Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 29, 2013

Mongella ‘awananga’ wanaotaka Ikulu


“Tuwe wakweli katika hili. Siku zote hatusemi ukweli, hatuwaambii ukweli wananchi...” Getrude Mongella 
Na Mwandishi Wetu, Mwananch
Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Ukerewe, Getrude Mongella amewananga baadhi ya wanasiasa kuwa si wazalendo, hawana maadili na wanatumia njia zisizopendeza kuwahadaa wananchi ili waingie Ikulu.
Mongella aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake, uliofanyika Beijing, China 1995, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Kongamano la Viongozi kujadili changamoto za kuongoza mabadiliko lililoandaliwa na Uongozi Institute.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alisema, “Watu wanapanda jukwaani na kuwadanganya wananchi mambo mbalimbali lakini lengo ni kuingia Ikulu.
“Tuwe wakweli katika hili. Siku zote hatusemi ukweli, hatuwaambii ukweli wananchi na kila siku akili za wengi ni kuitaka Ikulu wakati hawana hata ‘background’ ya nchi hii, tunatenda dhambi.”
Alisema viongozi wengi si wazalendo, wameibuka tu. “Viongozi wengi ni wa kufumba na kufumbua tayari wamekuwa viongozi, hawana uzalendo kabisa, na hawajui wanachokifanya na ndiyo maana maadili yanaporomoka.”
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment