Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Saturday, February 29, 2020


Unaweza usiamini nikikuambia embe bichi ni tiba ya ugonjwa furani, lakini amini kuwa kweli ni tiba, tena iliyo makini. Embe bichi linasaidia sana kwa mgonjwa wa maradhi ya kuhara. Tumia embe bichi kumaliza tatizo hilo.

Menya embe bichi, likate  vipande na kuviweka katika chombo, au tengeneza juice changanya na unga wa pilipili manga pamoja na asali, kisha tafuna vipande hivyo vyenye mchanganyiko huo.

Mchanganyiko wako utategemea kiwango cha vipande vya embe lako. Hata hivyo, usile zaidi ya embe mbili kwa kutwa moja. Endelea na tiba hii muda wa siku tatu.

Kuharisha ni kitendo cha kujisaidia kinyesi chenye majimaji mara kwa mara. Hali hiyo hutokea baada ya utumbo mdogo kuwa na maji mengi ambayo yanashindwa kutoka mwiilini kwa njia za kawaida kama ya mkojo na jasho hivyo yanatelemka kwenye utumbo mkubwa usio na uwezo wa kutunza maji.

Yakiwa huko mtu hujikuta anajisikia hali ya kutoa haja na ndipo maji hayo hutoka kupitia haja kubwa. Kimsingi utumbo mdogo una uwezo wa kupokea zaidi ya lita nane za maji kutoka kwenye vyakula au vinywaji vinavyopitia mdomoni na mengine kutoka sehemu mbalimbali katika mwili.

Tatizo la kuhara linaweza kusababishwa na kula kupita kiasi, kula mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbali, kuwa na hofu, hasira au wasiwasi, kuchacha chakula ndani ya tumbo, kula sumu, bakteria, virusi au vijidudu wenye vimelea.

MUUNGWANA BLOG

Thursday, February 27, 2020


Nchini China yeyote mwenye dalili ya kuambukizwa virusi vya Corona (Covid-19) akatoa taarifa kisha kupimwa na kugundulika na virusi hivyo atalipwa Yuan elfu 10, sawa na dola takriban elfu 1 na mia 5.

Hatua hiyo imechukuliwa na mamlaka ya jimbo la Hubey, katika mji wa Qianjiang katika kujaribu kudhibiti kusambaa kwa mlipuko wa maambukizi.

Mamlaka zimetaka watu wapewe motisha ili waweze kutoa taarifa juu dalili za kuambukizwa, Kwa yeyote atakayejisalimisha mwenyewe atalipwa kiasi cha Yuan elfu 10 takribani dola elfu 1 na mia tano.

Pesa hiyo itatolewa kwa wale tu ambao matokeo yao yatagundulika kuwa chanya, yaani wana maambukizi. Kwa wale ambao watahisi kuwa wameambukizwa na matokeo ya vipimo yakaonyesha hawajaambukizwa watalipwa yuan elfu 1, na kwa wale ambao kuna hakuna uhakika kama wameambukizwa au la watapewa yuan elfu 2. 
Muungwana Blog

 Saudi Arabia, MakkaMahujaji wakiwa msikiti wa Makka, Saudi Arabia

Serikali ya Saudi Arabia imezuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, ikiwemo wanaotembelea miji mitakatifu katika dini ya Kiislamu - Makka na Madina.
Mamilioni ya watu huingia Saudia mwaka mzima kufanya ibada ya Umra, na wengi zaidi huingia kwa pamoja kufanya ibada ya Hija.
Tofauti na Hija, Umra (ambayo pia hufahamika kama Hija ndogo) hufanyika katika kipindi chochote cha mwaka, na kwa sasa marufuku hiyo inawalenga mahujaji raia wa nchi za nje wanaoenda kuitekeleza.
Bado haijulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai kama itaathirika na zuio hilo pamoja na kusambaa kwa virusi vya corona duniani.
Saudia pia imewapiga marufuku watu kutoka nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.

Msikiti wa MadinaMsikiti wa Madina ni wa pili kwa utukufu katika Uislamu na ndipo alipozikwa Mtume Muhammad.
Mpaka sasa Saudia bado haina mtu ambaye amethibitika kuambukizwa virusi hivyo.
Makka, ndio mji ambao Mtume Muhammad alipozaliwa, na kuna msikiti mtakatifu zaidi. Madina ndipo alipofariki na kuzikwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudia inasema marufuku hiyo ni ya muda - lakini wizara hiyo haijataja lini marufuku hiyo itaondolewa.
Watalii ambao si wa kidini ambao wanatoka katika nchi ambazo virusi vya corona vimethibitisha kuingia pia watakataliwa kuingia Saudia.
Saudi Arabia imeeleza kuwa toka mwezi Oktoba imetoa viza zaidi ya 400,000 za watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.

'Dunia ijiandae kwa janga'

Coronavirus
Shirika la Afya Duniani (WHO) mapema wiki hii limeonya kuwa dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona.
WHO japo imesema kuwa ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi".
Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia.
Visa zaidi vya virusi ambavyo husababisha ugonjwa kupumua Covid-19, vinaendela kujitokeza, huku milipuko ya ugonjwa huo ikibainika katika mataifa mengi zaidi ya Uchina mabapo ndipo ulipoanzia.
Mpaka sasa zaidi ya watu 2,700 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Toka virusi vya corona viripotiwe mwezi Disemba, zaidi ya watu 80,000 duniani, kutoka katika mataifa takribani 40 tayai wameshaambukizwa virusi hivyo. Wengi wao wakiwa nchini Uchina.
Iran (ambayo imetenganishwa na Saudia kwa mkondo mwembamba wa bahari) mpaka sasa imesharipoti vifo 19 - ambayo ni namba kubwa zaidi ya watu kwa mataifa ya nje ya Uchina.
Hata hivyo vifo hivyo vinatokana na wagonjwa 139, hali ambayo inawafanya madaktari wa magonjwa ya kuambukiza kuhofia kuwa nchi hiyo inaweza kuwa na wagonjwa wengi zaidi inaowaficha.
Barani Ulaya hali ni mbaya zaidi nchini Italia ambapo mpaka sasa watu 400 wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo kutoka watu 80 siku ya Jumanne. Watu 12 tayari wameshafariki nchini humo kutokana na mlipuko huo.
Kwa Afrika ni nchi mbili mpaka sasa zimethibitisha kuingia kwa ugonjwa huo. Algeria na Misri kila moja imeripoti mgonjwa mmoja.

BBC

Thursday, July 4, 2019

Unene kwa sasa umekuwa moja ya kisababishi cha ugonjwa wa saratani nchini Uingereza kuliko uvutaji sigara, taasisi ya saratani nchini humo imeeleza.

 Mtu mwenye uzito mkubwa

Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani imesema, saratani ya ini, utumbo, ovari zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uzito mkubwa kuliko kuvuta tumbaku.
Inasema mamilioni wako hatarini kuugua saratani kwasababu ya uzito na kuwa watu wenye uzito mkubwa huzidi idadi ya wavuta sigara kwa wastani wa watu wawili kwa mmoja.
Lakini matangazo ya mabango ya kampeni kuhusu unene na hatari ya kupata saratani yamekosolewa kwa kujeli watu wanene.
Maangazo ya tahadhari kuhusu saratani
Si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kushutumiwa kukejeli watu wanene. Wengine wakisema kuweka tangazo hilo kama vile matangazo ya pakiti za sigara si jambo zuri.
Lakini taasisi hiyo imejitetea kuwa haiwalaumu watu walio na uzito mkubwa.
Wala haisemi kuwa uvutaji wa sigara ni sawa na kuwa na uzito mkubwa wakihusisha na hatari ya kupata saratani. Vyote viwili vinahatarisha afya.
Lakini taasisi hiyo imesema uzito mkubwa au unene husababisha wagonjwa wa saratani 22,800 kila mwaka, ukilinganisha na uvutaji wa sigara unasababisha watu 54,300 kuugua saratani.
Lakini wakati idadi ya wavuta sigara ikipungua, idadi ya watu wenye uzito mkubwa inaongezeka, suala la kushughulikiwa.

Wakati uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani ukibainishwa vyema, kibaiolojia bado haijaeleweka vyema
Kuwa na uzito mkubwa au mnene haimaanishi kuwa lazima mtu huyo apate saratani, lakini mtu huyo anaongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.
Ongezeko la hatari hujitokeza zaidi iwapo mtu ataongezeka uzito zaidi.
Kwa mujibu wa watafiti saratani mbalimbali zinahusishwa na uzito mkubwa: Saratani ya matiti kwa wanawake waliokoma hedhi (menopause), utumbo, ini, saratani ya damu, saratani ya ubongo, koo, tezi, figo, kongosho, tumbo,ovari.
Uhusiano kati ya unene na saratani ni kwa watu wakubwa pekee, ingawa kwa watoto wadogo ni muhimu kuwa kwenye tahadhari pia.

BBC

Saturday, April 21, 2018

Baada ya kujifungua akina mama wengi huendelea kunyonyesha mpaka miaka miwili, japokua wengine hunyonyesha chini ya hapo inategemea na mtazamo wa mtu. lakini kitaalamu mtoto anayenyonya kwa miaka miwili hua anakua vizuri na kua na uwezo sana wa kiakili. Kipindi cha kunyonyesha mama anaweza kuugua au kutumia dawa fulani fulani kwa ajili yake. Baadhi ya dawa hazitakiwi kutumika kwa mama kipindi hichi kwani zinaweza kumuathiri sana mtoto na kuharibu ukuaji wake

Dawa hizo ni kama ifuatavyo;

1. Chloramphenicol.
Hii ni antibayotiki, ni dawa inayotumika kuua bacteria ambao wanashambulia mwili. Kwa hapa Tanzania dawa hii mara nyingi hutumika kutibu ugonjwa wa typhodi. Dawa hii husababisha ugonjwa unaitwa grays syndrome yaani mtoto hubadilika rangi na kua rangi ya gray lakini pia huonyesha dalili kama kutapika, tumbo kuvimba, kukosa hamu ya kula, kushuka kwa joto na presha kushuka. Lakini pia dawa hii huzuia utengenezaji wa damu kutoka kwenye mifupa[aplastic anaemia]. Tatizo hili la damu likishaanza hakuna dawa inayoweza kumponya mtoto huyu.

2. Dawa ya mseto ya malaria.
Dawa hii hutumika kutibu malaria lakini hua inapita kwenye maziwa na kuingia kwa mtoto. Kama una mtoto mwenye chini ya kilo tano usimeze dawa hii kwani ikiingia kwa mtoto hawezi kuitoa nje lakini kama mtoto wako ana zaidi ya kilo tano unaweza kutumia.

3. Vidonge vya uzazi wa mpango.
Hizi ni dawa ambazo hua zina homoni za oestrogen na progesterone matumizi yake husababisha kiwango kikubwa sana cha homoni hizi mwilini na kuzuia mimba. Lakini dawa hizi hupingana na homoni ya prolactin ambayo ni muhimu kwa kutoa maziwa. Hivyo matumizi ya dawa hizi kwa mama mwenye mtoto chini ya miezi sita hupunguza maziwa kwa kiasi kikubwa.

4. Aspirin.
Aspirin ni dawa ya maumivu lakini pia hulainisha damu na kuifanya kua nyepesi sana hii ni hatari kwa mtoto kwani anaweza kuvuja damu mpaka kufa lakini pia husabibisha ugonjwa unaitwa reyes syndrome ambao huambatana na kuvimba maini na kichwa.

5. Dawa za cancer.
Kuna dawa aina mbali mbali za kansa ambazo mara nyingi huua seli za kansa au kuzuia zisikue. Kwa jinsi zinavyofanya kazi hupunguza kinga ya mwili ya mgonjwa pia hupita kwenye maziwa ya mama na kushusha kinga ya mtoto na kumfanya aharishe.

6. Ergotamine.
Hii ni dawa inayotumika kutibu maumivu makali ya kichwa kitaalamu kama migraine headache, mara nyingi huchangwanya na kemikali ya caffeine kufanya kazi vizuri. Matumizi yake hupunguza utengenezaji wa maziwa ya mama na huweza kuleta degedege kwa mtoto.

7. Drogens; 
hizi ni hormone ambazo zinapatikana kwenye mwili wa binadamu lakini pia zinatengenezwa kiwandani kutolewa kwa watu ambao wana upungufu wa homoni hizi. Kwenye mwili wa mwanamke homoni hizi hubadilika na kuwa oestrogen yaani homoni ya uzazi. Sasa matumizi ya dawa hizi hupunguza kiasi cha maziwa kwa mama.

Lakini kumbuka kuna dawa nyingine nyingi huenda sijazitaja hapo lakini hizo ni baadhi ambazo zinapatikana kwa wingi. katika kipindi hicho cha unyonyeshaji basi ni vizuri kuongea na doctor kabla ya kumeza dawa yeyote.

Wednesday, April 18, 2018

Kuna njia nyingi sana ambazo hujaribiwa na watu ili kupunguza mwili na tumbo lakini zinakuwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanayoishi hivyo kupelekea kushindwa njiani. Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu. Kwa kuwa kahawa huwezi kutumia zaidi ya round 3 kwa maana hiyo ukinenepa tena inabidi utafute njia nyingine.

Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka mwili. Mara nyingi vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa npyo vinatuponza.

Tutakuwa tunakuletea ratiba ya kupunguza uzito wako kwa muda wa mwezi mzima.

Vidokezo muhimu
Kupungua uzito kunategemea na kiwango cha mafuta cha mtu mwilini (body fat), uzito wa mtu, calories anazohitaji kwa siku, BMI yake pamoja na lengo la mtu la kupungua uzito. Je vyakula ninavyokula hunipa nguvu (calories) na uwezo wa kumudu majukumu yangu ya kila siku? Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiasi gani? Kwa wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya kiwango cha mafuta mwilini.

Kwa maana hiyo, si kila diet plan humfaa kila mtu, inaweza ikakufaa wewe lakini isimfae mtu mwingine.

Cha kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa wataalamu wa lishe (nutritionists), daktari, wataalamu wa mazoezi na nk. Kama utafuatilia diet plan hii, utaona kila siku unahitaji kunywa kikombe kimoja cha kahawa, ni vizuri kubadilisha unywaji wa kahawa kwa chai, yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa chai na  kadhalika. Kwa wale wenye ugonjwa wa shinikizo la damu (hypertension), anxiety disorders na nk, wanashauriwa kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai. Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu au limao ndani yake na hivyo kuongeza ladha.

Siku ya Kwanza (Day 1)
Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula chochote. Kwa wale wenye mashine ya tredmill basi pia tembea kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na spidi ndogo (kama namba 5 na kuongeza hadi spidi namba 8). Unaweza pia kukimbia kwa muda wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa muda wa nusu saa. Anza kukimbia kwa spidi ndogo (kwenye tredmill) halafu ongeza spidi yako, au unaweza kukimbia kwa spidi ya juu kama spidi 8 kwa muda wa dakika 5 na kisha kupunguza hadi spidi 5, hii inaitwa interval training, lengo ni kukupa uwezo wa kufikisha dakika 30, kuchoma mafuta mwilini, kupunguza mapigo ya moyo yarudi kwenye kiwango cha kawaida kwani wakati unafanya mazoezi mapigo ya moyo huongezeka sana, kuupa uwezo moyo wako wa kufanya kazi vizuri.

Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya moyo au wale ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo haya kama atrial fibrillation, ventricular tarchycardia na nk, wagonjwa wa pumu, ni vizuri kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa mazoezi (sports therapist) pamoja na kushauriana na daktari. 

Fanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) kati ya 15-20. Ukiona ni ngumu sana unaweza kuanza hata na sit-ups 10 na utakuwa unaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu na tumbo. 

Unaweza kutumia bench au kulala sakafuni. Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups kunywa maji ya uvuguvugu glass 4. Siyo lazima unywe yote kwa wakati mmoja. Unaweza kuwa unakunywa huku unaendelea na mambo mengine mpaka glasi 4 ziishe. Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu. Limao na ndimu siyo tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini. 

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha kahawa au chai kwa kuweka kijiko kimoja kidogo cha sukari (2.5ml spoon). Yai moja la kuchemsha. Slice moja ya mkate wa brown bread (mikate inayotengenezwa kwa ngano nzima nzima). Usithubutu kuweka siagi wala vinavyofanana  na hivyo.Kula matunda kadri uwezavyo lakini epuka ndizi tamu.

Chakula cha mchana (Lunch): ¼  Kuku wa kuchoma au wa kuchemsha na si vinginevyo. Salad au kachumbari ya mboga mboga tofauti lakini isiwe na mayonnaise. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 tena. Jitahidi kuepuka snacks kama ice cream, chocolate, biskuti nk. Jizoeshe kula matunda kwa wingi kila unapohisi njaa.

Jioni: Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) pamoja na kufanya sit-ups wakati unasubiri chakula cha usiku.

Chakula cha usiku (Dinner): Supu ya samaki yoyote yule bakuli kubwa la kutosha. Unaweza kutumia karoti, nyanya au tungule, broccoli, cauliflower, pilipili boga na za kuwasha, ndimu au limao, kitunguu maji na thomu na nk, epuka viazi vyovyote vile kwenye supu.
 
Siku ya pili (Day 2)
Tembea kwa nusu saa asubuhi (dakika 30) na fanya sit-ups 15-30. Baada ya mazoezi kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa kuweka kijiko kimoja cha sukari kidogo kama nilivyoeleza hapo awali. Sausage moja ya kuchemsha ya kuku au ya nyama ya ngombe. Slice moja ya brown bread pamoja na matunda mengi.

Chakula cha  mchana (Lunch): Ndizi moja ya kuchoma pamoja na kachumbari au salad ya mboga mboga aina yoyote lakini isiwe na mayonnaise. Mishikaki 2-3 ya nyama ya ngombe (isiwe ya nundu au nyama ya mafuta), kuku, samaki.

Jioni: Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) na baada ya hapo fanya sit-ups 15-20 kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. Epuka juisi aina yoyote ile iwe fresh au za kwenye boksi kwani mara nyingi watu wanahadaiwa na juisi za kwenye boksi zinazosema ni fresh na hazina kemikali yoyote, ukweli ni kwamba kampuni zinazotengeneza juisi hizi huwapa tenda kampuni za kutengeneza manukato ambazo ndizo hutengeneza maboksi haya na kuweka syrup na harufu kulingana na harufu ya tunda linalohitajika, mfano kama kampuni ya kutengeneza juisi inahitaji boksi la harufu ya embe basi watawatengenezea boksi hilo kwa kutumia syrup ya embe na harufu ya embe.
Pia juisi za kwenye boksi, wakati wa kutengenezwa huhifadhiwa kwa muda mrefu na kupitia mlolongo mrefu wa utengenezaji hivyo kuondoa virutubisho asilia muhimu pamoja na fibre ambazo ni muhimu sana kiafya.

Chakula cha usiku (Dinner): Supu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda. Epuka ndizi mbivu. Epuka vilevi vya aina yoyote vile km pombe, wine, sigara, tumbaku, khuberi na nk.
 
Siku ya Tatu (Day 3)
Mazoezi kama kawaida. Kimbia au tembea kwa dakika 30, kisha fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa kikiwa na kijiko kimoja cha sukari.

Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla au baada ya kula. Ndizi 2 za kuchemsha Bukoba siyo ndizi tamu (sweet banana). Bakuli la kutosha la supu ya mboga mboga (vegetable soup) ukishushia kwa matunda kwa wingi. Epuka ndizi mbivu. Hakikisha wakati wa kupika supu yako huweki mafuta ya kupikia au siagi n.k.

Jioni: Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 baada ya kufanya mazoezi. Unaweza kula matunda wakati unasubiria chakula cha usiku.
Chakula cha Usiku (Dinner): BBQ sausage 3 pamoja na salad au kachumbari.
 
Siku ya nne (Day 4)
Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa, kisha fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha kahawa au chai, weka kijiko kimoja cha sukari. Sindikiza kwa matunda ya aina yoyote. Epuka ndizi mbivu.

Chakula cha mchana (Lunch): Kiazi kimoja cha kuchemsha pamoja na mboga mboga za majani kama njegere, karoti, pilipili boga, broccoli, cauliflower, na nk. Sukumizia na supu ya uyoga (mushroom soup). Jitahidi supu zako usiweke mafuta wakati unapika. Glasi moja ya maziwa fresh (250ml-300ml).

Jioni: Mazoezi kama kawaida.
Chakula cha Usiku (Dinner): Vegetable platter, mboga za aina zozote unazopenda bila kuweka mafuta hata tone ikishindikana weka kijiko kimoja cha olive oil au mafuta ya alizeti. Samaki wa kuchoma au kuchemsha, kula mzima lakini asizidi robo kilo. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.
 
Siku ya Tano (Day 5)
Kimbia kwa dakika 30, kama utatembea, tembea kwa dakika 45. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu galsi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha kahawa au chai chenye sukari kijiko kimoja. Slice 1 ya mkate mweupe uliyopakwa siagi kidogo sana pamoja na mayai mawili ya kukaanga (Spanish omelet). Malizia kwa matunda.

Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla ya kula chakula cha mchana. Supu ya kuku bakuli moja tu. Hakikisha kuku wako umemtoa ngozi ya juu kabla ya kumpika. Unaweza kuweka tambi (spaghetti) kidogo kwenye bakuli la supu lakini siyo lazima. Tambi zisipikwe kwa mafuta bali zichemshwe tu.

Jioni: Kimbia kwa dakika 30 au tembea kwa dakika 45. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Chakula cha usiku (Dinner): Kula mboga mboga aina yoyote ile pamoja na matunda kwa wingi.
 
Siku ya Sita (Day 6) 
Tembea kwa dakika 45 au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. 

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Cornflakes na maziwa ambayo ni skimmed milk ama low fat (yenye mafuta kidogo). Kula matunda yoyote unayopenda. 

Chakula cha Mchana (Lunch): Kula beefcubes zilizochemshwa kiwango kidogo kama robo kilo. Unaweza kupendezesha kwa karoti, cauliflower, broccoli, pilipili hoho au njegere nk, weka kijiko kimoja cha mafuta ya alizeti au olive oil. 

Jioni: Mazoezi kama kawaida. 
Chakula cha usiku (Dinner): Kula tambi (noodles au spaghetti) zilizochemshwa na sauce yoyote utakayopenda ila isiwe na mafuta zaidi ya kijiko kimoja. Usisahau matunda kwa wingi.
 
Siku ya Saba (Day 7) 
Tembea kwa dakika 30-45, kama unakimbia basi kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30 kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. 

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa, yai moja la kuchemsha pamoja na maziwa fresh glasi moja. 

Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla ya kula. Supu ya mboga mboga bakuli moja la kutosha, ndizi ya kuchemsha moja (ndizi bukoba), malizia kwa matunda mengi, leo unaruhusiwa hata kula ndizi  mbivu au ndizi tunda. 

Jioni: Mazoezi kama kawaida 
Chakula cha usiku (Dinner): Nusu kuku au beef sausage, pamoja na wali maharage na salad au kachumbari ya aina yoyote ile ya kutosha lakini isiwe na mayonnaise, cheese au butter. 

Unaruhusiwa kunywa glasi 2 za white wine baada au wakati unakula kama ni kuku. Au glasi 2 za red wine baada au wakati unakula kama ni beef sausage. Ila kama ni kuku iwe kuku, kama ni beef sausage iwe hiyo na siyo vyote viwili.

Monday, April 16, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao.

Makonda amesema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari.


Kufuatia mwendelezo wa mvua hizo  Makonda ameziomba mamlaka husika kusimamisha  masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na Maafa.

Aidha   Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo madaraja, Barabara,shule pamoja na kuzibua mitaro.


Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya upanga  Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza  mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na kuwasihi wakazi wa jengo hilo pamoja na majirani kutafuta sehemu ya kujisitiri kwa wakati huu kwa mustakabali wa usalama wao.

Pamoja na hayo Makonda amewahimiza wananchi kufuatilia tahadhari zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa nchini pamoja na vyombo vya habari.
Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote.

Friday, April 13, 2018

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemsifu mtangulizi wake Rais msaatafu Jakaya Mrisho Kikwete na kusema kwamba, kama sio Kikwete leo asingekuwa Rais wa nchi hiyo.
Rais Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi hiyo huku akitanguliza uzalendo mkubwa ambapo Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka watake wasitake. 
Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya uzinduzi wa Taasisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema hayyo katika uzinduzi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) na kubainisha kwamba, ipo mifano mingi hai ya mambo ambayo ameyafanya Rais mstaafu Kikwete kwenye Serikali ya Awamu ya nne na baadhi ya miradi hiyo lipo la ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima, ujenzi wa miradi ya maji , umeme na kuimarisha sekta muhimu za afya, kilimo na vijana.
Rais Magufuli amesema: "Uzalendo wa mzee Kikwete kwa nchi yake umemfanya hata baada ya kustaafu kuamua kuanzisha taasisi ambayo amiezindua rasmi na vipaumbele vya taasisi hiyo havina tofauti na vile ambavyo anavitekeleza kwenye Serikali yake, hivyo ameahidi kumpa ushirikiana mkubwa kufanikisha malengo hayo na kuomba wadau wengine wakiwamo mabalozi nao kuunga mkono kazi za taasisi hiyo."
Kwa upande wake Rais Mstaafu Kikwete amesema kuwa anamshukuru Rais Magufuli kwa kukubali kuzindua taasisi hiyo na kuipa heshima ya hali ya juu na kutumia nafasi hiyo kuahidi kuwa lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kufanya kazi katika maeneo ambayo wameamua kuanza nayo zaidi kama sehemu ya kutoa mchango wao katika kushirikiana na Serikali kutekeleza majukumu yake.
Parstoday

Thursday, April 5, 2018

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni yakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako

1.Yogurt ( Maziwa mtindi )
Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako.

2. Matunda
Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matunda asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

3. Vitunguu saumu
Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Vitumie kwa kutafuna (kama unaweza) au weka kwenye chakula!

4. Uyoga
 Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

5. Supu ya kuku
Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto  husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

6. Viazi vitamu
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba  ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

7. Karoti
Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

8. Samaki
Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

9. Matikiti
Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu

10. Maji
Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau lita moja na nusu kwa siku ni muhimu kwa afya yako!

Saturday, March 31, 2018

Mara nyingi watu wengi tuanpenda kutumia simu mahali ambapo pana giza kwa muda mrefu, sisi tunapenda kukuita kukuchati. Kuchati huku nyakati za giza wakati taa imezimwa huwa na madhara yafuatayo.

Kwa sasa, idadi ya wagonjwa kuanzia miaka 30-40 wanatafuta matibabu makubwa. kutokana na matumizi ya simu za mkononi (smart phone) gizani.

Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko singapore amesema: anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.

Hii ni kwasababu wakati wa kutimia simu mahali penye giza huwa tunayalazimisha macho yetu yaweze kuona ya uwezo wake. Na ndo maaana kuna wakati unaweza ukatumia simu muda mrefu mahali penye giza mara baada ya kuacha kutumia simu utaona kama giza limezidi zaidi. Hali hiyo huyafanya macho yako yaanze kurudi katika hali ya ukawaida.

Pia utumiaji wa simu kwenye giza husababisha Kupata saratani ya macho. Hivyo ili uweze kuepuka saratani hivyo ni bora tuache kutumia simu za mikononi gizani ili tujikinge. Simu za mikononi (smartphone) zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani, unabadili mfumo wa seli macho na kupelekea matatizo ya saratani ya macho.

Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi wanazigundua watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo. Hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote hawa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.

 Utumiaji wa simu inaweza sababisha na ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.
.
Madaktari bingwa wa macho 254 kutoka mahosipitalini profesa Li Li atoa hoja kwamba kikubwa cha muhimu ni kwamba ni kuwa mbali na tabia za kutumia simu gizani. Sababu tabia hizi za kutumia simu (smartphone) kabla ya kulala zitakusababishia matatizo ya maisha yako kwa ujumla.

Hivyo ili kujiangalia sisi wenyewe na familia zetu, kwamba hakuna kuzima taa endapo unatumia simu ya mkononi. Wape taarifa haraka wote watumiaji wa simu za mikononi gizani wanaweza kupoteza kwa urahisi sana uwezo wa kuona.

Monday, March 26, 2018

MPENZI msomaji wa ukurasa huu wa afya, leo tuangalie ugonjwa unaojulikana kama mkanda wa jeshi. Tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu wenye ugonjwa huu wakionekana kuwa wana maambukizi ya VVU bila kuwa na uhakika wa afya zao au bila kutambua chanzo sahihi cha ugonjwa wenyewe.

Hali hii imewafanya baadhi ya watu kuamini kuwa mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi anakuwa na ugonjwa wa UKIMWI  jambo ambalo halina ukweli kwa asilimia mia moja kwani sio wote wenye ugonjwa huu wanakuwa na VVU.

Ugonjwa huu kitaalamu unajulikana shingles au herpes zoster ambapo ugonjwa huu husababishwa  na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya  kuungua yenye kuambatana na maumivu makali.

Visababishi
Dk Grace Chirwa kutoka Hospitali ya Temeke Dar es Salaam anasema kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster  ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga, virusi vya ugonjwa huo hubaki katika hali ya kupooza/ kutokuwa na madhara katika baadhi ya neva mwilini.

Baada ya kukaa mwilini kwa miaka kadhaa, iwapo kinga za mwili zitashuka kwa sababu yoyote virusi hawa hupata nguvu na kuwa imara jambo linalopelekea kutokea kwa ugonjwa wa mkanda wa jeshi. Ugonjwa huu unapotokea ni mara chache sana ugonjwa huo kujirudia mara ya pili kwa maisha ya mtu huyo.

Vihatarishi
Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu wa umri wowote ingawa watu wa makundi fulani wanakuwa katika hali ya hatari zaidi kupatwa na ugonjwa huo.
Makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi ni watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60, mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.
Pia watu ambao kinga zao za mwili zimepungua kwa sababu zozote zile ikiwemo mwenye maambukizi ya HIV, saratani pamoja na utapiamlo:

Licha ya hiyo ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama yalivyo magonjwa mengine. Inapotokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupata ugonjwa wa tete kuwanga au kupata chanjo yake akakutana na mgonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto huyo au mtu huyo anaweza kuugua ugonjwa wa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.

Dalili
Dk Chirwa anasema kuwa dalili ya awali kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yanayoambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi.
Maumivu hayo pamoja na   hisia hizo za kuungua  hutokea kabla ya vipele/ michubuko kutokea kwenye ngozi.

Kawaida ya dalili hizi za vipele au michubuko huusisha eneo fulani la mwili hasa kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, midomo au masikio.
Dalili nyingine za ugonjwa huu ni maumivu ya tumbo, homa, maumivu ya mwili mzima, kuwa na vidonda sehemu za siri, kuwa na maumivu katika sehemu za kichwa, kuwa na maumivu ya viungo, kuvimba kwa tezi pamoja na tatizo la kutoona iwapo  neva za maeneo ya uso zimeathirika.

Vipimo
Ni mara chache sana kufanya vipimo kwa ajili ya kutambua ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea. Kwa ujumla utambuzi wa ugonjwa huu hufanyika kwa kuangalia historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa. Pia vipimo vya damu FBP huonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu.

Matibabu
Matibabu ya mkanda wa jeshi hujumuisha matumizi ya dawa kama vile Acyclovir, Famciclovir na Valacyclovir kwa ajili ya kuua virusi wanaosababisha ugonwja huu. Dawa hizi husaidia kupunguza maumivu, kuzuia madhara zaidi ya ugonjwa huu na kupunguza muda wa ugonjwa.
Dawa hizi hutolewa angalau saa 72 baada ya mgonjwa kuanza kuhisi maumivu na hali ya kuungua.Wataalamu wa afya hushauri mgonjwa kuanza kutumia dawa kabla  vipele/ michubuko kujitokeza.

Jamii ya dawa za corticosteroids kama vile prednisolone husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwa badhi ya wagonjwa. Dawa nyingine zinazofaa kutumika ni pamoja na jamii ya antihistamines kwa ajili ya kupunguza muwasho, dawa za maumivu, calamine lotion kwa ajili ya kupunguza muwasho. Aidha mgonjwa anashauriwa kupata mapumziko ya kutosha

Matarajio
Ugonjwa huu huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu kupona wenyewe, na unapo pona inakuwa nadra sana mtu aliyewahi kuugua kurudiwa tena na ugonjwa huu kwa mara ya pili. Licha ya kupona kwa kipindi hicho, uwezekano wa maumivu yanayotokana na ugonjwa huo kudumu kwa muda wa miezi kadhaa hadi kwa mmoja unakuwepo ambapo husababishwa na uharibifu katika neva za mwili.

Madhara
Mtu aliyeugua ugonjwa huu anakuwa katika hatari ya kupatwa na  a kupatwa na shambulio jingine la ugonjwa huu, maambukizi ya bakteria, upofu iwapo eneo la jicho litahusika, ukiziwi, maambukizi katika utando wa ubongo (encephalitis), uwepo wa vimelea kwenye damu (sepsis) au ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt Syndrome iwapo utahusisha neva za uso.

Kinga
Ni muhimu sana watu kuepuka kugusa eneo lenye vipele au michubuko kwa mtu mwenye mkanda wa jeshi au tetekuwanga iwapo mtu anayetaka kufanya hivyo hajawahi  au kupata chanjo ya tetekuwanga.
Ni vema kupata chanjo dhidi ya virus wa Varicella zoster kama inapatikana katika nchi au eneo ulilopo ili kuepukana na kupatwa na tetekuwanga au mkanda wa jeshi.
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni). Lakini kumbuka ya kwamba tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni:
Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa.

Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Sunday, March 25, 2018

Watu wengi tumekuwa hatufahamu utumiaji wa pipilipili, hasa pilipili mbuzi. Naomba leo tuangalie kwa uchache faida hizo za pilipili mbuzi.

1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.

2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari.

3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

4. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili.

5. Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)

7. Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

8. Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.


Na Ferdinand Shayo,arusha
Zoezi la Uokoaji na upelekaji wa Misaada katika Vijiji vya Sinya na Leremeta Vilivyopo Wilayani Longido Mkoani Arusha vilivyozingirwa na maji kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani humo,limeendelea baada ya kupokea Mitumbwi miwili kutoka katika shirika la Honeyguide Foundation  itakayosaidia kuvusha Vyakula pamoja na watu wenye mahitaji maalum.


Wakipokea mitumbwi hiyo,wananchi wa Vijiji hivyo Mwananchi Solomon Lazer amesema kuwa mitumbwi hiyo itakuwa msaada kwao nakuiomba serikali kuongeza nguvu,huku mmoja wa wafanyakazi wa Shirika lilitoa msaada huo akisema Zoezi la uokoaji linakwenda vizuri nakusema endapo mvua zitaendelea kunyesha kuna haja ya kupatiwa vifaa vya kisasa zaidi.


Kwa upande wake Afisa tawala wa Wilaya hii Thoba Nguvila ambaye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya maafa anasema mpaka sasa hawajapokea taarifa ya Vifo iliyosababishwa na mafuriko hayo.

Mbunge wa Jimbo hili Dokta Steven Kiruswa akiwashukuru wadau wanaoendelea kutoa msaada nakuwashauri wananchi hao kuhama endapo hali itazidi kuwa mbaya.

Mafuriko hayo yamesababishwa na Mvua zinanoendelea kunyesha Wilayani humo,huku kaya zaidi ya Mia tatu zikizingirwa na Maji na kusababisha kukosa baadhi ya huduma muhimu nakukosekana kwa mawasiliano.

Saturday, March 24, 2018


Habari za muda huu mdau wa Muungwana blog, naomba nisipoteze muda kwa kusema mambo yasiyokuwa na maana bali niende moja kwa moja kati mada yetu ya leo.

Virusi vya UKIMWI kwa kifupi vinaitwa VVU. Virusi vya UKIMWI ni virusi vinavyoleta upungufu wa kinga mwilini ( UKIMWI ). UKIMWI kwa upande mwingine ni ugonjwa ambao  pale dalili zake zinapoanza kuonekana wazi.

Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kwamba mtu mwenye virusi vya UKIMWI, bado anaweza kuwa mtu mwenye kuonekana na afya nzuri.Virusi vipo katika damu yake, lakini, havijaanza kuzishambulia chembechembe nyeupe.

Kwa upande mwingine, mtu mwenye UKIMWI tayari mwili wake ni umepungua kinga na unashambuliwa na magonjwa mbalimbali na tayari ameanza kuugua ugonjwa huu.


Kumekua na kesi mbalimbali za vifo sababu ya watu kumeza dawa kisha kujisahau na kunywa pombe.hii ni changamoto kubwa sana kwenye sekta ya afya..kawaida dawa yeyote anayopewa binadamu kutibu kitu fulani ni sumu na ikichanganywa na baadhi ya kemikali kama pombe huweza kudhuru na kuua kabisa hivyo leo naenda kuzungumzia dawa kadhaa amabazo ukiona umezimeza usiguse pombe kabisa.

Dawa za kutibu bacteria[antibiotics]; 
hizi ni dawa ambazo hutumika mara kwa mara kwenye jamii kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, kikohozi, kifua kikuu, madonda ya tumbo na kadhalika.matumizi ya dawa hizi na pombe huweza kuua. mfano fragile. isoniazid,grisiofulvin. lakini pia  na baadhi ya dawa za malaria kama quinine na dawa za ya mseto ya malaria ni hatari zikitumika na pombe.

Dawa za kuzuia damu kuganda[ant cougulant]; 
kuna dawa amabazo hupewa kwa wajawazito mara nyingi kulainisha damu ili isigande....sasa matumizi ya pombe hufanya dawa hizi kushindwa kufanya kazi na kusabisha damu kuganda hivyo kuziba mishipa ya damu ana kuleta kifo..mfano warfin

Dawa ya kupunguza mgandamizo wa mawazo[ant depressant];
pombe huingilia kazi ya dawa izi na kufanya dawa hizo ziongezeke kwenye damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyopangwa. hii humfanya mgonjwa alegee sana mfano amitriptyline.

Dawa za kutibu kisukari[ant diabetic]; 
dawa za kisukari hutengenezwa kwa ajili ya kushusha kiasi kikubwa cha sukari mwilini, sasa matumizi ya dawa hizi na pombe husababisha hali moja kitaalamu kama lactic acidosis... dalili ya hali hii ni maumivu ya misuli,tumbo kuuma na kusikia usingizi.hali hii isipodhibitiwa hospitali huua.mfano metformin vidonge.

Dawa za mafua na aleji;[ant histamine]
hizi dawa hutolewa kutibu mafua, miwasho ya ngozi na kikohozi lakini dawa hizi pia husababisha usingizi na uchovu kila zikitumika.pombe huongeza uzingizi huu na uchovu mara duvu na kufanya mtu ashindwe kazi. mfano promethazine maarufu kama fenigani  na chlropherinamine maleate maarufu kama piriton.

Dawa za magonjwa ya akili;
dawa za akili kama chlopromazine hutolewa kwa wagonjwa wa akili kupunguza dalili a magonjwa haya kwa kuwapa usingizi...sasa matumizi ya pombe huongeza usingizi huu maradufu na kuwafanya washindwe kupumua hivyo huweza kuleta kifo.

Dawa za kutibu madonda ya tumbo; 
mara nyingi madonda hutibiwi na mchahnganyiko wa dawa tatu kitaalamu kama triple therapy, sasa moja ya mchanganyiko huo kama cimetidine, metronidazole,scenidazole au tinidazole hazitakiwi kuchanganywa na pombe kabisa sababu ya madhara ambayo zimeonyesha.

Dawa za moyo;
hichi ni kikundi kikubwa cha dawa ambacho hutumika kutibu matatizo ya moyo. matumizi ya dawa hizi wakati mwingine huingilia mfumo wa kazi wa mwili na kusababisha kizunguzungu na kuanguka wakati wa kusimama mfano methyldopa, hydralazine na isosorbine mononitrate na dinitrate lakini pia matumizi ya pombe hupunguza uwezo wa dawa ya presha kitaalamu kama propanalol na kuzuia uwezo wake wa kufanya kazi.

Dawa za maumivu makali;
kuna dawa za maumivu kali sana ambazo hutolewa kwa wagonjwa wenye maumivu makali kama ya kansa, uzazi na maumivu ya ajali. pombe huongeza wingi wa dawa hizi kwenye mfumo wa damu na kusababisha overdose yaani dawa kua nyingi mwilini pale inapomezwa na pombe hata kama ulimeza dozo sahihi.mfano morphine,pethidine, codeine,meperidine...hali hii huleta kifo mara nyingi kwani wasanii wakubwa kama michael jackson na prince waliuawa na hali hizi.

Dawa za usingizi;
dawa za usingizi kama valium hutumika kwa wagonjwa wenye kushindwa kupata usingizi na wakati mwingine kwenye chumba cha upasuaji. dawa hizi huleta usingizi mkali...matumizi ya dawa hizi na pombe huongeza usingizi huu, hupunguza mapigo ya moyo, hupunguza uwezo wa kupumua, kupoteza fahamu na kifo lakini pia dawa za kifafa kama phenytoin  hupunguzwa uwezo wake na pombe na kushindwa kuzuia uwezo wake wa kuzuia degedege za kifafa.

Mwisho;
kutaja dawa hizi haimaanishi kwamba dawa zote ambazo sijataja hapa zinafaa kunywa na pombe, hapana..kuna dawa bado zinafanyiwa utafiti kama zina madhara zikitumika na pombe lakini pia ni vizuri kujenga tabia ya kutokunywa pombe kabisa kama uko kwenye dozi ya ugonjwa wowote na hata kama una ugonjwa ambao unataka kumeza vidonge maisha yote kama kisukari, presha, ukimwi, kifafa na kadhalika basi ni vizuri ukaacha pombe kabisa.