Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Showing posts with label Teknolojia. Show all posts
Showing posts with label Teknolojia. Show all posts

Saturday, February 29, 2020



 Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufikirie yafuatayo:-
Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.
Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.

Eneo: Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye Meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa 3.25. Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na uwape vifaranga eneo la kuwatosha.

Sakafu: Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la sakafu.

Ukuta: Ingefaa kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe. Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafishaji wa nyumba au umwagiaji wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta 0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fito.

Mbao: Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea na wadudu.

Madirisha: Unaweza kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na mwanga wa kutosha katika nyumba ya vifaranga.

Paa: Mjengo wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe, mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja iezekwe bila kuchelewa.
MUUNGWANA BLOG

Saturday, April 7, 2018


Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli inaendelea kuimarisha uchumi wa viwanda hadi kufikia Februari 2018 viwanda vipya 3, 306 vimeanzishwa. - REUTERS


Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kaulimbiu yake ya kujenga uchumi unaotegemea viwanda na kwamba, hadi kufikia Februari 2018, viwanda vipya 3,306 vimekwishaanzishwa nchini. Ametoa kauli hiyo Jumatano, Aprili 4, 2018 Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge. Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji katika viwanda kwa kutoa vivutio vya kodi na visivyo vya kodi kwa wawekezaji mahiri (strategic investors); kuendeleza na kuboresha miundombimu wezeshi kama vile barabara, reli, bandari, umeme na maji. “Serikali itaendelea kuhuisha sera, sheria na kanuni pamoja na kufuatilia utendaji wa viwanda vilivyobinafsishwa na kuchukua hatua stahiki kwa wamiliki walioenda kinyume na mikataba ya mauzo,” amesema.
Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba mikoa na Halmashauri zote nchini zimeelekezwa kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya viwanda na kwamba katika mwaka 2018/2019, Serikali itatoa kipaumbele katika kutekeleza miradi ya kielelezo, uanzishwaji wa kanda maalum za kiuchumi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda. Akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa sekta ya hifadhi ya jamii kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema pamoja na miradi mingine NSSF na PPF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wanatekeleza mradi mkubwa wa uzalishaji wa sukari mkoani Morogoro.
“Lengo la mradi huo ni kuzalisha tani 250,000 za sukari na umeme megawati 40. Mradi huo unatekelezwa katika shamba la Mkulazi lililopo Ngerengere lenye ukubwa wa hekta 63,000 na shamba la gereza la Mbigiri lenye ukubwa wa ekari 12,000 lililopo Dakawa,” alisema. “Hadi sasa ekari 2,000 za mashamba ya miwa zimetayarishwa katika eneo la Mkulazi na ekari 1,100 zimepandwa miwa. Lengo la Serikali ni kukamilisha awamu ya kwanza ya ufungaji wa mitambo ya kiwanda cha Mbigiri ifikapo mwezi Desemba, 2018 ili uzalishaji uanze mwaka 2019,” alisema na kuongeza kuwa miradi hiyo itakapokamilika, itazalisha zaidi ya ajira 100,000.
Waziri Mkuu alisema tangu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo Juni 2017, ajira za moja kwa moja 780 na ajira zisizo za moja kwa moja  24,000 ikijumuisha wakulima wadogo wa mbegu na kilimo cha nje zimezalishwa. Akifafanua kuhusu ujenzi wa barabara kuu, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kuboresha mtandao wa barabara nchini ambapo katika kipindi cha Julai 2017 hadi Februari 2018, ujenzi wa Km. 776.45 za barabara kuu kwa kiwango cha lami umekamilika na Km. 1,760 zinaendelea kujengwa. Pia barabara zenye urefu wa Km. 17,054 zilikarabatiwa katika kipindi hicho.
Kuhusu ujenzi wa madaraja, Waziri Mkuu alisema madaraja ya Kilombero na Kavuu ujenzi wake umekamilika na kwamba ujenzi unaoendelea hivi sasa ni wa madaraja ya Sibiti, Mto Mara, Lukuledi, Ruhuhu, Momba na Mlalakuwa. Alisema madaraja mengine 996 katika maeneo mbalimbali nchini yamekarabatiwa. Kuhusu jitihada za Serikali kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema hadi kufikia Februari 2018, ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la TAZARA ulikuwa umefikia asilimia 70 na ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange) umeanza. “Maandalizi ya awamu ya pili hadi ya nne ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka yanaendelea. Katika mwaka 2018/2019, Serikali imepanga kujenga kilometa 597 za barabara kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami na kilometa 72 za kiwango cha lami zitakarabatiwa,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuliarifu Bunge juu ya uanzishwaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Roads Agency – TARURA) kwa lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji na kuongeza kasi ya wananchi kujiletea maendeleo. Alisema TARURA imepewa jukumu la kusimamia ujenzi na matengenezo ya mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 108,946.2 za vijijini na mijini. “Katika mwaka 2017/2018, TARURA imesimamia matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 4,183.3, madaraja 35, makalavati makubwa 43 na madogo 364 na drift nne,” alisema.
Waziri Mkuu ameliomba Bunge likubali kupitisha sh. 143,618,762,698 zikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2018/2019 ambapo sh. 74,527,321,698 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 69,091,441,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Vilevile, Waziri Mkuu aliliomba Bunge liidhinishe sh. 125,521,100,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo sh. 117,205,487,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,315,613,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMATANO, APRILI 4, 2018

Saturday, March 31, 2018

Mara nyingi watu wengi tuanpenda kutumia simu mahali ambapo pana giza kwa muda mrefu, sisi tunapenda kukuita kukuchati. Kuchati huku nyakati za giza wakati taa imezimwa huwa na madhara yafuatayo.

Kwa sasa, idadi ya wagonjwa kuanzia miaka 30-40 wanatafuta matibabu makubwa. kutokana na matumizi ya simu za mkononi (smart phone) gizani.

Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko singapore amesema: anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.

Hii ni kwasababu wakati wa kutimia simu mahali penye giza huwa tunayalazimisha macho yetu yaweze kuona ya uwezo wake. Na ndo maaana kuna wakati unaweza ukatumia simu muda mrefu mahali penye giza mara baada ya kuacha kutumia simu utaona kama giza limezidi zaidi. Hali hiyo huyafanya macho yako yaanze kurudi katika hali ya ukawaida.

Pia utumiaji wa simu kwenye giza husababisha Kupata saratani ya macho. Hivyo ili uweze kuepuka saratani hivyo ni bora tuache kutumia simu za mikononi gizani ili tujikinge. Simu za mikononi (smartphone) zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani, unabadili mfumo wa seli macho na kupelekea matatizo ya saratani ya macho.

Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi wanazigundua watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo. Hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote hawa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.

 Utumiaji wa simu inaweza sababisha na ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.
.
Madaktari bingwa wa macho 254 kutoka mahosipitalini profesa Li Li atoa hoja kwamba kikubwa cha muhimu ni kwamba ni kuwa mbali na tabia za kutumia simu gizani. Sababu tabia hizi za kutumia simu (smartphone) kabla ya kulala zitakusababishia matatizo ya maisha yako kwa ujumla.

Hivyo ili kujiangalia sisi wenyewe na familia zetu, kwamba hakuna kuzima taa endapo unatumia simu ya mkononi. Wape taarifa haraka wote watumiaji wa simu za mikononi gizani wanaweza kupoteza kwa urahisi sana uwezo wa kuona.

Saturday, March 24, 2018


Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amewataka watanzania kutumia mawasiliano ya simu kwa manufaa ya kujiletea maendeleo na sio kutumika katika masuala ambayo si sahihi.

Kauli hiyo wa Naibu Waziri imekuja leo wakati akifanya uzinduzi wa duka la simu ambapo ametoa takwimu kwamba asilimia 94 ya watanzania wanatumia mawasiliano kwa njia ya simu.

Aidha Mh. Nditiye amesema kwamba endapo mawasiliano hayo yatatumiwa vizuri yatasaidia nchi kupiga hatua za kimaendeleo.

Aidha Mh. Nditiye amewataka watoa huduma za mawasiliano kuhakikisha kuna kuwa na huduma bora na zinazokidhi mahitaji.

Thursday, March 15, 2018


Related image
Tanzania ni nchi yenye walaji wa nyama wengi na kuku huliwa kwa kiasi kikubwa sana. Hata kama bei zinapanda, ulaji unaendelea kukua. Matokeo yake ni kwamba kufuga kuku inaweza ikawa biashara yenye faida kubwa kwako kwa kuwa yanahitajika kwa wingi.

Kwa nini ufugaji wa kuku inafaida sana?
Kuku haina madhara mengi ya kiafya kama nyama ya ng’ombe na watu wengi wanazidi kutambua hilo Kuku wanakua kwa kasi kwa hiyo unaweza ukapata mapato makubwa kwa kipindi kifupi.

Kuku hailiwi nyumbani tu lakini pia kwenye migahawa, baa, hoteli na huduma zingine mbalimbali za chakula.

Kwa hiyo kama una nia ya kuanzisha biashara ya kufuga kuku, inabidi uchukue hatua zifuatayo:

1. Chagua aina ya kuku.
Kuna aina nyingi ya kuku, zikiwemo:

Kuku wa kienyeji
Bata
Bata Mzinga
Kanga
Bata Bukini
Tombo

Kwa sasa, tutaweka maelezo yetu kwa Kuku wa Kienyeji.

2. Amua unataka kufuga kuku kwa malengo gani ya kibiashara
Unaweza kufuka kuku kwa ajili ya biashara nyingi, zikiwemo:

• Kuku wa kuuza
• Kuku wa mayai
• Kuzalisha nyama ya kuku ya kuuza
• Kuzalisha chakula ya kuku ya kuuza
• Kuzalisha nyama na mayai ya kuku ya kisasa.

Fanya maamuzi kwa kuangalia kiasi cha pesa ulionayo kuanzisha biashara pamoja mahitaji ya eneo yako.

Ni muhimu sana kufanya utafiti wako (uliza wafugaji wengine wa kuku) kujua ni aina gani ya ufugaji wa kuku utakaokuletea faida zaidi pamoja na gharama za kuanzia.

Kwa hapa, sisi tunalenga ufugaji kwa ajili ya kuzalisha mayai na nyama.

3. Una pesa ya kutosha?
Ukubwa wa shamba lako la kuku litategemea mtaji wako. Kwa ujumla:

• Shamba ndogo itahitaji mtaji wa TZS 1.5m – TZS 3m.
• Shamba ya saizi ya kati itahitaji mtaji wa TZS 4m – TZS 10m.
• Shamba kubwa itahitaji mtaji wa TZS 20m au zaidi.

4. Shamba yako itakuwa maeneo gani?
Ukiwa unachagua eneo ya kuweka shamba lako, zingatia yafuatayo

• Bei ya kiwanja utakiweza?
• Gharama za kusafirisisha mayai na nyama ni za chini? Iko karibu na soko lako na wanunuaji?
• Watu wengi wanaishi kwenye hiyo eneo? Hii inaweza ikawa tatizo ukizingatia harufu litakalo kuwa linatoka shambani

Kuna usalama?
• Badala ya kutafuta kiwanja kipya, watu wengi wanafunga kuku kwenye eneo lao la nyumbani. Hii inapunguza gharama ila kabla ya kufanya hivi, kumbuka kufikiria majirani pamoja na kama kuna kanununi za kufuata.

5. Utatumia mfumo gani kwenye kibanda cha kuku?
Jinsi utakavyo wapanga kuku wako kwenye kibanda chao kitachangia faida yako kwa sana.

Kuwaachia huru-Mfumo huu umetumika tangu biashara ya kufuga kuku ulianza. Inawaachia kuku watembee wanavyopenda, ila kwa kuwaachia hivi inaweza ikawa na madhara yake, kama:

• Mahasimu wanaweza wakawaumiza
• Watu wanaweza wakawaiba
• Kuku wanaweza wakapotea
• Magonjwa yanaweza kusambaa
• Ni ngumu zaidi kufuatilia ukuwaji wao

Ila, ni rahisi kuweka mfumo huu na haina gharama kubwa.
Mfumo wa Chicken Liter/Deep Litter: Hii ni mfumo maarufu kwa shamba ndogo na za ukubwa wa kati. Kuku wanwekwa kwenye eneo iliyozungukiwa na fensi au ukuta, alafu vipisi vidogo vidogo vya mbao vinasambazwa chini kutumiwa kama kitanda.

Mfumo huu unamsaidia mkulima huyu kusimamia idadi kubwa ya kuku. Ila, ubaya ni kwamba ni rahisi kwa magonjwa kuenea.

Mfumo wa Battery Cage: Kwa kawaida, mfumo huu unatumika kwenye mashamba makubwa ya ufugaji kuku ila ina gharama kubwa. Kuku wanaingizwa ndani ya ngome ya chuma, zikiwa na sehemu maalum za kula na kunywa maji. Pia, kuna nafasi maalum ya kutaga. Kwa kuwa idadi ya kuku wanaowekwa kwenye kila ngome sio kubwa, ni rahisi kujua kuku yupi anaumwa au hatagi.

6. Unahitaji vifaa gani?
Zaidi ya kuwajengea kibanda, kuku wako watahitaji vifaa vingine kama:

• Vifaa vya kunywa
• Vifaa vya kula
• Viota
• Taa
• Makreti
• Inkubeta
• Pechi
• Mfumo wakutoa takataka
• Trei ya mayai
• Hita
• Ngome

Tafuta vifaa vya kufuga kuku, hapa.

7. Utawalisha nini kuku wako?
Je, utanunua chackula chao au utiakitengeneza mwenyewe?
Kutengeza chakula cha kuku kinahitaji mtaji mkubwa zaidi, ila, kadri muda unavyoenda, gharama yake inakuja kuwa china ya kununua chakula chao kila mara ikihitajika. Pia, unaweza ukajiongezea mapato kwa kuwauzia wafugaji wengine wa kuku.

Mwisho wa siku maamuzi yatategemea na kufanya utafiti wa zote mbili na kujua gharama zake dhidi ya maslahi yako.

8. Inabidi umwajiri mtu?
Kama ufugaji wa kuku haitakuwa kazi yako ya kudumu, utahitaji kumwajiri mtu/watu kukusaidia na usiamamizi. Baadhi ya watu utakawahitaji ni:

• Msimamizi wa biashara kwa ujumla
• Mhasibu
• Msimamizi wa kuku
• Mlinzi

Mtu wa kutangaza biashara yako – we unaweza kufanya kazi hii. Itabidi utafute namna ya kutangaza biashara yako kwenye intaneti kwa kupitia

orodha za biashara kama iliyopo ZoomTanzania , kwenye mitandao ya kijamii, kwa kuchapisha vipeperushi n.k

9. Chanjo za kuku na upimaji wa afya mara kwa mara.
Kadri biashari yako itakavyokuwa, ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa mganga wa mifugo na kuchanja kuku wako kuzuia magonjwa kusambaa.

Kumbuka, afya ni muhimu kuliko bei ya kuku wako. Ila, weka bei inayoeleweka.

Biashara inayolipa
Kufuga kuku inahitaji subira na kujitolea ila, faida zikianza kuingia utafurahi sana!

Tafuta kila kitu unachokihataji kuanza kufuga kuku hapa.



Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia wakati alipomtembelea ofisini kwake kufanya mazungumzo naye pia alitembelea Kituo cha kufufua umeme kwa njia ya Maji kilichopo Hale wilayani Korogwe

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili kutoka kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia kitu wakati walipotembelea kituo hicho
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia mitambo iliyopo kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakati walipotembelea kituo hicho kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe,Rehema Bwasi
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakitembelea mitambo iliyopo kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakati walipotembelea kituo hicho
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Meneja wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kulia ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia
Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme kutoka Tanesco Makao Makuu Bakaya Mtamakaya akizungumza wakati ziara hiyo ya Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kushoto kulia ni Meneja wa Uzalishaji wa Kituo cha Pangani Hydro Systems
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao cha pamoja mara baada ya Balozi huyo wa Sweden kutembelea kituo hicho cha Uzalishaji wa Umeme kulia Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt 
Meneja Uzalishaji wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kushoto akiteta jambo na na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt 





Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt kushoto

Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho.

SERIKALI ya Sweden imetoa kiasi cha fedha Bilioni 66 za kitanzania sawa na dola za Marekani milioni 30 ambazo zitatumika katika kukarabati mitambo katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Hale Hydro System wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wakati alipotembelea mgodi huo ambapo upo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga. Amesema kuwa Tanzania na Sweden zina historia za muda mrefu katika uhusiano wa kidplomasia na nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.

Amesema kuwa nishati ni jambo muhimu kwa maendeleo ya viwanda hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo kwa nia moja serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha katika kukarabati mgodi huo." Nishati ni jambo muhimu katika maendeleo ya viwanda na Tanzania tayari imeweka mikakati mizuri katika maendeleo ya viwanda hivyo,serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha kwa kukarabati mgodi huo "alisema.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amemshukuru balozi huyo kwa serikali ya Sweden kufadhili mradi huo,pia amemkaribisha balozi huyo kuwekeza katika sekta mbalimbali za kijamii na uchumi." Nawashukuru serikali ya Sweden kwa kufadhili mradi huo na mheshimwa Rais ameweka mazingira mazuri ya uwekezaji mkoani Tanga haswa katika sekta ya viwanda hivyo karibuni Tanga mje kuwekeza" alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Hale Mhandisi Steven Mahemba amesema kuwa mtambo huo umepunguza uzalishaji kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa mitambo.

" Kituo hiki kimejengwa kuanzia mwaka 1962 na kumalizika mwaka 1964 na kina muda wa takribani miaka 52 hivyo pia kutokana na uchakavu wa miundombinu take imepunguza uzalishaji kutoka megawati 21 mpaka 4 hadi 8" alisema.

Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka mitatu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Tuesday, March 13, 2018

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Historia Asilia ya Berlin Ujerumani (Berlin Museum of Natural History), Prof. Johannes Vogel kuhusu masalia ya mjusi wa Tanzania yaliyofadhiwa katika makumbusho hiyo.
.....................................................
Ujerumani na Tanzania zimekubaliana kuendeleza tafiti za masalia ya mijusi katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kutembelea Makumbusho ya Historia Asilia ya Berlin (Berlin Museum of Natural History) nchini Ujerumani yanapohifadhiwa pia masalia ya mijusi waliopatikana eneo la Mlima Tendaguru mkoani Lindi.

Maj. Gen. Milanzi aliongoza msafara wa Tanzania ulioshiriki maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin 2018 yaliyohitimishwa jana nchini Ujerumani. Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 7 mwezi huu yalihusisha taasisi 5 za Serikali na Makampuni binafsi 60 kutoka Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho hiyo, Prof. Johannes Vogel alimueleza Maj. Gen. Milanzi kuwa shughuli kubwa inayofanywa na makumbusho hiyo ni utafiti kwa ajili ya maendeleo ya sayansi, elimu na ufahamu wa mambo mbalimbali kuhusu Dunia, viumbe pamoja na mazingira ili maarifa na ufahamu huo usaidie binadamu kutawala maisha yake na mazingira yanayomzunguka.

Akizungumzia fursa zilizopo za kushirikiana kutafiti maeneo yalikopatikana masalia ya mijusi hao na viumbe wengine Prof. Johannes alisema, Makumbusho yake ipo tayari kushirikiana na Wanasayansi wa Tanzania ili kujenga uwezo wa kufanya utafiti na kupata matokeo yatakayochangia katika hazina ya maarifa na sayansi ya viumbe na mazingira.

“Ili kuwa na utafiti endelevu, ni vema kwa nchi ikawekeza kwa wataalamu wake ili kuendeleza utafiti na maendeleo ya sayansi. Hivyo tupo tayari kushirikiana ili kujenga uwezo kwa wasomi wa Tanzania kuweza hatimaye kufanya utafiti na kuleta maendeleo kwa nchi yao” alisema.

Akizungumzia kuhusu masalia ya mijusi waliopatikana Tendaguru na ambayo yanahifadhiwa katika makumbusho hiyo, alisema badala ya kuwarudisha nchini Tanzania, ni vema wakachukuliwa kuwa elimu, utafiti na maendeleo ya sayansi yanayopatikana kutokana na kuwafanyia utafiti ni kwa maendeleo na ustawi wa dunia nzima.

“Ichukuliwe kuwa huu ni urithi wa dunia nzima na hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa urithi huu hauachi ukapotea.  Hivyo, ni vema tukaimarisha utafiti katika eneo walikopatikana ili kupata masalia mengi zaidi na kuitangaza Tanzania katika Nyanja za utafiti.

“Makumbusho yangu ipo tayari kufanya ziara ya kuimarisha mazungumzo na mamlaka za Tanzania mapema iwezekanavyo ili utafiti katika eneo la Tendaguru uendelee kwa manufaa ya Tanzania na Dunia nzima”. alisema Prof. Johannes. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Milanzi aliahidi kuwapa ushirikiano ili kuwezesha tafiti hizo kufanyika kwa ajili ya ustawi wa sayansi na uchumi wa nchi zote mbili.  Alimkaribisha Prof. Johannes na timu yake kuja Tanzania mapema iwezekanavyo ili kujadili na kukamilisha makubaliano ya kuendeleza tafiti hizo.

Awali, Maj. Gen. Milanzi alipata fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk. Abdalla Possi. Miongoni mwa mambo waliyozungumza ni pamoja na masalia hayo ya mjusi wa Tanzania anayehifadhiwa katika moja ya makumbusho nchini humo.

Balozi Possi alisema kuwa kwa maoni yake haoni kuwa wazo la kuhamisha masalia hayo kurudishwa Tanzania kuwa litakuwa na tija kwa maendeleo ya utalii na utafiti wa sayansi kwa nchi yetu. 

Alitoa baadhi ya sababu kuwa sio kweli kuwa masalia hayo ndiyo kivutio kikubwa pekee kinachofanya wanasayansi na watalii wengi kutembelea makumbusho hiyo na hivyo kuipa mapato makumbusho hiyo. 

“Makumbusho inapata ruzuku kutoka serikalini na kiingilio ni sehemu ndogo sana ya mapato ya makumbusho hiyo.  Fedha nyingi za kufanyia shughuli za Makumbusho ya Berlin zinatokana na fedha zinazolipwa kwa ajili ya kufanya utafiti na si viingilio katika makumbusho” alisema Dk. Possi.

Alisema makumbusho hiyo ina mikusanyo mingi ya viumbe mbalimbali zaidi ya milioni 30 ikiwemo ya mijusi kutoka nchi nyingine duniani.  Mkusanyiko huo kwa pamoja unatoa mvuto kwa watafiti na watalii kutembelea na kufanya shughuli zao chini ya makumbusho hiyo. 

Dk. Possi alisema kuendelea kuwepo masalia hayo katika makumbusho hiyo kuna manufaa zaidi ya kuitangaza Tanzania kiutalii na utafiti wa kisayansi kuliko masalia hayo yatakapoondolewa katika makumbusho hiyo na kurejeshwa nchini Tanzania. 

Alisema kuwepo masalia hayo katika makumbusho hiyo ni kama Balozi wa utalii na utafiti wa kisayansi anayeitangaza Tanzania sehemu mbalimbali duniani. 

Akizungumzia mchakato unaoendelea hivi sasa hapa nchini wa kuandaa Utambulisho mpya wa Tanzania (National Branding), Balozi Possi alishauri kuwa ni vema mabadiliko yatakayopelekea kuondokana na utambulisho unaotumika hivi sasa ukaangaliwa kwa umakini kwa kuwa kuna hatari ya kupoteza msisitizo uliopo katika vivutio maarufu vya utalii nchini na kutoa fursa kwa washindani kutangaza utalii wao kupitia vivutio hivyo.

Alisema endapo hakuna athari kwa kutumia utambulisho wa sasa ambao ni maarufu (Tanzania the Land of Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar), ni vema zikaangaliwa pia athari zitakazopatikana kwa kuachana na “brand” inayotumika hivi sasa.

Alisema kuwa baadhi ya vitu vinavyotumika kwenye utambulisho wa sasa tayari ni “brand”.  Alitoa mfano kuwa Mlima Kilimanjaro ni Brand maarufu na inayojiuza, hali kadhalika kwa Serengeti na Zanzibar.
CCM Blog

Sunday, March 11, 2018



Asante ndugu msomaji kwa kua nasi siku zote, na napenda kuanza kukupaelimu kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka huu.
na leo nitaelezea kuhusiana na hasara za kutokupalilia mapema na faidia za kupalilia shamba lako mapema.
Wakulima wengi sana wamekua wakilichukulia swala la kupalilia kama ni swala la hiali tu, lakini ukweli ni kwamba wewe kama mkulima na unalengo la kupata mazao mengi yenye ubora swala la kupalilia kwa wakati ni swala la muhimu sana hivyo ni muhimu kulizingatia.

KUPALILIA-Kwa tafsiri rahisi kupalilia ni ilie hali ya kuondoa memea au majani ya saio itajika(magugu) shambani. kwa kitaalamu kitendo hiki kinaitwa (WEEDING).
Mkulia unaweza kuchagua njia sahihi ya kupalilia kulingana na uwezo, ukubwa wa shamba na aina ya mimea uliyo panda, kuna njia tofauti tofauti ya kupalilia kama zifuatazo
  • kwa kutumia jembe la mkono
  • kwa kutumia madawa(herbicides)
  • kwa kutumia jembe la ng'ombe
  • kwa kung'olea
usisite kuendelea kujifunza mengi zaidi kwa kujiunga moja kwa moja na blogi hii HAPA
  MAGUGU- magugu ni mmea wowote ule unao ota sehemu ambayo haiitajiki mfano kama shamba lako unapanda mpungu na ndani ya shamba ikawepo memea ya mahindi hivyo kwa wakati hua mahindi ni magugu na yanatakiwa kuondolewa shambani
pia kuna aina tofauti tofauti ya magugu kwa wakati mwingine nitakuletea somo la magugu na aina tofauti tofati ya magug, kwa somo letu la leo nitakuonesha kuhusiana na hasara za kutokupalilia kwa wakati muafaka.

MADHALA YANAYO YANAYO TOKANA NA UWEPO WA MAGUGU SHAMBANI
Kama nilivo elezea mwanza kua kuna hasara ya kutokupalilia kwa wakati, hivyo hapa nitaelezea hasara zinazo wezwa kulutwa na uwepo wa magugu shambani.
  • magonjwa
  • uwepo wa wadudu waharibifu
  • kugombea kwa virutubisho
  • kugombea kwa mwanga
  • kufa kwa mimea 
  • kupunguza ubora wa mazao 
  • na madhara makuu ni kukosa kwa mazao stahiki yaani kupata kidogo ukilinganisha na jinsi ulivo takiwa kupata.
NOTE; Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupalilia mapema na unaweza kupalilia mara mbili au zaidi kulingana na aina ya mmea au zao.