Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Showing posts with label Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Kitaifa. Show all posts

Saturday, February 29, 2020

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi  wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020.

 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi  wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kuhudhuria Misa ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay  jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akiongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli, akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi  waliposhiriki  Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020.

MUUNGWANA BLOG














Friday, February 28, 2020

Bernard MembeBernard Membe aligombea tiketi ya urais ndani ya CCM 2015 mchakato ambao uliisha kwa John Magufuli kupata ridhaa ya chama
.
Chama tawala nchini Tanzania CCM kimemfukuza uanachama aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bernard Membe.
Membe alikuwa akikabiliwa na tuhuma za maadili pamoja na viongozi wengine waandamizi wengine wawili makatibu wakuu wa zamani Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, ambao wao hawajafukuzwa.
Makamba amesamehewa, huku Kinana akionywa kwa karipio.
Akisoma taarifa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM hii leo, Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole amedai kuwa mwenendo wa Membe umekuwa si wa kuridhisha toka mwaka 2014.
"Kamati Kuu imeazimia kwa kauli moja kwamba Bernard Membe afukuzwe uanachama wa CCM. Uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonesha mwenendo wake kutoka mwaka 2014 ambako katika chama amewahi kupata adhabu nyingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha," ameeleza Polepole.

Kwa mujibu wa Polepole, uongozi wa chama hicho umeazimia kumsamehe Mzee Makamba kwa kuwa: "...amekuwa mtu muungwana na mnyenyekevu kwa mamlaka ya chama. Na ameomba asamehewe kwa barua."
"Mzee Kinana anapewa adhabu ya karipio kwa mujibu wa kanuni... Atakuwa katika hali ya matazamio kwa mda wa miezi 18 ili kumsaidia katika jitihada za kujirekebisha. Hatakuwa na haki ya kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama, japo ataruhusiwa kupiga kura kama atakuwa na dhamana hiyo," ameeleza Polepole.
'Membeatoa neno'
"Watanzania wenzangu nimepata habari ya kufukuzwa kwangu kutoka kwenye Chama changu cha CCM. Simu zinamiminika hadi nashindwa kuzijibu. Tulieni! Nitapata muda wa kuongea na wote muda si mrefu!"

BBC

















Thursday, February 27, 2020

Tanzania: Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na wa haki, hatukiuki haki za binaadamu ni propaganda tu
Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi imeihakikishia dunia kwamba uchaguzi mkuu ujao, utakuwa huru na wa haki.
Kabudi ameyasema hayo kwenye hafla ya kukaribisha mwaka mpya ambapo amekariri ahadi ya Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo aliyoitoa akizihakikishia jumuiya za kimataifa kuhusiana na suala hilo. Akizungumza na mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa jijini Dar es Salaam Kabudi amesema: “Mwaka huu Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wa sita tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa na uchaguzi huo utakuwa wa uwazi, huru na wa haki.” Ameongeza kwamba, Tanzania itawaalika waangalizi wa uchaguzi watakaotaka kushuhudia namna Watanzania wanavyotekeleza moja ya haki zao za msingi katika suala la kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wao.
 
Uchaguzi tarajiwa nchini Tanzania ambao wapinzani wana wasi wasi nao na hivyo kuitaka serikali iifanyie mabadiliko tume ya uchaguzi 
Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Tanzania ametoa kauli hiyo katika hali ambayo, kilio kikubwa cha vyama vya siasa ni kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, vikisema kuwa mfumo wa sasa wa tume iliopo unawapa mamlaka wakurugenzi kusimamia uchaguzi wakati ni wateule wa Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala cha CCM. Aidha akihutubia kikao cha 43 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi Waziri Kabudi pia alisema serikali ya Tanzania inaheshimu na itaendelea kuheshimu haki zote za binadamu zikiwemo za kisiasa na kwamba sheria zilizotungwa na bunge la nchi hiyo zina lengo jema la kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa Taifa lenye amani, umoja na utulivu. Alizidi kufafanua kuwa, madai yanayotolewa dhidi ya Tanzania kuwa inakiuka haki za binadamu ni propaganda zinatokana na hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, dawa za kulevya, uzembe katika ofisi za umma pamoja na hatua zinazochukuliwa kulinda rasilimali za Taifa.

Parstoday swahili

  


Na Amiri kilagalila,Njombe

Naibu waziri wa kilimo nchini Omary Mgumba amesema,Tanzania bado ina hali nzuri ya uwepo wa chakula kwa kuwa mpaka leo taifa lina utoshelevu wa chakula kwa zaidi ya asilimia 119.

Mgumba ametoa taarifa hiyo mkoani Njombe wakati wa kongamano la vijana katika kilimo mwaka 2020 lililowakutanisha takribani vijana 200 wa mikoa ya Njombe,Iringa na Ruvuma kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujishughulisha na kilimo chenye tija nchini.


"leo hii mpaka sasa kama taifa naomba niwaambie watanzania na vijana mlioko hapa tuna utoshelevu wa chakula zaidi ya asilimia mia moja na kumi na tisa"alisema Mgumba

Naibu waziri Mgumba amewaeleza vijana na watanzania kuwa kilimo kimeendelea kukuwa na kutoa mchango kwa uchumi wa nchi katika maeneo mbali mbali kwa kuwa takwimu zilizopo za mwaka 2018 zinaonyesha sekta ya kilimo inachangia asilimia 28.2 ya pato la taifa na sekta ndogo ya kilimo mazao inachangia zaidi ya asilimia 16.2 huku watanzania wanaoshiriki katika sekta ya kilimo wakiwa zaidi ya asilimia 58 na kusababisha kilimo kuwa na mchango mkubwa katika ajira.

Mgumba amesema wizara ya kilimo imeendelea kupata mafanikio makubwa kisera na taasisi ikiwemo kuanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja,na kusababisha ongezeko kutoka tani laki tatu na mbili mpaka kufikia tani laki nne na stini kwa mwaka.


Vile vile ametoa wito kwa vjana kujihusisha katika kilimo kwa kuwa nchi ya Tanzania ina eneo kubwa linalofaa kwa ajili ya kilimo.

"Nchi yetu ina eneo linalofaa kwa kilimo,ambalo linakadiliwa kuwa zaidi ya hekta milioni 44 linafaa kwa kilimo na mifugo hiyo ni fursa vijana mnatakiwa kuitumia,na kati ya hizo hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji"alisema Waziri Mgumba

Aidha amezitaka halmashauri zote nchini kusimamia kikamilifu mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake vijana na walemavu,pamoja na kutoa mikopo ya kueleweka kwa vijana ili waweze kuwekeza kikamilifu katika kilimo. 
Muungwana Blog

Friday, February 14, 2020



Msemaji wa Familia ya Marehemu Idd Simba, Ahmed Simba, amesema kuwa mwili wa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, utapumzishwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni, lengo likiwa ni kumpumzisha mahali ambapo Baba zake wote walizikwa.

"Sasa hivi tuko hapa Msasani nyumbani kwake, tutaondoka na mwili mpaka Msikiti wa Manyema utaswaliwa pale kisha tutaelekea Magomeni na atazikwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu, anazikwa kule kwa sababu Baba zake wote wamezikwa hapo" amesema Ahmad.

Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara Iddi Simba, alifariki Dunia siku ya jana Februari 13, 2020, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo alihudumu nafasi yake kati ya mwaka 2001 na 2002.

Muungwana Blog

Thursday, July 4, 2019

Unene kwa sasa umekuwa moja ya kisababishi cha ugonjwa wa saratani nchini Uingereza kuliko uvutaji sigara, taasisi ya saratani nchini humo imeeleza.

 Mtu mwenye uzito mkubwa

Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani imesema, saratani ya ini, utumbo, ovari zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uzito mkubwa kuliko kuvuta tumbaku.
Inasema mamilioni wako hatarini kuugua saratani kwasababu ya uzito na kuwa watu wenye uzito mkubwa huzidi idadi ya wavuta sigara kwa wastani wa watu wawili kwa mmoja.
Lakini matangazo ya mabango ya kampeni kuhusu unene na hatari ya kupata saratani yamekosolewa kwa kujeli watu wanene.
Maangazo ya tahadhari kuhusu saratani
Si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kushutumiwa kukejeli watu wanene. Wengine wakisema kuweka tangazo hilo kama vile matangazo ya pakiti za sigara si jambo zuri.
Lakini taasisi hiyo imejitetea kuwa haiwalaumu watu walio na uzito mkubwa.
Wala haisemi kuwa uvutaji wa sigara ni sawa na kuwa na uzito mkubwa wakihusisha na hatari ya kupata saratani. Vyote viwili vinahatarisha afya.
Lakini taasisi hiyo imesema uzito mkubwa au unene husababisha wagonjwa wa saratani 22,800 kila mwaka, ukilinganisha na uvutaji wa sigara unasababisha watu 54,300 kuugua saratani.
Lakini wakati idadi ya wavuta sigara ikipungua, idadi ya watu wenye uzito mkubwa inaongezeka, suala la kushughulikiwa.

Wakati uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani ukibainishwa vyema, kibaiolojia bado haijaeleweka vyema
Kuwa na uzito mkubwa au mnene haimaanishi kuwa lazima mtu huyo apate saratani, lakini mtu huyo anaongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.
Ongezeko la hatari hujitokeza zaidi iwapo mtu ataongezeka uzito zaidi.
Kwa mujibu wa watafiti saratani mbalimbali zinahusishwa na uzito mkubwa: Saratani ya matiti kwa wanawake waliokoma hedhi (menopause), utumbo, ini, saratani ya damu, saratani ya ubongo, koo, tezi, figo, kongosho, tumbo,ovari.
Uhusiano kati ya unene na saratani ni kwa watu wakubwa pekee, ingawa kwa watoto wadogo ni muhimu kuwa kwenye tahadhari pia.

BBC

Wednesday, July 3, 2019

   Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemtumia ujumbe maalumu Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli unaoelezea msimamo wa Serikali yake kuhusu kukerwa na matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa jimbo la Starehe, Charles  Njagua Kanyi maarufu kwa jina la Jaguar.

 Ujumbe huo wa maandishi umewasilishwa leo (Jumanne, Julai 02, 2019) na Balozi wa Kenya nchini, Dany Kazungu na kupokelewa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli, ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. 

Akipokea taarifa hiyo Waziri Mkuu amesema Watanzania wamefurahishwa na hatua mbalimbali zilizochukulia na Serikali ya Kenya dhidi ya mbunge huyo zinazodhihirisha kwamba matamshi hayo hayakuwa msimamo wa Serikali ya Kenya wala wananchi wake bali  ulikuwa ni msimamo  binafsi wa mbunge huyo.

Amesema siku zote Watanzania na Wakenya wamekuwa huru kuishi na kufanya kazi au biashara katika nchi za Afrika ya Mashariki na pale yalipotokea matatizo au kutokukubaliana serikali husika zilikaa mezani na kumaliza tofauti hizo.

"Uhusiano kati ya Kenya na Tanzania ni wa karibu mno na wa kidugu kwani kuna baadhi ya makabila yapo katika nchi mbili hizi kama vile Wamasai na Wakurya na  Wajaluo  hivyo ushirkiano katika masuala ya mbalimbali yakiwemo ya  kabiashara na ya kijamii haukwepeki."

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi na wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kujiepusha na kauli zenye viashiria vya  kujenga chuki, uhasama na migongano miongoni mwa wananchi kwani  kauli hizo zisipodhibitiwa mapema zinaweza kusabisha hofu na kutokuelewana miongoni mwao.

Waziri Mkuu  ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo na ndugu zao wa Kenya na wageni wote kutoka nchi za Afrika ya Mashariki na duniani kwa ujumla ambao wapo nchini wakifanya shughuli mbalimbali kwa mujibu wa sheria za nchi. 

“Mambo yetu yote katika nchi za Afrika ya Mashariki  hasa ya biashara na ya  kiuchumi kwa ujumla yataenda vizuri endapo  tutalinda na kudumisha amani, bila amani tutaogopana na tutashindwa kabisa  kushirikiana”, amesisitiza Mheshimiwa Majaliwa.

Waziri Mkuu  ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania kamwe ahaitaruhusu wala kufumbia macho kauli au vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uchochezi  dhidi ya nchi jirani  ili na kulinda na kuunga mkono juhudi mbalimbali za ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi zinazofanywa na viongozi  wakuu wa Mataifa ya Afrika.

Kwa upande wake Balozi Kazungu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni jijini Dodoma iliyowataka Watanzania kuwa watulivu na wayachukulie matamshi ya Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya, Njagua kuwa ni msimamo wake binafsi na siyo  msimamo wa Wakenya na Serikali yao.

Balozi Njagua mesema Msimamo wa Rais Kenyatta siku zote umekuwa ni kuwapokea na kuwakubali ndugu zao  wote wanaotoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioamua kuishi au kufanya biashara nchini Kenya.

Mwanzoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya Njagua alitoa matamshi ya kichochezi akiwataka raia wa kigeni kutoka Mataifa mbalimbali wanaofanya shughuli za kibiashara nchini Kenya wakiwemo Watanzania waondoke ndani ya muda wa saa 24.
CCM BLOG

Tuesday, July 2, 2019










 

PICHANI MCHUNGAJI KURWA AKIWA NA MCHUMBA WAKE BI ABIGAEL SHAMIM HAMAD MSUYA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA  SHAHADA YA KWANZA YA HABARI KATIKA CHUO KIKUU CHA  IRINGA (ZAMANI KIKIJULIKANA KWA JINA LA TUMAINI UNIVERSITY)

KWA MAWASILIANO WASILIANA KWA NAMBA 0713 654432

Rais wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza wananchi Chato mkoani Geita kwa kuitikia wito wa Serikali ya Tanzania kuongeza kwenye uzalishaji mali, hatua iliyochangia wilaya hiyo kupiga hatua za maendeleo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai Mosi, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli ametoa pongezi hizo wakati akiwasalimia wananchi hao katika eneo la Njiapanda, muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Chato akitokea Dar es Salaam.
Katika taarifa hiyo, imeeleza kuwa akiwa angani Rais Magufuli amefurahishwa kuona namna wananchi wa Chato walivyochangamka kimaendeleo kwa kujenga nyumba za kuishi za kisasa, majengo ya biashara, majengo ya huduma za jamii na mashamba ya mazao mbalimbali.
“Nawapongeza wakazi wa Chato, mnachapa kazi kwelikweli na maendeleo yanaonekana. Chato inabadilika, nilishasema asiyefanya kazi na asile, tuendelee kushikamana,” amesema Rais Magufuli.
Mbali na hilo, Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kushikamana na kutobaguana ili kulijenga Taifa kwa pamoja.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli yupo katika Kijiji cha Mlimani wilayani Chato kwa ajili ya mapumziko.
chanzo:ccm blog