Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 30, 2013

Uchaguzi wa Mali wapongezwa.

Wafanyakazi wa uchaguzi katika moja ya vituo vya uchaguzi.
                                            Wafanyakazi wa uchaguzi katika moja ya vituo vya uchaguzi.
Wakati Mali ikihesabu kura baada ya uchaguzi wake wa rais wa Jumapili  Waziri mkuu wa Ufaransa Jean Marc Ayrault amesifu uchaguzi huo kuwa wa mafanikio makubwa ambao utaipa Mali kila nafasi ya kuwa taifa huru la kidemokrasia na kuhakikisha maendeleo yake.

Ufaransa iliongoza uvamizi huko Mali baada ya miezi 18 ambayo ilipelekea mapinduzi ya kijeshi na wanamgambo wa kiislam kuchukua upande wa kaskazini mwa nchi.

Mwandishi wa VOA Anne Look anasema maafisa wa uchaguzi wanaripoti kuwa watui wengi walijitokeza kupiga kura na kwamba  wananchi wana  furaha na matumaini.
Ulinzi ulikuwa mkali na upigaji kura ulikuwa hauna ghasia  licha ya vitisho vya Watuareg wanaopigania kujitenga.

Wagombea ni pamoja na mawaziri wakuu wawili wa zamani  Ibrahm Boubacar  Keita na  Modibo   Sidibe . Wagombea wengine wa juu ni Soumaila Cisse ambaye aliongoza umoja wa fedha wa Afrika magharibi na mgombea asiyejulikana sana Dramane Dembele ambaye anaungwa mkono na chama kikubwa kuliko vyote huko Mali cha Adema.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment