Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, May 6, 2017

Faida ya majani ya mparachichi

Siku chache zilizopita tuliangazia macho katika kuona faida za kula parachichi, ni amani yangu kwamba ulijifunza jambo kubwa sana, hivyo naomba siku ya leo naomba tuangalie faida majani ya mmea wa parachichi katika mwili wa mwadamu.

Zifuatazo ni faida ya majani ya mparachichi.
Majani ya parachichi humsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi.

Unachotakiwa kufanya ni;

Chukua majani kiasi ya mparachichi, kisha yachemshe kwenye maji lita moja, ukijiridhisha yamekwisha chemka epua kisha yaache yapoe, kisha anza kunywa maji hayo kiasi cha nusu kikombe cha chai, kunywa muda wa asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja utaona mabadiliko.

1. Majani ya mparachichi  husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama.

2. Unachotakiwa kufanya ni
Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri.

3. Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha, ili kufanikiwa katika hili unapaswa kusaga majani hayo kisha weka kwenye sehemu yenye jeraha na utaona mafanikio,

4.Majani ya mparachichi pia husaidia kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Hizo ni faida chache kati ya nyingi ambazo hutibika na majani ya parachichi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment