Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Friday, February 14, 2020



Kivumbi cha Ligi Kuu ya England kinaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa, ambapo Wolves watakuwa nyumbani kuwakaribisha Leicester City.

Kocha wa Leicester, -Brendan Rodgers anasema kiungo mkabaji wake Wilfred Ndidi hana uhakika kama atakuwa sehemu ya kikosi chake kutokana na upasuaji wa goti aliofanyiwa katika siku za hivi karibuni huku Ryan Bennett akikosekana kutokana na vipengele vya mkataba wake wa mkopo akitokea Wolves.

Kwa upande wa Wolves, wanaimani mshambuliaji wao mweye nguvu nyingi Adama Traore atakuwa sehemu ya kikosi cha usiku wa leo licha ya maumivu ya bega aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Manchester United, lakini watamkosa Ruben Vinagre anayesumbuliwa na tatizo la misuli.

Muungwana Blog

Thursday, July 4, 2019

Klabu ya Chelsea imemtangaza Frank Lampard kuwa kocha wake mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuionoa klabu hiyo. 

 Lampard

Lampard, 41, anaondoka katika klabu anayoinoa kwa sasa Derby County kuchukua hatamu katika klabu ya Chelsea ambayo alikuwa ni mchezaji kinara kwa miaka 13.
Anarithi nafasi iliyoachwa wazi na Maurizio Sarri, ambaye ameondoka mwezi uliopita kwenda kujiunga na miamba ya Italia klabu ya Juventus.

Lampard ameiwakilisha Chelsea katika mechi 648 Chelsea, na kunyakua mataji 11 na timu hiyo.
Hata hivyo anaenda kuingoza Chelsea katika kipindi ambacho wamepigwa marufuku ya kufanya usajili katika madirisha mawili na chombo kinachosiamamia mchezo huo FIFA, lakini tayari wameshakata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa masuala ya michezo.
 Lampard
"Ninafuraha isiyo kifani kurejea Chelsea kama kocha mkuu," amesema Lampard.
"Kila mtu anajua mapenzi yangu kwa klabu hii na historia yangu hapa. Lakini, malengo yangu kwa sasa ni juu ya kazi hii mpya na kujipanga kwa msimu ujao."
"Nipo hapa kufanya kazi kwa bidii, na natamani kazi ianze mara moja."
Uteuzi wa Lampard unakuja siku tisa tangu klabu ya Derby ilipomruhusu kufanya mazungumzo na Chelsea. na siku 18 toka Sarri alipoondoka klabuni hapo.
Lampard anakuwa kocha wa 10 kuifundisha Chelsea toka klabu hiyo iliponunuliwa na Roman Abramovich 2003.
Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia amesema Lampard amedhihirisha uwezo wake kwa kuiongoza Derby kukaribia kupanda Ligi ya Primia.
"Ni moja kati ya makocha vijana wenye uwezo mkubwa kwa sasa," amesema na kuongeza, "Inatupa faraja kubwa kumkaribisha tena Chelsea. Frank anaijua vyema klabu hii.
Lampard ameondoka Derby na makocha wasaidizi wake wawili, Jody Morris na Chris Jones. Petr Cech ambaye alikuwa ni kipa wakati Lampard akiwa kiungo Chelsea ataungana nao akiwa kama Mkurugenzi wa Ufundi.

Safari ya Lampard Chelsea

Embedded video
Lampard alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya West Ham kwa dau la pauni milioni 11 mwaka 2001.
Ameshinda taji la Klabu Bingwa Ulaya, Ligi ya Europa, na mataji matatu ya Primia, makombe manne ya FA na mawili ya Ligi.
Chelsea walichukua taji lao la kwanza la Primia kwa miaka 50 msimu wa 2004-05 na Lampard alifunga magoli 13 katika msimu huo, ikiwemo magoli yote katika ushindi wa 2-0 ambao ndio uliipa Chelsea ubingwa.
Akiwa na magoli 211 Lampard ndiye kinara wa magoli wa muda wote kwenye klabu ya Chelsea.
Lampard aliondoka Stamford Bridge ambapo ndiyo maskani ya Chelsea mwaka 2014.
Kwanza alienda Manchester City kwa muda mfupi ambapo alicheza mechi 32 na kufunga magoli sita.
Baada ya hapo akajiunga na New York City ya Marekani na kucheza mchezo wake wa kwanza Augosti 2015.
Alitangaza kustaafu baada ya miaka 21 ya kusakata kandada mwaka 2017.
Lampard amechezea timu ya taifa ya England michezo 106 na kufunga magoli 29.

BBC

Wednesday, July 3, 2019

Ibrahim Ajibu amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu ya Simba akitokea Yanga. Ajibu msimu wa 2018-19 alikuwa kwenye ubora wake baada ya kutoa jumla ya pasi za mabao 17 na kufunga mabao sita. "Safari ya mtoto kuishi mbali na nyumbani imefikia ukingoni. Ibrahim Ajibu ameamua kufanya maamuzi sahihi ya kurudi nyumbani Msimbazi, ndio amerudi na amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza na kuwapa furaha Wanasimba. Karibu nyumbani Ajibu," imeeleza taarifa kutoka Klabu hiyo.

Tuesday, July 2, 2019










 

PICHANI MCHUNGAJI KURWA AKIWA NA MCHUMBA WAKE BI ABIGAEL SHAMIM HAMAD MSUYA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA  SHAHADA YA KWANZA YA HABARI KATIKA CHUO KIKUU CHA  IRINGA (ZAMANI KIKIJULIKANA KWA JINA LA TUMAINI UNIVERSITY)

KWA MAWASILIANO WASILIANA KWA NAMBA 0713 654432

Thursday, August 23, 2018

Mo Salah

Haki miliki ya pichaREUTERS
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Liverpool Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 26, na mshambulaiji wa Tottenham na England Harry Kane, wa miaka 25, wote walikataa nafasi ya kujiunga na Real Madrid baada ya timu hiyo kuu ya Uhispania kumuuza Mchezaji raia wa Ureno Cristiano Ronaldo, kwa timu ya Juventus. (El Pais - in Spanish)
Mashabiki wa Manchester United wamelipia bango lililo na ujumbe wa kutaka naibu mwenyekiti mtendaji Ed Woodward aondoke na litakalo peperushwa uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Burnley Septemba 2. (Mail)
Mlinzi wa Tottenham na England Danny Rose wanaweza kuhamishwa kwenda timu katika Ligue 1 Paris St-Germain. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 alikataa uhamisho wa mkopo kwenda katika ligi ya Ujerumani Bundesliga timu ya Schalke msimu huu wa joto. (Evening Standard)
Lakini Tottenham bado haijapokea ombi lolote la Rose, wala la mlinzi wa Ublegiji Toby Alderweireld, mwenye umri wa miaka 29. (Talksport)
Tottenham itashauriana na mashabiki kuhusu eneo la kuchezea mechi yake ya awamu ya tatu ya kuwania taji la Carabao baada ya kuthibitishwa wiki hii kwamba hawatoweza kuutumia uwanja wa Wembley. (Telegraph)
Keylor NavasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKeylor Navas
Manchester City inatafakari uhamisho wa dharura wa mkopo wa kipa wa Real Madrid Keylor Navas, mwenye umri wa miaka 31, baada ya Claudio Bravo, mwenye umri wa miaka 35 kujeruhiwa. (AS - in Spanish)
Mchezaji wa kiungo cha kati Phil Foden, mwenye umri wa miaka 18, huenda anatarajiwa kuitwa England huku Meneja Gareth Southgate akiripotiwa kuzungumza na Meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuhusu anavyoendelea (Sun)
Liverpool na Borussia Dortmund zinafanya mazungumzo kuhusu mkataba wa kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ubelgiji Divock Origi, mwenye umri wa miaka 23. (ESPN)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Ruben Loftus-Cheek,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa kiungo cha kati wa England Ruben Loftus-Cheek,
Chelsea inahitaji kumshawishi mchezaji wa kiungo cha kati wa England Ruben Loftus-Cheek, kuwa ana umuhimu mkubwa kwao ili aweze kuendelea kusalia Stamford Bridge. (Mirror)
Winga wa Chelsea Lucas Piazon huenda anaelekea katika timu mpya kwenye Ligue 1 Reims kwa mkopo. Mchezaji huyo alishiriki mechi tatu kwa timu ya the Blues tangu kujiunga nayo mnamo 2011 na kuwa kuichezea Fulham kwa mkopo kwa misimu miwili iliyopita. (Sun)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, atakutana na wamiliki wa timu ya Bordeaux leo Alhamisi khusu kuwa meneja mpya. (Mirror)
Cristiano RonaldoHaki miliki ya pichaREUTERS
Mchezaji wa kiungo cha meble wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo, amefichua kwamba Sir Alex Ferguson alimwambia apunguze chenga alizopiga akiwa Manchester United. (DAZN, via Manchester Evening News)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea, West Ham na timu ya taifa ya England Carlton Cole, mwenye umri wa miaka 34, ametangazwa kufilisika. (Sun)
Aliyekuwa refa katika ligi ya England Bobby Madley anatarajiwa kuhamia kwenda Norway baada ya kujiuzulu wadhifa wake. (Mail)
BBC

Msemaji wa kloabu ya Simba, Haji Manara, amewajia juu watu ambao wanabeza matokeo ya ushindi wa bao 1-0 walioupata usiku wa jana kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika ushindi huo bao hilo pekee la Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya dakika ya pili kipindi cha kwanza. Hata hivyo mashabiki wengi mitandaoni wamekuwa wakiubeza ushindi huo ukionekana ni mdogo sana tofauti na matarajio ya wengi ambapo ukilinganisha na ukubwa wa kikosi cha Simba kwa sasa.

kutokana na maneno hayo Manara kupitioa mtandao wa Instagram ameamuakuwajibu kwa kuandika:

Salaam 
wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!!
Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons!!


Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu..hisabati 3×3 ni tisa tu..hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane.

\
Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!


Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!


Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!


Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!


Hapo ndio Haji naonekana mtata..aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu.


Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba..kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya team toka kwa makocha.


Ni lazma mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu.


Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa cc..na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi..unachukua muda kdogo..


Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa draft au Chess ya kina kasparov na karpov..inahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake..vinginevyo ni kufanya uchale tu 
Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya..usifate mkumbo wa mitandaoni

Thursday, August 16, 2018

Saul na Koke wakisherehekea

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSaul na Koke walifungia Atletico Madrid muda wa ziada
Real Madrid walianza maisha bila mshambuliaji wao nyota wa zamani Cristiano Ronaldo na meneja Zinedine Zidane kwa kushindwa 4-2 katika debi ya kombe la Super Cup ya Uefa na wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid.
Mabao mawili ya muda wa ziada kutoka kwa Koke na Saul yaliwasaidia Atletico kushinda mechi hiyo iliyokuwa imemalizika 2-2 katika muda wa kawaida.
Ilikuwa mechi yao ya kwanza ya ushindani tangu Ronaldo alipohamia Juventus ya Italia kwa £99m majira ya joto na pia baada ya kuondoka kwa Zidane ambaye nafasi yake ilichukuliwa na aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya Uhispania Julen Lopetegui.
Atletico walishinda Super Cup kwa mara yao ya tatu na kuhakikisha kwamba hawajawahi kushindwa katika mechi za Super Cup kwani wameshiriki mara tatu.
Nyota wa zamani wa Chelsea Diego Costa alikuwa amewafungia Atletico mabao mawili muda wa kawaida, la kwanza sekunde 49 baada ya mechi kuanza na la pili kipindi cha pili.
Gareth Bale alikuwa amemuwezesha Karim Benzema kufunga bao la kwanza la Real kwa kichwa kabla ya nahodha wao Sergio Ramos kufunga penalti na kuwaweka kifua mbele 2-1 kwa muda baada ya Juanfran kuadhibiwa kwa kunawa mpira eneo la hatari.
Beki kamili Marcelo alipoteza nafasi ya kuwafungia Real bao la ushindi sekunde za mwisho za muda wa kawaida mechi hiyo, na kuwapotezea mabingwa hao wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya nafasi ya kuwa klabu ya kwanza ya kushinda kombe hilo mara tatu mtawalia.
Atletico Madrid's SaulHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSaul akisherehekea kufunga, nyuma yake ni Diego Costa
Mwaka jana, Real waliibuka washindi kwa kuwalaza Manchester United 2-1 na mwaka uliotangulia walikuwa wamewalaza Sevilla 3-2.
Ilikuwa ni mara ya nne katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa Super Cup ya Uefa kushindaniwa na klabu mbili za Uhispania, lakini mara ya kwanza kwa klabu kutoka jiji moja kukutana.
Maisha bila Ronaldo
Gareth BaleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGareth Bale alifunga dhidi ya Liverpool na kuwasaidia Real Madrid kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei
Real Madrid walipokuwa wanaonekana kutatizika kuyazoea maisha bila Ronaldo, Atletico ndio walioonyesha ustadi wa hali ya juu.
Hali kwamba Real hawakumnunua mchezaji anayeonekana kutazamiwa kujaza moja kwa moja pengo lililoachwa na Ronaldo inawatia wasiwasi mashabiki wa Real lakini bado kuna washambuliaji wenye uzoefu mkubwa.
Marco Asensio na Bale ni wachezaji wawili ambao watatumai kufaidi kutokana na kuondoka kwa Ronaldo.

Takwimu muhimu

  • Atletico Madrid ndio walishindi wa kwanza wa Europa League walioshinda Uefa Super Cup tangu walipofanya hivyo dhidi ya Chelsea mwaka 2012.
  • Real Madrid walifungwa mabao manne na zaidi katika mechi kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2015 dhidi ya Barcelona katika La Liga wakiwa chini ya Rafael Benitez - hawakuwahi kufungwa hivyo chini ya Zidane.
  • Lopetegui ndiye meneja wa kwanza wa Real Madrid kufungwa maba manne au zaidi katika mechi yake ya kwanza ya ushindani na klabu hiyo tangu Michael Keeping dhidi ya Celta Vigo mnamo Februari1948.
  • Bao la Costa la Atletico Madrid sekunde ya 49 ndilo la kasi zaidi kuwahi kufungwa katika mechi ya UEFA Super Cup.
  • Alifungia klabu hiyo mabao mawili mechi moja kwa mara ya kwanza tangu kurejea Atletico Madrid, mwisho alifanya hivyo akiwa na Chelsea dhidi ya Southampton katika Ligi ya Premia mnamo Aprili 2017.
  • Karim Benzema alifunga dhidi ya Atletico Madrid kwa mara ya kwanza tangu Oktoba 2015 katika mechi ya La Liga - alikuwa amekwenda mechi nane bila kuwafunga.
  • Ramos sasa amefunga mabao matano dhidi ya Atletico Madrid - ni dhidi ya Sevilla pekee Ramos (sita) amefungia Real Madrid mabao mengi zaidi. Mabao yote mawili ameyafunga katika michuano ya kushindania vikombe.


BBC

Monday, April 23, 2018

Mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya Difaa El Jadid, Simon Msuva ameendelea kung’ara kwenye ligi kuu ya Morocco.

Mshambuliaji huyo jana (Jumapili) amefanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao moja kati ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata katika ligi kuu dhidi ya Raja Casablanca.

Msuva alifanikiwa kufunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 76 ya mchezo huo huku goli la kwanza likifungwa na Ahaddad H dakika ya 45. Wakati huo huo bao la Raja Casablanca lilifungwa wa njia ya penalti na Iajour M dakika ya 41 ya mchezo huo.

Mchezo huo uliocheza kwenye uwanja wa Stade Ben Ahmed El Abdi (El Jadida (Mazghan)).
Mara baada ya meneja wa Arsenal, Arsene Wenger siku ya Ijumaa kutangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu, Jumapili hii amewatupia lawama mashabiki kwakukosa umoja hali inayopelekea kuaribu taswira ya timu hiyo.

Kwa mara ya kwanza jana siku ya Jumapili, Wenger ameeleza sababu ya maamuzi yake ya kuachia ngazi ambapo amesema kuwa hakuchoka kuifundisha timu hiyo bali aliamua kufanya hivyo baada ya kuona baadhi ya mashabiki wakiandamana wakimuhitaji aondoke jambo ambalo limekuwa likimuumiza na kuvuruga taswira ya klabu.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68 hapo jana aliamua kuweka wazi sababu zilizomfanya kumaliza ukomo wa utawala wake wa miaka 22 ndani ya klabu ya Arsenal.

Sikuchoka kuifundisha Arsenal, wenga ameyasema hayo mara baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1 dhidi ya West Ham.

Sikuchoka kuifundisha Arsenal, binafsi ninaamini hii klabu inaheshima dunia nzima, ni zaidi hata ya Uingereza. Mashabiki wetu hawana umoja na hivyo kujenga taswira mbaya kwa klabu jambo ambalo linaniuma, taswira hii tunayo ijengea timu yetu siyo kitu ambacho mimi nakipenda.

Sifanyi hivi kwa kutengeneza vichwa vya habari vya kijinga, nahitaji kile ninachokifikiria kwenye klabu yangu kifanikiwe na hicho ndiyo kitu muhimu pekee  kwangu.

Nimesafiri sana na klabu hii na kujionea namna inavyoheshimika duniani, tunaangushwa kwa namna tunavyocheza, kwa namna ya tabia zetu zilivyo kwa sasa na vile tunavyo wafanya watu watuchukulie hivyo nahitaji kuondoka na kuiacha taswira ya timu ikiwa kwenye muonekano mzuri. Ijapokuwa kuna fedha nyingi kwenye mchezo zaidi hata ya matokeo ya uwanjani.

Wenger amejiunga na Arsenal mwaka 1996  akiwa ni meneja wa pili kutoka nje ya Uingereza au Ireland kupata nafasi ya kuzinoa timu za nchi hiyo na kuisaidia kwa kiwango kikubwa mabadiliko ya soka Epl.

Akifanikiwa kutwaa taji la ligi akiwa na Arsenal mwaka 1998, 2002 na 2004 bila kufungwa ‘Invincibles’ msimu mzima huku ikifanikiwa kuvutia mashabiki.

Wenger amesema kuwa mchezo ni zaidi ya kushinda au kufungwa kiasi kwamba anadhani kubwa kwake ni kuhakikisha anatanua wigo kwa timu hiyo kwa watoto wanaopenda soka Afrika, China,  America. na lengo lake kubwa ni kuzalisha vipaji kwa vijana wadogo.

Mfaransa huyo amesema kuwa kuna Arsene Wenger mmoja tu uwanja wa Emirates. Ninajiskia furaha pale mashabiki wanapokuwa na furaha.

Najaribu kuvutia miundombinu ya klabu na maendeleo ya mchezaji mmoja mmoja na kuwekeza katika aina ya uchezaji wetu. Ninaamini nitaiyacha timu hii ikiwa na mipango imara na hiyo ilikuwa lengo langu lakini pia kumuachia nafasi mrithi wangu atakae kuja kuchukua nafasi hii na pengine kufanya vema zaidi yangu mimi kwa miaka 20 ijayo, hilo ndilo tarajio langu.

Nafasi kubwa ya Arsenal iliyopo kwa sasa ni michuano ya Europa League hatua ya nusu fainali dhidi ya Atletico Madrid siku ya Alhamisi. Kwa kuwa sasa Arsenal ipo nje ya ‘top four’ kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza ikitwaa ubingwa huo itapata nmafasi ya kushiriki Champions League.

Nimetumia miaka yangu 22 ndani ya klabu na niliipatia miaka yenye mafanikio, nilikuja hapa nikiwa na miaka 46 na nilifanya kazi kwa siku saba bila hata kupumzika ni siyo sita bali siku saba kwa wiki nzima. Najua nitapitia wakati mgumu kwenye maisha yangu baada ya kuachana na timu hii lakini nawashukuru sana na nasema kwaherini.

Wenger mpaka sasa hajatangaza kama atakwenda kujiunga na klabu gani licha ya kuwa huwenda asifundishe Uingereza.
TIMU ya Singida United imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Haukuwa ushindi mwepesi kwa Singida, kwani ililazimika kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kumaliza kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kabla ya kwenda kushinda 2-1 katika dakika 30 za nyongeza.

JKT Tanzania ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wake hatari, Hassan Matalema dakika ya 38, kabla ya Tafadzwa Kutinyu kuisawazishia Singida United dakika ya 54.

Mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 na mshambuliaji kutoka Zimbabwe, Kutinyu akaifungia bao la ushindin Singida United dakika ya 98.

Singida United itacheza fainali Juni 2, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha dhidi ya Mtibwa Sugar iliyoitoa Stand United kwa kuwachapa 2-0 mjini Shinyanga Ijumaa.

Bingwa pamoja na kupata Sh. Milioni 50, pia ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mshindi wa pili atapata Milioni 10, wakati Mchezaji Bora atazawadiwa Sh. Milioni 1 sawa na Kipa Bora, Mfungaji Bora, huku Mchezaji Bora wa Fainali akiondoka na Sh. 500,000.

Saturday, April 21, 2018

kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogb

Image captionkiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba
Wazo la kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba kurudi Juventus ni 'ndoto' kulingana na afisa mkuu wa klabu hiyo Giuseppe Marotta. (Mediaset, via Manchester Evening News)
Paris St-Germain wamewasiliana na ajenti Mino Raiola kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba. (ESPN)
Riyad MahrezHaki miliki ya pichaEMPICS
Image captionRiyad Mahrez
United Itahitaji kulipwa £140m iwapo Pogba anataka kuondoka Old Trafford mwisho wa msimu huu miaka miwili baada ya kulipa dau lililovunja rekodi ya uhamisho la £89m ili kumsajili. (Mail)
Manchester City bado inamnyatia mshambuliaji wa Leicester na Algeria 27 Riyad Mahrez na inajiandaa kutoa kitita cha £65m mwisho wa msimu huu. (Sun)
Manchester United wanapigiwa debe kumsajili mshambuliaji wa Watford na raia wa Brazil 20 Richarlison mbele ya Bayern Munich na PSG. (Mail)
West Ham wanamnyatia kipa aliyepo kwa mkopo Joe Hart ,31, kutoka Manchester City kwa kanadarasi ya kudumu. (Mirror)
Image captionWest Ham wanamnyatia kipa aliyepo kwa mkopo Joe Hart ,31, kutoka Manchester City kwa kanadarasi ya kudumu. (Mirror)
West Ham wanamnyatia kipa aliyepo kwa mkopo Joe Hart ,31, kutoka Manchester City kwa kanadarasi ya kudumu. (Mirror)
Usakaji wa saini ya mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu huu kutatokana na uwezekano wa iwapo raia wa Wales Gareth Bale ataondoka katika klabu hiyo. (Mail)
Jack Wilshere
Image captionJack Wilshere
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anatumai kiungo wa kati Jack Wilshere, 26, atatia saini kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo. (Goal)
Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce yuko tayari kumsaini mchezaji huyo wa Uingereza kwa uhamisho huru huku kandarasi ya Wilshere ikiisha mwisho wa msimu huu.. (Liverpool Echo)
Santi Carzola 33
Image captionSanti Carzola 33
Wenger pia yuko tayari kumpatia kandarasi mpya Santi Carzola 33, lakini hajui iwapo mchezaji huyo wa Uhispania atacheza tena.(telegraph)
Juventus iko tayari kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania 25 Alvaro Morata lakini iwapo atakubali kupunguza mshahara wake.. (Sun)
Juventus iko tayari kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania 25 Alvaro Morata
Image captionJuventus iko tayari kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania 25 Alvaro Morata
Mmiliki mkuu wa klabu ya Bordeaux nchini Ufaransa amesema kuwa klabu hiyo huenda ikamuuza mshambuliaji wao raia wa Brazil Malcolm mwisho wa msimu huu. (Sudouest, via Goal.com)
RB Leipzig inataka kumsajili mshambuliaji aliye kwa mkopo Ademola Lookman, 20, kutoka Everton kwa mkataba wa kudumu (Daily Star)
Mchezaji wa Bordeaux na raia wa Brazil MalcolmHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa Bordeaux na raia wa Brazil Malcolm
Kungo wa kati wa Brazil Brazilian Andreas Pereira, 22, anasema kuwa lengo lake ni kurudi Manchester United na kuimarika baada ya kipindi chake cha mkopo katika klabu ya Valencia kukamilika. (South China Morning Post)
Brighton inataka kumsajili mshambuliaji wa Strasbourg na Cameroon Stephane Bahoken. (Express).
BBC