Writen by
sadataley
5:28 AM
-
0
Comments
Wapendwa Washarika kitabu hiki cha Mwanzo ni cha mwanzo kweli, tofauti na Agano Jipya ambalo linasadikiwa kuchukuwa takribani nusu karne ambayo ni kuanza kuandikwa kati ya mwaka 50-100 Baada ya Kristo (AD) ili kukamilika kuandikwa kwake si hivyo kwa Agano la Kale ambalo linaaminika kuchukuwa milenia nzima yaani mwaka wa 1400-400 Kabla ya Kristo (BC) .
Tunaona katika Agano la Kale kuwapo na Vitabu vya Kihistoria, Kinabii na Mashairi. Huku Lugha rasmi inayotumika ni Kiebrania (Hebrew) na Kiaramaiki (Aramaic)kwa baadhi ya vitabu.
Wapendwa watu wa Mungu leo tunapewa kitabu hiki cha Kihistoria (Pentateuch) ili kituwezeshe kutafakari jsiku hii ya mazingira.
Kitabu hiki cha Mwanzo kimeandikwa na Musa kama ilivyo dhamira ya historian a kwa kuwa ni cha kwanza ndicho kinabeba historia nzima ya kuanza kwa ulimwengu na maisha ya mwanadamu kwa ujumla. Mlamgo tuliopewa kuusoma ni eneo muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu awaye yeyote, ni Uumbaji wa kila kitu. Na hapa leo ni namna ambavyo Mungu anaviweka wakfu na kumkabidhi huyu mwanadamu (Adamu). Ili aweze uvitunza na kuvitiisha.
Kikanisa na kwa mujibu wa Kalenda yetu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania toleo la mwaka 2016, leo ni Jumapili ya nne Kabla ya Pasaka na tunapaswa kutafakari zaidi juu ya Mazingira.
MAZINGIRA NI NINI?
Wapendwa Washarika Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni jua hewa, ardhi na maji.
Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu namazingira.
KWA NINI TUTUNZE MAZINGIRA?
Wapendwa wangu shughuli za wanadamu zinaidhuru sayari yetu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Matatizo kama vile kuongezeka kwa joto duniani yanapozidi kuwa mabaya, wanasayansi, serikali, na viwanda vinazidisha jitihada za kukabiliana na hali hiyo.
Je, sisi mmoja-mmoja tuna wajibu wa kusaidia kutunza mazingira? Ikiwa ndivyo, tunaweza kusaidia kwa kadiri gani? Biblia inatoa sababu nzuri kwa nini tunapaswa kufanya mambo yenye manufaa kwa dunia. Pia inatusaidia tuwe na usawaziko katika jitihada zetu. Tukumbuke kuwa "sisi ni nchi ya pili duniani nyuma ya Brazil kwa ubora wa uoto wa asili". Prof Maghembe TBC Radio 28.02.2016 saa 12:06 Asubuhi
KUTENDA KUPATANA NA KUSUDI LA MUNGU.
Mungu aliumba dunia iwe makao ya bustani kwa ajili ya wanadamu. Alisema kwamba kila kitu alichokuwa amefanya kilikuwa “chema sana” na akampa mwanadamu mgawo wa ‘kuilima na kuitunza dunia.’ (Mwanzo 1:28, 31; 2:15) Mungu anahisije kuhusu hali ya sasa ya dunia? Kwa wazi, yeye anachukizwa sana mwanadamu anapokosa kuitunza dunia, kwa kuwa Ufunuo 11:18 inatabiri kwamba ‘atawaharibu wale wanaoiharibu dunia.’ Kwa hiyo, hatupaswi kupuuza hali ya dunia.
KUSAIDIA KUISAFISHA DUNIA
Shughuli za kawaida za wanadamu hutokeza kiasi fulani cha takataka. Mungu ametupa zawadi ya majira yaani mizunguko ya asili ya dunia ili kuondoa takataka hizo, kusafisha hewa, maji, na ardhi. (Methali 3:19) Mambo tunayofanya yanapaswa kupatana na mizunguko hiyo. Hivyo, tunapaswa kuwa waangalifu tusishiriki katika kuharibu zaidi mazingira ya dunia. Utunzaji kama huo unaonyesha kwamba tunawapenda majirani zetu kama sisi wenyewe. (Marko 12:31) Fikiria mfano katika nyakati za Biblia.
Mungu aliagiza taifa la Israeli lizike kinyesi cha wanadamu “nje ya kambi.” (Kumbukumbu la Torati 23:12, 13) Hilo lilifanya kambi iwe safi na uchafu ulioza haraka. Vivyo hivyo, leo Wakristo hujitahidi kutupa takataka upesi na kwa njia inayofaa. Tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa tunapotupa vifaa vyenye sumu.
Takataka nyingi zinaweza kuboreshwa ili zitumiwe tena. Ikiwa sheria inasema kwamba takataka zitumiwe tena basi kutii sheria kama hizo ni sehemu ya kumlipa “Kaisari vitu vya Kaisari.” (Mathayo 22:21) Huenda jitihada nyingi zaidi zikahitajika ili kutumia tena takataka, lakini kufanya hivyo kunaonyesha kuwa mtu anatamani kuona dunia ikiwa safi.
KUHIFADHI MALIASILI ZA DUNIA
Wapendwa Washarika ili kutimiza mahitaji yetu ya chakula, makao, na mafuta, na hivyo kuendeleza uhai wetu, lazima tutumie maliasili za dunia. Kutambua kwetu kwamba mali hizo ni zawadi kutoka kwa Mungu kutaonekana tunapotumia mali hizo. Waisraeli walipotamani nyama jangwani, Yehova aliwapa kware wengi sana. Pupa iliwafanya watumie vibaya na kwa ubinafsi zawadi hiyo, nao wakamkasirisha sana Yehova Mungu. (Hesabu 11:31-33) Mungu hajabadilika tangu wakati huo. Kwa sababu hiyo, Wakristo wenye dhamiri nzuri huepuka kutumia maliasili vibaya kwani kufanya hivyo kunaweza kuwa ishara ya pupa.
Huenda wengine wakaona kuwa wana haki ya kutumia nishati au mali nyingine za asili kupita kiasi. Lakini, maliasili hazipaswi kutumiwa vibaya eti kwa sababu tunaweza kuzigharimia au ziko kwa wingi. Baada ya Yesu kulisha umati mkubwa, alielekeza kwamba samaki na mikate iliyosalia ikusanywe. (Yohana 6:12) Alijitahidi asipoteze kile ambacho Baba yake alikuwa ameandaa.
KUWA NA USAWAZIKO
Ndugu zangu kila siku sisi hufanya maamuzi yanayoathiri mazingira. Je, tuchukue hatua za kupita kiasi kama vile kujitenga na jamii ya wanadamu ili kuepuka kuidhuru dunia? Biblia haipendekezi mahali popote jambo kama hilo. Fikiria mfano wa Yesu. Alipokuwa duniani, aliishi maisha ya kawaida ambayo yalimwezesha kutimiza kazi aliyopewa na Mungu ya kuhubiri. (Luka 4:43) Isitoshe, Yesu alikataa kujihusisha katika siasa ili kutatua shida za jamii ya wakati huo. Alisema hivi waziwazi: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu.”—Yohana 18:36.
Hata hivyo, ni muhimu kwetu kufikiria jinsi tunavyodhuru mazingira tunapofanya maamuzi fulani kama vile kununua vifaa vya nyumbani, kusafiri, na kujihusisha na tafrija. Kwa mfano, wengine huamua kununua vitu ambavyo vimeundwa au vinavyotumika katika njia ambayo haiharibu sana mazingira. Wengine hujitahidi kupunguza muda wanaotumia katika utendaji unaochangia uchafuzi au unaotumia vibaya maliasili.
Hakuna haja kwa mtu yeyote kuwalazimisha wengine wafuate maamuzi yake kuhusu kutunza mazingira. Hali hutofautiana ikitegemea mtu binafsi na eneo analoishi. Lakini sisi sote tunawajibika kibinafsi kwa sababu ya maamuzi tunayofanya. Kama Biblia inavyosema, “kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe.”Wagalatia 6:5.
Muumba aliwapa wanadamu madaraka la kutunza dunia. Kuthamini mgawo wetu na kumheshimu Mungu na kazi zake za uumbaji kwa unyenyekevu kunapaswa kutuchochea tufanye maamuzi ya akili na ya kudhamiria kuhusu jinsi tunavyoitunza dunia.
