Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

KITAIFA

KIMATAIFA

KANISA

KITAIFA

KIMATAIFA

Advertise Space

AFYA

MICHEZO

TEKNOLOJIA

Latest News

Saturday, October 28, 2023

 

KKKT- DMP USHARIKAA WA KIJITONYAMA

SIKU YA BWANA YA KUKUMBUKA MATENGENEZO YA KANISA (Reformation)

USHUHUDA WETU- TUNATENGENEZA MAMBO YALIYOHARIBIKA

ZABURI 25:14-22, 1KOR  3:16-17, YOHANA 2:15-17

29.10.2023

 

Leo tunatafakari juu ya matengenezo ya Kanisa ambayo ndio ushuhuda wetu. Ushuhuda ni neno la kuthibitisha na kuelezea mambo yalivyokuwa au kutokea, ni uthibitisho/ushahidi.

 

Mungu alipoumba dunia na kuifanya kuwa kanisa lake halikuwa na haja ya matenegenezo kwa sababu aliona kila kitu ni chema (Mw 1:31) Ila baada ya anguko ndipo umuhi wa matengenezo ulipoanza kuonekana.

 

Matengeno ya Kanisa yalianza mara moja baada ya anguko la mwanadamu, mwanadamu alianza kuona udhaifu na Mugu akaona mtu wake anahitaji matengenezo ili aweze kuwa mwema tena ndipo Mungu aliamua kuanza matengenezo kwa kuwatengenezea Mavazi ya ngozi wanadamu wale wa kwanza kuficha udhaifu. (Mwanzo 3:21)

 

Tunamuona pia Yoshua alipoona Kanisa la Mungu linataka kujichanganya na miungu mingine aliamua kusimama na kuonyesha msimamo kuwa Kanisa lenye michanagnyiko linahitaji kutengenezwa na liwe na msimamo mmoja ndipo aliposema mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu kama ninyi mnataka kuendelea kuabudu miungu. (Yoshua 24:15)

 

Katika Agano Jipya kwanza tunamuona Yesu mwenyewe katika somo tulilolisoma alipofika Yerusalemu na kukuta hekaluni zinafanyika biashara na sasa kugeuzwa kuwa soko aliamua kufanya matengenezo yake kwa  kuondoa uchafu wote na wafanya biashara wote kule hekaluni. (Yn 2:13-17)

 

Tunamuona Mtume Paulo nae anaweka mkazo zaidi kwa kuwataka Wakoritho kujitambua zaidi kwamba wao  ni hekalu la Roho Mtakatifu. Kutokukubaliana na mambo ya hovyo hovyo yafanyike na wao kukaa kimya. hata sasa wengi tumekaa kimya na tunashindwa  kukemea na kuingia na kufanya matengenezo huku tukishuhudia utapeli na ongezeko la waalimu wa uongo linazidi ndani ya Kanisa ambalo Mungu amelinunua kwa bei ya thamani.

 

Matengenezo ya Kanisa yaliendelea baadae na hata kuzaliwa kwa Kanisa la Kilutheri Duniani,  sasa katika somo hili nataka ujiulize kwa nini wewe ni Mlutheri? na Mlutheri ni nani?

 

Yawezekana usiwe na majibu ya haraka ila nitakapofikia mwisho wa somo hili utapata majibu.

 

Kanisa letu la Kilutheri kila Jumapili ya kila mwaka mwishoni mwa mwezi wa kumi karibu na tarehe 31 huadhimisha sikukuu ya matengenezo ya kanisa yaliyofanyika tarehe 31/10/1517.

Ilipofika mwakani (2017) Kanisa la kilutheri Duniani lilifikisha miaka miatano(500) ya matengenezo yake, Lazima tujihoji je bado tupo kwenye msingi wa neno la Mungu au tayari tumeshatoka? Tufanye nini ili kuendeleza kazi njema ya Kuutangaza ufalme wa Mungu hapa duniani? Matengenezo haya lazima yawe ushuhuda wetu kweli katika matendo yetu na sio kinadharia tu.

 

USHUHUDA WETU

Kama nilivyoeleza maana ya Ushuhuda wetu mimi nina ujasiri wa kusema kuwa nimekuwa Mlutheri kwa sababu nilizaliwa katika imani hiyo nikiendelea kujiboresha kumjua Mungu zaidi.

 

Jina mlutheri limetokana na chimbuko toka jina la Dkt. Martin Luther, baba wa matenegenezo ya kanisa aliyekuwa na lengo la kurekebisha na kutengeneza baadhi ya mafundisho na taratibu zilizokuwa zikifanywa na kanisa la wakati ule kanisa la Kirumi(RC) ambazo zilikuwa hazijengwi kweneye msingi wa Neno la Mungu ili kurejea katika msingi wa Kibiblia.

 

Dkt. Martin Luther alizaliwa na kukulia nchini Ujerumani na alisoma masomo ya falsafa na sheria akiwa kijana mdogo, lakini baadae aliamua kujiunga na masomo ya Theolojia ambapo mwaka 1507 alibarikiwa kuwa padre wa katoliki na baadae alifundisha chuo cha theolojia Wittenberg. Wakati akifundisha chuoni Luher alichukizwa na mafundisho na matendo yaliyokuwa yakifanywa na Kanisa katoliki kama vile mamlaka ya papa, vyeti vya msamaha, wakristo kuzuiwa kusoma biblia nk, ndipo tar 31/10/1517 aliandika maoni (sentensi) 95 kwenye mlango wa Kanisa la Wittenberg  ambazo zilizungumzia juu ya ukosefu wa elimu ya Kibiblia, matendo mabaya na kutokuwajibika miongoni mwa viongozi wa Kanisa, yeye alikuwa na lengo la kuwarejesha kwenye maandiko Matakatifu.

 

Dr martin Luther alisimamia ukweli wa neno la Mungu katika kupambana na mafundisho potofu yaliyofanya wokovu ufikie hatua ya kununuliwa kwa hela kupitia vyeti vya msamaha pamoja na mapungufu mengine. Tunaweza kusema kuwa Luther alishuhudia ukweli wa injili kiasi cha kuwa tayari kufa kwa ajili ya ukweli pale aliposema “Hapa nasimamia ukweli wa neno la Mungu, sitabadili msimamo, nisaidie Mungu wangu” “Here I Stand, Lord Help Me”

 

Dkt. Martin Luther hakuwa na lengo wala nia ya kuanzisha dhehebu jipya, bali alitaka tu kusahihisha kile alichokiona kama ukiukwaji wa wazi wa mafundisho ya Biblia ila alitakiwa kukana maandishi yake ila alisema asipothibitishiwa kutoka biblia kuwa amekosea hayupo tayari kuyakanusha ndipo alipohesabiwa kuwa mzushi na kuhukumiwa Kunyongwa ila alifanikiwa kutoroka na kujificha.

 

Ndipo mwaka 1597 watheolojia waliokaa katika mji wa Wittenberg huko ujerumani walitafsiri jina ulutheri kumaanisha ‘Kanisa la kweli’ ambalo limejengwa kweneye msingi wa neno la Mungu ila Martin Luther alipendelea neno Kiinjili zaidi.

 

Hivyo tunaitwa Walutheri kwa sababu tunafuata misingi na mafundisho ya Dr. Martin Luther na aliweka mkazo katika mambo haya: -

  1. Mafundisho rasmi ya Kilutheri ya wakati wote na mahali pote huonyesha sisi sote

wenye dhambi na tunapokewa jinsi tulivyo kwa neema ya Mungu lakini hatuaswi kubaki jinsi tulivyopokelewa.(Rumi 6:1-4) na tujue kuwa ya kale yamepita tutazame mapya (1Kor 5:17) na tukazane kuzaa matunda(Mt 7:19) na huku tukiwajali wengine (Mt 25:36-46).

  1. Leo hii Mlutheri anafahamika kuwa ni muumini wa dini ya Kikristo ambaye

anaabudu katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ambalo ni ushirika wa watakatifu ambao injili inatangazwa kwa usafi na sakramenti zinatolewa kwa usahihi wake. Kama Luther alivyotafsiri maana ya Kanisa kuwa ni pale ambapo injili inahubiriwa na kupokelewa tena na Sakrament ya Ubatizo na Ushirika wa Meza ya Bwana vinatolewa kwa usahihi wake.

  1. Mlutheri anamwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na

kubatizwa katika Utatu Mtakatifu, ambapo anasafishwa dhambi zake na kupokelewa katika kundi la waaminio na kufanyika mwana wa Mungu  kwa njia ya imani tu. (SOLAR FIDES)- Roman 1:17.

  1. Mlutheri anaamini juu ya mafundisho, mafunuo, mapenzi na ahadi za Mungu

kupitia maandiko matakatifu yaani Biblia, kuwa ndio msingi wa maisha yake. (SOLAR SCRIPTURA).

  1. Mlutheri anakubali na kuamini ya kuwa wokovu wa mwanadamu unapatikana

kwa Neema ya Mungu tu. (SOLAR GRATIA).

  1. Mlutheri anakubali na kuamini ya kuwa katekisimo ndogo ya Dkt Martin Luther,

ukiri wa Nikea, Mitume, Athanasio na ungamo la Augusburg lisilobadiika ndio maelezo sahihi tena ya wazi ya neno la Mungu

 

KKKT imejali maisha wa kiroho ya waumini wake kwa kuzingatia Biblia na kuna vitabu vingine kama kitabu cha nyimbo TUMWABUDU MUNGU WETU pamoja na kalenda ya mwaka inayomwongoza kila mlutheri popote alipo kwa neno la Mungu kila siku asubuhi na jioni.

 

Nyakati hizi kumetokea mafundisho mengi sana ambayo yanawachanganya washarika wetu. Ni lazima sisi tufuate na kuenzi utaratibu wa ibada yetu ili watu waweze kutambua kuwa sisi walutheri wenye umoja na tumebobea katika mafundisho sahihi ya neno la Mungu na sakramenti zake zinatolewa kwa usafi wote

 

Kwa msingi wa katiba ya KKKT tunapaswa kuuenzi, kuulinda na kuimarisha umoja wetu, twapaswa sisi kushuhudia kila kona juu ya neema ya Mungu kwetu. Waasisi wa KKKT waliweka wazi msingi wa Imani utakaofuatwa  ambao ni

 

 Kanisa lililojengwa juu ya msingi mmoja, Yesu Kristo, hukiri kwamba Neno la Mungu lililoandikwa katika Agano la Kale na Agano jipya  ndio msingi pekee wa uhakika wa Imani na maisha ya kanisa. Katika umoja wa Kanisa moja duniani, huungama ungamo la Mitume, Nikea, na la Athanasio; hukubali pia maungamo ya Kanisa la Kilutheri hasa ungamo la Augusburg lisilobadilishwa na katekisimo ndogo ya Martin Luther kuwa maelezo au mafafanuzi sahihi ya neno la Mungu. Sharika zote, na wachungaji, sinodi na dayosisi za kanisa hili zitakubali na kufuata nsingi huu wa imani.

 

HITIMISHO

Tunapoona habari hizi za matengenezo ya kanisa na historia nzuri za watu waliotetea imani yao hata kwa mateso yatatuhimiza sisi wa leo kuendelea kuona kuwa kanisa la Mungu linapaswa kujifunza kwa usahihi ukweli wa neno la Mungu pasipo kuyubishwa.

 

Tunapoona neno la Mungu linayumbishwa tusikubali hali hiyo tunapaswa kukemea kwa ukali kama alivyofanya katika hekalu ya Yerusalemu na tunapaswa kupatwa na wivu tunapoona kweli ya neno la Mungu inapindishwa.

 

Matengenezo ya Kanisa ni jambo endelevu ili kuendelea kupokea neema ya Mungu katika ukombozi kwenye maisha yetu.

 

Tunapewa pia wito wa kujenga umoja wetu katika familia zetu, umoja wa kifamilia, umoja wa jumuiya na sala, umoja wamitaa ya Sharika, umoja wa sharika, umoja wa jimbo, Dayosisi na Kanisa zima.

 

Wapendwa washarika kwa kupitia siku hii ya matengenezo ya kanisa, tunaletewa wito kujifanyia tathimini katika Imani zetu, mienendo na maisha yetu kwa ujumla. Je bado tupo katika msatari wa kumfuata Yesu au la? Lazima tujihoji je bado tupo kwenye msingi wa neno la Mungu au tayari tumeshatoka? Tufanye nini ili kuendeleza kazi njema ya Kuutangaza ufalme wa Mungu hapa duniani? Matengenezo haya lazima yawe ushuhuda wetu kweli katika matendo yetu na sio kinadharia tu.

 

Mungu na atusaidie sote, amen.

Friday, January 27, 2023


Kanisa ni nini? Lilianza lini? Ni kwa nini kuna madhehebu mengi?

Neno kanisa kwa Kiyunani ni ekklesia. Neno hili lina maana ya, “kilichotengwa kwa kusudi maalum; kusanyiko.”

Jambo la kwanza la kujifunza ni kwamba Biblia inalizungumzia kanisa kwa namna mbili tofauti: Kanisa la ulimwengu wote kama mwili mmoja, na kanisa la mahali fulani kama taasisi.

KANISA LA ULIMWENGU WOTE – MWILI

Maana: Kanisa la Ulimwengu Wote ni jumla ya waamini wote wanaounda mwili wa Kristo kwa njia ya ubatizo kwa Roho Mtakatifu, na liliundwa siku ya kwanza ya Pentekoste, ni tofauti kabisa na taifa la Israeli na haliishii mahali fulani au dhehebu fulani tu.

Kila mtu, akiwa hai au amekufa, ambaye aliwahi kumpokea Yesu Kristo na kumwamini kama Bwana na Mwokozi wake, tangu siku ile ya Pentekoste hadi sasa, ni mmoja wa Kanisa la Ulimwengu, yaani mwili wa Kristo ambapo yeye, Kristo ndiye kichwa (Waefeso 1:22)

YESU ALISEMA NINI KUHUSU KANISA?

Soma Mathayo 16:18-19

Kristo alilizungumzia kama la wakati ujao

Kristo alipozungumza maneno haya, kanisa lilikuwa ni kitu cha wakati ujao kwa hiyo halikuwepo wakati akiwa hapa duniani. Je, ni nani msingi ambako kanisa limejengwa? Ni nani au ni nini ambacho ni mwamba, Kristo alichokuwa anaelezea?

Petro mwenyewe anasema kwamba Kristo ndiye Mwamba (1 Petro 2:4-8; 1 Wakorintho 3:11, hakuna msingi mwingine; Waefeso 2:20).

Au inaweza ikawa kwamba ukiri wa Petro, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai”, ndio mwamba, kwa sababu kila mtu anayejiunga na kanisa la ulimwenguni lazima aamini kwamba huu ndio ukweli kuhusu Yesu.

KANISA LILIZALIWA LINI?

Soma: Matendo 1:5 na 2:1-4

Kanisa lilizaliwa siku ya Pentekoste, kama siku kumi hivi baada ya Yesu kupaa kwenda mbinguni. Roho Mtakatifu alishuka ili kumwingiza kila mwamini katika mwili wa Kristo na kumkalia kila mwamini kibinafsi kabisa. Pentekoste kwa Roho Mtakatifu ilikuwa ni kama Krismasi kwa Yesu. Alikuja kuhusianisha waamini wote kwa namna mbalimbali.

Paulo analizungumzia kanisa kama siri:

Soma Waefeso 3:6

Siri hii ni kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wanaungana na kuunda kitu kimoja kwa njia ya ubatizo wa Roho Mtakatifu. Sifa pekee kwa ajili ya kujiunga ni imani katika yule Mwokozi aliyefufuka. Kanisa ni kitu kipya kabisa ambacho huundwa na Wayahudi na Watu wa Mataifa.

Kwa hiyo ni wazi pia kwamba, kila mwamini tangu siku ya Pentekoste, akiwa hai au amekufa, ni kiungo katika mwili wa Kristo, ambao ni kanisa la ulimwengu wote. Waamini waliokwishafariki dunia wako pamoja na Bwana wakisubiri siku ambayo tutakuwa pamoja.

KANISA LA MAHALI – ASASI

Maana. Kanisa la mahali ni kusanyiko la waamini waliojipambanua wanaofuata mapokeo fulani na mfumo fulani wa uongozi, na ambao wanaigusa jamii kwa ajili ya Kristo kwa njia ya kumwabudu Mungu hadharani, wakiwajenga waamini, na kuhubiri injili kwa waliopotea.

Kuna tofauti kati ya kanisa la ulimwengu wote na kanisa la mahali. Kanisa la ulimwengu wote lina waamini tu, lakini kanisa la mahali lina watu ambao wanadai kuwa ni waamini wakati kwa kweli hawaamini kabisa. Inawezekana ukawa muumini wa kanisa la mahali lakini ukawa sio mwamini katika mwili wa Kristo. Hii inafanyika kwa njia ya ujinga au udanganyifu. Baadhi ya makanisa wana masharti ambayo inabidi uyafuate lakini hawakuambii kwamba imani katika Kristo ndiyo ambayo kwa kweli inaokoa, wala hawaangalii kwamba mtu amefanya uamuzi huo wa kuamini. Watu wengine wanaweza kudai kuwa wanaamini lakini ukweli ni kwamba ni waigizaji tu, ni wanafiki. Katika kanisa letu, huwa tunawataka watu wanaotaka kujiunga na kanisa letu watoe ushuhuda wao kuwa ni lini walifanya uamuzi wa kumpokea Kristo kama Mwokozi wao. Lakini hata kwa hilo bado tunaweza kudanganywa. Ni Mungu tu ndiye anayeijua mioyo!

NI KWA NINI KUNA MADHEHEBU MENGI YA KIKRISTO?

Madhehebu mengi yalianza kwa kukubaliana kuhusu mapokeo ya mafundisho fulani na kutokukubaliana katika mengine kama vile namna ya ubatizo, kama mtu anaweza kupoteza wokovu wake, namna za uponyaji wa kimwili, karama za kiroho na namna za kuabudu kanisani. Ninaamini kwamba aina nyingi za madhehebu tulizo nazo zinakidhi mahitaji ya watu wa aina mbalimbali. Kuna wanaopenda liturgia ya namna fulani, kuna wanaopenda mafundisho ya ndani sana ya Biblia, kuna wanaopenda burudani, wengine wanapenda nyimbo za kuchangamka na kuamsha hisia na wengine ni kwa kiasi tu.

UONGOZI WA KANISA

Kuna aina tatu kuu za uongozi wa kanisa.

Uongozi wa ki-episkopo (Episcopos): Katika uongozi huu mamlaka ya kanisa hukaa katika Askofu. (Kwa Wamethodisti ni ule rahisi; ila kwa Waanglikana ni mgumu kidogo; na kwa Wakatoliki wa Rumi utawala upo kwa Papa)

Uongozi wa ki-presibiti (Presbuteros): Mamlaka ya kanisa ipo katika kundi la wawakilishi ambao wamepewa mamlaka na kusanyiko lote pamoja na wazee. (Hii ipo kwa kanisa la Presibiterian na makanisa mengine)

Uongozi wa Kusanyiko: Huu ni uongozi unaosisitiza juu ya nafasi ya kila Mkristo mmoja-mmoja, jambo linalofanya kusanyiko liwe na uamuzi wa mwisho katika maamuzi. Kila mwamini ana kura ya maamuzi. (Hii ipo kwa makanisa ya ki-Baptisti na makanisa mengine ya Kiinjili, pia makanisa huru na ya kiBiblia.) Kanisa letu ni muunganiko wa hayo mawili ya mwisho. Tunaongozwa na wazee na kusimamiwa na mtu mmoja aliyeajiriwa, na kusanyiko huwa linapiga kura juu ya Mchungaji wanayemtaka. Mchungaji Msaidizi, Wazee, na bajeti.

WAZEE WA KANISA

Uongozi wa Kiroho ni wajibu wa wazee. Sifa za wazee tunazipata katika 1 Timotheo 3:1-7 na Tito 1:6-9, ambapo kazi hii wamepewa wanaume. Wanao wajibu wa kulilinda kanisa dhidi ya mafundisho potofu na kulihudumia kanisa kama wachungaji wanaochunga kundi la Mungu. (Matendo 20:17, 28).

MASHEMASI

Mashemasi wanafanya kazi ya uongozi katika mamlaka waliyo nayo wazee. Hawa huwa wanatunza washirika walio na mahitaji katika kanisa. Wanawake wanaweza kuwa mashemasi. (Warumi 16; 1 Timotheo 3:8-11.)

TARATIBU ZA KANISA

Taratibu: “Ni mambo ya nje yaliyoelezewa na Kristo yanayofanywa na kanisa.”

Makanisa mengi huziita sakramenti.

Sakramenti: “Sakramenti ni kitu kinacholetwa kwenye milango ya fahamu kikiwa na nguvu, kwa uwezo wa kiungu, sio kwa ajili ya kuweka alama tu, lakini pia kikiwa na uwezo wa kuleta neema.” (Kwa mujibu wa Baraza la Katoliki).

Hatuamini kwamba ama Chakula cha Bwana au ubatizo ni namna ya kupeleka neema. Tunaamini kwamba vitu hivi hufanywa kwa kuyatii maagizo ya Kristo na kutoa taswira ya kile ambacho tayari kimeshafanyika ndani ya mioyo yetu. Matendo haya yote hukumbusha juu ya kufa, kuzikwa na kufufuka kwa Kristo.

UBATIZO

Soma: Mathayo 28:19

Namna: Kuzamisha ndiyo maana ya msingi ya neno ubatizo (baptize)

Kuzamisha hutoa picha ya umuhimu wa ubatizo, ambapo ni kifo cha mtu wa kale na kufufuliwa kwa mtu mpya. Kanisa hili linabatiza kwa kuzamisha, lakini linabishana na kugawanyika juu namna za kubatiza jambo ambalo halina tija. Kila mwamini anapaswa kubatizwa mara baada ya kujua kuwa Kristo aliagiza hivyo. Ni ushuhuda wa hadharani kwamba umeungana na Kristo. Kama ulibatizwa kabla ya kuamini, usisite kubatizwa tena kama mwamini. Ubatizo ni utii kwa Bwana wako.

CHAKULA CHA BWANA, USHIRIKA AU EKARISTI

Soma: 1 Wakorintho 11:23-32.

Kuna makusudi kadhaa ya kushiriki Chakula cha Bwana au Meza ya Bwana.

Ni ukumbusho wa maisha na kifo cha Bwana wetu. Mkate usiotiwa chachu unawakilisha maisha makamilifu ya Bwana wetu ambayo yalimpa sifa ya kuwa sadaka inayokubalika kwa ajili ya dhambi zetu. Inawakilisha mwili wake ambao ulibeba dhambi zetu pale msalabani. Mvinyo unawakilisha damu yake aliyoimwaga kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu.

1 Wakorintho 11:26 inasema kwamba chakula hiki hutangaza mambo ya msingi ya injili. Hutangaza mauti ya Bwana.

Ni kutukumbusha kwamba Yesu Kristo anarudi tena na tunapaswa kuendelea kushiriki hadi ajapo.

Inapaswa itukumbushe kuhusu Umoja wetu sisi kwa sisi katika mwili wa Kristo na ushirika tunaoushiriki kama viungo katika mwili huo (1 Wakorintho 10:17).

 

 

NI NANI ANAYEWEZA KUSHIRIKI?

Mtu asiyeamini hapaswi kushiriki kwa sababu karamu hii ni utambulisho kwa hao ambao wamekiri imani katika kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo kwa ajili ya upatanisho wa dhambi zao.

Je, mwamini yeyote anaweza kushiriki bila kujali kuwa ni wa dhehebu gani? Jibu ni ndio. Hii ni Meza ya Bwana na waamini wote wa kanisa la ulimwengu wanaalikwa. Sio meza ya kanisa la kiBaptisti, kikatoliki au kipentekoste. Migawanyiko hii ni kinyume na wito wa watu wote kuwa wamoja katika kanisa la ulimwengu wote. (Uliofanyika Lausanne)

Onyo! 1 Wakorintho 11:27-32: Tunapaswa kuipeleleza mioyo yetu Na kuungama dhambi zetu kabla ya kushiriki Meza ya Bwana. Vinginevyo tunaweza kubadilishwa—Kama vile kugusa au hata kufa.

KUSUDI LA KANISA LA MAHALI

  • Kuabudu na kuonyesha upendo wake kwa Bwana (Ufunuo 2:4).
  • Kuwahudumia waamini wake ili waweze kutiana moyo katika kupendana na kufanya matendo mema (Waebrania 10:24).
  • Kushiriki katika kulitii Agizo Kuu. Yaani kwamba Injili ihubiriwe katika huduma za kanisa ili wasioamini waipokee na kuokoka.
  • Kuwajali waamini wake ambao wana mahitaji, kama wajane, yatima na maskini (Yakobo 1:27; 1 Timotheo 5:1-16).
  • Kufanya matendo mema katika ulimwengu (Wagalatia 6:10).
  • Kuzalisha Wakristo waliokomaa, wenye msimamo na watakatifu (Wakolosai 1:28; Waebrania 6:1; Waefeso 4:14-16). Hii inaweza kumaanisha kuwa na nidhamu katika eneo la maadili na usafi katika mafundisho (1 Wakorintho 5, 2 Timotheo 2:16-18).

VIELELEZO VYA KANISA LA ULIMWENGU

Kristo ni Mchungaji na sisi ni kondoo (Yohana 10) – utunzaji na usalama

Kristo ni mzabibu na sisi ni matawi (Yohana 15) – kuzaa na kupata nguvu

Kristo ni jiwe la Pembeni na sisi ni mawe katika jengo (Waefeso 2:19-21) –Jiwe la pembeni hutoa mwelekeo na huwekwa mara moja tu.

Kristo ndiye Kuhani Mkuu na sisi ni ufalme wa makuhani (1 Petro 2) –tunajitoa kwake, nafsi zetu na huduma zetu.

Kristo ni Kichwa na sisi ni viungo vya mwili Wake (1 Wakorintho 12)—akiwa kama Kichwa, huongeza; na sisi kama viungo tunahudumiana kwa kutumia karama za kiroho ambazo ametugawia.

Kristo ni Bwana-Arusi na sisi ni bibi-arusi wake (Waefeso 5:25-33, Ufunuo 19:7-8)—upendo wa milele na ukaribu.

Kristo ni Mrithi na sisi ni warithi-wenzake (Waebrania 1:2, Warumi 1:17)—tutaushiriki utukufu wake.

Kristo ni Malimbuko na sisi ni mavuno (1 Wakorintho 15:23)—ufufuko wake unatuhakikishia kuwa na sisi tutafufuka.

Kristo ni Bwana na sisi ni watumishi Wake (Wakolosai 4:1, 1 Wakorintho 7:22)—mtumishi hufanya mapenzi ya bwana wake. Bwana naye humtunza mtumishi wake.

SASA TUNAYATENDEAJE KAZI MAMBO HAYA?

Inatupasa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa tunajiunga na kanisa la ulimwengu wote, bila kujali kuwa tunaabudu kwenye dhehebu gani. Kuwa katika kanisa la ulimwengu wote kunafanyika wakati mtu anapompokea Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wako. Kuna uhakika mkubwa sana katika kujua kwamba wewe ni miongoni mwa walioko katika kanisa la ulimwengu wote, yaani Mwili wa Kristo. Uhakika huu unatakiwa ukutie moyo kujitambulisha katika kanisa la mahali ambapo utaweza kukua na kutumika. Kanisa kama la kwetu halihitaji uwe mwanachama ili upate huduma zetu. Lakini huoni kwamba ni vizuri kuunga mkono na kutoa ufadhili mahali ambapo unapokea baraka na ukuaji wa kiroho kwa kujiunga kikamilifu? Kujiunga kikamilifu ni kujitambulisha na watu waliopo hapo. Hiyo ndio familia yako. Ndiko unakotoa sadaka zako kifedha. Ndipo pia utakaposaidia wale walio na mahitaji. Unafanya ushirika wako hapo, yaani UNAJITOA KIKAMILIFU! Kama umekuwa ukija kusali katika hilo kanisa kila Jumapili, kwa nini usiamue kulifanya kanisa lako na ujiunge kabisa? Madarasa ya waamini wapya hufanyika mara nne kwa mwaka. Huwa yanafanyika kwa Jumapili mbili mfululizo zinazofuatana asubuhi. Ukipenda kujiunga utaonana na mzee wa kanisa, atakuuliza maswali na kukuongoza ili uweze kutoa ushuhuda wako. Kisha utatambulishwa rasmi katika kanisa.

HISTORIA YA KILUTHERI ILIVYOBADILISHA USO WA UKRISTO.

Nini kilichoanza kama jitihada nchini Ujerumani ili kurekebisha Kanisa Katoliki la Kirumi iliongezeka kwa kupinga kati ya Kanisa hilo na wafuasi, kuwa mgawanyiko ambao utabadilisha uso wa Ukristo milele.

HISTORIA YA KANISA LA LUTHERAN INATOKA MARTIN LUTHER.

Martin Luther , profesa wa teolojia na wa teolojia huko Wittenburg, Ujerumani, alikuwa muhimu sana kwa matumizi ya Papa ya indulgences ya kujenga Basilica ya Mtakatifu Petro huko Roma mapema miaka ya 1500.

Makosa yalikuwa nyaraka za kanisa rasmi ambazo zinaweza kununuliwa na watu wa kawaida kwa kudai kuondokana na haja yao ya kukaa katika purgatory baada ya kufa. Kanisa Katoliki lilifundisha kwamba purgatory ilikuwa mahali pa kutakasa ambako waumini walisamehe dhambi zao kabla ya kwenda mbinguni .

Lutheri alitetea upinzani wake katika Vikwazo vya Nne na Tano , orodha ya malalamiko aliyotumikia hadharani kwenye mlango wa Kanisa la Castle huko Wittenburg, mnamo mwaka wa 1517. Aliwahimiza Kanisa Katoliki kujadili masuala yake.

Lakini vurugu zilikuwa ni chanzo muhimu cha mapato kwa kanisa, na Papa Leo X hakuwa wazi wa kujadiliana nao. Luther alitokea mbele ya baraza la kanisa lakini alikataa kurejesha taarifa zake.

Mwaka wa 1521, Luther aliondolewa na kanisa. Mfalme Mtakatifu wa Roma Charles V alitangaza Luther kuwa sheria ya umma. Hatimaye, fadhila itawekwa juu ya kichwa cha Luther.

HALI YA PEKEE YALIYOMSAIDIA LUTHER

Maendeleo mawili yasiyo ya kawaida yaliruhusu harakati ya Luther kuenea.

Kwanza, Luther alikuwa mpendwa wa Frederick Mwenye hekima, Mkuu wa Saxony. Wakati askari wa Papa walijaribu kuwinda Luther, Frederick akaficha na kumlinda. Wakati wa wakati wake wa kutengwa, Luther aliendelea kufanya kazi kwa kuandika.

Maendeleo ya pili ambayo yaliruhusu Matengenezo ya kukamata moto ilikuwa uvumbuzi wa vyombo vya habari.

Luther alitafsiri Agano Jipya kwa Ujerumani mwaka 1522, na kuifanya kupatikana kwa watu wa kawaida kwa mara ya kwanza. Alifuata hiyo kwa Pentateuch mnamo mwaka wa 1523. Wakati wa maisha yake, Martin Luther alitoa matukio mawili, nyimbo nyingi, na mafuriko ya maandiko yaliyoeleza teolojia yake na kuelezea sehemu muhimu za Biblia.

Mnamo mwaka wa 1525, Luther alikuwa ameoa ndugu wa zamani, alifanya ibada ya kwanza ya ibada ya Kilutani, na kumchagua waziri wa kwanza wa Lutheran. Luther hakutaka jina lake kutumika kwa kanisa jipya; alipendekeza kuiita Evangelical. Mamlaka ya Wakatoliki walifanya "Lutheran" kama neno la kudharau lakini wafuasi wa Luther walivaa kama beji ya kiburi.

MAREKEBISHO YANAANZA KUENEA

Mwandishi wa Kiingereza William Tyndale alikutana na Luther mwaka 1525. Tafsiri ya Kiingereza ya New Testament ya Tyndale ilichapishwa kwa siri nchini Ujerumani. Hatimaye, nakala 18,000 zilipelekwa kwa usafirishaji nchini England.

Mnamo mwaka wa 1529, Luther na Philip Melanchthon, mtaalamu wa kidini wa Kilutheri, walikutana na mrekebisho wa Uswisi Ulrich Zwingli huko Ujerumani lakini hakuweza kufikia makubaliano juu ya Mlo wa Bwana . Zwingli alikufa miaka miwili baadaye kwenye vita vya Uswisi. Taarifa ya kina ya mafundisho ya Kilutheri , Kukiri ya Augsburg, ilifunuliwa kabla ya Charles V mwaka 1530.

Mnamo mwaka wa 1536, Norway ilikuwa ya Lutheran na Sweden ilifanya dini ya Lutheran kuwa dini ya serikali mwaka 1544.

Martin Luther alikufa mwaka wa 1546. Kwa miongo kadhaa ijayo, Kanisa Katoliki la Kirumi lilijaribu kuondokana na Kiprotestanti , lakini wakati huo Henry VIII alikuwa ameanzisha Kanisa la Uingereza na John Calvin alianza Kanisa la Reformed huko Geneva, Uswisi.

Katika karne ya 17 na 18, Wareno wa Ulaya na Scandinavia walianza kuhamia Ulimwenguni Mpya, na kuanzisha makanisa katika kile kilichokuwa Marekani. Leo, kutokana na jitihada za umishonari, makutaniko ya Kilutheri yanaweza kupatikana ulimwenguni kote.

BABA WA MATENGENEZO YA KANISA

Ingawa Lutheri anaitwa Baba wa Reformation, pia ameitwa jina la Reformer aliyependa. Vikwazo vyake vya mapema kwa Ukatoliki walikazia ukiukwaji: kuuza dhamana, kununua na kuuza wa ofisi za kanisa la juu, na siasa zisizopendeza zinazohusika na upapa.

Hakuwa na nia ya kugawanya kutoka Kanisa Katoliki na kuanza dini mpya.

Hata hivyo, kama alilazimika kutetea nafasi zake zaidi ya miaka kadhaa ijayo, Luther hatimaye alipiga marufuku teolojia ambayo ilikuwa katika hali isiyo na mazungumzo na Ukatoliki. Mafundisho yake kwamba wokovu ulikuja kwa neema kupitia imani katika kifo cha Yesu Kristo, na si kwa kazi, ikawa nguzo ya madhehebu kadhaa ya Kiprotestanti. Alikataa upapa, wote saraka mbili, nguvu yoyote ya ukombozi kwa Bikira Maria, kuomba kwa watakatifu, purgatory, na hilari kwa waalimu.

Jambo muhimu zaidi, Luther alifanya Biblia - "sola scriptura" au Maandiko pekee - mamlaka pekee ambayo Wakristo wanapaswa kuamini, mfano wa karibu Waprotestanti wote wanafuata leo. Kanisa Katoliki, kinyume chake, linaamini kuwa mafundisho ya Papa na Kanisa hubeba uzito sawa na Maandiko.

Zaidi ya karne nyingi, Lutheran yenyewe imegawanywa katika makundi mengi ya dini, na leo inashughulikia wigo kutoka kwa ultra-conservative kwa matawi ultra-liberal.

(Vyanzo: Concordia: Ushahidi wa Kilutheri , Concordia Publishing House; bookofconcord.org, reformation500.csl.edu)

Kwa mujibu wa vyanzo ndani ya KKKT inaelezwa kuwa Mwaka 1887 kazi ya Injili kwa Kanisa la Kilutheri ilianzishwa nchini Tanganyika (baadaye Tanzania) na Chama cha “Misioni cha Berlin III” au “Evangelical Missionary Society for East Africa” (EMS) kutoka Ujerumani. Kituo cha kwanza cha misheni kilikuwa ni Kigamboni, Dar es Salaam.

Chama cha pili, yaani “Chama cha Misioni Berlin I”, nacho kutoka Ujerumani, kiliingia Tanganyika kikitokea Afrika ya Kusini na kuanza kazi Nyanda za Juu Kusini mwaka 1891 kilipoanzisha kituo cha misheni sehemu iitwayo Ipagika au Pipagika (Wangemannshöhe) katika Dayosisi ya Konde.

Mwaka 1890 “Chama cha Berlin III” kilibadilika na kuchukua sura mpya baada ya kubadili sera yake na kujulikana kwa jina la “Bethel” au “Misioni ya Bethel”. Misioni hii ikafika Tanga na kuanza kazi eneo la Mbuyukenda. Baadaye Misioni ya Bethel iliamua kufkisha Injili ya Kristo nje ya mipaka ya Tanganyika.

Wamisioari waliohusika walipanga kwenda Rwanda kupitia Bukoba. Walipofika Bukoba mwaka 1910 wakashawishika kufungua kituo Bukoba na ile nia ya kuanzisha kazi ya misioni Rwanda ikawa imesitishwa. Chama cha tatu kufka Tanganyika ni “Chama cha Misioni cha Leipzig” (nacho kilitokea Ujerumani).

Kiliingia nchini mwaka 1893 na kuanza kazi ya misioni Kaskazini ya nchi kwa kuweka kituo cha misheni Kidia, Old Moshi.

Kutokana na vyama hivyo vitatu kijiti cha kueneza Injili ilipokelewa na wenyeji toka kwa wamisionari wa Ujerumani.

Na vyama vingine vya misioni vilivyofka baadaye kutoka Ulaya na Marekani navyo vilieneza Injili kwa kufundisha Neno la Mungu kwa upendo na kwa usahihi, hasa baada ya Vita ya I ya Dunia (1914 - 1918) na Vita ya II ya Dunia (1939 - 1945).

Pamoja na kueneza Injili, Kanisa lilianza kutoa huduma mbalimbali za kijamii na diakonia kwa lengo la kumhudumia mwanadamu kikamilifu – kimwili, kiroho na kiakili. Makanisa saba yanayojitegemea ambayo baadaye yaliungana na kuunda Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika yalianzishwa.

Mnamo Juni 1963 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanganyika (KKKT) likaundwa. Baada ya KKKT kuanzishwa Kanisa la Ubena-Konde (eneo la Nyanda za Juu Kusini) likaitwa Dayosisi ya Kusini; Kanisa la Uzaramo-Uluguru likaitwa Dayosisi Mashariki na Pwani; Kanisa la Usambara-Digo likaitwa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki; Kanisa la Kaskazini likaitwa Dayosisiya Kaskazini; Kanisa la Mbulu likaitwa Dayosisi ya Mbulu; Kanisa la IrambaTuru likaitwa Dayosisi ya Kati na Kanisa la Kaskazini Magharibi likaitwa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.

Yapo maeneo nchini ambayo yalikuwa yanafanya kazi ya Injili kama misheni nayo ni: Mkoani Mara, Mashariki ya Ziwa Victoria, Ruvuma, Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Kusini Mashariki ambayo sasa ni Dayosisi.

Dayosisi za mwanzo nazo kwa kutegemea vigezo vya kikatiba na historia zikaendelea kugawanyika na hadi 2014 KKKT ikawa na Dayosisi 26 kama ifuatavyo: Dayosisi ya Kusini, Dayosisi ya Konde; Dayosisi ya Iringa; Dayosisi ya Kusini Kati; Dayosisi ya Kusini Magharibi; Dayosisi Mashariki na Pwani; Dayosisi ya UlangaKilombero; Dayosisi ya Morogoro na Dayosisi ya Dodoma. Nyingine ni Dayosisi ya Kaskazini Mashariki; Dayosisi ya Kaskazini; Dayosisi ya Kaskazini Kati; Dayosisi ya Pare; Dayosisi ya Meru; Dayosisi ya Mbulu, Dayosisi Mkoani Mara; Dayosisi ya Kati; Dayosisi ya Kaskazini Magharibi; Dayosisi ya Karagwe; Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria; Dayosisi ya Ruvuma; Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria; Dayosisi ya Kusini Mashariki na Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Tabora na sasa Kigoma.

Pamoja na KKKT kuwa na Dayosisi 26 bado kuna maeneo machache nchini ambayo ni ya misheni. Maeneo ya Misioni ndani ya nchi ni: Zanzibar.

Pia KKKT imekuwa ikifanya kazi ya umisheni katika nchi jirani kwa kushirikiana kwa hali na mali na makanisa dada na mashirika ya misheni kutoka ng’ambo. Katika misheni hizo watumishi hutumwa kuanzisha kazi ya misheni lakini pia washarika wa KKKT wamekuwa chachu ya kuanzishwa misioni nchi jirani.

Juhudi za kazi ya misioni ya nje zimesaidia kuzaa makanisa katika nchi jirani ambayo yanalelewa na KKKT. Misioni ya KKKT nje ya nchini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC), Kenya, Zambia, Msumbiji, Rwanda, Burundi na Uganda.


Ads Place 970 X 90