Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 29, 2013

Kampeini zaelekea kileleni Zimbabwe

 
Rais mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo yuko nchini Zimbabwe kama mwangalizi wa uchaguzi mkuu 
Kampeini za kisiasa nchini Zimbabwe zinamalizika hii leo kabla ya uchaguzi mkuu hapo Jumatano wiki hii.
Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change ambaye pia ni Waziri MKuu ,Morgan Tsvangirai, hii leo atahutubia mkutano wa hadhara mjini Harare katika uwanja alikofanya mkutano wake hio jana Rais Robert Mugabe.
Viongozi hao wawili wamekua katika serikali ya muungano tangu mwaka wa 2008 na wametofautiana kuhusu muda uliowekwa kufanyika uchaguzi. Kumekua pia na madai ya wizi wa kura, na vitisho dhidi ya wafuasi wa MDC.
Shirika la kimataifa linalotathmini hali ya mizozo The International Crisis Group limeonya kwamba hakuna mazingira ya uchaguzi huru na haki Zimbabwe.
Huku zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya watu nchini Zimbabwe kupiga kura kumchagua rais mpya. Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita , serikali imekuwa ya muungano wa Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai ambao ulikuwa unasuasua
Rais Mugabe ana umri wa miaka 89 na amekuwa mamlakani tangu mwaka 1980 na anagombea kwa mara nyingine.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment