Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 30, 2013

KISA CHA WATOTO MATEKA GHANA

Polisi nchini Ghana wanawahoji wazazi walioshtakiwa kwa kuwafungia nyumbani wanao walio kati ya umri wa miaka minne na minane tangu kuzaliwa kwao.
                          
Polisi walivamia makao yao yenye vyumba vinne mjini Accra,siku ya Ijumaa na kuwaokoa watoto hao , mvulana mmoja na wasichana wawili.
Wazazi hao waliwaambia polisi kuwa hawakutaka kuwatoa wanao nje kwa hofu ya kukusanyika na watu waovu.
Watoto hao sasa wamepelekwa katika makao ya kuwatunza watoto huku kukiwa na hofu kuwa wazazi wao huenda ni wagonjwa wa akili.
Mwandishi wa BBC mjini Accra anasema kuwa kisa hicho kimewashangaza sana watu mjini humo.
Inaarifiwa watoto hao walifungiwa nyumbani tangu kuzaliwa kwao na hawamkujua yeyote isipokuwa wazazi wao.
Aidha watoto hao waliishi katika chumba kimoja, huku Kondoo na kuku wakiwa katika vyumba viwili huku wazazi wao wakilala katika chumba chao kwenye nyumba hiyo iliyikuwa imejaa uvundo.
Nyumba ilionekana kama isiyoishi watu na licha ya kuwa haikuwa imesafishwa kwa miaka mingi, kuta zake zilikuwa na michoro.
Polisi walivamia nyumba hiyo baada ya jirani mmoja mwenye shauku kuwaarifu .
Wazazi wa watoto hao wanahojiwa na polisi pamoja na madaktari wa magonjwa ya kiakili mjini Accra, huku watoto hao wakipewa malezi na familia moja.
Msemaji wa polisi alisema kuwa wazazi wa watoto hao hawakuwahi kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba yao.
Watoto waliwaarifu polisi kuwa baba yao ambaye hakuwa na ajira, aliwasomesha hesabu na kiingereza nyumbani kwao.
Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment