Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 31, 2013

KIONGOZI WA ZAMANI WA MALI AONGOZA KWA KURA

Waziri Mkuu wa zamani nchini Mali Ibrahim Boubakar Keita anaongoza kwa kura za Urais, katika uchaguzi unaonuia kurejesha utawala wa demokrasia nchini humo. Duru za serikali zinasema aliyekua Waziri wa Fedha, Soumaila Cisse anafuata Bw Keita, huku theluthi moja ya kura ikiwa imehesabiwa.
Ibarhim Boubakar Keita
Upande wa Bw. Cisse imepinga matokeo hayo na kutaka tume ya kimataifa kuhesabu kura za uchaguzi huo wa Jumapili. Mali ilikumbwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka jana pamoja na maasi Kaskazini mwa nchi. Ufaransa ilituma kikosi cha wanajeshi 4,000 kuyakomboa maeneo ya kaskazini kutoka kwa wanamgambo wa kiisilamu.
Vuguguvu la Ukombozi wa jamii ya Tuareg ikisaidiana na wapiganaji wa kiisilamu walitwaa eneo nzima la Kaskazini, kabla ya muungano huo kusambaratika. Makundi hayo yalifanikiwa kunyakua Kaskazini mwa nchi baada ya jeshi kuipindua serikali ya kiraia ikilalamikia kutopata ufadhili kukabiliana na maasi Kaskazini mwa nchi.
Mapema mwezi huu, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilitumwa Mali ili kusaidia katika shughuli za uchaguzi na kurejesha utawala wa kidemokrasia.Ufaransa umepongeza uchaguzi wa Mali, huku Muungano wa Ulaya ukisema shughuli hiyo ilifanyika bila visa vyovyote. Bw Keita maarufu kama "IBK" ana sifa ya kuwa na mabavu.
Mwanasiasa huyo aliendesha kampeini yake kwa ujumbe wa kurejesha hadhi kwa Mali akisema taifa liliisha hadhi yake kwa kuomba msaada wa Ufaransa ili kuinusuru dhidi ya kuporomoka.Viongozi wa kidini wengi wakiwa Waisilamu waliwaomba raia kumpigia kura, pia anaonekana kuungwa mkono na jeshi. Bw. Cisse aliunda chama cha Union for the Republic and Democracy (URD) mwaka wa 2003 na ametaka jeshi kutojihusisha na siasa.Jumla ya wagombea 27 walichuana Urais, huku watu milioni 6.8 wakijiandikisha kupiga kura nchini Mali.

ZIMBABWE YAPIGA KURA KUPATA UTAWALA MPYA

Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang'atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.
  Wapiga kura Zimbabwe
Foleni ya Wapiga kura
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.

Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika{AU}, Kanda ya Kusini mwa Afrika{SADC} na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata. Bw.Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.
Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo.Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura leo ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali mpya.
Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.
Imewekwa na Happy Adam

SERIKALI YATANGAZA WANAOKWENDA UALIMU

Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa wakuu wa vyuo wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa ni wale waliopo kwenye orodha iliyotolewa na wizara na si vinginevyo.
                         Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr  Shukuru Kawambwa. 

Dar es Salaam. Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.

Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alisema wanafunzi wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo walivyopangiwa kuanzia Agosti 15, mwaka huu.
“Usajili utafungwa Agosti 25 saa 12:00 jioni, ‘Joining instructions’ (fomu ya maelekezo ya kujiunga) zitatumwa kwa wahusika kupitia anuani zao.... fomu hizi pia zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,” alisema.
Taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyotolewa baadaye jana ilisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na cha sita vinavyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) , ada ya muhula wa kwanza Sh100,000 au Sh200,000 kwa mwaka.
Wanatakiwa kuwa na “Sare ya chuo kulingana na maelekezo ya chuo husika, fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi,” inasema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa wakuu wa vyuo wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa ni wale waliopo kwenye orodha iliyotolewa na wizara na si vinginevyo.
Wengi wa wanafunzi hawa ni wale waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012 na kidato cha sita mwaka huu. Kwa upande wa wale wa kidato cha nne, matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yalionyesha kuwa watahiniwa 159,609 wa shule walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne.
Inaonyesha pia kuwa kwa upande wa Tanzania Bara, wanafunzi 34,599 walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu na kati yake waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi walikuwa ni 34,213.
Kwa upande wa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, watahiniwa waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 44,366 kati yao 40,242 wakiwa ni wa shule. Matokeo hayo yanaonyesha pia kuwa, watahiniwa 35,880 ndiyo waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu.
Kwa mujibu wa Kitabu cha Takwimu cha Wizara ya Elimu (Best), mwaka 2012 wanafunzi 17,095 walichaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya ualimu nchini.
Imewekwa na Happy Adam

KIFO NI BORA KULIKO KUOLEWA.

Ni mara baada ya mtoto kutoka Yemeni mwenye umri wa miaka 11 kutaka kuozeshwa na wazazi wake,akili kwa kusema kwamba elimu ni bora kuliko kuolewa.
Watch this video
Mtoto mwenye umri wa miaka 11 aliyekimbia kutokana na wazazi wake kutaka kumuoza.

"unaweza kupata furaha pale unapoozwa wakati umri hauruhusu?" mtoto huyo aitwaye  Nada Al-Ahdal aliuliza.

Mtoto huyo aliweza kulalamika na kuwalaani wazazi wake marabaada ya kutaka kumuoza mtoto huyo ili waweze kupata fedha kwaajili ya mahitaji yao.

"kifo kitakuwa ni furaha kwangu" Nada Al-Ahdal alisema kwa masikitiko makubwa.
Mtoto huyo pia aliweza kuzungumza kwa niaba ya watoto wote ambao huolewa kabla ya umri wao huko Yemeni,na aliweza kusema kwamba ni kipi hasa kinachofanya mpaka waolewe kabla ya wakati na aliweza kuuliza kwamba ipi ni haki yao anbayo wanaipata na badala yake kuishia kuolewa tu.

pia imeweza kuthibitika kwamba ni asilimia kubwa ya watoto ambao huweza kuolewa kabla ya umri huko Yemeni.
kwahabari zaidi:http://edition.cnn.com/2013/07/30/world/yemen-child-marriage/index.html?hpt=hp_c1

Imewekwa na Happy Adam

PAPA FRANCIS ALIA NA MTOTO WA BRAZIL AMBAYE ANAPENDA KUWA KUHANI.

Huko Rio de Janeiro, Brazil, Nathan de Brito ambaye ni mtoto mdogo amfanya Papa Francis kutoa machozi baada ya kumwambia kuwa atapenda kuja kuwa kuhani.
                 
                 Papa Francis akidhihirisha, kilio na Nathan wakati wa WYD
"mimi nataka kuwa kuhani wa Kristo, mwakilishi wa Kristo,"mtoto huyo aitwaye de Brito ambaye  alimtia wasiwasi katika masikio ya Papa Francis, baada ya kuruka vikwazo na kufanya njia yake ya kupenda kuwa kuhani katika taifa lake la  Brazil.
"Mimi naenda kuomba kwa ajili yenu, lakini ninawaomba kuomba kwa ajili yangu," Papa Francis alijibu, wakiongozwa na machozi na kuaganana naye.

Imewekwa na Happy Adam


Tuesday, July 30, 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHINAWATRA AWASILI NCHINI TANZANIA KWA ZIARA YA SIKU TATU.


Raisi wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimpokea Waziri Mkuu wa Thailand bi Yingluck Shinawatra katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere leo hii.



                  Mh.  Rais  Jakaya Kikwete akimkaribisha Waziri  Mkuu huyo wa Thailand.


Waziri  Mkuu wa Thailand akisalimiana na viongozi wa hapa nchini Tanzania.


hapo ni Waziri  Mkuu wa Thailand bi.Yingluck Shinawatra akikagua gwaride mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwl.Julius Nyerere.


Waziri  Mkuu Yingluck Shiwawatra na mwenyeji wake Mh.Jakaya Kikwete wakikagua ngoma za asili baada ya waziri huyo kuwasili nchini.


Waziri  Mkuu Yingluck Shinawatra akisalimiana na baadhi ya raia wa Thailand waishio nchini Tanzania.


Raisi Jakaya Kikwete alipowasili katika Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Bi.Yingluck Shinawatra


Rais Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Waziri  Mkuu  Bi.Yingluck Shinawatra jijini daresalaam leo.

Imewekwa na Happy Adam

PAPA APINGA MADAWA YA KULEVYA

Kiongozi wa kanisa katoliki, Baba mtakatifu Francis, amekosoa vikali mipango ya kutaka kuhalalisha madawa ya kulevya Amerika ya Kusini.
                      
                          Baba Mtakatifu akiwa katika ziara yake nchini Brazil
Aliyasema hayo wakati alipotembelea klikini mpya ya kuwatibu waraibu wa dawa za kulevya mjini Rio de Janeiro.
Uruguay inakaribia kuidhinisha uuzaji wa Marijuana au Bhangi huku baadhi ya nchi katika kanda hiyo zikitafakari hatua sawa na hiyo.Vyanzo vya matumizi mabaya ya madawa ya kulevya lazima vitatuliwe, alisema papa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini Brazil.
Awali Papa Francis mzaliwa wa Argentina alishiriki misa yake ya kwanza katika ziara yake katika kanisa la Our Lady of Aparecida.
Aliwaonya maelfu ya waumini dhidi ya kukumbatia sana pesa, mamlaka na raha za dunia.
Baada ya ziara yake eneo la Aparecida, nchini Brazil Papa alirejea mjini Rio de Janeiro.
Wakati wa ufunguzi wa kliniki ya kutoa matibabu kwa waraibu wa madawa ya kulevya, aliwakumbatia waliokuwa watumizi wa dawa hizo, huku akiwasikiliza wakisimulia yaliyowakumba wakati wa uraibu wao.
"ni muhimu kukabiliana na vyanzo vya matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, kuhakikisha haki na kuwafunza vijana kuhusu umuhimu maadili mazuri katika jamii, kuwasaidia wanaokabiliwa na matatizo na kuwapa matumaini,'' alisema Papa.
Papa Francis pia alionya dhidi ya mipango ya kuhalalisha madawa ya kulevya katika kanda ya Amerika ya Kusini huku akiwalaani walanguzi wa madawa hayo.
Imewekwa na Happy Adam

KISA CHA WATOTO MATEKA GHANA

Polisi nchini Ghana wanawahoji wazazi walioshtakiwa kwa kuwafungia nyumbani wanao walio kati ya umri wa miaka minne na minane tangu kuzaliwa kwao.
                          
Polisi walivamia makao yao yenye vyumba vinne mjini Accra,siku ya Ijumaa na kuwaokoa watoto hao , mvulana mmoja na wasichana wawili.
Wazazi hao waliwaambia polisi kuwa hawakutaka kuwatoa wanao nje kwa hofu ya kukusanyika na watu waovu.
Watoto hao sasa wamepelekwa katika makao ya kuwatunza watoto huku kukiwa na hofu kuwa wazazi wao huenda ni wagonjwa wa akili.
Mwandishi wa BBC mjini Accra anasema kuwa kisa hicho kimewashangaza sana watu mjini humo.
Inaarifiwa watoto hao walifungiwa nyumbani tangu kuzaliwa kwao na hawamkujua yeyote isipokuwa wazazi wao.
Aidha watoto hao waliishi katika chumba kimoja, huku Kondoo na kuku wakiwa katika vyumba viwili huku wazazi wao wakilala katika chumba chao kwenye nyumba hiyo iliyikuwa imejaa uvundo.
Nyumba ilionekana kama isiyoishi watu na licha ya kuwa haikuwa imesafishwa kwa miaka mingi, kuta zake zilikuwa na michoro.
Polisi walivamia nyumba hiyo baada ya jirani mmoja mwenye shauku kuwaarifu .
Wazazi wa watoto hao wanahojiwa na polisi pamoja na madaktari wa magonjwa ya kiakili mjini Accra, huku watoto hao wakipewa malezi na familia moja.
Msemaji wa polisi alisema kuwa wazazi wa watoto hao hawakuwahi kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba yao.
Watoto waliwaarifu polisi kuwa baba yao ambaye hakuwa na ajira, aliwasomesha hesabu na kiingereza nyumbani kwao.
Imewekwa na Happy Adam

WASIWAS KUHUSU UCHAGUZI ZIMBABWE

Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kanda ya Afrika Kusini, Bernard Membe, ameelezea wasiwasi mkubwa kuwa daftari la wapiga kura lingali kutolewa siku moja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.
                            

                            Mugabe anamenyana na Morgan Tsvangirai kwenye uchaguzi mkuu
Hii ni licha ya kuwa daftari hilo kuwa kiungo muhimu kwenye uchaguzi utakaofanyika Jumatano.
Shughuli ya kupiga kura itamaliza serikali ya Muungano kati ya MDC na chama cha rais Mugabe Zanu-PF .Chama cha MDC chake hasimu wa rais Mugabe, Morgan Tsvangirai, kimesema kinajiandaa kwenda mahakamani kuweza kupata daftari hilo.
Rais Mugabe anataka kugombea urais hata baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka 33. Anamenyana na waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Ikiwa imesalia siku moja kabla ya upigaji kura, hakuna chama kilichopokea sajili la wapiga kura.
Mahasimu hao wawili wakuu, wamekuwa wakigawana mamlaka tangu mwaka 2009, baada ya mkataba kuafikiwa kwa usaidizi wa muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini SADC, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa uliosababisha vurugu za baada ya uchaguzi 2008.
Bwana Membe, ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Tanzania alisema kuwa daftari la wapiga kura sio siri kubwa na kuwa lilipaswa kutolewa zamani sana.
"lazima itolewe kwa wapiga kura ili waweze kuhakiki majina yao, waweze kujua watakapopiga kura,'' alisema bwana Membe.
Katibu mkuu wa chama cha MDC Tendai Biti alisema kuwa chama hicho kitachukua hatua za kisheria dhidi ya tume ya uchaguzi ili kuweza kupata sajili hilo.

imewekwa na Happy Adam

WAKATOLIKI WANAISHI KATIKA "NCHI NGENI" BAADA YA JINSIA MOJA KUHALALISHA NDOA ASEMA ASKOFU PHILIPO EGAN

Kufuatia kuhalalisha Wakatoliki ndoa za jinsia moja ni ngeni katika nchi na lugha isiyo ya kawaida na desturi, Askofu wa Portsmouth amesema.
                               Bishop Philip Egan (Photo: Mazur)
                                                                   Askofu Philipo Egan
Katika taarifa iliyotolewa na dayosisi yake, Askofu Philip Egan alisema kuwa pamoja na matumizi makubwa ya kuzuia mimba, uzazi na masuala ya ngono na kuwa na waliojitenga, na kusababisha radhi bila wajibu mkubwa na ngono nje ya ndoa.

Askofu Egan alisema: "Kama Wakatoliki,watakuwa kama Israeli katika Misri, sisi sasa tunaingia  katika nchi ngeni kwamba tunaongea lugha ya kigeni na desturi isio ya kawaida. Kwa nini sisi tupende ngono, na maisha ya familia ambayo hayatatupeleka popote katika dunia hii ya leo, Serikali, NHS na watunga sera wapaswa kuelewa nini kuhusu mambo ya ndoa, ngono na familia.

"Mbunge Orwellian jaribio redefine alisema kwamba ndoa imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya kimazingira,kijamii na hivyo kuweza kuifanya jamii na watu walioko katika jamii hizo kuwa na changamoto mbalimbali na katika kanisa pia  kama yale ya Uingereza na Wales: kwa wale ambao wanataka kuoa katika makanisa yetu, wazazi  wanapaswa kuwalea watoto katika njia iliyo ya haki kwa watoto zao na kuwafundisha maadili ya kanisa.Na viongozi wa dini wanatakiwa kushiriki katika huduma ya uchungaji ili kuweza kuwaweka watu katika njia ambazo ni za haki na ambazo zitafaa kuigwa na jamii nzima kwa ujumla kabla ya kupata athari zingine katika jamii zetu.

Imewekwa na Happy Adam

PAPA FRANCIS AOMBA KWA AJILI YA MAJERUHI NA WALE WOTE WALIOKUFA KWA AJALI YA BASI HUKO ITALIA.

Papa Francis ametuma ujumbe wa rambirambi kwa waathirika wa ajali ya basi ambayo iliua watu wapatao 38 nchini Italia.   People crowd a sport hall set up for the funeral service of some of the victims of Sunday's bus crash, in Pozzuoli, near Naples (Photo: PA)
hao ni baadhi ya watu ambao walikusanyika kwenye moja ya viwanja huko Italia kwaajili ya kuanza huduma ya mazishi ya baadhi ya waanga waajali hiyo.

Kulingana na taarifa zakutokea kwaajali hiyo zimesema kwamba watu 38 wafariki papohapo na wengine 19 walipotiwa kuwa walijeruhiwa vibaya sana ni mara baadaya gari hilo kuwakatika mwendokasi na kuwa katika mteremko mkali sana na hatimaye kuacha njia  na kupinduka na kusababisha ajali hiyo kutokea.

Ujumbe wa Papa, iliyosainiwa na Katibu wa Jimbo Kardinali Tarcisio Bertone na kupelekwa kwa Askofu Mkuu Kardinali wa Naples, Cresenzio Sepe, alisema: "alisoma habari ya kusikitisha ya ajali kubwa ambayo ilitokea katika maeneo ya barabara za viaduct A16 Napoli-Canos, ambapo  watu wengi watu  waliweza kupoteza maisha, ambao baadhi yao walikuwa ni watoto, Baba Mtakatifu anashiriki maumivu makubwa, wakati wa kuhakikisha maombi yake ya dhati kwa ajili ya waathirika wengi.


"Baba Mtakatifu aliomba kwakusema kwamba wao watapewa mapumziko ya milele na awaombea  Baraka kwamba Bwana  awaponye wale wote ambao walijeruhiwa na kutoa faraja kwa wale wanaoomboleza kwaajili ya wapendwa wao waliofariki mara tu ya ajali hiyo."


Imewekwa na Happy Adam




10 wauawa kwenye mashambulizi Nigeria

Kumetokea msururu wa mashambulio katika eneo lenye idadi kubwa ya wakristu, mjini Kano, Kaskazini mwa Nigeria.
                 
                         
         Kuna hofu kuwa mashambulizi ya kulipiza kisasi huenda yakafanyika
Ripoti zinasema kuwa watu kumi wamefariki na wengine kujeruhiwa.
Eneo hilo limewahi kulengwa na washambuliaji wa kundi la kiisilamu la Boko Haram.Walioshuhudia mashambulizi hayo wanasema kuwa mabomu yalitegwa karibu na baa moja iliyokuwa na watu wengi,baadhi wakicheza mchezo wa Pool na table tennis.
Takriban watu 20 waliuawa katika eneo hilo mwezi Machi wakati basi moja lililokuwa na abiria kushambuliwa kwa bomu.
Polisi pia walisema kuwa watu kadhaa walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumatatu jioni.
Mmoja wa walioshuhudia mashambilizi hayo aliambia shirika la habari la AP kuwa moja ya milipuko ilionekana kutoka katika gari moja aina ya Mercedes-Benz liliokuwa limeegeshwa karibu na duka moja liliokuwa linauza vileo na vinywaji vingine mbali mbali.
''Baada ya shambulizi la kwanza , nilijirusha katika bomba moja, kujificha. Kulikuwa na milipuko mitatu,'' alisema Kolade Ade aliyeshuhudia milipuko hiyo.
Eneo hilo limewahi kulengwa katika siku za nyuma na kundi la Boko Haram ambalo linapigana likitaka kuwa na utawala wa kiisilamu katika jimbo la Kano lililoko Kaskazini mwa nchi.
Kundi hilo ambalo jina lake linamaanisha ''elimu ya kimagharibi ni haramu'' limekuwa likilenga shule za umma kwa mashambulizi pamoja na kuwashambulia raia wa kawaida.
Tangu kundi hilo kuanza harakati zake mwaka 2009, zaidi ya watu 2,000 wameuawa.
Licha ya kuwa hakuna kundi lolote limedai kuhusika na mashambulizi yaliyotokea kwenye basi mjini Kano,mapema mwaka huu, kundi la Boko Haram lililaumiwa sana.
Wadadisi wanasema kuwa mji huo wenye idadi kubwa ya waisilamu una wasiwasi kuwa huenda kukatokea mashambulizi ya kulipiza kisasi, hasa kwani watu hujitokeza kwenye barabara sana wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.

imewekwa na Happy Adam

Afya ya Mandela yaendelea kuimarika

Rais mstaafu nchini Afrika Kusini , Nelson Mandela aliyelazwa hospitalini tangu tarehe nane mwezi Juni, anaonyesha dalili za afya yake kuimarika.
             
      Mandela alitaka sana kuona kuwa kombe la dunia linachezewa nchini humo
Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali. Hata hivyo Mandela mwenye umri wa miaka 95 angali hali mahututi ambayo inadhibitiwa na madaktari.

Mandela ambaye ni rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa.Rais Jacob Zuma amewataka watu kuendelea kumuombea Mandela na kuwashukuru wale waliotenda mema kwa niaba ya Mandela.
Alifungwa jela miaka 27 baada ya kuanzisha vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Anajulikana na ukoo wake kwa jina Madiba, na alichaguliwa kama rais wa Afrika Kusini mwaka 1994 baada ya wazungu kumaliza utawala wao na kisha akaondoka mamlakani baada ya miaka mitano ya kutawala nchi.
Katika taarifa yake, bwana Zuma alitoa wito kwa wafanyabiashara kuunga mkono mradi unaofadhiliwa na wakfu wa Mandela kujenga hospitali ya watoto.
"Madiba anapenda sana watoto, na anawatakia afya nzuri. Anatutaka tuhakikishe kuwa wanaishi maisha mazuri katika siku za baadaye,'' alisema Zuma.
Wakfu wa Mandela , ungependa kujenga hospitali yenye uwezo wa kuwashughulikia watoto 238 wa kulazwa pamoja na kuwatibu watoto kote nchini Afrika Kusini.

imewekwa na Happy Adam

Vifo kutokana na HIV vyapungua Afrika

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba Afrika imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
                        
              UNAIDS inasema kuwa vifo vinavyotokana na HIV vimepungua Afrika kwa asilimia 40
Vifo vinavyotokana na maradhi ya Ukimwi Mashariki na Kusini mwa Afrika vimepungua kwa asili mia 40.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi- UNAIDS umehusisha hatua za sasa na kutolewa kwa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi.
Umoja wa Mataifa umesema mataifa ya Botswana, Ethiopia, Kenya, Zambia na Zimbabwe yamepunguza idadi ya watu wanaokufa kwa ukimwi kwa zaidi ya nusu.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa Maradhi nyemelezi ya kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005.

imewekwa na Happy Adam

Tume ya Haki za Binadamu Tutamshtaki Waziri Mkuu mahakamani

Kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Alijibu: “Ni lilelile nililosema... Mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... Hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria. “Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... Wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... Maana tumechoka.”
Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana wakati akitoa ripoti ya utafiti ya miezi sita kuhusu mambo mbalimbali ya haki za binadamu kuwa kituo hicho kiko katika hatua za mwisho za kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ili kumfungulia kesi Waziri Mkuu.
“Kauli ya Pinda inavunja Katiba ya nchi ya usawa mbele ya sheria ambayo ni Ibara ya 13 (1). Hivyo tumekusudia kumfungulia kesi Waziri Mkuu ambaye amevunja Katiba,” alisema.
Sungusia alisema kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi wa juu wa Serikali ni kinyume cha Katiba, sheria za nchi na misingi ya haki za binadamu hivyo.
“Pinda alitoa kauli ile kama msimamo wa Serikali, tulitarajia angefuta kauli yake aliyotoa bungeni ya kuwabariki polisi kupiga raia katika mkutano ulioisha wa Bunge la Bajeti lakini hakufanya hivyo,” alisema.
Ofisi ya Waziri Mkuu wajibu
Akizungumza madai hayo jana, Katibu wa Waziri Mkuu, Deusdedit Buberwa alisema: “Hayo unayoniambia ni mapya kabisa. Mimi sifahamu chochote, kwani sijaona hata barua yao. Ningeweza kuzungumza kama ningepata barua au hata kusikia, lakini hakuna hicho kitu.”
Utafiti wa mauaji
Akitoa taarifa ya utafiti huo, Mtafiti wa LHRC, Pasience Mloe alisema katika kipindi cha miezi sita mwaka huu, kumekuwa na vifo 303 vilivyotokana na imani za kishirikina.
Alisema idadi hiyo ni kubwa kwani inakaribia sawa na takwimu za mwaka mzima wa 2012 ambao watu 336 walipoteza maisha kwa sababu hizohizo.
Mloe alisema utafiti huo ulibaini kuongeza kwa ubakaji wa watoto kwani katika kipindi hicho cha miezi sita, 394 walifanyiwa ukatili huo.

Waziri Sitta: Kuna wabunge mizigo CCM

Busega. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo kwani hata wakienda bungeni, hawachangii na wanabebwa na chama.
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alisema hayo juzi jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama.
“Ukweli ni kwamba, baadhi ya wabunge wa jinsi hii hawatufai. Wanakwenda bungeni hawachangii, wanakwenda bungeni hawana hata hoja za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo,” alisema Sitta.
Sitta alisema licha ya aina hiyo ya wabunge, pia wapo wale ambao hawafiki majimboni kwao kukagua shughuli za maendeleo.
“Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... inawezekana hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa wakiomba tena kura,” alisema na kuongeza:
“Haiwezekani mbunge akakaa mjini na kushindwa kwenda kuwatembelea watu wake jimboni. Mbunge anakwenda jimboni kwa kuchungulia halafu wananchi wanamshabikia na kumpa kura?
“Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana hawayajui lakini watu hawaendi majimboni, wananchi watayafahamu vipi haya maendeleo?”
Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya, Sitta alisema: “Kwanza kuna viashiria vya baadhi ya watu kuanza kuipinga Katiba mahakamani. Watu hao wasiungwe mkono kwani ndio wanaoanza chokochoko.
“Katiba tunayoitaka ni kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na Watanzania na si ya wengine. Hivyo hatuna budi kila mmoja kutumia nafasi hiyo kuwasilisha mchango wake wa kuboresha kwenye Mabaraza ya Katiba.”
Aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba watumie nafasi kuwasilisha hoja zinazojenga na wasiwe mamluki wa kuharibu mchakato mzima.
Awali, Sitta alishiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Kiloleli, Wilaya ya Busega na kuchangia Sh3 milioni.
Akizungumza katika harambee hiyo, iliyotarajiwa kukusanya Sh217,538,000, Sitta aliwataka wazazi kuwalea watoto wao katika misingi ya dini ambayo baadaye hutoa viongozi bora na wenye maadili... “Huwezi kuchukua tu mtu awe kiongozi, lazima wafunzwe misingi ya maisha na uongozi.”

SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA AGAPE LASAIDIA UJENZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO HUKO KKKT DAYOSISI YA KUSINI


                  Mama Mchungaji akipanda mti kama ishara ya kuanza kwa ujenzi huo

Naam ni katika eneo la ujenzi tayari na huku Msaidizi wa Akofu Dr. George Fihavango akiongozi uwekaji wa jiwe la msingi

Baadhi ya Washiriki wa uzinduzi huo wa ujenzi

Uchaguzi wa Mali wapongezwa.

Wafanyakazi wa uchaguzi katika moja ya vituo vya uchaguzi.
                                            Wafanyakazi wa uchaguzi katika moja ya vituo vya uchaguzi.
Wakati Mali ikihesabu kura baada ya uchaguzi wake wa rais wa Jumapili  Waziri mkuu wa Ufaransa Jean Marc Ayrault amesifu uchaguzi huo kuwa wa mafanikio makubwa ambao utaipa Mali kila nafasi ya kuwa taifa huru la kidemokrasia na kuhakikisha maendeleo yake.

Ufaransa iliongoza uvamizi huko Mali baada ya miezi 18 ambayo ilipelekea mapinduzi ya kijeshi na wanamgambo wa kiislam kuchukua upande wa kaskazini mwa nchi.

Mwandishi wa VOA Anne Look anasema maafisa wa uchaguzi wanaripoti kuwa watui wengi walijitokeza kupiga kura na kwamba  wananchi wana  furaha na matumaini.
Ulinzi ulikuwa mkali na upigaji kura ulikuwa hauna ghasia  licha ya vitisho vya Watuareg wanaopigania kujitenga.

Wagombea ni pamoja na mawaziri wakuu wawili wa zamani  Ibrahm Boubacar  Keita na  Modibo   Sidibe . Wagombea wengine wa juu ni Soumaila Cisse ambaye aliongoza umoja wa fedha wa Afrika magharibi na mgombea asiyejulikana sana Dramane Dembele ambaye anaungwa mkono na chama kikubwa kuliko vyote huko Mali cha Adema.

Wafuasi wa Morsi waendelea kuandamana

Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohammed Morsi wamepanga maandamano zaidi kuelekea kambi za kijeshi. Pia wameitisha maandamano makubwa hapo kesho Jumanne.
                       
      Mjumbe wa Ulaya Catherene Ashton yuko Misri kujaribu kutuliza hali
Haya yanajiri huku, Mjumbe wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya akiwa mjini Cairo kwa mazungumzo ya kumaliza taharuki zinazoendelea kufuatia mauaji ya zaidi ya waandamanji 70 wengi wakiwa wafuasi wa Muslim Brothehood .
Maelfu ya wafuasi wa Mohammed Morsi wameendelea kupiga kambi nje ya msikiti mashariki mwa Cairo kwa majuma kadhaa sasa na wanapanga kuendelea na maandamano yao usiku kucha.
Waandamanji hao wameitisha maandamano makubwa hapo kesho jumanne kuelekea katika kambi kuu ya jeshi.
Wanajeshi waliomuondoa madarakani Bw. Morsi wameonya waandamanaji dhidi ya kuhatarisha usalama wa kitaifa.
Wanajeshi wamesema yeyote atakayekiuka amri atakabiliwa vilivyo.Tayari viongozi wengi wa Muslim Brotherhood wamekamatwa au wamewekewa vibali vya kukamatwa.
Huku haya yakiarifiwa Mjumbe wa muungano wa Ulaya Chatherene Ashton anakutana na pande zote za kisiasa nchini Misri. Hata hivyo hali ya sasa ni dhahiri kwamba hakuna ushawishi wowote wa kimataifa utakaobadilisha mzozo wa sasa.

Pasipo ‘Haki Ardhi’ amani itatoweka nchini

Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), juzi iliandaa kongamano ambalo mada yake kuu ilikuwa Mustakabali wa Amani na Usalama wa Wananchi Tanzania Miaka 50 Ijayo.
Kwa habari zaidi ingia http://www.magazetini.com/news/pasipo-%E2%80%98haki-ardhi%E2%80%99-amani-itatoweka-nchini

Monday, July 29, 2013

TASWIRA KATIKA KONGAMANO LA AMANI NA MUSTAKABALI WA TANZANIA IJAYO BAADA YA MIAKA 50 LILILOFANYIKA CHUO KIKUU UDSM


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiandika maelezo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa wakati alipokuwa anachangia mada ya Mustakabali wa Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akijibu hoja mbalimbali za washiriki katika Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuzijibu hoja mbalimbali za washiriki katika Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto) akifurahi jambo wakati alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa mara baada ya kufungwa kwa Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria. Picha na Felix Mwagara. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

WANAFUNZI WA SHULE YA LUTHERAN JUNIOR SEMINARI MOROGORO WAANDAMANA HADI KWA ASKOFU WAKIMTAKA KUMUONDOA MKUU WA SHULE

 
Picha ya Kanisa lililopo hapo shuleni

Sehemu ya wanafunzi wakiwa na bango lenye moja ya ujumbe wakati katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) asubuhi ya leo

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Junior Seminari wakiwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wakimsikiliza Askofu wa Kanisa hilo, Jacob Mameo Ole Paulo (hayupo pichani) mara baada ya jumla ya wanafunzi 600 wa kidato cha kwan
za hadi sita kufanya maandamano yaliyoanzia shuleni hadi ofisi za askofu yaliyoanza majira ya saa 12 asubuhi wakimtaka kumuondoa kazini mkuu wa shule hiyo kwa madai mbalimbali.

Wafuasi wa Morsi waendelea kuandamana

 
Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohammed Morsi wamepanga maandamano zaidi kuelekea kambi za kijeshi. Pia wameitisha maandamano makubwa hapo kesho Jumanne.
Haya yanajiri huku, Mjumbe wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya akiwa mjini Cairo kwa mazungumzo ya kumaliza taharuki zinazoendelea kufuatia mauaji ya zaidi ya waandamanji 70 wengi wakiwa wafuasi wa Muslim Brothehood .
Maelfu ya wafuasi wa Mohammed Morsi wameendelea kupiga kambi nje ya msikiti mashariki mwa Cairo kwa majuma kadhaa sasa na wanapanga kuendelea na maandamano yao usiku kucha.
Waandamanji hao wameitisha maandamano makubwa hapo kesho jumanne kuelekea katika kambi kuu ya jeshi.
Wanajeshi waliomuondoa madarakani Bw. Morsi wameonya waandamanaji dhidi ya kuhatarisha usalama wa kitaifa.
Wanajeshi wamesema yeyote atakayekiuka amri atakabiliwa vilivyo.Tayari viongozi wengi wa Muslim Brotherhood wamekamatwa au wamewekewa vibali vya kukamatwa.
Huku haya yakiarifiwa Mjumbe wa muungano wa Ulaya Chatherene Ashton anakutana na pande zote za kisiasa nchini Misri. Hata hivyo hali ya sasa ni dhahiri kwamba hakuna ushawishi wowote wa kimataifa utakaobadilisha mzozo wa sasa.
Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili

Kampeini zaelekea kileleni Zimbabwe

 
Rais mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo yuko nchini Zimbabwe kama mwangalizi wa uchaguzi mkuu 
Kampeini za kisiasa nchini Zimbabwe zinamalizika hii leo kabla ya uchaguzi mkuu hapo Jumatano wiki hii.
Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change ambaye pia ni Waziri MKuu ,Morgan Tsvangirai, hii leo atahutubia mkutano wa hadhara mjini Harare katika uwanja alikofanya mkutano wake hio jana Rais Robert Mugabe.
Viongozi hao wawili wamekua katika serikali ya muungano tangu mwaka wa 2008 na wametofautiana kuhusu muda uliowekwa kufanyika uchaguzi. Kumekua pia na madai ya wizi wa kura, na vitisho dhidi ya wafuasi wa MDC.
Shirika la kimataifa linalotathmini hali ya mizozo The International Crisis Group limeonya kwamba hakuna mazingira ya uchaguzi huru na haki Zimbabwe.
Huku zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya watu nchini Zimbabwe kupiga kura kumchagua rais mpya. Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita , serikali imekuwa ya muungano wa Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai ambao ulikuwa unasuasua
Rais Mugabe ana umri wa miaka 89 na amekuwa mamlakani tangu mwaka 1980 na anagombea kwa mara nyingine.

20 wauawa kwenye makabiliano Nigeria

 
Vijana hawa wanaungwa mkono na jeshi na hata wamepewa mafunzo kukabiliana na Boko Haram
Takriban watu 20 wameuawa nchini Nigeria baada ya makabiliano makali kati ya makundi ya vijana waliojihami na wapiganaji wa kiisilamu.
Hii ni kwa mujibu wa jeshi na vijana wanaotoa ulinzi kwa wanavijiji.
Kulingana na vijana hao wanaotoa ulinzi kwa niaba ya serikali, wapiganaji walivamia kijiji cha Dawashe kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi , kukabiliana na wapiganaji hao wa kiisilamu ambao nao walilipiza kisisasi kwa kutumia silaha nzito huku wakiwaua raia.
Kikundi hicho cha ulinzi kiliibuka mwezi Mei na kuanza harakati zake wakati huo.
Kimeahidi kusaidia serikali kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu mgogoro huu kuanza mwaka 2009.
Kundi la Boko Haram linasema kuwa linapigana dhidi ya serikali kutaka kuwa na utawala wa kiisilamu kote Nigeria.
Jeshi linatizama wapiganaji hao kama washirika wake na hivyo limewapa mafunzo kulisaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wa kiisialamu.
Kiongozi wa vijana hao Aliko Musa alisema kuwa watu 25 waliuawa mjini Dawashe katika jimbo la Borno ambalo ndilo kitovu cha harakati za Boko Haram.
Naye msemaji wa jeshi Haruna Mohammed Sani alithibitisha kuwa watu 20 waliuawa.

Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili/habari/2013/07/130729_bokoharam_vigilante.shtml

Mali yapongezwa kwa uchaguzi mkuu

 
                             Wapiga kura kwenye foleni Mali
Uchaguzi mkuu wa Urais nchini Mali umesifiwa kwa ambavyo ulifanywa. Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kuwa wapiga kura wengi walijitokeza kupiga kura wakati wachunguzi kutoka barani Ulaya wakisema kuwa uchaguzi wenyewe umefanyika bila vurugu.
Hata hivyo idadi ya waliopiga kura katika eneo la Kaskazini ilikuwa chini ikilinganishwa na maeneo mengine ya nchi.
Wapiganaji wa kiisilamu waliteka eneo la Kaskazini mwa nchi kabla ya wanajeshi wa Ufaransa kuja nchini humo kusaidia na harakati za kuwafurusha wapiganaji hao wakisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika.
Kura zimeanza kuhesabiwa katika uchaguzi wa urais ambao unatarajiwa kulianzisha upya taifa hilo kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka uliopita.
Wadadisi wanasema huenda kukawa na duuru ya pili ya uchaguzi huo.
Wachunguzi wameelezea kuwa wapiga kura walijitokeza kwa wingi katika mji mkuu wa Bamako pamoja na maeneo mengine ya Kusini mwa taifa hilo.
Mwandishi wa habari wa BBC nchini humo amesema kuwa wengi wa wapiga kura walitaka vidole vyao kutotiwa wino.
Amesema waasi wa Tuareg ambao wanadhibiti eneo kubwa la Kaskazini wamepinga uchaguzi huo licha ya kukubali shughuli hiyo kuendelea.
Wagombea 27 walishiriki kwenye uchaguzi huo na ikiwa hapatakuwa na mshindi bayana huenda duru ya pili ikafanyika tarehe 11 mwezi Agosti.
Hata hivyo wachanganuzi wamekuwa wakihoji ikiwa nchi hiyo iko tayari kwa uchaguzi.
Takriban watu milioni 6.8 walikuwa na uwezo wa kupiga kura katika vituo 21,000 kote nchini.
Chanzo:htpp/www.bbc.co.uk/swahili/habari/2013/07/130729_mali_uchaguzi.shtml

RAIS KIKWETE AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA LEO HII


Hongereni na kazi ni maneno ya Rais  Jakaya Kikwete kwa Wanahabari wa Mkoa wa Kagera

Pichani Rais Jakaya Kikwete akiwa na Wanahabari wa Mkoa wa Kagera

Pichani Rais jakaya Kikwete akizungumza na viongozi wa Serikali na Taasisi mbalimbali katika sehemu yake ya majumuisho ya ziara yake Mkoani Kagera



Picha na habari kwa jisaani ya Issa Michuzi

WAZIRI MKUU WA THAILAND KUTUA TANZANIA KESHO


Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra

Habari na Issa Michuzi

Mongella ‘awananga’ wanaotaka Ikulu


“Tuwe wakweli katika hili. Siku zote hatusemi ukweli, hatuwaambii ukweli wananchi...” Getrude Mongella 
Na Mwandishi Wetu, Mwananch
Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Ukerewe, Getrude Mongella amewananga baadhi ya wanasiasa kuwa si wazalendo, hawana maadili na wanatumia njia zisizopendeza kuwahadaa wananchi ili waingie Ikulu.
Mongella aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake, uliofanyika Beijing, China 1995, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Kongamano la Viongozi kujadili changamoto za kuongoza mabadiliko lililoandaliwa na Uongozi Institute.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alisema, “Watu wanapanda jukwaani na kuwadanganya wananchi mambo mbalimbali lakini lengo ni kuingia Ikulu.
“Tuwe wakweli katika hili. Siku zote hatusemi ukweli, hatuwaambii ukweli wananchi na kila siku akili za wengi ni kuitaka Ikulu wakati hawana hata ‘background’ ya nchi hii, tunatenda dhambi.”
Alisema viongozi wengi si wazalendo, wameibuka tu. “Viongozi wengi ni wa kufumba na kufumbua tayari wamekuwa viongozi, hawana uzalendo kabisa, na hawajui wanachokifanya na ndiyo maana maadili yanaporomoka.”

Papa Francis: MIMI NI NANI KUHUKUMU MASHOGA?

Papa Francis amesema watu ambao ni mashoga haipaswi wawe wanatengwa na jamii badala yake tuishi nao kwa upendo na amani kama watu wengine katika jamii.
Pope Francis speaks to reporters during flight from Brazil
            Pope Francis arriving in Rome, 29 July 2013
        Pichani Papa Francis akishuka katika ndege akitokea nchini Brazil
Msimamo wa Papa Francis juu ya watu mashoga unaonekana  ni tofauti na ule ya mtangulizi wake
Akizungumza na waandishi  akiwa njiani kutoka  nchini Brazil ambako pia  alisaini msimamo wa Kanisa Katoliki ya kwamba matendo ya ushoga yalikuwa ni ya watu wenye dhambi. Pia aliendelea kwa kusema kwamba "Kama mtu ni shoga ana imani na anamwabudu Mungu, mimi ni nani kuhukumu naye?" Yeye pia alisema alitaka jukumu kubwa kwa wanawake katika Kanisa, lakini alisisitiza hawakuweza kuwa makuhani.
Papa aliwasili katika Jiji la  Roma Jumatatu hii baada ya ziara ya wiki nzima ya Brazil, ambayo ilikuwa ni  safari yake ya kwanza nje ya nchi kama Papa . Papa ambaye aliongoza  kilele cha  mkutano mkubwa  huko  Copacabana pwani Rio de Janeiro  ambako ndiko zilifanyika sherere za kilele cha Tamasha  cha Tamasha la  Vijana Duniani.
Tamasha hilo linakadiliwa kuhudhuriwa na takribani ya watu milioni tatu.