Writen by
sadataley
10:40 AM
-
0
Comments
Mdau wa GK hapana shaka kwamba kama kuna mtu hii leo akiulizwa ni kwaya gani ya kanisa la African Inland Church (A.I.C) Tanzania anayoifahamu, hapana shaka jibu jina la kwaya ya AIC Chang'ombe (CVC) halitakosekana mdomoni mwake, je unajua ni kwasababu gani? KWA TAARIFA YAKO ni kwamba kwaya hii yenye makazi yake Chang'ombe kwa sokota jijini Dar es salaam, imejizolea mashabiki lukuki ndani na nje ya nchi yawezekana kuliko kwaya yoyote ya kanisa la A.I.C Tanzania.
KWA TAARIFA YAKO moja ya vitu vilivyoitambulisha kwaya hii, ni uimbaji wao hasa utunzi wa
Papaa Clement Buhembo |
nyimbo waziimbazo ambazo zimeonekana kuwagusa wengi toka walipotoa album
ya Vunja nguza za giza ikiwa ni DVD yao ya kwanza kuwatambulisha wakiwa
wamerekodi Habari Maalum ya jijini Arusha, baada ya hapo wakaja na
Gusa, kabla mambo hayajapoa wakatoa Jihadhari na mpinga Kristo, mambo
yakanoga zaidi wakatoa album ya Usiku wa manane ambayo bado hawajaipatia
mdogo wake.
Je umewahi kujiuliza kwamba imekuwaje kwaya hii imeweza kuvuta maelfu kununua kanda zao kila wanapotoa toleo jipya? KWA TAARIFA YAKO
licha ya kuwa na watunzi mbalimbali wa kwaya hiyo wakiongozwa na
mwalimu wao aitwaye Steven Deffa, kwaya hii inamtunzi wake mwingine wa
nyimbo ambaye nyimbo alizozitunga zimeitambulisha kwaya hiyo zaidi huyu
si mwingine bali ni mwalimu Clement Buhembo almaarufu kama Papaa,
mwalimu huyu ametunga nyimbo kama Vunja, Gusa, Badirika, Jihadhari na
mpinga Kristo, Usiku wa manane na nyimbo nyinginezo za kwaya hiyo ya
Chang'ombe.
KWA TAARIFA YAKO mwalimu huyu kipawa chake amekifundisha na kwa kwaya nyingine kama Kinondoni Revival wimbo uitwao Hakikisha ulio kwenye album yao ya Mtu wa nne, hapana shaka unaipata album ya Kekundu kutoka kwa kwaya ya vijana Makongoro Mwanza ni kazi nzuri ya mwalimu huyu, je umewahi kuisikiliza album iliyopita ya AIC Dar es salaam Choir? moja ya album ambayo mimi binafsi mpaka leo naona ni kati ya album bora zilizowahi kurekodiwa na kwaya hiyo, sikiliza wimbo uitwao Huwezi utunzi wake Papaa huku pia ukipata muongozaji makini mwanadada Mercy Nyagwaswa Mwalukasa. KWA TAARIFA YAKO Papaa hakuishia hapo ameifundisha kwaya ya Ukombozi Msasani Lutheran nyimbo mbili ambazo hata hivyo bado kwaya hiyo haijaingia studio kuzirekodi.
KWA TAARIFA YAKO Papaa amezitungia nyimbo kwaya mbalimbali za kanisa lake la AIC na nje ya kanisa hilo kama nilivyozitaja hapo juu. Licha ya kufundisha katika kwaya nyingi lakini bado Chang'ombe wameonekana kuendana na namna ya utunzi wa nyimbo zake, kwakuwa katika album zote alizoshiriki utunzi na kwaya hiyo, basi zitatokea kupendwa sana, hata sasa GK imepata taarifa kwamba wakati album ya Usiku wa manane ikingali ikifanya vizuri sokoni, tayari mwalimu huyo ameshafundisha nyimbo nyingine kali za album nyingine ya kwaya hiyo ambayo bado haijajulikana wataingia lini studio, mwezi Disemba mwaka jana ilitimiza miaka 25 toka kuanzishwa kwake.
Papaa wa tatu kutoka kushoto, akiwa na watunzi wengine wa nyimbo wa kwaya ya Chang'ombe wakati wa jubilee ya miaka 25 ya kwaya hiyo Desemba mwaka jana. |
KWA TAARIFA YAKO Papaa ana wanafunzi wake ambao nao wanafuata nyayo zake kwakufundisha kwaya mbalimbali kwa nyimbo zenye muelekeo wa Papaa. Pamoja na uimbaji mzuri wa kwaya ya Chang'ombe, GK inaweza pia kuthubutu kwamba kwa Tanzania ndiyo kwaya inayoongoza kwakuwa na sare nyingi na nadhifu hata unapoangalia video zake unajua hii kwaya wote vibosile kutokana na kuonekana kuvaa sare za gharama kumbe ni mpangilio tu wa mavazi na uchaguzi mzuri wa sare. Ni kwaya yenye maono makubwa ya kiroho na kimwili pia kwa maana ya kuwasaidia wanakwaya wake BONYEZA HAPA
Mrs Lydia Kashimba akiongoza wana wa Gusa, kugusa pindo la Mungu uwanja wa Kambarage Shinyanga. |
Mrs Bahati Meshack akiongoza wenzake kumsifu mungu, uwanja wa Kambarage Shinyanga. |
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo vinginevyo, tukutane wiki ijayoo…...
Habari ni kutoka www.gospelkitaa.co.tz
No comments
Post a Comment