“Environmental justice is based on the principle that all members of a society have the right to clean air, water, and soil, as well as a right to live in communities where they can raise their families and send their kids out to play in healthy and nurturing natural environments. Further, it embraces the notion that no one possesses the right to degrade and destroy the environment, whether the government at all levels, private industry, or individual citizens. Finally, environmental justice includes a guarantee of equal access to relief and the possibility of meaningful community participation in the decisions of government and industry”.Hii imewasiliswa katika maadhimisho ya 20 ya Kuheshimu mchango wa Dr Martin Luther King katika utunzaji wa mazingira iliyotolewa katika chuo Kikuu Yale chini ya Yale Peabody Museum of Natural History Sunday, Jan 17- 18, 2016
UHUSIANO WA MAISHA NA MAZINGIRA YETU
Ni wazi kuwa maisha katika uso wa Dunia hutegemea huduma ubora wa huduma zitolewazo na mazingira husika. Ukiangalia mfumo wa ikolojia wa misitu, bahari, mbugani na kwenye udongo utaona uwepo wa maji, hewa nzuri na rutuba ya udongo ndivyo vinavyopelekea wanyama na mimea kuwepo na kupendezesha mazingira.
HEWA – ni sehemu muhimu ya mazingira kwani viumbe hai vyote hupumua ili kumudu maisha. Wakati wanyama wanavuta hewa ya oksijeni mimea huvuta hewa ya Kaboni dayoksaidi wakati wa mchanga ili kutengeneza chakula, hewa ambayo wanyama huitoa kama hewa chafu. Hapa tulijifunza uhusiano kati ya wanyama na mimea katika kuishi na pia katika kuweka usawa wa hewa safi angani.
UDONGO – ni maada ambamo mimea hupandwa na kukulia pia wanyama hupata mahitaji yao kama Chakula kutoka kwenye udongo na pia udongo hufanya nchi kavu ambapo binadamu na Wanyama wengi huishi. Lakini pia udongo unahifadhi wadudu wadogo wadogo wengi tusioweza kuwaona kwa macho ambao husaidia kurutubisha udongo na kuifanya mimea iweze kustawi na pia mizizi iweze kupata maji na hewa. Hapa tunaona umuhimu wa udongo katika kuboresha maisha kwa kuifanya mimea iweze kukua.aa
JUA – ni chanzo kikubwa asilia cha nishati ya mwanga na joto. Nishati ya mwanga kutoka katika Jua mbali na kutupatia joto na kusaidia kufanyika kwa mvua na kupunguza baridi katika uso wa Dunia, bado ni muhimu sana katika kuisaidia mimea kuweza kutengeneza chakula chake chenyewe. Bila kuwepo kwa mwanga wa Jua mimea itashindwa kutengeneza chakula na kupelekea kufa, hivyo kuwafanya wanyama wanaotegemea mimea kufa, ambao nao watawafanya wanyama wala nyama kufa akiwamo binadamu anayekula nyama na mimea.
MAJI – yamechukua sehemu kubwa ya Dunia yetu, ni sehemu kubwa ya miili yetu na maisha ya viumbe wengi hutegemea maji kwa ajili ya kuwa hai. Maji hupatikana katika maeneo mbali mbali kama kupitia mvua na hupatikana kwa wingi katika mito, maziwa, visima, bahari, barafu ,unyevu na Umande na pia chini ya ardhi. Maji huzunguka kwa kuvukizwa kutokana kwenye uso wa Dunia na kupanda juu na kutengeneza mawingu ambayo baadae hurudi Duniani kama mvua au theluji na kufanya maisha yaendelee Duniani.
Mvua inaponyesha kiasi kikubwa cha maji yake huanguka ardhini na kisha kuzama chini na kufanya Chemchem, maji yanayotiririka hufanya Mito nayo mito hutiririka hadi katika maziwa au Bahari kisha maji ya bahari yanapopata joto mtiririko hujirudia.
KUTEGEMEANA KATIKA MAZINGIRA (IKOLOJIA) – Wapendwa Washarika viumbe hai vimegawanyika katika makundi mawili nayo ni Mimea na Wanyama. MIMEA hutegemea mazingira ufu na ndilo kundi pekee lenye kujitengenezea chakula chake chenyewe kwa kutumia chumvichumvi za ardhini, maji,gesi ya kabon dayoksaid na mwanga wa jua na kufanya mimea kukua katika udongo au maji. Mimea bado hutegemea wanyama kuweza kustawi kutokana na samadi inayotokana na wanyama kisha huoza na kufanyika mbolea inayorutubisha udongo.
WANYAMA hutegemea kupata hewa safi ya oksijeni iliyotengenezwa na mimea, ambayo hutumika kutengenezea nishati kutokana na chakula kilichosharabiwa katika mwili.
MZUNGUKO WA KABONI – hutokana na kutegemeana kwa viumbe hai kwa ni Kabonidoiksaidi iliyoko hewani ambayo hutumika na mimea kutengeneza chakula. Mimea huliwa na baadhi ya wanyama kisha wanyama hao huliwa na wanyama wanaokula nyama.kisha mizoga ya wanyama na mimea huoza na kutoa kaboni inayorudi angani.
Hapa kwetu Tanzania sisi huungana na wenzetu duniani kote kila mwaka, tarehe tano Juni ni siku ya mazingira duniani. Watu katika nchi mbali mbali hapa ulimwenguni huadhimisha siku hii kwa namna mbali mbali, wengi aghalabu hufanya shughuli mbali mbali za utunzaji wa mazingira. Kwa hapa kwetu nchini, sherehe hizi huambatana na kufanya kazi za utunzaji mazingira, kama vile uokotaji wa taka mahali mbali mbali, upandaji wa miti sehemu za wazi na kadhalika. Lakini kwa upande mwingine, hapa nchini kwetu upandaji wa ,miti kitaifa hufanyika kila mwaka siku ya Januari mosi, yaani siku ya mwaka mpya. Nadhani hii tarehe imewekwa makusudi kwa sababu kwa maeneo mengi (kama si yote) hapa nchini huwa ni msimu wa mvua. Kwa hiyo ili miti iliyopandwa iote vizuri, ni lazima ipate maji ya kutosha, kutokana na mvua hizi.
Wapendwa Washarika dunia imeanza kuonja machungu ya kutotunza mazingira (Global Warming) na kupelekea kujaribu kuzisaidia na kuanzisha mradi wa malipo kwa wote wanao miliki misitu maarufu Carbon yote hii ni kujaribu kuhamisisha upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.
Kanisa letu limeanza kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kuanzisha Programu maalum ya Uhai na Mazingira chini Bibi Patricia Mwaikenda. Programu hii mpaka sasa imeshaandaa Sera ya Mazingira ya Kanisa, kuanzisha miradi ya mitambo wa kuzalisha nishati mbadala ya kinyesi (Biogasi) na kuanzisha miradi ya upandaji wa miti kwa ushirikiano wa kanisa na wenzetu wa Ushirikiano wa Makanisa ya Ulaya (Lutheran Mission Cooperation)- LMC).
Na mwaka jana 9Disemba,2015 ilikuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa na tumeona jana kwetu hapa Dar Es Saalam na mikoa mingine kuwa ilikuwa ni siku maalum usafi wa mazingira ambayo kwa sasa inaonekana kuwa itakuwa hivyo kwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Kwa kuwa Kanisa lipo katikati ya jamii na wanajamii ndiyo washarika na ndiyo wafuasi wa Yesu basi tushirikiane kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu na kuacha kulalamika tu. Tukumbuke hii ni kwa ajili ya ustawi wa afya zetu na vizazi vinavyokuja.
Tukumbuke kuwa kulingana na tafiti inaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2,050 watu bilioni sita duniani hawatakuwa kabisa na huduma ya maji, kwa nini sisi tujione tu salama? Na tujuwe kuwa vita ijayo ni ya kugombea zrdhi na maji na hapa kwetu Tanzania tayari viashiria vimeanza baina ya mapigano ya wakulima na wafugaji katika maeneo yetu.
“Our lives begin to end the day we become silent about things that matter.”
— Dr. Martin Luther King, Jr.
Tumsifu Yesu Kristo .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment