Writen by
sadataley
1:58 PM
-
0
Comments
Askofu Lucas Yudah Mbedule
Ufafanuzu wa Kibiblia
kuhusu
1.
Siku
ya Mitende na Juma Takatifu
2.
Usiku
wa Kuwekwa(Kuanzishwa) Chakula cha Bwana.
3.
Ijumaa
Kuu( Mashtaka,Hukumu,Mateso na Kifo cha Yesu Kristo
4.
Jumapili
ya Pasaka( Yesu Amefufuka)
5.
Jumatatu
ya Pasaka( Yesu Mfufuka anajidhihirisha kwa watu wote)
Neno Pasaka linaanza tangu
Agano la Kale (Kutoka 12;18-20) Katika historia ya Ukombozi wa Wana wa Israel Misri.
Huko walikotumikishwa na Farao na Wa
Misri. Neno Pascha ni neno la Ki
ebrania lenye maana ya Kupita,kuvuka kuondoka na na neno ambalo kwa Kiingereza
ni PASSOVER, Kwa maana ileile kupata,aukuvuka na neno hilo lilitohole wa moja
kwa moja kwenda kwa lugha ya Kiswahili na kuitwa “Pasaka” toka Ki ebrania na Kiingereza na kulitumia kama neon la
Kiswahili( Luka 22:1) hapa Pasaka inaakisi tukio la kukombolewa kutoka Misri.
Hivyo Wayahudi waliiadhimisha
siku hii kila Mwaka wakati wa Mwezi wa
NISSAN ambao ni kati ya Mwezi Machi na Aprili( maana yake unaanzia (Tarehe 15 Machi
hadi 15 April hivi kipindi hiki huitwa Nissan yaani kinagusa miezi miwili
pamoja.
Mfano kalenda ya
Kiyahudiinasomekahivi
1.
Nissan ni
Mwezi wa Kwanza ( Machi – April)
2.
Iyar ni Mwezi wa Pili ( April
– Mei)
3.
Sivan ni Mwzi wa Tatu ( Mei – Juni)
4.
Tammuz ni Mwezi wa Nne ( Juni – julai)
5.
Av ni MweziTano ( Julai – August)
6.
Elul NI Mwezi wa Sita ( August – Septemba)
7.
Tishri Mwzi wa Saba ( Septemba – Oktoba)
8.
Cheshvan
Mwezi wa Nane ( Oktoba –Novemba)
9.
Kislev
ni Mwezi wa Tisa ( Novevemba – Desemba)
10.
Tevet ni Mwezi wa Kumi ( Desemba – Januari)
11.
Adari(Leap
years only) Mwezi wa kumi na moja(
Januari-Februari)
12.
Adari
( unaitwa adaribeit in leap years) Mwezi wa kumi na mbili( Februari – Machi)
Hivi ndivyo Wayahudiwa
navyoisoma miezi yao( kwao miezi ni majira siyo siku. Kwa hiyo majira husika yakibadilika
ndivyo hutaja Mwezi. Linganisha na sisi kipindi cha Mvua za vuli, hatuangalii
Tarehe tunaangalia majira.
Na hivyo hata wakati
wa Yesu amaeikuta ikiadhimishwa(Mathayo 26;1-5).
Waliiadhimisha kukumbuka
Mateso yao kule Misri, na jinsi walivyokombolewa na Mungu kwa njia ya Mtumishi
wake Musa( Kutoka 3:7ff)
Katika Kutimiza Mpango
wa Wokovu Yesu anaingia Katika Historia ya Wokovu wa Wayahudi ili Wokovu wa
watu wote.
Kwa hiyo tunapoangalia
maana ya Maadhimisho haya, tunapaswa kuangalia kwanza Mwanzo wa Juma
linalotangulia Pasaka, Tunaingizwa kuchunguza( habari hii inasimuliwa na Injili
zote Nne yaani Mathayo,Marko,Luka na
Yohana) tofauti na habari ya kuzaliwa ambapo Marko hazungumzi kuzaliwa.
Yesu anavyoingia Yerusalemu Kama Mfalme, lakini kwa Jicho la
Wayahudi wanamwona ni Mfalme wa Kidunia.
Siku ambayo huitwa
siku ya Mitende au siku ya Matawi, aina hii ya majani ilitumiwa na Wayahudi kwa
mapambo Katika sikukuu hasa wakiwapokea watawala wao Zaidi kwa Kaisari pekee.
Pia mshtuko mwingine
Katika hisia za viongozi wa serikali ya Kirumi ni Wimbo ambao Yesu anaimbiwa
..Hosia na Mbarikiwa ajaekwajina la Bwana….(……..)Inaonekana pia uliongeza hasira
kwao kwa kuwa huyu anayeimbiwa na kupokelewa
kwa heshima kubwa hana cheo wala nafasi Katika utawala wa Kirumi.
Maadhimisho ya Siku ya Alhamisi ya Pasaka
Kama
siku ya Kuwekwa au kuanzishwa Meza ya Bwana (Lord’s Supper) na Kukanwa kwa Yesu
na kuachwaPekee yake.
Wakristo tunakutana
kwa maana ya kujiimarisha Kiroho kwa kutafakari
upendo wa Mungu( Yohana 3:16)
kumtoa Mwana wake, hapa siku tunaona na kujikumbusha hatua kwa hatua tena za
awali za Maandalio ya Yesu kuagana na wanafunzi wake , Yesu
kuwaombea, tena kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana( Mathayo 26:26)
Ndiyo maana makanisa yote(
mainline Churches) huadhimisha tendo hilo kama Sakramenttakatifu (Eucarist).
Kwa Mkristo kuiheshimu
kuitunza siku hii ingepaswa kuwa tabia
ya Muhimu kwa kuwa ndiyo kiini cha Historia ya Ukombozi ambao Mungu aliupanga
kwa Mwanadamu.(Yn 3;16)
Maadhimisho ya Ijumaa Kuu (Good Friday)
Kama kukumbuka(Commemorate) Mashitaka,hukumu,Mateso na
Kifo.Ni siku muhimu kwa kutafakari mashtaka, Hukumu,Mateso na kifo cha Yesu.
Kuiadhimisha siku hii
ni kuingia kwa undani kuona uzito wa tendo la Yesu Kufa badala yetu sisi tulio stahili
kufa. Watu wengi hawachukulii uzito unaostahili IBADA hizi labda kwa kukosa maelezo
sahihi kwa kuwa kadiri siku zinavyokuja uzito wa Ibada hizi unapungua kabisa.
Pengine Nyimbo na
Mahubiri hayaandaliwi kutuingiza kwa undani kutafakari maana ya Siku hii Katika
maisha ya Kiroho.
Pia ni nafasi ya
kutafakari ni jinsi gani vyombo vyetu vya kutunza sharia na haki za watu kama
mahakama na vyombo vya ulinzi vinatoa haki kwa raia wake.( rejeahukumu ya Yesu kubambikiziwa
mashitaka)
Vyombo vyetu vya Makanisa
ni kwa jinsi gani vin ajali na kutunza hali Katika kuamua mashauri yao
Muhimu: Siku ya
Alhamishi ni (Commemoration not Celebration) Kuadhimisha kwa Kukumbuka siyo Kusherehekea.)
Ni tendo kubwa hapo la Kukumbuka. Maana yake tunaadhimisha kwa kukumbuka. Mfano
tunaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha ndugu tuliyempenda( to Commemorate) lakini
katika Jambo la furaha , tunasherehekea( to
Celebrate). Ibada ya Kufufuka hiyo ina mambo yote mawili( Tunakumbuka na
Kusherehekea Ushindi wa Yesu kutoka Mauti. Ikor 15:55-5.
Maadhimisho ya Pasaka yenyewe
Jumapili inayofuata Ijumaa
Kama siku ya Wakristo kukumbuka kufufuka kwa Yesu
Kristo kutokaMauti na Kaburi.Ushindi dhidi ya Kifo na dhambi,.
Siku hii muhimu wake
Mkubwa ni Ushindi kwa kuwa Yesu kuwa amefufuka toka kaburi, Mungu amemfufua ni
siku ya furaha kwa Wakristo na matumaini ya maisha ng’ambo ya kifo cha kimwili.
Yesu anjidhihirisha kuwa ni mshindi wa Mauti (Ikorinth 15;55-56).
