Writen by
sadataley
1:33 PM
-
0
Comments
Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz na Marco Rubio wamemshambulia vikali mgombea Donald Trump kwenye mdahalo kabla ya siku muhimu ya uchaguzi wa mchujo wiki ijayo.
Maseneta hao walijaribu sana kumkosoa Trump ambaye ameshinda uchaguzi wa mchujo majimbo matatu kati ya manne yaliyoandaa uchaguzi kufikia sasa.
Mjadala uliangazia sana uhamiaji, huduma ya afya na wagombea wa asili ya Amerika Kusini.
Lakini, sawa na midahalo ya awali, wagombea walianza upesi kushambuliana.
Kwa zaidi ya saa mbili, Rubio na Cruz walimshambulia Trumo kuhusu biashara wakimtaka kuwa mtu asiye wa kuaminika. Walishutumu pia sifa zake kama mhafidhina na pia kukosa kwake kutoa maelezo ya kina kuhusu sera zake.
Aidha, walisema amezoea kutamba kwa kutumia vitisho.
"Kama hangerithi $200m, unajua Donald Trump angekuwa wapi? Angekuwa akiuza saa Manhattan," alisema Bw Rubio wakati mmoja.
Bw Rubio pia alikosoa Trump kutokana na mpango wake wa kutoa elimu mtandaoni kupitia Chuo Kikuu cha Trump ambao ulifeli. Kadhalika, alimshutumu kwamba amekuwa akiwaajiri wageni kufanya kazi katika miradi yake ya ujenzi badala ya Wamarekani.
Bw Trump alimjibu: "Mimi nimewaajiri maelfu ya watu. Wewe hujawahi kuajiri mtu hata mmoja.”
Licha ya shutuma hizo, Bw Trump alionekana kutoyumbishwa.
Bw Trump ameendelea kujiongezea umaarufu licha yake kutoa matamshi yenye utata hasa kuhusu kuzuiwa kwa Wamarekani kuzuru Marekani na kujengwa kwa ua kuzuia wahamiaji kutoka Mexico.
Jumanne wiki ijayo, ijulikanayo kama Jumanne Kuu, mamilioni ya wapiga kura katika majimbo 11 watapiga kura za mchujo.
Robo ya wajumbe wanaohitajika kujipatia tiketi ya chama cha Republican wanapatikana majimbo hayo.
Bw Trump kwa sasa anaongoza majimbo 10 kati ya 11 yatakayoshiriki mchujo huo Jumanne.
Kwa sasa ana wajumbe 82, Cruz ana 17 naye Rubio ana 16. Ili kushinda tiketi ya chama cha Republican, mgombea anahitaji wajumbe 1,237 kitaifa.
Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton na Bernie Sanders watashindania wajumbe 1,004 Jumanne Kuu. Kwa sasa, Clinton ana wajumbe 505 naye Sanders 71.
Wagombe awatakaoteuliwa hutangazwa rasmi na vyama wakati wa mikutano mikuu Julai, miezi minne kabla ya uchaguzi Novemba.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment