Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 31, 2014

Serikali ina njia tatu za kurejesha ‘mabilioni ya Uswisi’


Waziri wa Fedha, Saada Mkuya akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika moja ya Vikao vya Bunge mjini Dodoma. Picha ya Maktaba. 
Na Elias Msuya, MwananchiDar/Uswisi. Kuna njia tatu ambazo Serikali ya Tanzania ikiamua kuzitumia inaweza kurejesha mabilioni ya fedha zake ambazo zimefichwa nchini Uswisi na kwingineko duniani, Mwananchi limebaini.
Uchunguzi ulifanywa na gazeti hili nchini Tanzania na Uswisi unaonyesha kuwa, Mosi, Serikali inaweza kuharakisha kurejesha fedha hizo ikiwa itatumia vyombo vyake vya dola kama vile mahakama kutaka maelezo na majina ya walioweka fedha katika nchi husika.
Pili Tanzania inaweza kupata fedha zake ikiwa itajiunga na Taasisi iitwayo Organization of Economic Cooperation (OECD), ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wanachama wake kurejesha fedha ambazo zimekuwa zikihamishwa kwa njia ya ukwepaji wa kodi (transfer pricing), na tatu ni kujiunga ‘Global Forum on Transparence and Exchange’.
Taarifa ya 2012 ya Benki Kuu ya Uswisi (SNB) iliripoti kuwapo kwa Sh314 bilioni kutoka Tanzania, lakini katika taarifa yake ya mwaka jana, 2013 kiasi hicho kiliripotiwa kupungua na kufikia Sh291 bilioni.
Dk Mark Herkenrath ambaye ni Ofisa Programu wa Taasisi ya Alliance Sud inayojishughulisha na harakati za kupinga uwekaji wa fedha haramu nchini Uswisi, alimwambia mwandishi wa gazeti hili nchini humo kuwa Tanzania inaweza kuwasiliana na Serikali ya Uswisi ikiwa inahitaji taarifa zozote kuhusu fedha zake zilizofichwa nchini humo.
“Kama kuna ombi la kimataifa na likakubaliwa na mamlaka ya Uswisi, taarifa zinaweza kutolewa. Serikali zinazodai kuibiwa fedha zinapaswa kuomba zenyewe taarifa ili zipewe, lakini katika uhalisia hili halitokei. Ni sawa na kumwomba mwizi ajitaje mwenyewe,” Herkenrath na kuongeza:
“Kwa mfano kama kuna uchunguzi Tanzania ambao unahusisha watu na ushahidi ukapatikana, Uswisi iko tayari kusaidia. Ni kwa fedha zilizopatikana kwa njia haramu tu.”
Mkuu wa kikosi kazi cha kurejesha fedha na mali cha Uswisi, Pascale Baeriwyl akizungumza na mwandishi wa Mwananchi mjini Bern, alisema Tanzania inaweza kurejesha fedha zake kama Serikali itakuwa na nia ya dhati ya kufanya hivyo.
“Hadi sasa Uswisi imesharudisha Dola za Marekani 1.8 bilioni kwenye nchi zilizotoka,” alisema Baeriwyl na kuongeza: “Zinaitwa fedha za watawala (potentate funds) ambazo huwekwa kwenye taasisi za nje za fedha. Uswisi inayo mikakati ya kuhakikisha kuwa fedha na mali haramu haziingizwi katika taasisi zake za fedha,” alisema.
Hata hivyo, Balozi Anne Lugon- Moulin ambaye ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia nchi zinazozungumza Kifaransa kusini mwa Jangwa la Sahara alisema, Uswisi peke yake haiwezekani kufanikisha urejeshwaji wa fedha kama Serikali ya Tanzania haitatoa ushirikiano wa kutosha.
“Uswisi peke yake haiwezi kufanikisha kazi hii kama Tanzania haitoi ushirikiano. Ndiyo maana tunafadhili taasisi zinazopambana na utoroshwaji wa fedha haramu na mashirika ya misaada ambayo pia yanafanya kazi Tanzania,” alisema Moulin.

Liverpool yailaza Mancity


Liverpool yailaza manchester city katika Mechi ya kirafiki,
Liverpool iliwalaza mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti timu hizo zilipokutoshana nguvu 2-2 katika muda wa kawaida katika mechi ya kirafiki ya kuwania taji la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup).
Mechi hiyo iliyovutia mashabiki elfu 50,000 katika uwanja wa yankee ulioko New York ilianza bila ya msisimko kipindi cha kwanza kikikamilika matokeo yakiwa ni suluhu bin suluhu.
Lakini katika kipindi cha pili, mabingwa hao walidhibitisha niya yao mapema kupitia bao la Stevan Jovetic.
Kiungo cha kati wa Liverpool ,Jordan Henderson aliisawazishia timu yake kabla ya Jovetic kuirejeshea City uongozi .
Uongozi huo hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu kwani Raheem alifanya mambo kuwa 2-2.
Waandalizi waliamua mechi hiyo ikamilishwe kwa kupiga matuta ya penalti.
Na hapo vijana wa Brendan Rodgers walitamba na kujikatia tikiti ya nusu fainali ambapo sasa watachuana na AC Milan ya Italia .
City sasa itakwaruzana na Olympiakos ya Ugiriki.
Mchuano huo unajumuisha timu 8 za kimataifa.

Wednesday, July 30, 2014

Court allows 9/11 cross to remain standing at Ground Zero

Cross at Ground Zero December 19, 2004. Credit: Samuel Li/Wikimedia.
Cross at Ground Zero December 19, 2004.
Rejecting arguments from an atheist group, a federal appeals court ruled Monday that the iconic cross found at the site of the 2001 World Trade Center attacks may remain at the 9/11 Museum.

“The history of 9/11 would not be complete without including the impact the Ground Zero Cross had in inspiring rescue workers and Americans generally,” said Eric Baxter, counsel for the Becket Fund for Religious Liberty, in a July 28 statement.

“Displaying the cross in a display about ‘Finding Meaning at Ground Zero’ is perfectly appropriate,” he continued.

The Becket Fund for Religious Liberty had filed a brief supporting the museum’s ability to display the cross, which was discovered amid piles of rubble by recovery workers in the aftermath of the Sep. 11, 2001 attacks on the World Trade Center in New York City.

Nearly 20 feet tall, the cross was formed by two intersecting metal beams from the fallen skyscrapers. It became a place of gathering and prayer for recovery workers at the site, with many people posting prayers and petitions to the structure.

Since 2011, the cross has been part of the World Trade Center Museum. In July 2011, however, American Atheists filed suit against the display, charging that the presence of the cross was offensive and marginalized them as atheists.

The suit added that the presentation of the cross led to injury “in consequence of having a religious tradition not their own imposed upon them through the power of the state.”

In 2013, a district court upheld the display of the cross, saying that it had a secular purpose and did not “create excessive entanglement between the state and religion.”

American Atheists appealed that ruling, arguing that the display still “alienates non-Christians seeking to commemorate the dead, wounded and other affected persons,” and that “the overwhelmingly dominant display of the cross over any other religious symbolism is a violation of the Establishment Clause.”

But in their July 28 ruling, federal judges on the Second Circuit Court of Appeals decided that “displaying The Cross at Ground Zero to tell the story of how some people used faith to cope with the tragedy is genuine, and an objective observer would understand the purpose of the display to be secular.”

They continued, noting that the cross is included in an exhibit entitled “Finding Meaning at Ground Zero,” which includes artifacts from a variety of faith perspectives as well as non-religious pieces. Therefore, the judges said, “an objective observer would not view the display as endorsing religion generally, or Christianity specifically.”

The ruling drew praise from Jay Sekulow, chief counsel of the American Center for Law and Justice, which had also filed a brief in support of the cross remaining in the memorial museum.

“This decision is a significant constitutional victory that protects the freedom to display religiously-themed artifacts of historical or artistic significance without running afoul of the Constitution,” Sekulow said.

“This bizarre legal challenge from an atheist group was exposed for what it was – a skewed legal challenge that had no merit.”

FIFA inachunguza ubaguzi wa rangi

FIFA yaanzisha Uchunguzi kuhusiana na Ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji wa Manchester City
Fifa imeanzisha uchunguzi kubaini ukweli wa madai ya mchezaji wa Manchester City kuwa alidhulumiwa kutokana na rangi yake timu hiyo ilipokuwa Croatia.
Shirikisho hilo la soka duniani linaendeleza uchunguzi huo kufuatia madai ya Seko Fofana, 20, kuwa alidhihakiwa walipokuwa wakishiriki mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.
Wakati huohuo shirikisho hilo limeiagiza shirikisho la soka la Italia kuanzisha uchunguzi dhidi ya ,Carlo Tavecchio ambaye anatuhumiwa kwa kutamka maneno ya kuwadunisha wachezaji wenye asili ya Afrika.
Msemaji wa FIFA ameiambia BBC kuwa wanakusudia kutafuta suluhu ya tukio lililompelekea kocha wa City Patrick Vieira kuwaondoa wachezaji wake uwanjani.
Kwa upande wake shirikisho la kandanda la Croatia limeanzisha uchunguzi wake.
Msemaji huyo alisema kuwa mwenyekiti wa jopo la kuchunguza dhulma kwa misingi ya rangi Jeffrey Webb anafuatilia kwa karibu matukio hayo.

KATIBA: Mzee Kisumo amhadharisha Rais Kikwete

Moshi. Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo amemtaka Rais Jakaya Kikwete na chama chake, CCM kuwa makini na msimamo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akisema haamini kama umoja huo umesema kila unachokusudia kukifanya.
Badala yake Kisumo alisema kinachofanywa na Ukawa ni mbinu za kujiimarisha kisiasa, jambo alilolisema iwapo CCM na Serikali yake haitakuwa makini, huenda ikaingia katika mtego na kushindwa kujinasua baada ya umoja huo kuimarika.
Kauli ya Mzee Kisumo imekuja wakati ambao viongozi wa Ukawa wameendelea kusisitiza kwamba wataendelea kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoanza mjini Dodoma, Agosti 5 mwaka huu, hadi pale madai yao yatakapozingatiwa.
Ukawa ambao unaundwa na Vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais, wanasisitiza kwamba lazima Bunge hilo lijadili Rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wakitaka pendekezo la muungano wa serikali tatu lizingatiwe.
Kamati zote 12 za Bunge hilo katika maoni ya wengi zilipendekeza muundo wa Serikali mbili tofauti na uliopendekezwa katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema kinachotakiwa ni Ukawa kurudi bungeni wakabishane kwa hoja na kama wakishindwa, bado wenye uamuzi wa mwisho juu ya Katiba ni wananchi kwa kupiga kura ya ndio au hapana.
Awananga Z’Bar
Wakati huohuo, Kisumo alisema kuna unafiki miongoni mwa wanachama wa CCM Zanzibar ambao alisema wanasaliti kwa siri sera ya chama hicho ya muundo wa serikali mbili.
Alionyesha kushangazwa na baadhi ya wana CCM Zanzibar kupinga waziwazi sera hiyo ya CCM na kushabikia serikali tatu.
“CCM ina kamati maalumu kule Zanzibar na Tanzania Bara vilevile, lakini inaelekea kamati ile ya Zanzibar haina nguvu ya kuwabana wachache hawa wanaokiuka sera zake,” alisema Kisumo aliyepata kuwa mdhamini wa CCM kwa muda mrefu.
Kisumo alitoa mfano uamuzi wa kumvua uanachama aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yusuph Himid kuwa haukupata uungwaji mkono Zanzibar.
“Kama sera ya CCM ni serikali mbili sasa anapotokea mtu anashabikia serikali tatu ni lazima chama kiwe na msimamo kuwa huyu siyo mwenzetu na uamuzi huo uungwe mkono,” alisema.

Mnaigeria agundulika kutumia dawa


Chika Amalaha
Mshindi wa medali ya dhahabu toka Nigeria Chika Amalaha amesimamishwa kwa muda kushiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola baada ya vipimo kuonyesha kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 16,alishinda medali ya dhahabu katika kunyanyua vitu vizito baada ya kuinua uzito wa jumla ya kilo 196,kwa upande wa wanawake wenye uzito wa kilo 53.
Vipimo vya awali alivyofanyiwa vilionyesha kuwa ametumia dawa aina ya Amilorde na hydrochlorothiazide ,ambazo zote zimepigwa arufuku michezoni.
Binti huyo anatarajiwa kuchukuliwa kipimo cha pili hapo kesho jumatano.
Mwanariadha huyo chipukizi wa Nigeria alishinda medali ya dhahabu Ijumaa iliyopita huku Dika Toua akiipatia Papua New Guinea medali ya ya kwanza kwenye michezo hii ya Jumuiya ya madola mwaka huu inayoendelea mjini Glasgow,ambapo Santoshi Matsa wa India aliipatia medali ya Shaba nchi yake kwea kushika nafasi ya tatu.
Amalala ni mwanariadha wa kwanza kugundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu kwenye michezo hiyo ya jumuiya madola,ambapo Mwanariadha wa mbio za kuruka viunzi mita 400 Rhys Williams kutoka Wales,na mkimbiaji wa mbio za Mita 800 Gareth Warburton pia wa Wales wakiwa wamelazimika kukosa michuano hiyo kutokana na kukabiliwa na tuhuma za matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Wanariadha wote hao wanakanusha kutumia dawa yoyote iliyopigwa marufuku huku wakiwa wanafahamu.

Wanajeshi 2 wa Cameroon watimuliwa kazi

Rais Biya amewafuta kazi wanajeshi wawili kwa utepetevu
Rais wa Cameroon, Paul Biya, amewafuta kazi maafisa wakuu 2 wa jeshi baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi ndani ya nchi hiyo.
Katika taarifa iliyopeperusha katika kituo cha redio ya taifa hakuna sababu yeyote iliyotolewa kwa kutimuliwa kazi kwa kanali Youssa Gedeon na luteini kanali Justin Ngonga.
Wadau wa maswala ya usalama katika magharibi mwa Afrika hata hivyo wanashauri kuwa huenda Biya ameanza kuhofia uwezo wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi ndani ya Cameroon.
Rais Biya amewafuta kazi wanajeshi wawili kwa utepetevu
Jumapili iliyopita kundi la Boko Haram lilimteka mke wa naibu waziri mkuu .
Yamkini Boko Haram ilimteka pamoja na msaidizi wake kiongozi mmoja wa kidini pamoja na meya wa mji wa Kolofata.
Mwandishi wa BBC aliyeko Yaounde Cameroon Muhaman Babalala anasema tukio hilo la utekaji nyara lilidhibitisha utepetevu wa maafisa wa usalama nchini Cameroon.
Kundi la Boko Haram linaanza kupanua eneo la mashambulizi yake
Maafisa hao wawili walikuwa wakiongoza doria katika mpaka wa Cameroon na Nigeria.
Kundi la Boko Haram limekuwa likipigania kuundwa kwa taifa la kiislamu kaskazini mwa Nigeria lakini katika siku za hivi punde limetekeleza mashambulizi ndani ya ardhi ya Cameroon.
Wapiganaji hao wamelaumiwa kwa vifo vya wanajeshi wanne mbali na utekaji nyara wa wageni nchini Cameroon.

MARIDHIANO: Katiba ,Katiba ,Katiba


“Ni muhimu  kudumisha amani nchini, tusizipe nafasi tofauti zetu za kidini kwani tusipokuwa waangalifu tunaweza kusababisha mvurugano katika jamii yetu” Alhad Mussa Salum 
Na Waandishi Wetu, MwananchiDar na Mikoani. Karibu katika kila mkusanyiko wa swala ya Idd el Fitri, neno “Katiba” lilitajwa wakati viongozi wa dini ya Kiislamu walipokuwa wakitoa mawaidha yao ya sikukuu hiyo kusherehekea kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Mfungo wa Ramadhani.
Katika mahubiri hayo, viongozi hao wa kidini walitaka mchakato wa Katiba uzingatie masilahi ya umma.
Mahubiri hayo yamekuja zikiwa zimebaki siku saba kabla ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba kuendelea mjini Dodoma, lakini kukiwa na sintofahamu kutokana na wajumbe wanaounda Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao kwa madai ya kutozingatiwa kwa maoni yaliyotolewa na wananchi.
Ukawa wanadai mjadala wa Katiba ni lazima ujikite kwenye Rasimu ya Katiba, ambayo imebeba mapendekezo ya wananchi na hali kadhalika kutaka wajumbe wenzao, hasa kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kujenga hoja kwa kutumia kejeli, matusi na mizaha.
Jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), liliisihi Ukawa kurudi bungeni ili kuweza kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya, lakini likasema mjadala huo uzingatie Rasimu ya Katiba.
Katika salamu zake za Idd, Katibu Mkuu wa Bakwata, Alhaji Suleiman Lolila alisema tayari fedha nyingi za umma zimeshatumika kuandaa mchakato wa Katiba Mpya, hivyo siyo busara kususia mchakato wake katika hatua zake za mwisho.
“Baraza linawasihi waliosusia warejee bungeni kwa sababu gharama kubwa zimeshatumika na kama kuna tofauti ziende zikajadiliwe na kumalizwa ndani ya Bunge,” alisema Lolilo.
Aliongeza kuwa Baraza linasikitika kwani maoni ya Waislamu hayakutiliwa maanani katika kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya na kwamba wanaamini yatazingatiwa katika hatua zinazofuata za mchakato huo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia Baraza la Idd jijini Dar es Salaam, alisema  mchakato wa Katiba Mpya una lengo zuri kwa masilahi ya taifa na katika mtikisiko ambao wamepitia hadi sasa ni vyema ukafikia mwisho na maelewano yapatikane.
“Walioko nje ya Bunge nawaomba warudi ndani kwani huko ndiko tunakoweza kujadiliana, tukatofautiana na kufikia hatua kufika makubaliano na nashukuru hata viongozi wa dini mmeligusia hilo,” alisema Pinda.
Alieleza kwamba kwa sasa kilio cha Watanzania wengi ni kuona Bunge la Katiba likiendelea kwa wale walio nje kurudi ndani kisha kujitazama upya na kupitia kuhusu udhaifu wote wa Katiba ya zamani na kurekebisha kwa ajili ya kupata Katiba nzuri itakayotupeleka mbele kwa miaka mingine mingi ijayo.

Monday, July 28, 2014

Marufuku ya Utumizi wa magari Nigeria



Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul Fitr.
Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.
Kundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la gari
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.
Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.
Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.

ASKOFU MPYA WA DAYOSISI MPYA YA RUVUMA ASIMIKWA. NI ASKOFU WA KKKT-DAYOSISI YA RUVUMA NAYE NI ASKOFU AMON MWENDA.

PG4A7267
Pichani ni Waziri Mkuu Mh. Peter Pinda akimkabidhi zawadi Askofu Amon Mwenda huku Mkuu KKKT Askofu Gehaz Alex Malasusa akisoma ujumbe wa Neno la Mungu uliandikwa katika picha hiyo maalum. Tukio hilo lilifanyika jana Mjini Songea na kuhudhuliwa na mamia ya watu.
PG4A7279
Pichani ni Waziri Mkuu Mh. Peter Pinda akimkabidhi zawadi Askofu Amon Mwenda huku Mkuu KKKT Askofu Gehaz Alex Malasusa akifurahia tukio hilo.

Pinda atoa angalizo Uchaguzi Mkuu 2015


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.PICHA|MAKTABA 
Na Joyce Joliga, MwananchiSongea. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewataka Watanzania wasikubali kuchagua viongozi wanaotafuta uongozi kwa kutumia fedha kwani zinaweza kuleta machafuko.
Alisema hayo jana wakati wa ibada maalumu ya kumsimika Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Ruvuma, Amon Mwenda kwenye kanisa hilo la Usharika wa Songea iliyohudhuriwa na mamia ya waumini na viongozi mbalimbali.
“Ndugu zangu ninawaambia kuwa msigeuze uchaguzi kuwa mtaji, bali tuzingatie taratibu na sheria za uchaguzi ambazo ndiyo mwongozo unaoweza kutusaidia.
“Ninawasihi wananchi wawe makini na viongozi wanaopenda kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Kama mtu ana nia ya kweli ya kuongoza ni kwa nini atumie fedha ili kupata nafasi ya uongozi?” alisema na kuongeza:
“Tatizo ni kwamba hata wananchi hivi sasa wanakubali kupokea kile kinachotolewa na wagombea. Atakuja huyu atakupa hiki na mwingine naye atakupa kile, lakini ujue akiingia madarakani anaanza kurudisha haraka vile alivyowagawia.”
Aliwaomba viongozi wa dini na waumini kuendelea kuliombea taifa ili Mungu aliepushe na janga la watu kupenda rushwa.
Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wazidi kuuombea mchakato wa kupata Katiba Mpya ili wajumbe wote warejee ndani ya Bunge na kuikamilisha kazi waliyoianza.
Alisema Watanzania kwa sasa hivi wanahitaji kumwomba Mungu ili waendelee kuwa na amani.
Waziri Mkuu pia aliwataka Watanzania kujikita zaidi katika kilimo ambacho kitaweza kuwakomboa na kuondoa umaskini unaowakabili.
Alisema kila mwananchi anapaswa kufanya kazi kwa bidii ili aweze kumudu maisha yake ya kila siku akitolea mfano wa shughuli za kilimo na ujasiriamali badala ya kusubiri kusaidiwa.
Waziri Pinda alisema Dayosisi mpya ya Ruvuma inapaswa kuweka mipango yakinifu ya maendeleo ambayo itaweza kuisaidia Serikali kupunguza changamoto zilizopo kwa kuanzisha miradi ya elimu, afya na shughuli mbalimbali za kijamii.
Awali, akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kusimikwa rasmi, Askofu Mwenda alisema dayosisi mpya ya Ruvuma imezaliwa katika kipindi chenye changamoto nyingi za kidunia na utandawazi ukiwamo mmomonyoko mkubwa wa maadili.

Hata hivyo, akiainisha malengo ya dayosisi hiyo ambayo anakuwa Askofu wake wa kwanza, Askofu Mwenda alisema mbali ya kufundisha neno la Mungu, dayosisi hiyo itahimiza ufanyaji kazi ili wakazi wake wawe na akiba ya chakula cha kutosha.
Alisema watashirikiana na Serikali na wadau wa ndani na nje kutoa huduma za kijamii hasa elimu na afya.
Aliahidi kukabiliana na changamoto za sasa ambazo alizitaja kuwa ni mmomonyoko wa maadili, rushwa, mauaji ya albino, unajisi wa watoto na ubakaji wa wanawake.
Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo, Askofu Mkuu wa KKKT, Dk Alex Malasusa alisema Kanisa lingependa kupata viongozi ambao ni wacha Mungu.
Askofu Malasusa alisema inashangaza kuona kuna baadhi ya watu wanagombea nafasi za uongozi lakini hawana mapenzi na Mungu aliyewaumba watu anaotaka kuwaongoza.

Malecela: Siku 60 hazitoshi kukamilisha Katiba Mpya

 
Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela.PICHA|MAKTABA 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela amesema siku 60 zilizotengwa kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya kabla ya kupelekwa kwa wananchi hazitoshi kwa kazi hiyo.
Akizungumza na katika mahojiano maalumu mjini Dodoma hivi karibuni, Malecela alisema: “Watahitaji siku zaidi…
Nadhani kosa moja ambalo tumelifanya ni la kujaribu kuweka muda maalumu wa kupitisha Rasimu ya Katiba.
Hata hivyo, huu muda tuliouweka hatukuuweka kutokana na uzoefu wa ama nchi fulani, maana tuangalie nchi zilizoandika katiba zao, tuseme nchi fulani walichukua miezi fulani kwa hiyo sisi itachukua siku fulani. Hebu angalia, kanuni tu zilichukua siku 40 na katika hizi siku 40 walizungumza sura ya pili na sita tu.”
Bunge Maalumu la Katiba litaanza Agosti 5, mwaka huu mjini Dodoma kwa siku 60 kukamilisha awamu ya pili ya mchakato huo baada ya kumalizika awamu ya kwanza mwanzoni mwa mwaka huu.
Akizungumzia mchakato mzima wa Katiba Mpya Malecela alisema: “Bado ninaamini inawezekana tukapata Katiba Mpya kama tutakwenda na moyo wa kusema nipe nikupe na haya mambo ya watu kutoka kwenye mazungumzo unajua mara nyingine tunaangalia hapa tu.
“Nimekwenda katika sehemu nyingine za dunia. Mfano wa Jamhuri ya Ireland na Serikali ya Waingereza ilichukua miaka mingapi wakae chini? Iliwachukua miaka mingi lakini walikaa chini wakazungumza wakafikia mahali walipo sasa hivi hakuna mgogoro.
“Wewe ulifikiria Marekani katika siku hizi itakuwa na ubalozi Iran? Lakini sasa hivi wanafikiria kufungua ubalozi Iran. Kwa hiyo mimi nasema tufuate mifano ya nchi nyingine, tusikate tamaa haraka.
Kuhusu hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi, kususia vikao vya Bunge hilo alisema: “Hawa wametoka naamini bado watu wanaweza wakazungumza nao na nyie vyombo vya habari mkawasaidia kuwatolea mifano mingi tu duniani na kumekuwa na migogoro mahali pengine. “Chukua mfano wa Sudan Kusini miezi miwili, mitatu iliyopita siyo walikuwa wakipigana, huyu Rais anasema yule ni mhaini na yule akatoa vikwazo, mimi siji lazima hiki na hiki kifanyike lakini sasa hivi wako wapi! Si wako wanazungumza na mimi nadhani wanaelekea kuunda serikali ya maridhiano.
“Kwa hiyo sikati tamaa, bado nina hakika kwamba wenzetu waliotoka bado kuna nafasi ya kuzungumza nao kwa kuwapa maelezo na wao watakuwa na fikra zao.”
Alisema kila upande utatoa maoni yake na kufikia mwafaka na kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana.
Kuhusu Tanzania kama inahitaji Katiba Mpya kwa sasa, Malecela alisema: “Mimi hapo nadhani nitawakera kidogo kwa sababu mawazo yangu yako vingine kabisa.
“Suala la Katiba mimi ambaye nimekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa miaka 15 na mara nyingi Katiba zilizokuja ama zimetokana na Tanu au na CCM. Sasa Serikali ya CCM ilileta mapendekezo ya kutunga Katiba Mpya. Nilionana na Tume na nilikaa nao kwa saa mbili kwa hiyo kama ni mawazo yangu niliyatoa huko yote.
“Nafikiri tujaribu kuwa makini. Mradi tumefika mahali tumekuwa na Bunge la Katiba sasa sisi sote hasa viongozi tuliobaki hebu tuwe kama watu wanaoangalia mpira.  “Unajua mpira unaona mchezaji kachoka lakini unasema kimbiakimbia, kumbe mwezako nguvu zimemwishia.
“Tukianza kusema maneno hapa katikati, mimi nikisema watasema unaona hata Malecela kasema... Tuwaachie wenzetu wa Katiba, hawa wajumbe wa Katiba, wakae wazungumze, tutaelewana tu!”
Aliwapongeza wajumbe wa Bunge la Katiba kwa kuendesha Bunge bila kanuni lakini baadaye wakasimama na kujitengenezea utaratibu wao.
“Mfano mdogo, Yanga na Simba unawafungia katika chumba kimoja halafu unawaambia watengeneze sheria za mpira. Watafika mahali fulani wakimuona mchezaji wa Yanga mrefu sana, Simba watasema kwenye kanuni tuweke wachezaji wasizidi futi fulani. Hata hivyo, walifikia mahali fulani wakakubaliana.
Imeandikwa na Frank Sanga, Habel Chidawali na Sharon Sauwa.

Liverpool yamsajili Divorc Origi


Divorc Origi katika mojawapo ya mechi za Ubelgiji
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi hatimaye amejiunga na timu ya Liverpool.
Baba yake Origi, Mike Okoth, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu taifa ya Kenya Harambee Stars amethibitsha mwanawe Divorc amesaini mkataba na Liverpool ambao walifurahishwa na mchezo wake mzuri alipoiwakilisha Ubelgiji kwenye kombe la dunia.

Uingereza:Urusi isiandae michuano

FIFA yaikabidhi Urusi haki za kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Naibu waziri mkuu nchini Uingereza Nick Clegg ametoa wito wa Urusi kupokonywa haki za kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2018.
Ameliambia gazeti la Sunday Times kwamba haiwezekani kwa michuano hiyo kufanyika nchini humo kufuatia hatua ya Urusi kuwaunga mkono waasi wa Ukraine mashariki mwa taifa hilo wanaoushukiwa kwa kuitungua ndege ya abiria ya Malaysia hivi majuzi.
Amesema kuwa ulimwengu utaonekana myonge iwapo utaruhusu michuano hiyo kuendelea nchini Urusi.
Urusi imelaumu Ukraine kwa kuanguka kwa ndege hiyo iliowauawa takriban watu 300.

Papa aomba vita vimalizwe

Pope FrancisPapa Francis ameomba amani kwa dhati katika hotuba ya kila juma katika medani ya St Peter's mjini Rome.
Aliacha kusoma hotuba aliyoandika kuomba vita vimalizwe na hisia ikisikika kwenye sauti:
"makaka na madada, hapana vita, hapana vita, nawafikiria hasa watoto ambao wananyimwa matumaini ya maisha ya maana, ya siku za mbele, watoto waliokufa, walioumia, watoto walioachwa na vilema, waliokuwa yatima, watoto ambao wanacheza na mabaki ya vita, watoto wasiojua kucheka.
Acheni kupigana.
Nakuombeni kwa moyo wangu wote.
Tafadhali, acheni sasa hivi!"

Saturday, July 26, 2014

Israel na Hamas watangaza kusitisha mapigano kwa masaa 12 hii leo

Mkutano wa mjini Cairo hapo jana ulihudhuriwa na John Kerry waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon
Mkutano wa mjini Cairo

Na Martha Saranga Amini
Jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas wamesema hii leo watasitisha mapigano kwa masaa 12 kuanzia saa 2 asubuhi wakati suala la kusitishwa kwa kudumu bado ni kitendawili kwa sasa.

Wakielezea hatua hiyo Wapiganaji wa Hamas wamesema kundi lao na wapiganaji wengine huko Gaza wameafikiana na hoja ya kitaifa ya kujali ubinadamu,ambapo baadaye Israel nayo ilithibitisha kuwa itasitisha mapigano kwa kile ilichokiita ni kufungua dirisha la ubinaadamu katika ukanda wa Gaza.
Taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani ya kundi la Hamas huko Gaza imetoa onyo kwa watu kutokaribia majengo yaliyolipuliwa na kambi za kijeshi kwa kuhofia masalia ya mabomu.
Hata hivyo kuliripotiwa ghasia mapema jumamosi na kuingiza mapigano hayo katika siku ya 19 ambapo mashambulizi ya anga ya Israel yameua takribani watu 19 wakiwemo watoto 4 wahudumu wa afya huko gaza wameeleza.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Katibu Mkuu wa Umoja wa Matayfa Ban Ki Moon wamekuwa katika mstari wa mbele kupata mwafaka ambao hadi sasa haijabainika suluhu litapatikana lini.

Mourinho : Drogba ni Chelsea damu.


Mourinho : Drogba ni mChelsea damu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .
Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 36 aliwahi kushinda mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia mwaka wa 2004-2012 kabla ya kuguria Galatasaray.
Mourinho alidhibitisha kuwa The Blues inatafakari kurejea kwake Uingereza na kuwa anatumai uhamisho huo utatekelezwa bila hisia kali .
"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na timu kwa jumla''.
Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .
Drogba akiwa Galatasaray.
Aliondoka Stamford Bridge mwaka wa 2012 baada ya kutinga penalti iliyoisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich .
Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013.

Wanariadha wa Kenya walalama Scotland.


Wanariadha wa Kenya wakiwa mjini Glascow
Kikosi cha Kenya katika mashindao ya Jumuiya ya madola, yanayoendelea mjini Glascow, kinakabiliwa na wakati mgumu, kutoka na matatizo kadhaa.
Sasa imebainika kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya hawana vifaa vya michezo.
Naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya Tecla Lorupe amesema kuwa wao walifahamishwa siku ya Alhamisi kuwa baada ya wanariadha hawajapokea vifaa na sare zao za michezo.
Lorupe ambaye, ni bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za masafa marefu za Marathon, amesema wao wameshangazwa sana na tukio hilo.
Wanariadha wa Kenya katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini New Delhi
Amesema kumekuwa na matatizo ya kuwasilisha vifaa hivyo vya wanamichezo wa Kenya, kutoka kwa kampuni inayotengeneza mavazi hayo.
Aidha amesema nusura mabondi wa Kenya wakose kushiriki katika mashindano ya mwaka huu, kutokana na ukosefu wa vifaa vyao.
Lorupe amesema walipata bahati wakati, kamishna wa michezo nchini Kenya Gordon Oluoch alipolazimika kutumia fedha fedha zake kununua vifaa hivyo ambavyo vilitumika na mabondia siku ya Ijumaa.
Siku ya Alhamisi, muogeleaji wa Kenya Jason Dunford aliondolewa katika shindano ya mita hamsini butterfly, kutokana na kile alichokitaja kama kutopata vifaa kwa wakati unaofaa.
Mbali na wanariadha kukosa vifaa na mavazi yao, wasimamizi wa michezo mbali mbali nao wanalalamika kuwa hawajapata marupurupu yao.
Hali hii imelleta wasi wasi katika kambi ya kenya huku baadhi ya wanariadha wakiondolewa mapema katika mashindano ya mwaka huu.
Tecla Lorupe
Baadhi yao wanasema, hali duni katika kambi ya maandalizi na hapa mjini Scotland huenda ikaadhiri matokeo ya timu ya Kenya.

PICHA ZA IBADA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWIMBAJI WA NEW LIFE BAND

Angalia picha mbalimbali za ibada ya mazishi ya aliyekuwa mpigaji ngoma(drums) na mwimbaji wa New life band ya jijini Arusha marehemu Eglah Bavuma ambayo yamefanyika jana ijumaa nyumbani kwao mkoani Kigoma na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waimbaji wenzake wa New life band, Upendo Nkone, kwaya ambayo amewahi kuifundisha marehemu wakati akiwa mkoani Kigoma, wazazi, ndugu jamaa na marafiki.

Baba mzazi wa marehemu mwenye fulana nyeupe akiwa msibani nyumbani kwake mjini Kigoma.
New life band wakiimba msibani hapo.
New life band na sura zenye huzuni za kuondokewa na mpendwa wao.
Mchungaji wa kanisa la Pentekoste Patandi mjini Arusha ambako marehemu alikuwa akiabudu akizungumza machache katika msiba huo.
Upendo Nkone akiimba kwa uchungu wa kuondokewa na kaka yake.
Kwaya iliyokuwa ikifundishwa na marehemu kwa takribani miaka 10 kabla hajatoka mkoani Kigoma, ikiimba msibani hapo.

Askofu Kumenya wa kanisa la FPCT akihubiri katika msiba huo.
Kiongozi wa New life band Fortunatus Mabondo akizungumza na watu waliofika msibani hapo.
Baadhi ya umati wa watu waliofika msibani siku ya jana.
Huzuni ikiwa imetawala.
New life band walishindwa kujizuia kuonyesha hisia zao juu ya kuondokewa na mwenzao.
Maua yakiwekwa juu ya kaburi la Eglah.
Hakika Eglah ameacha huzuni kwa wengi.
New life band baada ya mazishi wakiwa katika picha ya pamoja©New life band. Habari na Gospel Kitaa 

Katiba Mpya njia panda, Ukawa waapa kuendelea kususia vikao


Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta akisisitiza jambo juzi, baada ya mkutano wa Kamati ya Maridhiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Rafael Rubava 
Na Fidelis Butahe, MwananchiDar es Salaam. Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiazimia kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), viongozi wa kundi hilo wamesema hawatishwi na uamuzi huo na kwamba wataendelea kususia vikao hivyo.
Kikao kilichokuwa kiwe cha mashauriano kilichoitishwa juzi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta kiliazimia kuzifanya marekebisho baadhi kanuni za uendeshaji kwa lengo la kusimamia nidhamu wajumbe wake, hatua inayotafsiriwa kwamba inawalenga Ukawa.
Jana Sitta akizungumza na Mwananchi Jumamosi alisema mabadiliko yanayokusudiwa kufanywa yatahusisha masuala ya nidhamu, yakiwamo fujo na utoro, mambo ambayo hivi sasa hayawezi kudhibitiwa moja kwa moja na mwenyekiti wa Bunge hilo.
Sitta alikuwa akitoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake jana na kusomwa mbele ya waandishi wa habari na Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad, ikieleza maazimio ya kikao ya usuluhishi alichokuwa amekiitisha kwa ajili ya kutanzua mzozo unaotishia kukwama kwa mchakato wa Katiba Mpya.
Hata hivyo, Ukawa unaoundwa na wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka Vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na baadhi ya wajumbe kutoka Kundi la 201 walioteuliwa na Rais, walisusia kikao hicho na kusababisha uamuzi uliofikiwa kuwa wa upande mmoja.
Hata hivyo, wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, viongozi wa Ukawa ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na yule CUF, Profesa Ibrahim Lipumba walisema hawatishwi na mabadiliko ya kanuni yanayokusudiwa kufanywa na kwamba wataendelea kususia vikao hivyo hadi hoja zao zitakapozingatiwa.
Ukawa walitoka bungeni siku chache kabla ya kuahirishwa kwa awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu mwezi Aprili mwaka huu, kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatumia wingi wa wajumbe wake kutaka kufutwa kwa baadhi ya mapendekezo ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
Kauli ya Sitta
Sitta aliliambia gazeti hili kuwa moja ya kasoro katika uendeshaji wa Bunge ni pale makundi kama Ukawa na Tanzania Kwanza yanapotambuliwa kama makundi rasmi ya Bunge Maalumu, wakati makundi rasmi ni wabunge, wawakilishi na Kundi la Wajumbe 201 wa kuteuliwa na Rais.
“Bunge hili lina uhuru wa ajabu ambao ni mkubwa kuliko Bunge jingine lolote, Bunge ambalo hata uongozi wake hauwezi kumchukulia mtu hatua kwa utovu wa nidhamu eti mpaka umuone mtu anafanya makosa, umpeleke kwenye Kamati ya Kanuni na hivyo ndiyo inakuwa imekwisha maana kama ana watetezi wake wanamtetea,” alisema Sitta na kuongeza:
“Matokeo yake wananchi wanalalamika kwamba hakuna nidhamu bungeni na kwamba kiti kimeshindwa kuchukua hatua, sasa unachukuaje hatua wakati kanuni zetu ndivyo zilivyo?”
Aliendelea: “Yako mambo mengi yanapaswa kufanyika na tuna siku 63 tu za kukamilisha kazi tuliyopewa sasa hatuwezi kutumia fedha za umma na watu wengine wanafanya mzaha, leo huyu anachukua posho, mara anaondoka, haya mambo lazima yatafutiwe dawa.”

Kauli hiyo ya Sitta inaungwa mkono na taarifa iliyotolewa mapema jana ikisema Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge kutokuwa na vipengele vinavyozuia utoro, ukosefu wa nidhamu na matendo mengine yanayolenga kuvuruga mchakato wa Katiba, ni kasoro ambayo lazima itafutiwe ufumbuzi katika kikao kijacho.
Taarifa hiyo inasema kitendo cha Ukawa kuendelea kususia Bunge, kinapuuza wito wa jamii kupitia makundi mbalimbali pamoja na madhehebu ya dini na juhudi za usuluhishi za kutaka kuwezesha vikao vya Bunge hilo viendelee.
“Mambo hayo yote yanazua mashaka kuhusu lengo la wasusiaji kwamba pengine ajenda ya viongozi hawa ni nyingine na siyo upatikanaji wa Katiba. Kwa mtindo huu wa kususa ni vigumu kuweza kupata mwafaka” inasomea sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Sitta.
Mbowe na Lipumba
Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe alisema haamini kwamba kauli kama hizo zimetolewa na Sitta ambaye ni msomi na mwanasiasa mzoefu anayefahamu misingi ya hoja na maridhiano.
“Kanuni hazitungi Katiba, Katiba inatungwa na utashi wa wale tuliopewa dhamana ya kufanya kazi hiyo, sasa ni kwa bahati mbaya kwamba Sitta anafikiri vitisho vya kutunga kanuni za kutubana vitasaidia, haviwezi kusaidia chochote,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Ukawa hatutishwi na mabadiliko ya kanuni, waende wakabadilishe ili dunia nzima iwashuhudie wakipitisha Katiba ya upande mmoja, wasikwepe hoja wanapaswa kutafakari mantiki ya hoja zetu na siyo kutoa vitisho vya kutulazimisha kwenda bungeni, Katiba ni hiari na wala haitungwi kwa vitisho.”
Kwa upande wake Profesa Ibrahim Lipumba alisema Bunge Maalumu la Katiba haliwezi kubadili kanuni ili kumbana au kumfuta mjumbe wa Bunge hilo bila kwanza kubadilishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
“Kwanza, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inatakiwa kufanyiwa marekebisho na Bunge la Jamhuri ya Muungano na siyo Bunge Maalumu la Katiba. Pili, hata Rais aliyeteua wajumbe 201 wa Bunge la Katiba hawezi kuwafukuza kwa sababu haijaelezwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sasa Bunge la Katiba litaweza vipi kuwafukuza,” alihoji.
Profesa Lipumba alisema wajumbe 201 waliteuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kufafanua kuwa hata wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi nao hawawezi kufukuzwa kwa kubadilishwa kwa kanuni za Bunge la Katiba.
“Mbunge wa Jamhuri ya Muungano au Baraza la Wawakilishi ili apoteze sifa za kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba ni lazima kwanza apoteze sifa za kuwa mbunge,” alisema.
Alisema kuwa msimamo wa Ukawa ni kutoshiriki kikao cha Bunge hilo hadi hapo wajumbe wote 629 wa Bunge hilo watakapokubaliana kuheshimu Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi yenye msingi wa muundo wa serikali tatu na siyo serikali mbili.

Taarifa ya Kamati
Mapema katika taarifa iliyosainiwa na Sitta kisha kutolewa kwa waandishi wa habari na Hamad, inaeleza kuwa vikao vya Bunge Maalumu hilo vitaendelea mpaka mwisho hata kama Ukawa wataendelea kususia vikao vyake.
“Kuanzia Agosti 5 Bunge liendelee kwa kuzingatia upya baadhi ya kanuni zake ambazo ni kikwazo katika kuhakikisha kuwa kazi ya kujadili na kupitisha Katiba inayopendekezwa inakamilika ndani ya siku 63 zilizosalia kisheria, yaani 60 za nyongeza na tatu pungufu ya zile siku 70 za awali,” inasomeka taarifa hiyo.
Hamad alisema kikao cha juzi kimeamua Bunge hilo kuendelea kutokana na kuwa na masuala mengi muhimu ya kikatiba ambayo yanawaunganisha Watanzania, yakiwamo usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi, kuikarabati Tume ya Uchaguzi (Nec), kurekebisha kikatiba masuala ya muungano na ukomo wa vipindi vya uongozi.
Taarifa hiyo ilieleza kukerwa na mikutano ya Ukawa inayofanyika katika mikoa mbalimbali nchini. “Hatua ya baadhi ya wajumbe wa Ukawa kwenda kwa wananchi na maoni yao imekuwa siyo mwafaka na siyo wakati wake. Bunge la Katiba liwajibike katika siku za usoni kujibu upotoshwaji wowote kuhusu mchakato wa Katiba kadiri ulivyojitokeza” alisema Hamad.

World Council of Churches - INVITES CHURCHES TO PARTICIPATE IN UN DIALOGUE ON CULTURE AND DEVELOPMENT

Encouraging faith-based perspectives in the United Nations (UN) initiated dialogue on culture and its role in shaping the post-2015 development agenda, the World Council of Churches (WCC) UN office in New York invites churches to participate in an e-consultation.

Led by the United Nations Population Fund, the United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization and the United Nations Development Programme, the Culture and Development consultation seeks participation through e-discussions and papers on best practices in the development areas. Poverty reduction, education, gender equality and women’s empowerment, sustainable cities and urbanization, environment and climate change, as well as inclusion and reconciliation, are the sub-themes of the consultation.

Churches are invited to provide a range of inputs, including papers, documents, perspectives, and intellectual and experiential knowledge. Participants can access the forum through an e-consultation link where the content is available in English, French, Spanish, Russian and Portuguese. The deadline for submissions is 8 August.

The e-discussions and papers, as well as outcomes of the national and global consultations, will feed into the United Nations Development Group report on the outcome of the Culture and Sustainable Development resolution; and the report of the UN Secretary General on the post-2015 development agenda, which will be issued in the fall of 2014.

The year 2015 has marked the target for the Millennium Development Goals that have shaped national and international social programmes since 2000, and current discussions in the UN aim at establishing new methods for sustainable development world-wide.

According to the UN, the “goal of the consultation is to stimulate the exchange of views, experiences and perspectives on the how culture relates to development.”

“We cannot neglect churches’ heritage of working in development areas,” said Rudelmar Bueno de Faria, the WCC’s representative to the UN.

He stressed the importance of faith-based perspectives from churches and Christian organizations in the dialogue on culture and development. “Churches’ voices and experiences are paramount to help shape the global development agenda, based on justice and peace,” he said.

Jason Dunford atangaza kustaafu



Jason Dunford akiwa mjini Glascow
Aliyekuwa bingwa wa Jumuiya ya madola katika shindano la uogeleaji mita 50 Butterfly, Mkenya Jason Dunford ametangaza kuwa atastaafu rasmi baada ya mashindano ya mwaka huu.
Akiongea baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo baada ya kumaliza katika nafasi ya tano, Dunford amesema kuwa, ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kile alichokitaja kama ukosefu wa msaada wa kutosha kutoka kwa wasimamizi wa michezo nchini Kenya.
Amelalamika kuwa hakupewa vifaa vya michezo ili kumwezesha kushiriki vyema katika mashindano ya mwaka huu.
Amesema, kinyume na mashindano mengine alipata mavazi yake ya michezo siku moja tu kabla ya kuingia kidibwini.

CAR:Waasi wataka nchi kugawanywa



kundi la wapiganaji nchini CAR
Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamekataa makubaliano ya kusitsisha vita na kutaka taifa hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
Afisa mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la Seleka ameiambia BBC kwamba wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo yalioafikiwa siku ya jumatano kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.
Joseph Zoundeiko amewalaumu Wakristo wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa kuleta amani na kusema kuwa taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
Mapigano ya miezi kadhaa kati ya makundi ya Wakristo na yale ya Waislamu katika taifa hilo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni wakiwachwa bila makao.
Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
lakini kundi la Human Rights Watch linasema kuwa wapiganaji hao wameelekea katika maeneo ya mashambani na kwamba wameanza kuzishambulia jamii za Wakristo.
Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili.

Gaza:Israel na Hamas wasitisha vita


Kiongozi wa Hamas na mwenzake wa Israel

Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wamekubaliana kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu kuanzia leo asubuhi.
Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.
Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .
Bwana Kerry amesema atendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.

Friday, July 25, 2014

SIMBA, YANGA ZAHUSIKA KUIBOMOA MTIBWA SUGAR KILA MWAKA, MEXIME ALALAMA!

IMG_0733 (1)

SONY DSC 
Mecky Mexime- Kocha wa Mtibwa Sugar
Na Baraka Mpenja, Dar e salaam MTIBWA sugar kila mwaka inabomolewa na timu nyingine za ligi kuu soka Tanzania bara kwa kuwasajili wachezaji wengi muhimu wanaong`ara klabuni hapo. Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mzalendo, Mecky Mexime amesema amejikuta kila mwaka anakuwa na kazi ya kujenga upya timu, kwasababu msimu unapoisha, wachezaji watatu au wanne wa kikosi cha kwanza wananunuliwa na timu nyingine zikiwemo Simba na Yanga. “Timu nyingi zinaangalia kwetu Mtibwa, kila mwaka tunabomolewa, kila mwaka unajenga upya timu, kwasababu wanaondoka wachezaji watatu wanne, tena wachezaji muhimu”. Alisema Mexime. “Sisi...
Kwa habari zaidi ingiahttp://shaffihdauda.com/?p=4124

Meriam Yahya Ibrahim akutana na Papa Francis

White House inasema ina furaha kuu kwamba mwanamke raia wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kukataa kukana imani yake ya kikristo yuko salama na kwamba yuko njiani kuja Marekani.
Meriam Yahya Ibrahim aliwasili Roma Italia Alhamisi pamoja na mume wake na watoto wadogo wawili ikiwa ni pamoja na mtoto wa kike mchanga aliyezalia jela huko Sudan.
Muda mfupi baada ya kuwasili Meriam na familia yake walikutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis. Msemaji wa Vatikan alisema  Papa Francis  alimshukuru Meriam kwa imani yake na ujasiri wake.
 Susan Rice, mshauri wa maswala ya ulizni wa kitaifa Marekani, alisema Marekani  itapata nguvu za kutetea uhuru wa kidini kwa kutumia mfano wa Meriam Ibrahim wakati inapotetea wale wanaonyimwa haki hizo .
Jaji mmoja wa Sudan alimhukumu kifo mama huyo mwezi Mei kwa kukataa kukana imani yake ya Kikristo.Kwa mujibu wa sheria za Sudan,watoto  wa wanaume waislam wanategemea kuwa waislam. Meriam alilelewa na mamake mkristo.
 Mwezi jana mahakama  ilifutilia mbali hukumu yake ya kifo na Meriam na familia wakatafuta hifadhi katika ubalozi wa Marekani mjini Khartoum.

MOURINHO ATHIBITISHA DROGBA KUREJEA


437018_heroa
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amethibitisha kuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Didier Drogba anarudi darajani. Nyota huyo raia Ivory Coast  aliitumikia Chelsea kwa miaka 8 na kuondoka mwaka 2012  ambapo alijiunga  Galatasaray ya  Uturuki baada ya kutwaa kombe la UEFA dhidi ya Bayern Munich. Ingawa ana miaka 36 kwasasa, Mourinho anaamini bado anaweza wa kucheza ligi kuu nchini England na michuano ya kimataifa. ...
Kwa habari zaidi ingiahttp://shaffihdauda.com/?p=4114

The ecumenical movement remembers Rubem Alves, 1933-2014

The ecumenical movement remembers Rubem Alves, 1933-2014
Photo: Instituto Rubem Alves
24 July 2014
By Theodore Gill (*)
Rubem Alves of Brazil, one of the foundational thinkers behind Latin American “liberation theology”, died at the age of 80 on Saturday 19 July. This scholar, teacher, activist, psychotherapist and author is being commemorated by colleagues, former students, journalists and others, including heads of state. Brazilian President Dilma Rousseff hailed him on her Facebook page as “one of the most respected intellectuals of Brazil.”
Different admirers are recalling him from a number of perspectives. For some church members and ecumenical organizations, Alves is being remembered as one of the great educational innovators who helped hone Christian social ethics in light of the theology of liberation, and helped shape the field of ecumenical formation in partnership with theological institutions in North and South, as well as programmes of the World Council of Churches (WCC), the World Student Christian Federation (WSCF), SODEPAX and similar international bodies and conferences of the churches.
Alves once remarked, “Prophets are not visionaries who announce a future that is coming. Prophets are poets who design a future that may happen. Poets suggest a way.” In just this sense, Rubem Alves served as a poet and prophet aligned with the ecumenical movement in times of both turmoil and potential.
As a young student of theology at Campinas, Brazil in the 1950s, Alves joined a group of fellow seminarians “spending their summer vacation,” in his words, “as industrial workers in a factory in Vila Anastácio, São Paulo. The experience was inspired by the worker priests in France who stopped expecting that factory workers would come to church, and decided to meet them where they lived and worked.”
Through the 1960s, Alves alternated between service as a Presbyterian parish pastor and study as a graduate researcher in theology. During the military dictatorship, he was listed as one of the pastors sought by the military and so left to pursue further study outside Brazil.
He earned graduate degrees from Union Theological Seminary in New York City and Princeton Theological Seminary, also in the USA. Although he and the young Catholic theologian Gustavo Gutierrez were then working and publishing on what they termed the “theology of liberation”, these two thinkers did not meet until 1969 near Geneva at an ecumenical consultation of SODEPAX, the ecumenical joint committee on society, development and peace that was co-sponsored by the WCC and the Roman Catholic Church.

Philosophy, life and works of Rubem Alves

Alves is often credited with having informed the philosophy of SODEPAX, and particularly the ethical principles behind its approach to decision-making and social action. At the same time, he became involved as a participant in seminars and conferences convened under the auspices of Church and Society in Latin America (ISAL), a programme that had been strongly encouraged and augmented following the WCC Conference on Church and Society held at Geneva in 1966.
Through the WCC education office staffed by Brazilian educator Paulo Freire, ISAL and the WSCF, chaired from 1968 to 1972 by his former doctoral supervisor M. Richard Shaull, Alves became a figure well-known at international ecumenical conferences and symposia. This culminated in his 1979 presentation at the WCC Church and Society Conference on faith, science, technology and the future, held at the Massachusetts Institute of Technology in Cambridge.
After returning to Brazil, Alves became a university professor whose interests ranged from educational theory to constructive philosophy. His writing encompassed many fields, including books for children. He eventually added psychotherapy to his portfolio and established his own clinic.
The Rev. Sonia Gomes Mota, a minister of the United Presbyterian Church of Brazil and executive secretary of CESE, a Brazilian agency supporting human rights, justice and peace, knew Alves when she was a young girl and he was her pastor. Earlier this week, she recalled his role in her church:
“Rubem Alves was part of a group of pastors, male and female leaders, who reflected and organized different ways of being a Reformed church. This process led to the creation of the United Presbyterian Church of Brazil (IPU), now a member of the WCC. With his erudition, his ecumenical and social commitment, he helped draft the founding documents that are a basis of the IPU. He was not interested in giving us moral lessons or transmitting the absolute and indisputable truth. As a good theologian, philosopher and educator, he was more interested in making us think, reflect and question the immutable truths of theology and urged us to envision new possibilities and new ways of living our faith. Rubem led us to deserts and invited us to be gardeners and planters of hope.”
In later years, Alves would retain a pastoral and prophetic touch with the people he encountered, but his association with institutional religion became more reserved.
Following the death of Richard Shaull, the theologian and one-time WSCF leader under whom he had studied at both Campinas and Princeton, Alves composed a brief but heart-felt tribute that was published by the World Alliance of Reformed Churches in its journal Reformed World titled “Through the eyes of Dick Shaull” in September 2006. He depicted his late friend as a poet and a prophet who often fell out with people of influence in the churches. Alves wrote, “Prophets are cursed beings.”
He concluded the essay on his mentor’s passing in these words: “Now he is enchanted. He departed. Of course, I will plant a tree in his honour in my lonely little orchard, on a mountain top, at the side of a volcano, near the trees of other conspirators… In their silence, when no one is around, the trees will talk to each other.”
[933 words]
(*) Written by Theodore Gill, senior editor of WCC Publications in Geneva and a minister ordained by the Presbyterian Church (U.S.A.), with report from Marcelo Schneider, WCC communication liaison for Latin America based in Brazil.

AMBASSADORS OF CHRIST 'KWETU PAZURI' WAPIGA HATUA NYINGINE

Ambassadors wakiwa kwenye sare za kupendeza wakati wakirekodi album mapema jumanne usiku wiki hii.
Kwa mara nyingine kwaya ya Ambassadors of Christ ya nchini Rwanda siku ya jumanne wiki iliyopita ilirekodi dvd yake live huko Kigali nchini Rwanda ikipewa jina la 'Ibatebuli recording concert' na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi wa kwaya hiyo ambayo walivaa sare zao nadhifu na zenye kupendeza.
Tukio hilo la kurekodi ambalo jina lake 'Ibatebuli' ni lugha ya Tonga inayozungumzwa nchini Zambia na Malawi linamaanisha wavunaji ikiwa ni tafsiri ya wimbo wao maarufu wa 'Abasaruzi' ambao kwasasa pia umetafsiriwa kwa lugha hiyo ya Tonga ikiwa ni kupanua wigo zaidi wa injili kwa kwaya hiyo ambayo ilipokelewa kwa kishindo nchini Zambia mwishoni mwa mwaka jana ilipokwenda kutoa huduma licha ya kwamba Zambia ina kwaya zenye nguvu na uimbaji maridadi. 
Kwaya hiyo ambayo imekuwa ikitoa album zake kwa lugha ya kwao kinyarwanda pamoja na kiganda huzitafsiri nyimbo zao kwa lugha ya kiswahili pia jambo ambalo si tu linaongeza wigo wa uinjilishaji lakini pia mapato ya kwaya hiyo yanaongezeka na kuwawezesha kusonga mbele na huduma yao. Ambapo kwasasa wameanza mikakati ya kuimba lugha nyingi zaidi ikiwemo hiyo ya Tonga ili kuwafikia watu wengi zaidi ili wamjue Mungu.

Nelson pamoja na dada yake Sara Uwera wakiimba kwahisia wakati wa kurekodi.
Yusto akiimba huku sura ikiwa imejaa matumaini wa kile akiimbacho.
Flora pamoja na Pepe wakiimba kwa furaha.
Jimmy mmoja kati ya solo wa muda mrefu akipaza sauti yake kumtukuza Mungu.



Joseph naye hakuwa nyuma kumtukuza muumba wake.
KJ Marcello akiimba kwa tabasamu kubwa. Ndiye mmiliki wa picha zote.
Ambassadors wakiimba.
Picha ya pamoja baada ya huduma.
Ambassadors of Christ Choir ©Kj Marcello na Habari hii kwa hisani ya Mtandao wa Gospel Kitaa