Kiini kikuu: Ni furaha, Haleluya Bwana Amefufuka Kwelikweli,
Watu waondolewe hofu na mashaka yote dhidi ya Shetani dunia na Kifo. Katika
Ibada hizo za furaha waoneshwe matumaini yaliyong’ambo ya maisha haya kuwa kuna
Maisha mapya.
Watu waoneshwe jinsi
Yesu alivyo na nguvu dhidi ya maumivu na Shida zetu. Lakini pia waonyeshwe kuwa
Yesu anatenda mwenyewe lakini pia anatumia vyombo vya kidunia ili kuendelea
maisha ya hapa Duniani pia( Yohana 9:7 Yesu anataka kuonyesha kuwa Hospitali zetu
pia ni vyombo vya kutunza uhai na maisha yetu. Yesu anataka watu waishi duniani
vizuri na kufurahia uumbaji kwa kuwafufua waendelee na maisha yao ya kila siku,
lakini pia Yesu anaruhusu pia kifo ilitufike ng’ambo ya pili yaani uzima wa
milele( Yohana 11;43)
Jumatatu ya Pasaka
Kama maadhimisho ya Kukumbuka
Yesu Mfufuka anavyojitokea na kujidhihirisha kwa watu Katika maisha yao ya
kawaida kama (a) kutembeanao Safarini (b)
kuzungumza nao(c) kulanao(d) kubarikinyumba na maisha yao.Lk 24:13-35)
Kleopa na Mwenzake asiyejui
kana jina walitembea na Yesu kitambokirefu, walizungumza naye kitambo kirefu hata
pia walimdharau kwanini amechelewa kujua habari zilizo pomjini? Luka 24:17-18, Wakasimama wakakunja nyuso zao;
Wakamwuliza Yesu;……. Je wewe pekee yako
u Mgeni Katika Yerusalem, hata huya juiyaliyotukia?
Pia habari hii
inaonyesha kuwa tunaposafiri inaonekana wako wanaojulikana kwa majina na
Ukristo wao lakini wengine hawajulikani hata kama wapowapo(Kleopa anatajwa
Katika kujadiliana na Yesu.
Wewe Jina lako linafahamika
wapi Zaidi kwa Yesu au nje ya Yesu?
Siku
hii ni ya muhimu pia ni maalumu kwa kutakari Jinsi Yesu Mfufuka ambavyo anajitokeza
kwa mtu mmojammoja kama Mungu pamoja na watu wakeyaaniEmanuel ( Luka 1:23)
Ndiyo tunakutana na
Yesu Katikati ya wasafiri,Yesukatikati ya mazungumzo ya kawaida na Yesu
katikati ya familia na anashiriki chakula baada ya kukaribishwa.
Fundisho la Ibada hii ya Jumatatu ni kuwa
Bwana Yesu anavunja na kuvukamipaka na vikwazonakuingia Katika maisha ya
mtu mmojammoja na vikundivya watu(Mfano wa jumuiandogondogo Katika maisha ya
Kanisa).
Lakinitunajifunza kuwa;
1.
Watu
wanawezakujisahau na kwendamwendamrefu wa maisha bila kumsikiliza na kumwelewa
Yesu wa kumpanafasi.
2.
Familia
inaweza kwenda mwendo mrefu wa maisha bila kumkaribisha Yesu na kumpa nafasi
Yesu ili awe Baraka kwa familia.
3.
Kanisa
pia linaweza kwenda mwendo mrefu bila kumkaribisha Yesu wa kumshirikisha Yesu.
Tunaweza kumhubiri,kumwimba
na kumtaja Yesu lakinitusimfahamu wala kumsikiliza.
Msingi mkubwa wa
Sikukuu hizi Katika Kanisa na Jamii unapaswa
kuwa ni kama KIOO cha kujiangalia na kujitathimini hali yetu ya wakati husika kufuata
mazingira husika kifamilia,kijamini,kisiasa na kiutamaduni.Ujumbe mkuu wa majira ya Pasakani AMANI. Mungu awabariki wote
ilitukafanyike viwanda vya kuzalisha amani. Naawape Mwanga wa kufahamu mambo
hayo kwa ajili ya kukua ki roho.
Kwa jina la Baba na
la Mwana na la Roho Mtakatifu Amen.
Imeeandaliwa na Askofu Lucas Mbedule Judah (KKKT DAYOSISI YA KUSINI
MASHARIKI MTWARA)
No comments
Post a Comment