Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 31, 2013

KIONGOZI WA ZAMANI WA MALI AONGOZA KWA KURA

Waziri Mkuu wa zamani nchini Mali Ibrahim Boubakar Keita anaongoza kwa kura za Urais, katika uchaguzi unaonuia kurejesha utawala wa demokrasia nchini humo. Duru za serikali zinasema aliyekua Waziri wa Fedha, Soumaila Cisse anafuata Bw Keita, huku theluthi moja ya kura ikiwa imehesabiwa.
Ibarhim Boubakar Keita
Upande wa Bw. Cisse imepinga matokeo hayo na kutaka tume ya kimataifa kuhesabu kura za uchaguzi huo wa Jumapili. Mali ilikumbwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka jana pamoja na maasi Kaskazini mwa nchi. Ufaransa ilituma kikosi cha wanajeshi 4,000 kuyakomboa maeneo ya kaskazini kutoka kwa wanamgambo wa kiisilamu.
Vuguguvu la Ukombozi wa jamii ya Tuareg ikisaidiana na wapiganaji wa kiisilamu walitwaa eneo nzima la Kaskazini, kabla ya muungano huo kusambaratika. Makundi hayo yalifanikiwa kunyakua Kaskazini mwa nchi baada ya jeshi kuipindua serikali ya kiraia ikilalamikia kutopata ufadhili kukabiliana na maasi Kaskazini mwa nchi.
Mapema mwezi huu, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilitumwa Mali ili kusaidia katika shughuli za uchaguzi na kurejesha utawala wa kidemokrasia.Ufaransa umepongeza uchaguzi wa Mali, huku Muungano wa Ulaya ukisema shughuli hiyo ilifanyika bila visa vyovyote. Bw Keita maarufu kama "IBK" ana sifa ya kuwa na mabavu.
Mwanasiasa huyo aliendesha kampeini yake kwa ujumbe wa kurejesha hadhi kwa Mali akisema taifa liliisha hadhi yake kwa kuomba msaada wa Ufaransa ili kuinusuru dhidi ya kuporomoka.Viongozi wa kidini wengi wakiwa Waisilamu waliwaomba raia kumpigia kura, pia anaonekana kuungwa mkono na jeshi. Bw. Cisse aliunda chama cha Union for the Republic and Democracy (URD) mwaka wa 2003 na ametaka jeshi kutojihusisha na siasa.Jumla ya wagombea 27 walichuana Urais, huku watu milioni 6.8 wakijiandikisha kupiga kura nchini Mali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment