Writen by
sadataley
12:07 PM
-
0
Comments
Katibu mkuu wa Umoja wa Afrika, Ban Ki-moon, anatazamiwa kufanya mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, ili kuongeza nguvu muafaka wa amani utakaositisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka miwili nchini humo.
Msemaji wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini anasema kuwa visa vya uchomaji nyumba na wizi wa mabavu vinaendelea katika mji wa Malakal, kufuatia mapigano ya juma lililopita yaliyosababisha vifo vya watu 18.
Serikali sasa imekubali kutumwa kwa majeshi yanayomtii naibu Rais Riek Machar kupiga doria katika mji mkuu Juba, juma lijalo.
Ni mara ya kwanza kwa majeshi hayo kurejea katika mji huo, tangu mapigano yaanze miaka miwili iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment