala na Meya wa Kinondoni ndio hao watakaoshiriki kumchagua meya wa Dar es Salaam,” alisema Mwalimu na kuongeza: “Jambo lilikuwa wazi siku nyingi, lakini CCM kilikuwa kikifanya jitihada za kuvuruga kwa kuleta mamluki. Tumeona wakileta wabunge kutoka mikoa mingine na kutoka Zanzibar.” Aliilaumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akisema ilijaribu kuvuruga uchaguzi huo kwa kisingizio cha kuomba taarifa kutoka mamlaka nyingine. “Kesho tuna taarifa kuwa watu hawa baada ya kushindwa njama za nje wanakusudia kuharibu uchaguzi ndani ya ukumbi kwa ama kufanya vurugu, kuleta polisi wengi, kusingizia kuna vurugu, kusingizia huyu hivi huyu vile. Wakamate madiwani wetu na wabunge wawatoe nje,” alidai Mwalimu na kuongeza: “Hilo likishindikana wanakusudia kutangaza matokeo kwa nguvu yatakayotoa mshindi kwa CCM. Nadhani wote tunakumbuka kilichotokea Tanga.” Alisema uchaguzi huo siyo vita wala vurugu na unaongozwa na taratibu, kanuni na sheria inayoonyesha nani anafaa kugombea na nani anafaa kupiga kura. “Hatutarajii kuona polisi kesho. Ni wajumbe 161 wanapiga kura na mshindi atatangazwa biashara imekwisha. Kwa hiyo hatutarajii kuona magari ya washawasha, mabomu ya machozi wala rundo la askari. Kesho ni uchaguzi wa meya,” alisema. Amewataka watu wasiokuwepo kwenye idadi ya 58 ya Kinondoni, 49 wa Temeke na 54 wa Ilala kutojitokeza kwenye ukumbi huo ili kuepusha vurugu. “Uchaguzi ni namba na namba zimejionyesha zinatubeba, tunategemea Isaya Charles Mwita kesho atatangazwa kuwa meya wa Dar es Salaam na atatangazwa ili awatumikie wananchi,” alisema. Kuhusu uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero, Mwalimu alisema utata wake unafanana na wa Dar es Salaam na kuzitaka mamlaka kutafuta suluhu ili uchaguzi huo ufanyike mapema. “Tukimaliza figisufigisu ya Dar es Salaam, tunaelekea Kilombero, eti zinatafutwa tafsiri za nani mpiga kura halali na nani siyo. Kama lilivyomalizwa Dar es Salaam, wapiga kura halali wanajulikana. Kilombero nako tunataka uchaguzi uitishwe chini ya wapiga kura halali,” alisema Mwalimu. Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Kilio cha wafanyakazi waliomzuia Majaliwa chamfikia waziri

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, amesikiliza kilio cha wafanyakazi wa Kampuni ya Tarmal ambayo ni Wakala wa Kampuni ya PSI. Jenista alikwenda jana kusikiliza kilio cha wafanyakazi hao baada ya juzi kumfikishia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, baada ya kuzuia msafara wake uliokuwa ukitoka katika hafla ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Sh bilioni 10 vilivyotolewa na umoja wa kampuni zinazozalisha vinywaji laini kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Wafanyakazi hao waliopo katika Ghala la PSI lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam, waliuzuia msafara wa Waziri Mkuu na kumwambia baadhi ya kero wanazokumbana nazo wawapo kazini. Baada ya Jenista kufika katika ofisi za kampuni hiyo, aliwapa muda wafanyakazi kutoa malalamiko yao na kwa kupokezana walisema kilio chao kikubwa ni suala la mishahara midogo pamoja na mikataba. Pia walisema jambo jingine ni makato yao ya mishahara kutopelekwa katika Mfuko wa Pensheni wa PPF. “Tumekuwa tukikatwa fedha zetu huku tukiambiwa kuwa zinaenda PPF kumbe hazipelekwi, mfano tangu mwaka 2014 hakuna fedha yoyote iliyopelekwa, sisi tukienda kufuatilia tunaambiwa hakuna fedha iliyopelekwa,” alisema Amani Athumani kwa niaba ya wenzake. Pia alisema ushirikiano baina ya mwajiri na waajiriwa ni mdogo na wanaweza kupeleka matatizo yao lakini wasipate majibu, hawapandishiwi mishahara na kama wakipandishiwa ni Sh 500 pia hailipwi kupitia benki. Baada ya kumaliza kuwasikiliza, Jenista alilazimika kutoa maagizo yatakayowezesha upatikanaji wa haki zao. Katika maagizo yake aliunda kamati ndogo itakayojadili malalamiko ya watumishi hao na baada ya siku tano itatoa mrejesho wa makubaliano yaliyofikiwa. “Naagiza kamati hii niliyoiunda ambayo ina wawakilishi watano kutoka miongoni mwa watumishi hawa, uongozi wa kampuni, mwakilishi kutoka PPF pamoja na wataalamu wa wizara na itaanza kufanya kazi leo (jana) na baada ya siku tano itarudi hapa kuleta mrejesho wa yale waliyokubaliana,” alisema Jenista. Alisema kazi ya kamati hiyo itakuwa ni kupitia mikataba yote na kupitia taarifa za makato ya fedha zilizopaswa kupelekwa PPF na kuomba uongozi wa kampuni hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha. Pia aliuagiza uongozi wa Tarmal kuhakikisha unawezesha wafanyakazi hao kuunda chama chao kitakachokuwa kinashughulikia malalamiko yao. Katika hatua nyingine, baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tech Park inayoshughulika na uzalishaji wa mifuko ya kupakia saruji walimzuia kuondoka hadi atakapowasikiliza shida zao. Hata hivyo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Antony Mavunde, alilazimika kukatisha safari yake na kwenda kusikiliza malalamiko yao. Wafanyakazi hao walimweleza Mavunde kuwa kwa muda mrefu wanafanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi huku mishahara wanayolipwa ni midogo. “Kazi tunayoifanya ni kubwa wakati malipo tunayolipa ni madogo ukilinganisha na ukubwa wa kiwanda chenyewe ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya Afrika vinavyozalisha mifuko ya saruji inayotumika nchi nzima,” alisema James Charles. Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Sultan, alisema wananyanyaswa na raia wa kigeni walioko kiwandani hapo, kupewa mikataba mifupi, mishahara midogo na makato yao kutopelekwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Chanzo:http://mtanzania.co.tz Baada ya kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi hao, Mavunde aliagiza hadi kufika Ijumaa ya wiki ijayo uongozi wa kampuni hiyo uwe umewapa waajiriwa wao mikataba inayoendana na taratibu zote na kuhusu mishahara aliagiza wataalamu wa wizara kukaa na uongozi na wawakilishi wa wafanyakazi hao kujadili stahiki hizo. “Kufikia Jumatatu nataka niletewe nakala za vibali vya hao wafanyakazi wageni raia wa India na ripoti ya kuwa ni Watanzania wangapi hao wageni wamewaongezea ujuzi kama sheria za kazi zinavyosema,” alisema Mavunde. Kuhusu malalamiko ya makato ya mishahara yao kutopelekwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii, Mkurugenzi Uendeshaji wa PPF, Asunta Mallya, alisema ofisi yake imekuwa ikiifuatilia kampuni hiyo lakini imekuwa na usumbufu. “PPF imekuwa ikifuatilia sana stahiki za wafanyakazi hawa na mwajiri wao amekuwa akituletea shida na hadi sasa tunamdai zaidi ya shilingi milioni 74 na tumekwisha kumpeleka mahakamani ili kulipa fedha hiyo,” alisema Mallya.

EU na Marekani wamtaka Besigye kuwasilisha mashtaka mahakamani

Ujumbe wa mabalozi wa Umoja wa Ulaya EU pamoja na balozi wa Marekani mjini Kampala wamekutana na kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye nyumbani kwake Kasangat siku ya Ijumaa. Ujumbe huo uloongozwa na balozi wa EU nchini Uganda Bw. Kristian Schmidt, ulizuiliwa kwanza na polisi kuingia nyumbani kwa kiongozi wa chama cha Forum for Democratic Change FDC, hadi kuwasili kwa mkuu wa idara ya kuajiri watu katika polisi Bw. Felix Andrew Kaweesi. Akizungumza baada ya mkutano wao Bw Schmidt amesema lengo la mkutano ni kujadili masuala matatu muhimu. Kuendelewa kushikiliwa kwa Besigye nyumbani kwake na vituo vya polisi, uwezekano wa kuwasilisha mashtaka mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi na utumiaji wa lugha inayoweza kuchochea ghasia. Ujumbe huo wa Mabalozi umetoa wito pia kwa serikali ya Kampala kutomweka mateka Besigye nyumbani kwake na kuheshimiwa haki zake za binadam. Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi uliitaka tume ya uchaguzi ya Uganda kutoa maelezo kamili ya matokeo ya uchaguzi wa rais ulofanyika terehe 18 February. Siku ya Jumanne ujumbe ya ufuatiliaji uchaguzi ya EU ulitembelea ofisi za FDC katika juhudi za kukusanya ushahidi wa kasoro na wizi wa kura wakati wa uchaguzi huo wa rais.

Usitishwaji wa vita waanza kutekelezwa Syria

Kumekuwa na usitishwaji wa mapigano usiku kucha nchini Syria baada ya makubaliano ya kusitisha dhuluma kuanza kutekelezwa. Maeneo ya mbele ya vita katika mji ulio kaskazini wa Allepo yaliripotiwa kutulia mapema asubuhi huku nao mji wa Damascus na vitangoji vyake vikiripotiwa kutulia. Lakini wanaharakati wanasema kuwa na makabiliano ya hapa na pale kati ya serikali na waasi katika mkoa wa pwani wa Latakia Vyombo vya habari vya serikali vilisema kuwa bomu la kutegwa ndani ya gari liliwaua watu wawili katika mkoa wa Hama Usitishwaji huo mkubwa tangu miaka mitano iliyopita haushirikishi wanamgambo wa Islamic State na kundi la Nusra Front lililo na uhusiano na Al Qaeda.

Uchaguzi Iran: Kura zahesabiwa

Kura zinahesabiwa nchini Iran baada ya upigaji kura wa kuchagua bunge jipya na jopo la wataalamu ambalo humteua kiongozi mkuu wa nchi hiyo. Muda wa kupiga kura uliongezwa mara kadha siku ya Ijumaa. Uchaguzi huo ndio wa kwanza tangu Iran itie sahihi makubaliano na nchi zenye uwezo mkubwa duniani kuhusu mpango wake wa nuklia. Waandishi wa habari wanasema kuwa hofu kubwa kwa wapiga kura wengi ni uchumi, ikiwa utainuliwa na makubaliano ya nuklia ambayo yalisababisha kuondolewa kwa vikwazo

Gavana wa New Jersy Chris Christie akimuunga mkono Donald Trump

Katika kile kinachoonekna kama hatua ya kushangaza katika kinyanganyiro cha urais nchini Marekani gavana wa jimbo la New Jersey Chris Christie amemuunga mkono billionea Donald Trump katika uteuzi wa chama cha Republican. Bwana Trump aliitaja hatua hiyo kama aliyokuwa akiihitaji zaidi. Wawili hao walikuwa mahasimu hadi wiki mbili zilizopita wakati bwana Christie alifutilia mbali kampeni yake. Bwana Christie alisema kuwa Trump alikuwa katika nafasi bora ya kumshinda Hillary Clinton ambaye anatafuta nasafi ya kuwania urais kupitia chama cha Democratic. Hio leo Clinton atatafuta uteuzi katika jimbo la South Carolina ambalo bwana Trump alishinda kupitia chama cha Republican.

Wanajeshi wabakaji wafungwa jela Guatemala

Mahakama kuu nchini Guatemala imewahukumua wanajeshi wawili wa zamani kifungo cha mamia ya miaka gerezani kwa kuwabaka na kuwafanya watumwa wanawake wa asili wakati wa mzozo wa miaka ya 80 nchini humo. Kamanda wa zamani wa kambi ya Sepur Zarco na mkuu wa majeshi Heriberto Valdez Asij waliwalazimisha wanawake hao kufanya kazi kwa zamu wakipika na kufanya usafi wakati ambapo pia walibakwa na wanajeshi katika kambi hiyo. Wawili hao walipatikana na hatia ya kuwaua waume wa wanawake hao baada ya kushtumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa mrengo wa kushoto.

Friday, February 26, 2016

Marais wa Afrika watamatisha ziara yao Burundi

Marais wanne pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia, ambao wamekuwa ziarani nchini Burundi kujaribu kuishawishi serikali ya nchi hiyo na upinzani kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao, walimaliza ziara hiyo Ijumaa jioni. Marais wanne pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia, ambao wamekuwa ziarani nchini Burundi kujaribu kuishawishi serikali ya nchi hiyo na upinzani kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao, wamemaliza ziara hiyo leo jioni. Marais wanne pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia, ambao wamekuwa ziarani nchini Burundi kujaribu kuishawishi serikali ya nchi hiyo na upinzani kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao, wamemaliza ziara hiyo leo jioni. Bujumbura- Marais wanne pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia, ambao wamekuwa ziarani nchini Burundi kujaribu kuishawishi serikali ya nchi hiyo na upinzani kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao, walimaliza ziara hiyo Ijumaa jioni. Hata hivyo, viongozi hao hawakutoa taarifa yoyote kuhusu kile walichokubaliana na pande husika. Rais wa afrika ya kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe huo wakati marais hao wakikutana faraghani na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika ikulu yake mjini Bujumbura. Zuma amewaambia waandishi wa habari kuwa wamekubaliana mengi na wadau waliozungumza wakati wa ziara hiyo iliyoanza jana Alhamisi. Hata hivyo hakuyataja waliyoyajadili na amekataa kujibu maswali ya wandishi wa habari akisema kuwa maswali yatajibiwa hapo kesho baada ya kutoa tangazo la yale waliokubaliana. Marais hao ni pamoja na kiongozi wa Mauritania Muhamed Ould abdelaziz, wa Senegal Macks Sall, wa afrika ya kusini Jacob zuma, Rais wa Gabon Ali Bongo pamoja wa waziri mkuu wa Ethipitia Haile Mariam desalein.

Gianni Infantino ndio rais mpya wa Fifa

Gianni Infantino ndiye aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa. katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa. Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich. Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum'baini mshindi wa moja kwa moja. Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili. Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter. Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita . Image copyrightGetty Image caption Infantino akiwahutubia wajumbe Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo. Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ''kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa''.

Together Towards Life: Mission and Evangelism in Changing Landscapes

The Commission on World Mission and Evangelism (CWME) has, since the WCC Porto Alegre Assembly in 2006, been working and contributing toward the construction of a new ecumenical mission affirmation. The new statement will be presented to the WCC 10th assembly at Busan, Korea, in 2013. Since the integration of the International Missionary Council (IMC) and the World Council of Churches (WCC) in New Delhi, 1961, there has been only one official WCC position statement on mission and evangelism which was approved by the central committee in 1982, “Mission and Evangelism: An Ecumenical Affirmation.” This new mission affirmation has been unanimously approved by the WCC Central Committee held in Crete, Greece on 5 September 2012. It is the aim of this ecumenical discernment to seek vision, concepts and directions for a renewed understanding and practice of mission and evangelism in changing landscapes. It seeks a broad appeal, even wider than WCC member churches and affiliated mission bodies, so that we can commit ourselves together to fullness of life for all, led by the God of Life!

Robbins: It's over; Trump is going to be the Republican nominee

The GOP establishment has been wrong at every turn, and Donald Trump has been right, says Mel Robbins The only thing that's shocking about all this is that while Trump is always on the attack, no one has made a direct hit back, she says He still has to amass delegates, but he's leading in the polls, and he's upended Ted Cruz, Jeb Bush and Ben Carson Mel Robbins is a CNN commentator, legal analyst, best-selling author and keynote speaker. In 2014, she was named outstanding news talk-radio host by the Gracie Awards. The opinions expressed in this commentary are solely those of the author He just added Nevada to the growing list of caucus primary wins, and while he needs more delegates to clinch it, who the heck can stop him now? He is leading in national polls and in many state polls; he's succeeded in upending rivals such as Ted Cruz, Jeb Bush and Ben Carson; and there's no one in sight who can stop him. The only question is when will the GOP embrace him? The answer: no time soon. The establishment doesn't like him because it can't control him. Yet he's the only conservative candidate who stands a chance against Hillary Clinton. The polls may reflect Marco Rubio doing well as a conservative uniter, but no one will hammer Clinton's biggest weakness better than Trump, and that's Clinton fatigue. Sorry, Bernie fans, the Democratic nomination is hers to lose. Bush has limped away from the race in a manner that validates almost every insult Trump had flung at him (these are just from the past two weeks):

Idadi ya watu Japan yapungua kwa milioni moja

Takwimu rasmi ya idadi ya watu nchini Japan, imeashiria kuwa idadi ya watu nchini humo ilipungua kwa takriban watu milioni moja katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Hii ni mara ya kwanza kwa idadi ya watu nchini humo kushuka tangu mwaka wa 1920, licha ya kuwa wataalamu walikuwa wamebashiri kutokea kwa hali hiyo miongo kadhaa iliyopita, wakisema kuwa kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na kutokuwepo kwa watu wanaoingia nchini humo kuishi. Tatizo hilo linatarajiwa kuwa mbale zaidi, utafiti uliofanywa na taasisi inayohusika na masuala ya sensa , umebainisha kuwa asilimia arobaini ya raia wa Japan watakuwa na umri wa miaka sitini na tano au zaidi ifikiapo mwaka wa 2050, na hivyo kuzua wasi wasi kuwa gharama ya kuwatunza watu wakongwe nchini humo itapanda zaidi.

Marekani: Besigye anafaa kuachiliwa huru

Besigye amekuwa akizuiwa kutoka nyumbani Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa wito kwa serikali ya Rais Yoweri Museveni kumwachilia huru kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye kutoka kwa kizuizi cha nyumbani. Ubalozi huo umesema kiongozi huyo anafaa kuruhusiwa kutembea bila kuzuiwa. Dkt Besigye amezuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya uchaguzi Alhamisi wiki iliyopita na hukamatwa na polisi kila anapojaribu kuondoka nyumbani na kisha kurejeshwa nyumbani jioni. “Dkt Besigye amekuwa akizuiliwa na polisi tangu uchaguzi wa tarehe 18 Februari, na hajafunguliwa mashtaka yoyote, na alinyimwa haki yake ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi wa tarehe 24 Februari (uchaguzi wa serikali za mitaa,” ubalozi huo umesema kupitia taarifa. Maafisa wa ubalozi huo leo walimtembelea Dkt Besigye nyumbani kwake wakiandamana na maafisa kutoka Umoja wa Ulaya. Waangalizi wa EU wakosoa uchaguzi Uganda Baada ya kuzuiwa kwa muda na maafisa wa usalama, mwishowe waliruhusiwa kukutana na kiongozi huyo. Ubalozi huo wa Marekani pia umetoa wito kwa serikali kuacha kuhangaisha na kuwakamata maafisa wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) chake Dkt Besigye. Aidha, wameeleza wasiwasi wao kutokana na kuchelewa kwa Tume ya Uchaguzi kutoa matokeo kamilifu ya uchaguzi wa urais. “Hili, pamoja na kuzuiliwa kwa Dkt Besigye na kukamatwa kwa mawakala wa chama, kumetatiza uwezo wa raia kutathmini hesabu ya kura na ikiwezekana kupinga matokeo ya uchaguzi kortini katika kipindi kinachohitajika cha ndani ya siku kumi,” ubalozi huo umesema. Dkt Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi sawa na wagombea wengine wawili wa urais, Amama Mbabazi na Abed Bwanika. Mapema leo, mawakili wa Dkt Besigye walisema walikuwa wakitafakari uwezekano wa kupinga matokeo hayo mahakamani.

Uchaguzi wa rais wa Fifa waingia raundi ya pili

Infantino ameongoza raundi ya kwanza Upigaji kura wa kuamua atakayekuwa rais wa shirikisho la soka duniani Fifa umeingia raundi ya pili baada ya kukosekana kwa mshindi wa moja kwa moja raundi ya kwanza. Mshindi alitakiwa kupata theluthi mbili ya kura. Katibu mkuu wa Uefa Gianni Infantino ndiye aliyepata kura nyingi akiwa na kura 88, akiwa na kura tatu zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa. Prince Ali bin al-Hussein alifuata akiwa na kura 27, huku Jerome Champagne akiwa wa mwisho na kula saba. Mfanyabiashara wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya upigaji kura kuanza. Matokeo ya raundi ya kwanzaPrince Ali - 27 Sheikh Salman - 85 Jerome Champagne - 7 Gianni Infantino - 88 Kwenye raundi ya pili, wagombea wote watapigiwa kura na iwapo kuna atakayepata zaidi ya nusu ya kura, atatangazwa mshindi. Akikosekana mtu kama huyo, basi uchaguzi utaingia raundi ya tatu na mgombea aliyepata kura chache zaidi raundi ya kwanza ataondolewa. Wajumbe kutoka mataifa 207 yanayotambuliwa na Fifa duniani wanashiriki uchaguzi huo mjini Zurich kuamua mrithi wa Sepp Blatter. Kabla ya upigaji kura kuanza, mageuzi kadha yalipitishwa, lengo likiwa kufanya Fifa kuwa na uwazi na uwajibikaji zaidi. Kufuatia mabadiliko hayo, mishahara yote ya maafisa wa Fifa inafaa kuwekwa wazi siku za usoni. Kutakuwa pia na kipimo kwenye muhula wa urais. Baraza jipya pia litaundwa kuchukua nafasi ya kamati kuu tendaji, ambalo litakuwa na mwakilishi mwanamke kutoka kila shirikisho.

Daktari mkeketaji apokonywa leseni Misri

Mahakama nchini Misri hatimaye imempokonya leseni daktari aliyepatikana na hatia ya mauaji ya kutokusudia ya msichana wa miaka 13 ambaye alifariki baada ya kufanyiwa ukeketaji. Raslan Fadl alikuwa daktari wa kwanza nchini Misri kuwahi kushtakiwa na ukeketaji,hata baada ya uovu huo kupigwa marufuku 2008. Hukumu yake ya miaka 2 jela ilipongezwa kuwa ushindi mkubwa na wanaharakati wanaokabiliana na ukeketaji. Lakini ripoti za hivi karibuni zilisema kuwa Fadl hakufungwa na kwamba bado alikuwa anaendelea kuhudumu kama daktari. Licha ya marufuku hiyo ,zaidi ya wasichana asilimia 90 na wanawake walio na umri wa kati ya miaka 15 na 59 nchini humo wamekeketwa katika miaka ya hivi karibuni ,kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Singapore archbishop slams Madonna concert as 'pseudo-art'

Singapore's music fans can do better than Madonna, the local Catholic archbishop has said. The American pop star will stop in Singapore on Sunday Feb. 28 as part of her “Rebel Heart” tour – and Archbishop William Goh says the concert is “causing a stir” among Catholics and other Christians. In response, he urged the faithful to reflect on how Christianity offers a contrasting vision of the arts and the world. “As the people of God, we should subscribe to authentic arts that lead us to God through the appreciation of beauty, harmony, goodness, truth and love, respect, unity and the transcendent,” he said Feb. 20. He encouraged Christians and others not to support “the 'pseudo arts' that promote sensuality, rebellion, disrespect, pornography, contamination of the minds of the young, abusive freedom, individualism at the expense of the common good, vulgarity, lies and half-truths.” The music star Madonna is notorious for her exploitation of Christian symbols and iconography, as well as her provocative performances. On her current tour, scantily-clad dancers wear nuns' habits while dancing on cross-shaped stripper poles. Madonna was barred from performing in Singapore in 1993 after local authorities classified her performance as obscene and "objectionable to many on moral and religious grounds." Archbishop Goh encouraged the faithful not to support people whose art denigrates and insults religions, while “including anti-Christian and immoral values promoted by the secular world.” André Ahchak head of communications for the Singapore archdiocese, discussed the archbishop’s stand. “Archbishop William Goh has pointed out that Catholics should know that they must not do, say, support or promote anything contrary to their faith or the gospel in every aspect of moral life, lest they betray Christ their Lord,” Ahchak told CNA Feb. 24. Ahchak said that the Catholic Church urges respect for all religions, respects freedom of speech and does not favor prejudice or discrimination against any artist. He explained that the Church instead favors holistic human development. He pointed to the Church’s role as a patron of the arts. He also said several other Christian groups have welcomed Archbishop Goh’s stand against the Madonna concert. “Many Catholics and non-Catholics have written privately to thank and support (the archbishop) for addressing tenets and issues of faith,” Ahchak said. “To those who disagree with the Church's moral stand, we respect their views since they do not share our faith in Christ and His gospel.” Archbishop Goh’s statement said attendance at Madonna concerts would show a misunderstanding of the faith. “There is no neutrality in faith: one is either for it or against it,” he said. “Being present (at these events) in itself is a counter witness. Obedience to God and His commandments must come before the arts.” The archbishop has made presentations to various ministries and statutory boards of Singapore. He said that given the multi-racial and multi-religious nature of Singapore, “we cannot afford to be overly permissive in favor of artistic expression at the expense of respect for one’s religion, especially in these times of heightened religious sensitivities.” The authorities have assured the archbishop that there are restrictions in place to ensure that content deemed offensive to religious beliefs would not be allowed on stage. Because of the show’s sexual references, the show is restricted to those aged 18 and older. Ahchak said that Archbishop Goh’s preaching and pastoral letters have been consistent in promoting faith formation. In his homily for the 50th anniversary of Singapore independence in 2015, the archbishop emphasized four pillars that have helped Singapore become an advanced country: self-sacrifice; justice and equality; economic development; and moral and spiritual development. That homily pledged the Church’s cooperation with the government “to prevent moral decadence, to strengthen the institution of marriage and to promote justice, peace and harmony.”

Peniel Rajkumar investing in hope, dialogue and bridges between religions

Rev. Dr Peniel Rajkumar, WCC programme executive for Interreligious Dialogue and Cooperation. 25 February 2016 As the World Council of Churches (WCC) programme executive for Interreligious Dialogue and Cooperation, Rev. Dr Peniel Rajkumar describes himself as a bridge between WCC member churches and Eastern Religions, in particular the Hindu and Buddhist religious traditions. “I work for conversation and cooperation between faiths, so that together we can work for the greater common good,” Rajkumar says. “To do this, I focus on the grassroots-level, on youth, activists and religious leaders so that interreligious dialogue can be shaped by a spirit of honesty. I believe this dialogue should be based on hospitality, and that it should become a sign of hope.” “In a way, I see my role as re-inventing dialogue as a dialogue of life, and for life,” Rajkumar adds. YATRA – A unique training initiative An essential part of Rajkumar’s youth-oriented work is YATRA, a training initiative of the WCC aimed to equip young ecumenical leaders to embrace the challenges and opportunities of their multi-religious contexts. Rajkumar explains, “The word YATRA stands for Youth in Asia Training for Religious Amity, and it is a unique training initiative of the WCC. For two weeks, the young leaders engage in inter-religious learning and cross-cultural living. This creates an environment of discovery and discernment for the participants.” He continues, “Through lectures and exposure visits, we discover the richness of other religious traditions, and through personal reflection and group work we learn to see the influence of religious pluralism on our own Christian faith. This, we hope, will give inspiration to engage in ministries of justice and peace from an interfaith perspective.” Why the WCC engages in YATRA “YATRA is WCC's investment in hope,” says Rajkumar. “The combination of young people and inter-religious engagement has an immense potential for overcoming violence today. And by equipping young religious leaders to work alongside other religious communities, YATRA can inspire a movement among our churches, to set sail and catch the wind of the Spirit in working for justice, peace and the greater common good.” The purpose of YATRA “Yatra is part of the WCC's vision of a Pilgrimage of Justice and Peace,” Rajkumar says. “YATRA means pilgrimage in several Indic languages, and the programme is framed in many ways like a pilgrimage, where people come together with open minds ready to learn from the other, open hearts ready to love the other and open hands ready to live and serve alongside the other.” YATRA soon to gather in Jakarta Rajkumar, together with the 30 young ecumenical leaders from Asia, will be going to Jakarta in May this year for the YATRA training. Looking forward to the meeting ahead, Rajkumar says he is excited that the next YATRA programme will be held in Jakarta. He reflects, “As a predominantly Muslim country, but with a vibrant multi-religious presence, Indonesia will be an exciting laboratory for learning. The focus of this year's YATRA is Religion and Public Space, and we hope to learn much about how various religions understand their public role theologically, as well as witness in person how this public role is practiced in the Indonesian context.” “With these theoretical and practical insights we will imagine prophetic ways for churches to engage, alongside other religions, with public issues in our own contexts,” Rajkumar concludes.

Cruz na Rubio wamshambulia Donald Trump

Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz na Marco Rubio wamemshambulia vikali mgombea Donald Trump kwenye mdahalo kabla ya siku muhimu ya uchaguzi wa mchujo wiki ijayo. Maseneta hao walijaribu sana kumkosoa Trump ambaye ameshinda uchaguzi wa mchujo majimbo matatu kati ya manne yaliyoandaa uchaguzi kufikia sasa. Mjadala uliangazia sana uhamiaji, huduma ya afya na wagombea wa asili ya Amerika Kusini. Lakini, sawa na midahalo ya awali, wagombea walianza upesi kushambuliana. Kwa zaidi ya saa mbili, Rubio na Cruz walimshambulia Trumo kuhusu biashara wakimtaka kuwa mtu asiye wa kuaminika. Walishutumu pia sifa zake kama mhafidhina na pia kukosa kwake kutoa maelezo ya kina kuhusu sera zake. Aidha, walisema amezoea kutamba kwa kutumia vitisho. "Kama hangerithi $200m, unajua Donald Trump angekuwa wapi? Angekuwa akiuza saa Manhattan," alisema Bw Rubio wakati mmoja. Bw Rubio pia alikosoa Trump kutokana na mpango wake wa kutoa elimu mtandaoni kupitia Chuo Kikuu cha Trump ambao ulifeli. Kadhalika, alimshutumu kwamba amekuwa akiwaajiri wageni kufanya kazi katika miradi yake ya ujenzi badala ya Wamarekani. Bw Trump alimjibu: "Mimi nimewaajiri maelfu ya watu. Wewe hujawahi kuajiri mtu hata mmoja.” Licha ya shutuma hizo, Bw Trump alionekana kutoyumbishwa. Bw Trump ameendelea kujiongezea umaarufu licha yake kutoa matamshi yenye utata hasa kuhusu kuzuiwa kwa Wamarekani kuzuru Marekani na kujengwa kwa ua kuzuia wahamiaji kutoka Mexico. Jumanne wiki ijayo, ijulikanayo kama Jumanne Kuu, mamilioni ya wapiga kura katika majimbo 11 watapiga kura za mchujo. Robo ya wajumbe wanaohitajika kujipatia tiketi ya chama cha Republican wanapatikana majimbo hayo. Bw Trump kwa sasa anaongoza majimbo 10 kati ya 11 yatakayoshiriki mchujo huo Jumanne. Kwa sasa ana wajumbe 82, Cruz ana 17 naye Rubio ana 16. Ili kushinda tiketi ya chama cha Republican, mgombea anahitaji wajumbe 1,237 kitaifa. Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton na Bernie Sanders watashindania wajumbe 1,004 Jumanne Kuu. Kwa sasa, Clinton ana wajumbe 505 naye Sanders 71. Wagombe awatakaoteuliwa hutangazwa rasmi na vyama wakati wa mikutano mikuu Julai, miezi minne kabla ya uchaguzi Novemba.

Kiongozi mpya wa Fifa kuchaguliwa

Shirikisho la soka duniani Fifa litampta kiongozi mpya leo wajumbe 207 watakapokusanyika mjini Zurich, Uswizi kumchagua mrithi wa Sepp Blatter. Blatter, 79, aliongoza shirikisho hilo tangu 1998. Aling’atuka mwaka jana kutokana na tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo. Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi. Watano hao ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne. Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda. Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki). Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe. Hauhitaji Media PlayerPata usaidizi kuhusu Media PlayerBonyeza 'Enter' kuendelea au kurejea mwanzoni Kuna mataifa 209 wanachama wa FIFA lakini Kuwait na Indonesia kwa sasa hawashirikishwi, hivyo wajumbe watakaopiga kura ni 207. Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa. Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na anayepata kura nyingi kutangazwa mshindi. Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi raundi ya pili. Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.

Shambulio la risasi laua kadhaa Marekani

Watu kadhaa wameuawa na wengine thelathini kujeruhiwa katika kwa risasi magharibi mwa jimbo la Kansas nchini Marekani. Maafisa wa polisi wamesema mwanaume aliyepiga risasi hizo ameuwawa baada ya shambulio lililotokea katika mji wa Hesston. Mkuu wa polisi wa kituo cha eneo hilo T.Walton amesema polisi wanafuatilia uhalifu uliotokea na kuna uwezekana kuwa na majeruhi zaidi. "hili ni tukio la kutisha na baya lililowahi kutokea katika mji wa wilaya Harvey na Hesston Newton.Limesambaa nje na tafadhali mtuvumilie wakati tunaendelea kulitatua tatizo hilo.Mnapaswa kuwa makini,tunaenda kujaribu kupata taarifa zote kwa hali na mali,kuna wengi ambao watakutana na majonzi kabla ya haya yote kuisha" alisema mkuu huyo wa Polisi shuhuda mmoja ameeleza alichokiona na kukisikia.. ''yote ambayo ninayajua ni kwamba niliona watu wakikimbia na nikadhani walikuwa wanakimbia moto,hivyo nikasogea hatua chache na kusikia milio ya risasi na watu zaidi wakikimbia na milio hiyo ilizidi na mimi pia nikaanza kukimbia''

Obama kumaliza uhasama Syria?

Raisi Obama amepanga kuchukua hatua ya kumaliza uhasama unaondelea nchini Syria kwa kuwapa onyo vyama vyote vinavyohusika na mgogoro ambao unaangaliwa na dunia na kama wataweza kutimiza ahadi zao. Taarifa zilizokuja usiku wa kuamkia Leo,zinasema raisi Obama amechukua hatua madhubuti ili kumaliza mgogoro huo.Amesema mgogoro ambao upo kati ya waasi pamoja na kampeni baina ya kikundi cha kigaidi cha wanamgambo wa kiislamu wa IS una maana kuwa mwisho mwa mgogoro huo hautaweza kuisha kwa haraka. Lakini raisi huyo amesisitiza pia kuwa hiyo ni fursa ya kuweza kuwa na maongezi ya amani. Wanaharakati wanasema waasi wanakumbana na mashambulizi makali ya anga kaskazini mwa jimbo la Latakia na kwa waasi waliopo karibu na Damascus.

Thursday, February 25, 2016

Kamishna mpya wa haki za binadamu Baerbel Kofler

Mbunge wa chama Social Demokratik Bärbel Kofler ameteuliwa kuwa Kamishna mpya wa haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani.Bibi Kofler anachukua nafasi ya Christoph Strässner aliejiuzulu jumatatu iliyopita Kamishna mpya wa haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani Baebel Kofler Kamishna mpya wa haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani Baebel Kofler Baraza za mawaziri la Ujerumani lilimteua mbunge huyo kutoka jimbo la Bavaria kuushika wadhifa huo kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Berlin. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 48 ni mwanachama wa chama cha Social Demokratik kilichomo katika serikali ya mseto. Kamishna huyo mpya wa haki za binadami ni mjumbe wa kamati ya Bunge inayoshughukilia ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo na pia yumo katika kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya nchi za nje. Kamishna wa hapo awali Christoph Strässer aliejiuzulu alisema katika mahojiano kwamba aliuchukua uamuzi huo baada ya sheria za kuomba hifadhi ya ukimbizi kufanywa ngumu zaidi nchini Ujerumani. Kamishna mpya ,Bärbel Kofler amesema kutimiza wajibu wa kibinadamu ndiyo msingi wa kila kitu. Anakusudia kuchukua hatua ili Ujerumani ionyeshe wajihi wa kibinadamu katika kushuhgulikia dhiki za wakimbizi duniani. Mwanasiasa huyo anachukua wadhifa huo katika kipindi kigumu kutokana na mgogoro mkubwa wa wakimbizi. Ujerumani imeshawapokea wakimbizi zaidi ya Milioni moja mnamo kipindi kifupi. Mgogoro huo pia umesababisha magawanyiko miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya. Nchini Ujerumani upinzani dhidi ya wakimbizi unaongezeka.Japo idadi ya wanaowapinga wakimbizi ni ndogo,wasi wasi unaongezeka juu ya upinzani huo. Baadhi ya nyumba za kuwahifadhia wakimbizi zimeshambuliwa. Bärbel Kofler aliingia katika Bunge la Ujerumani mnamo mwaka wa 2004. Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa mwenyewe, yeye pia ni mjumbe wa jumuiya ya wafanyakazi ya IG Metall. Amesema anatambua kwamba jukumu analochukua ni kubwa Ameeleza kuwa Ni jukumu linalohitaji uwajibikaji mkubwa .Majukumu yameongezeka katika miaka iliyopita hivi karibuni. Majukumu na maswali yataongezeka juu misaada ya kibinadamu." Kamishna huyo mpya wa masuala ya haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani bibi Bärbel Kofler amesema siyo Syria na nchi jirani zinazokabiliwa na changamoto kubwa. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amemsifu Kamishna huyo mpya kuwa mtu mwenye uwezo wa kuzikabili changamoto. Kofler alizaliwa katika mji wa Fresilassing,katika jimbo la Bavaria, na alifanya kazi Benki baada ya kumaliza masomo.Mnamo mwaka wa 1987 alifanya masomo tekinolojia ya habari na mawasiliano kwa njia ya mtandao Pia alifanya masomo ya lugha za kirusi na kihispaniola kwenye Chuo kikuu cha Salzburg. Mnamo mwaka wa 1999 alienda kuwa mhadhiri kwenye chuo kikuu cha ufundi mjini Moscow. Chanzo: DW SWAHILI

Gesi zaidi yagunduliwa pwani ya Tanzania

Waziri wa madini na nishati wa Tanzania Sospeter Muhongo akihutubia wanahabari awali Tanzania imegundua takribani futi za ujazo trillioni 2.17 za Gesi katika eneo la Ruvu lililoko katika Mkoa wa Pwani kilomita chache kutoka mji mkuu wa biashara-Dar es Salaam. Huu ni ugunduzi mkubwa zaidi wa gesi pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa Badra Masoud, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania, ugunduzi huu wa gesi una thamani ya takribani shilingi za Tanzania trillioni 12 sawa na takribani dola za Kimarekani bilioni 6. Tanzania bado inaamini huenda kuna gesi zaidi itagundulika kwa kuwa utafiti zaidi bado unaendelea. Msemaji huyo wa Wizara ya Nishati amesema kuwa utafiti kuhusu Gesi hii umedumu kwa takribani miaka hamsini ukihusisha makampuni mbalimbali. Aidha Bw Masoud amesema uvunaji wa gesi hii utaanza muda wowote mara tu baada ya kukamilika kwa miundombinu ambapo gesi nyingine itauzwa nje na nyingine itaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wanahabari awali alidokeza kuwa baadhi ya wakazi wa mji wa biashara wa Dar es Salaam tayari wameshaanza kunufaika moja kwa moja na gesi ambayo iligunduliwa katika maeneo mengine ya katikati ya bahari huko Mnazi Bay na Songo songo mkoani Mtwara na Lindi ambapo gharama ya matumizi ya nyumbani haivuki dola kumi za Kimarekani kwa mwezi. Kwa mujibu wa Waziri Muhongo, Tanzania imetenga takribani dola milioni 6 za kimarekani za kufanyia tathmini na kuwalipa watu watakaokutwa katika eneo ambalo kutajengwa mtambo mkubwa wa gesi mkoani Lindi. Mradi ambao utakuwa wa tatu kwa ukubwa katika historia ya Tanzania baada ya ule wa Reli inayoiunganisha Tanzania na Zambia, TAZARA, na bomba lililojengwa kusafirisha gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.

Kenyatta: Wakenya 'wanajua kuiba'

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa shutuma kali dhidi ya raia wake kuhusu jinamizi la ufisadi akiwa kwenye ziara rasmi ng'ambo. Akihutububia kundi la Wakenya wanaoishi nchini Israel, Rais Kenyatta alisema ni jambo la kusikitisha kwamba taifa la Kenya linasifika kwa mambo mabaya ikiwa pamoja na ufisadi uliokithiri, ukabila wa hali ya juu na matusi yanayoendelezwa hasa na wanasiasa. Rais Kenyatta yumo katika ziara rasmi nchini humo. “Sisi kama Wakenya pia, Mungu ametupatia nchi ambayo ni nzuri mara 20 kuliko hii tuko hapa (Israel). Lakini tukitembea ni kulia, ni kuiba ...,” alisema. “… tuko na ujuzi pia, ya kuiba, ya kutukanana, ya kufanya mambo mengine maovu, ya kuleta ukabila. Bw Kenyatta alisema licha ya Kenya kuwa taifa lenye utajiri mkubwa, kasumba ya ufisadi miongoni mwa viongozi na raia imelemaza ustawi wa taifa hilo. Je, Kenya ni taifa la wanyang’anyi? Kukiri kwa Rais Kenyatta akiwa ziarani Israel kwamba ufisadi umemea mizizi katika taifa lenye uchumi bora zaidi kanda ya Afrika Mashariki, kunajiri huku jinamizi hilo likiendelea kugonga vichwa vya habari, na kutawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya. Kashfa ya mamilioni ya pesa kuporwa kutoka mfuko wa huduma ya vijana wa taifa (NYS) na vigogo serikalini, ndiyo sakata ya ufisadi ya hivi karibuni inayokumba utawala wa Rais Kenyatta. Mwaka jana, Kenyatta aliwapiga kalamu mawaziri watano na maafisa wengine wakuu serikalini kutokana na madai ya ulaji rushwa. Majuzi Jaji Mkuu Dkt Willy Mutunga alizua mjadala mkali mitandao ya kijamii baada yake kunukuliwa na gazeti la Uholanzi akisema kwamba Kenya ni taifa la “wanyang’anyi”. Dkt Mutunga alinukuliwa akisema kwamba wananchi wanapigana vita na magenge ya watu sawa na ‘mafia’ ambayo yanaongozwa na viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wafisadi.

Zuma awasili Burundi kwa mazungumzo

Rais Zuma na Rais Nkurunziza wakikagua gwaride uwanja wa ndege Bujumbura Viongozi watano wa nchi za Afrika, wakiongozwa na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, wamewasili Burundi kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini humo. Ujumbe huo unaoongozwa unajumuisha marais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, Senegal Macky Sall na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn. Ziara yao inajiri siku chache tu baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuzuru taifa hilo na kumhimiza Rais Pierre Nkurunziza akubali mazungumzo. Umoja wa Afrika umekuwa ukiishinikiza Burundi kukubali kushiriki mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kumaliza machafuko yaliyoanza Aprili mwaka jana. Machafuko hayo yalitokana na hatua ya Rais Pierre Nkurunziza ya kutangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu. Aliwania baadaye na kushinda. Hali ilizidishwa na jaribio la mapinduzi ya serikali mwezi Mei ambalo lilifeli. Watu zaidi ya 400 wamefariki na maelfu wengine kutoroka makwao tangu Aprili mwaka jana. Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema uwanja mkuu wa ndege wan chi hiyo leo umekuwa na shughuli nyingi. Viongozi hao watano wamewasili wakitumia ndege zao za kibinafsi. Bw Zuma, kabla ya kuwasili, alituma ndege mbili za kijeshi za kubeba mizigo ambazo zilikuwa na magari ya kijeshi ya kutumiwa na maafisa wa kulinda usalama wake. Viongozi hao, waliolakiwa na mwenyeji wao Rais Nkurunziza, hawakuhutubu baada ya kuwasili. Viongozi hao wanatarajiwa kuishinikiza serikali ya Rais Nkurunziza kukubali mazungumzo yatakayoshirikisha pande zote kwenye mzozo huo. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Burundi Alain Aime Nyamitwe amesema serikali hiyo inakubali mazungumzo japo kwa masharti.

Upinzani nchini Uganda wasisitiza kupinga matokeo

Sheria ya uchaguzi ya Uganda inatoa siku 10 za kuasilisha malalamishi kuanzia siku ya kutangazwa matokeo. Chama kiku cha upinzani nchini Uganda kimesema kinafanya kila kiwezalo kutafuta ushahidi utakaopelekea kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Februari 18. Sheria ya uchaguzi ya Uganda inatoa siku 10 za kuasilisha malalamishi kuanzia siku ya kutangazwa matokeo. Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FDC Mugisha Muntu amesema chama chake kinafanya kila juhudi ili kuwasilisha ushahidi kabla ya wakati uliowekwa kumalizika. Hata hivyo ameongeza kuwa kumekuwa na dhuluma na ukandamizaji kutoka kwenye vyombo vya usalama vya serikali ikiwemo idara ya polisi. Muntu ameyasema haya kufuatia kukamatwa mara kadhaa kwa Dkt Kizza Besigye aliekuwa mgombea urais wa chama cha FDC. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Badru Kiggundu alimtangaza rais Yoweri Museveni kuwa mshindi kwa kujipatia asilimia 60.07 ya kura zilizopigwa huku Besigye akifuatia kwa asilimia 35.37 za kura.

Austria yatetea uamuzi wa kuandaa mkutano bila Ugiriki

Austria imetetea uamuzi wake wa kuandaa mkutano wa kilele na Mataifa ya Balkan, utakaojadili mikakati ya kupunguza wimbi la wakimbizi bila ya kuialika Ugiriki. Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria, Sebastin Kurz amesema viongozi kutoka mataifa tisa ya Balkan watahudhuria mkutano huo wa kilele ingawa Ugiriki haijaalikwa kwa sababu nchi hiyo haina nia ya kupunguza wimbi la wakimbizi na badala yake inataka kuendelea kuwaachia waingie kupitia Macedonia, ambako wanapata njia kuelekea ukanda wa kaskazini. Mkutano huo uliopewa jina ''Kudhibiti Uhamiaji kwa Pamoja'' utawahusisha mawaziri wa mambo ya nje na wale wa mambo ya ndani kutoka Albania, Bosnia, Bulgaria, Croatia, Kosovo, Macedonia, Montenegro, Serbia na Slovenia. Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Karl-Heinz Grundboeck amesema mikutano kama hiyo huwa inafanyika kwa kuzingania mfumo na washiriki wa kudumu. Mawaziri hao watajadiliana masuala kadhaa kama vile uangalizi na udhibiti wa mikapa na jinsi ya kukabiliana na magenge yanayofanya biashara ya kuwasafirisha binadamu kimagendo, pamoja na kuimarisha utoaji wa taarifa kuhusu sera za nchi zao. Mkutano huo wa Vienna pia utajaribu kuwa na msimamo wa pamoja kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika siku ya Alhamisi. Hata hivyo, uamuzi huo wa Austria umeikasirisha Ugiriki ambayo imetoa lalamiko la kidiplomasia dhidi ya mkutano huo iliyouita usio wa kirafiki. Wizara ya mambo ya nje ya Ugiriki imesema kutengwa kwake kunamaanisha mkutano huo wa kilele ni jaribio la kuchukua maamuzi bila ya nchi hiyo kuwepo, ambayo moja kwa moja inaiathiri nchi hiyo pamoja na mipaka yake. Ugiriki imeilalamikia hatua ya Austria, ikisema kuwa mkutano huo ni sawa na usiokuwa wa kirafiki na unaopingana na sera za Ulaya.Sera ya hivi karibuni ya Macedonia ya kukataa kuingia kwa raia wa Afghanistan, ambao ni moja ya makundi makubwa ya wahamiaji, tayari imesababisha mrundikano mkubwa kwenye mpaka wa Ugiriki. Maafisa wa Ugiriki wameukosoa mkutano huo wakisema unadhoofisha juhudi za kuwa na uamuzi wa pamoja wa Umoja wa Ulaya kwa kuzingatia suala la mzozo wa wakimbizi. Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras amemwambia waziri mkuu mwenzake wa Uholanzi, Mark Rutte, kwamba maamuzi kuhusu wimbi la wakimbizi lazima liangaliwe kwa pamoja bila ya nchi yoyote kutengwa. Halmashauri ya Umoja wa Ulaya pia imekosoa hatua za hivi karibuni za kuwazuia wakimizi katika njia ya Balkan, ikisema kuwa ni kinyume cha sheria. Ama kwa upande mwingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria, Sebastin Kurz, ameikosoa sera ya Ujerumani kuhusu wakimbizi, akisema inakanganya. Amesema mwaka uliopita, Austria ilikubali mara mbili zaidi ya maombi ya watu wanaoomba hifadhi kama ilivyokuwa kwa Ujerumani na kusisitiza kuwa hilo halitotokea kwa mara ya pili. Kurz pia amezungumzia ukosoaji uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere kuhusu sera ya Austria ya kuweka kiwango maalum cha wakimbizi 80 wanaoomba hifadhi kuingia nchini humo kwa siki, huku ikiwaachia wengine 3,200 kwenda nchi nyingine, ingawa wengi wao huelekea Ujerumani. Waziri huyo amesisitiza kuwa Austria inataka kushirikiana na Ujerumani, hivyo wanatarajia kwamba Ujerumani itasema kama imeajiandaa au haijajiandaa kuwapoka wakimbizi, au kama haiko tena tayari kuwapokea. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Austria, Johanna Mikl-Leitner amesema ana matumaini kwamba watapata jibu pa pamoja na Umoja wa Ulaya na kwamba inabidi kwa sasa wapunguze wimbi la wakimbizi.

Ban Ki-moon kufanya mazungumzo Sudan Kusini

Katibu mkuu wa Umoja wa Afrika, Ban Ki-moon, anatazamiwa kufanya mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, ili kuongeza nguvu muafaka wa amani utakaositisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka miwili nchini humo. Msemaji wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini anasema kuwa visa vya uchomaji nyumba na wizi wa mabavu vinaendelea katika mji wa Malakal, kufuatia mapigano ya juma lililopita yaliyosababisha vifo vya watu 18. Serikali sasa imekubali kutumwa kwa majeshi yanayomtii naibu Rais Riek Machar kupiga doria katika mji mkuu Juba, juma lijalo. Ni mara ya kwanza kwa majeshi hayo kurejea katika mji huo, tangu mapigano yaanze miaka miwili iliyopita.

Ugiriki yatishia EU kuhusu wahamiaji

Ugiriki imetishia kupinga maamuzi yote katika mkutano ujano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu uhamiaji iwapo nchi wanachama hazitakubaliana kugawana kwa uwiano wahamiaji na wakimbizi. Hatua hiyo imekuja wakati Austria na baadhi nchi za Balkani kutoa wito kupunguzwa kwa wahamiaji wanaovuka mipaka ya nchi zao. Akihutubia bunge mjini Athens Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema haikubaliki kwamba nchi yake iachiwe kukabiliana na tattizo hilo pekee yake. "tunachokataa kufanya ni kukubali mabadiliko katika nchi yetu kuwa ghala kubwa la nafsi za watu , na wakati huo huo tuendelee kuchukua hatua ndani ya Umoja wa Ulaya na katika mikutano ya viongozi wa Umoja huo kana kwamba hakuna jambo lolote baya. Kuanzia sasa na kuendelea Ugiriki haitakubalina na makubaliano kama hatutahakikishiwa mgawanyo wa uwiano wa mzigo na wajibu wa makazi ya wakimbizi miongoni wa nchi wanachama." Wakati huo huo mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya zinakutana mjini Brussels asubuhi hii kuzunguzia suala la tatizo la wakimbizi huku onyo likitolewa kama tatizo hilo litaendelea itakuwa vigumu kulishughulikia. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kufanya mikutano miwili kuhusu suala la wahamiaji mwezi ujao ili kujaribu kuwa na sera kabla wimbi jingine la wahamiaji.

Beijing yaipita New York kwa mabilionea

Jiji la Beijing limelipita jiji la New York katika kuwa na idadi kubwa ya mabilionea, ripoti mpya ya shirika la Hurun kutoka Uchina inasema. Mabilionea 100 kwa sasa wanaishi katika jiji hilo kuu la Uchina, wakilinganishwa na mabilionea 95 wanaoishi New York, ripoti hiyo inasema. Jiji la Shanghai, kitovu cha kiuchumi nchini Uchina, limo nambari tano. Hurun, shirika ambalo hufuatilia utajiri na huduma za kifahari nchini Uchina, limekuwa likitoa orodha ya matajiri wa kupindukia duniani kwa miaka mitano iliyopita, wakihesabu mabilionea kwa dola za Kimarekani. Wang Jianlin ndiye mtu tajiri zaidi Uchina, kwa mujibu wa Burun Waligundua kwamba Beijing imepata mabilionea 32 wapya tangu mwaka jana, na kuiwezesha kupita New York ambayo ilipokea mabilionea wanne wapya pekee. Kwa ujumla, Uchina pia imeipita Marekani kwa kuwa na mabilionea wengi zaidi duniani. Hata hivyo Wamarekani bado wanatawala katika orodha ya mabilionea 10 wakuu zaidi katika orodha hiyo ya Hurun. Uchina ina mabilionea 568 baada ya kuongeza mabilionea 90 nayo Marekani ina mabilionea 535. Uchina sasa ina mabilionea wengi kuliko Marekani Mabilionea wa Uchina kwa pamoja wana utajiri wa $1.4 trilioni (£1.01 trilioni), ambao ni sawa na mapato ya jumla ya Australia. Mtu tajiri zaidi Uchina bado ni Wang Jianlin, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa $26bn (£18.8bn). Mmarekani tajiri zaidi ni Bill Gates aliye na $80bn, akifuatwa na Warren Buffett mwenye utajiri wa $68bn. Nambari tatu inakaliwa na tajiri wa mavazi kutoka Uhispania Amancio Ortega aliye na utajiri wa $64bn. Ripoti hiyo ya Hurun inasema kwa sasa kuna mabilionea 2,188 duniani, ambayo ni rekodi mpya.

Zuma kuelekea Burundi kwa mazungumzo ya amani

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anatarajiwa kuelekea nchini Burundi siku ya Alhamisi kwa mazungumzo yanayolenga kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo. Bwana Zuma na viongozi wengine wa muungano wa Afrika wanaitaka serikali ya Burundi kuanzisha majadiliano na viongozi wa upinzani na kukubali kupelekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani nchini humo. Serikali tayari imesema kuwa haitazungumza na baaadhi ya maafisa wa upinzani ambao anaaamini hawako tayari kurudisha amani nchini humo. Mgogoro huo ulianza baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa urais. Ghasia zilizozuka zilifichua mgawanyiko wa kikabila uliokuwepo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2000 uliowaacha watu 300,000 wakiwa wamefariki.

Wednesday, February 24, 2016

Muhubiri TB Joshua mashakani tena

Watu zaidi ya 100, wengi wao kutoka Afrika kusini walikufa wakati jengo la kanisa la Muhubiri TB Joshua lilipoporomoka, Watoto wawili wa Afrika kusini wanamshitaki muhubiri wa kanisa kubwa na maarufu nchinini Nigeria TB Joshua kwa kifo cha baba yao, wakili wao Bolajii Ayorinde ameiambia BBC. Wato hao mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na mwingine wa miaka sita wamewasilisha nyaraka za mashtaka katika mahakama ya mji mkuu wa Nigeria, Lagos, wakidai fidia ya zaidi ya dola $521,000; kutoka kanisa la Synagogue Church of All Nations, vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti. Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekuwa wakisisitiza kwamba hawana kosa lolote Baba yao alikua miongoni mwa watu 116 waliokufa wakati jengo la makazi yanayomilikiwa na kanisa hilo lilipoporomoka mjini Lagos mwaka 2014. Mwaka jana mahakama ya uchunguzi wa vifo iliamuru TB Joshua anapaswa kushtakiwa juu ya kuporomoka kwa jengo, akisema kanisa hilo linahusika kwasababu ya uzembe wa kiuhalifu. Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekua wakikana kufanya kosa lolote.

Blaise Compaore sasa ni raia wa Ivory Coast

Rais wa zamani wa Burkinafaso Blaise Compaore sasa ni raia wa Ivory Coast Rais alieondolewa madarakani nchini Burkina Faso Blaise Compaore amepewa uraia wa Ivory coast , na hivyo kuondolewa kwa matarajio ya kurejeshwa nyumbani kukabiliana na mashtaka ya mauaji dhidi yake . Agizo la kumpatia uraia lilitolewa na rais Alassane Ouattara mnamo mwezi wa Novemba 2014, lakini amri hiyo imefahamika sasa. Blaise Compaore amekua uhamishoni Ivory coast tangu alipopinduliwa na jeshi mwaka 2014 Bwana Compaore anatafutwa kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya kiongozi maarufu wa wa zamani wa Thomas Sankara mwaka 1987. Utawala wake wa miaka 27 ulimalizika mwezi Octoba -2014 baada ya wimbi la maandamano ya upinzani. Thomas SankaraImage copyright Blaise Compaore anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kiongozi wa zamani Thomas Sankara pichani Bwana Compaore, ambae mkewe ni raia wa Ivory Coast, amekua uhamishoni nchini Ivory Coast tanga alipopinduliwa mwezi Octoba 2014. Kibali cha kumkamata kilitolewa mwezi Desemba. Bwana Sankara, aliekua na itikadi za mrengo wa kushoto alionekana kama "Che Guevara wa Afrika ", anaangaliwa na waafrika wengi kama shujaana alirithiwa na Bwana Compaore,ambae alikua naibu wake. Mazingira ya kifo chake yamebakia kuwa si ya kufahamika.

Obama nominates Adventist Senate Chaplain Barry Black to Supreme Court

WASHINGTON, D.C. — President Barack Obama has nominated Rear Admiral Barry Black, U.S. Senate Chaplain, to the US Supreme Court. If confimed by the Senate, Black would replace recently deceased Justice Antonin Scalia and would be the first Seventh-day Adventist to serve as a US Supreme Court Justice. Black who has served for over a decade in his current role as Chaplain of the US Senate enjoys widespread popularity among lawmakers and is expected to receive bipartisan support as a nominee for Supreme Court Justice. “Having an Adventist as a Supreme Court justice could come in really handy,” said General Conference Religious Liberty spokesperson Walt Densie with a dreamy look in his eyes. “Not only could future Judge Barry Black guard against the persecution of religious minorities but he could set the record straight on everything from the Adventists’ origins of haystacks and cornflakes to finally mandating that Ellen White’s head be carved into Mount Rushmore.”

Wanafunzi waliochochea wenzao wajisalimisha India

Wanafunzi wawili wa kihindi waliodaiwa kuwachochea wanafunzi wa chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru kuandamana huko Delhi wamejisalimisha kwa polisi wenyewe. Umar Khalid na Anirban Bhattacharya ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitafutwa na polisi. Kukamatwa kwa kiongozi wa muungano wa wanafunzi wa chuo hicho Kanhaiya Kumar, mapema mwezi huu ndiko kulikosababisha ghasia katika sehemu nyingi nchini India. Baada ya Bwana Kumar kukamatwa, wanafunzi wengine ambao wametajwa kuhusiana na maandamano hayo walitoweka lakini wakajitokeza katika chuo kikuuu cha JNU siku ya Jumapili usiku. Polisi hawakuingia katika chuo hicho lakini jumanne usiku Umar Khalid na Anirban Bhattacharya waliondoka katika chuo hicho kwa hiari na kujisalimisha kwa polisi. Polisi hawaruhusiwi kuingia vyuoni bila idhini ya viongozi wa chuo,ripoti zimesema. Polisi wamewata wanafunzi waliosalia - Ashutosh Kumar,Anant Prakash Narayan, Riyazul Haq na Rama Naga -kujisalimisha.

Donald Trump ashinda Nevada

Mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda katika jimbo la Nevada nchini Marekani, na hivyobasi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho. Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu ,kufuatia ushindi wake katika jimbo la New Hampshire na Carolina kusini. Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili. Maafisa wa chama hicho wamesema wamekuwa wakichunguza ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura. Baadhi ya watu waliojitolea pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za bwana Trump,lakini maafisa wamesema kuwa hatua hiyo sio kinyume na sheria. Chanzo:BBC SWAHILI

Tuesday, February 23, 2016

Cameron aonya kujiondoa Umoja wa Ulaya

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ameonya kwamba kura ya maoni juu ya kubakia nchi yake katika Umoja wa Ulaya au la, inaweza kuhatarisha uchumi na usalama wa taifa hilo. Akilihutubia bunge jana, Cameron alimshambulia Meya wa jiji la London, Boris Johnson hasimu wake wa muda mrefu ambaye ametamka hadharani kwamba anaunga mkono Uingereza ijiondoe kwenye Umoja wa Ulaya, akimtuhumu kuchukua msimamo huo kwa maslahi ya kisiasa. Meya Johnson alimtaka Cameron aelezee kwa undani namna makubaliano yaliyofikiwa Brussels, Ubelgiji wiki iliyopita yatakavyoyaleta mamlaka katika sehemu yoyote ya utungaji wa sheria kwenye bunge la Uingereza. Hata hivyo Cameron ambaye ni kiongozi wa chama cha kihafidhina, alijibu akisema yataipa serikali mamlaka makubwa zaidi juu ya mafao, uhamiaji na uwezekano wa kuondoka kutoka kwenye umoja wa karibu kabisa. ''Kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya huenda ikatufanya kwa muda kujiona tuko huru, lakini je itatupa kweli mamlaka zaidi, ushawishi na uwezo mkubwa wa kuweza kutekeleza mambo yetu? Lakini tukiondoka kwenye Umoja wa Ulaya, je tutakuwa na mamlaka ya kuzuia biashara zetu kutobaguliwa? Hapana,'' alisema Cameron. Amewaambia wabunge kura ya maoni itakuwa ''uamuzi wa mwisho'' na amewahakikishia wapiga kura kwamba hali ya baadaye ya nchi hiyo itakuwa bora zaidi, ikiendelea kubakia mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Baadhi ya wachambuzi wanaamini iwapo Uingereza itajiondoa katika Umoja wa Ulaya, Johnson anaweza akawa Waziri Mkuu. Matokeo ya hivi karibuni ya utafiti wa maoni ya wapiga kura yameonyesha wingi mdogo ya wapiga kura wanaotaka kubakia kwenye umoja huo, lakini idadi kubwa bado hawajaamua kuhusu kura hiyo ya maoni iliyopangwa kufanyika Juni 23, mwaka huu. Wakati huo huo, viongozi wa zaidi ya theluthi tatu ya makampuni makubwa nchini Uingereza wameonya kuwa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya kunaweza kuuweka hatarini uchumi wa nchi hiyo na kutishia ajira. Kwenye barua yao ya pamoja iliyochapishwa katika gazeti la leo la Times, kiasi ya viongozi 198, akiwemo Roger Carr, mwenyekiti wa BAE Systems, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mafuta ya BP, Bob Dudley na Ron Dennis, mkuu wa McLaren, wameelezea kuuunga mkono mpango wa Cameron, kuhusu mageuzi katika Umoja wa Ulaya. Wamesema Cameron ametekeleza ahadi zake za kuimarisha ushindani ndani ya Umoja wa Ulaya na wanaamini kwamba kujiondoa katika umoja huo, kutakwamisha uwekezaji, kuhatarisha ajira na kuuweka uchumi katika hatari. Hapo jana, Paundi ya Uingereza ilishuka thamani dhidi ya Dola ya Marekani kutokana na hofu ya matokeo ya kura ya maoni.

Ban Ki Moon: Nkurunziza amekubali kufanya mazungumzo na upinzani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amekubali kufanya mazungumzo na upande wa upinzani kuumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo. Ban ambaye anafanya ziara yake ya kwanza Burundi tangu mzozo kuzuka nchini humo mnamo mwezi Aprili mwaka jana, aliwasili jana alasiri na leo amefanya mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza mjini Bujumbura. Mkutano huo unakuja baada ya Katibu huyo wa Umoja wa Mataifa kukutana na viongozi wa vyama vya kisiasa na wa asasi za kiraia katika juhudi za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Burundi ambao umedumu kwa miezi kumi. Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema ziara ya Ban ni muhumu sana kwani wanatumai atamshinikiza Rais Nkurunziza hatimaye kukubali kufanya mazungumzo ya kina na yasiyo na masharti na wapinzani wake. Ban Kuzuru Congo na Sudan Kusini Baada ya mazungumzo hayo na Rais Nkurunziza, Ban ataizuru Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na pia Sudan Kusini ambako kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi Desemba mwaka 2013. Ban anatarajiwa kuzifufua juhudi zinazodhamiria kupatikana kwa suluhisho la amani kwa mzozo wa kisiasa wa Burundi ambao ulichochewa na azma ya Nkurunziza kugombea muhula wa ttau madarakani kinyume na sheria. Serikali ya Burundi inaonekana kulegeza msimamo wake dhidi ya wapinzani wake kwa kukubali ujumbe wa viongozi wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwasili nchini humo baadaye wiki hii na kufutilia mbali waranti za kimataifa za kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani. Saa chache kabla ya kuwasili kwa Katibu huyo wa Umoja wa Mataifa, watu wawili waliuawa na wengine tisa walijeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na washambuliaji waliokuwa katika pikipiki. Meya wa mji wa Bujumbura Freddy Mbonimpa ambaye ameyalaani mashambulizi hayo na kuyataja vitendo vya kigaidi vinavyowalenga raia wasio na hatia amesema mji huo umekuwa mtulivu kwa siku kadhaa zilizopita. Mbonimpa amesema washambualijai hao wamefanya mashambulizi hayo ili kudhihirisha uwepo wao wakati ambapo Burundi inamtarajia mgeni muhimu. Haijabainika wazi ni nani hasa aliyehusika katika mashambulizi hayo ya maguruneti ambayo yameongezeka katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita. Maafisa wa usalama, waasi na upinzano wanalaumiana kwa mashambulizi hayo yanayosababisha mauaji. Wakati huo huo, Ufaransa imewasilisha pendekezo katika Umoja wa Mataifa la kupelekwa kwa askari wa Umoja huo nchini Burundi ili kutuliza ghasia. Ufaransa inatumai kuwa pendekezo hilo litaidhinishwa kabla ya marais wa Afrika wakiongozwa na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kuwasili Burundi siku ya Alhamisi wiki hii kwa mazungumzo na Nkurunziza. Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Francois Delattre amesema wanataka kuchukua fursa ya kuwepo juhudi za pamoja za jumuiya ya kimataifa kukomesha ghasia na kutafuta suluhisho la tija Burundi. Mzozo huo wa Burundi umesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na wengine zaiidi ya 240,000 wamelazimika kutorokea nchi nyingine. Maelfu ya watu wamekamatwa na maafisa wa usalama wanashutumiwa kwa kuwaua watu kiholela na kukiuka haki nyingine za kibinadamu. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa Burundi iko katika hatari ya kutumbukia tena katika vita vya wenyewe kama vilivyoshuhudiwa kati ya mwaka 1993 hadi mwaka 2005 ambapo kiasi ya watu laki tatu waliuawa.

Obama atoa mpango wa kufunga jela ya Guantanamo

Gereza la Guantanamo kwa sasa lina wafungwa 91 Rais wa Marekani Barack Obama amewasilisha mpango wa kufungwa kwa jela ya Guantanamo Bay, moja ya malengo yake ambayo bado alikuwa hajatimiza. Habari hizo zimetangazwa na ikulu ya White House. Wizara ya ulinzi ya Marekani imependekeza wafungwa 91 ambao bado wanazuiliwa katika gereza hilo warejeshwe nchi zao asili au wahamishiwe magereza ya jeshi la Marekani au magereza ya kiraia. Lakini Bunge la Congress limekuwa likipinga wazo hilo na linatarajiwa kupinga mpango huo wa Rais Obama. Mfungwa akataa kuondoka Guantanamo Wafungwa wawili wa Guantanamo wapelekwa Ghana Gereza hilo hugharimu Marekani $445m (£316m) kila mwaka. Maafisa wakuu wa utawala wake waliambia wanahabari Jumanne kwamba kufungwa kwa jela hiyo ni hitaji la usalama wa kitaifa. "Kutekelezwa kwa mpango huu kutaimarisha usalama wa taifa kwa kuwanyima magaidi ishara muhimu ambayo wamekuwa wakitumia katika propaganda, kuimarisha uhusiano na marafiki wakuu na washirika katika kukabiliana na ugaidi, na kupunguza gharama,” afisa wa vyombo vya habari wa Pentagon Peter Cook amesema kupitia taarifa. Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. Hamsini kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru. Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya amshambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia „wapiganaji maadui”. Rais Barack Obama amesema anataka kufunga gereza hilo kabla ya kuondoka madarakani mapema 2017.