Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, January 31, 2014

MAELFU WASHIRIKI KUMZIKA MAMA MZAZI WA MCHUNGAJI HIMID SAGGA

















Urais 2015: Malecela amtolea uvivu Lowassa


Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, John Malecela.PICHA|MAKTABA 
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Vita ya urais kupitia CCM inazidi kushika kasi baada ya Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, John Malecela kuutaka uongozi kumchukulia hatua Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kuanza mapema kampeni.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda kumtuhumu Lowassa kuwa anakiyumbisha chama hicho kutokana na kampeni za kutaka kuwania urais wa 2015.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma jana, Malecela alisema Sekretarieti ya CCM inapaswa kuwachukulia hatua kali makada wanaojipitisha maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kusaka urais, kabla ya chama hicho kupanga muda.
Aliwafananisha walioanza mbio za urais kupitia CCM na watu wanaowahi kukimbia kabla ya kipenga kupigwa na kusema hawawezi kupimwa sawa na wale wanaosubiri kuanza rasmi kwa kampeni. Alimpongeza Makonda kwa ujasiri wa kukemea hatua hiyo ya Lowassa bila woga.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Lowassa alijibu kupitia msaidizi wake kuwa hana la kusema. “Nimezungumza na Mheshimiwa Lowassa juu ya suala hilo lakini amenituma niwaambie kuwa hana ‘comment’ (hana la kusema),” alisema msaidizi wake huyo.
Fulana hadharani
Alipoulizwa swali la kwa nini ameamua kumtaja Lowassa pekee huku kukiwa na makada wengi wanaojipitisha kupiga kampeni za urais, kabla ya kujibu, Malecela ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu, aliingia ndani ya nyumba yake na kutoka akiwa ameshikilia mfuko uliokuwa fulana mbili.
Alitoa fulana hizo, moja ikiwa na rangi nyeusi na kahawia na nyingine yenye rangi nyekundu na nyeupe zikiwa zimeandikwa ‘Friends of Edward Lowassa’ (Marafiki wa Edward Lowassa).
“Hivi kuna mwingine aliyefanya hivi? Na hizi zimegawiwa nchi nzima. Ehhh! Hivi kuna mwingine kafanya hivi? Sijui, niongezee nini tena zaidi ya hapo,” alisema Malecela huku akionyesha fulana hizo.
Malecela ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Taifa la CCM, alisisitiza kuchukuliwa kwa hatua haraka kwa vitendo hivyo akisema harakati za Lowassa kuwania urais kupitia chama hicho zimesababisha mgawanyiko.
“Jinsi tunavyochelewa kuchukua hatua ndivyo tunavyoweza kuleta mpasuko ndani ya chama. Hapa najiuliza, ile misingi imara ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi iko wapi? Mpaka tumwachie mtoto (Makonda) akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?” alisema.
Alitahadharisha kuwa chama kisipotoa karipio au tamko kuhusu suala hilo, wanaotumia fedha kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi ili kupata madaraka wataharibu misingi bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wa CCM.
“Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudi za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana na Katibu Mwenezi Nape Nnauye za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga,” alisema na kuongeza kuwa juhudi hizo zisibezwe.
Malecela aliishauri Sekretarieti ya CCM kuchukua hatua mara moja, kwa maelezo kuwa Makonda asingesema hayo yote kama hana uhakika wa ushahidi.
Alisema waasisi wa chama hicho walikijenga kwa tabu na hakuna aliyediriki kutumia fedha kutaka madaraka... “Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa masilahi ya wananchi ndivyo vilivyotuongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na Serikali.”
Alisema vijana na wanachama wa CCM wanataka kujua msimamo wa chama chao.
Akizungumzia kauli hiyo ya Malecela, Nnauye alisema: Tumemsikia, ushauri wake tutaufanyia kazi.” Hakutaka kuzungumzia zaidi suala hilo.
Tangu Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli kuandaa hafla kubwa kusherehekea Mwaka Mpya nyumbani kwake Monduli ambako alitangaza kuanza rasmi safari aliyoiita ya matumani ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, majisafi na maendeleo ya uhakika, makada wa chama hicho wameingia katika malumbano makubwa.
Malumbano hayo ambayo Malecela amesema hayana tija kwa chama na hayaleti umoja na mshikamano ambao umekuwapo kwa miaka mingi, yalipamba moto baada ya hivi karibuni baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa chama hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Geita, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ kumjia juu Mwenyekiti wa Singida, Mgana Msindai kwa kudai wenyeviti wote walikuwa wanamuunga mkono Lowassa.

Hata hivyo, Msindai ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM wa mikoa, alikanusha kutoa kauli hiyo kwa maelezo kwamba alikuwa akiwazungumzia wenyeviti aliokuwa amefuatana nao Monduli katika hafla hiyo.

MATUKIO YA SAFARI YA MWISHO YA MAMA MZAZI WA MCHUNGAJI HIMID SAGGA KATIKA PICHA









IGAD:Waangalizi kuenda S. Kusini


Wanajeshi wa Sudan Kusini
Shirika la kikanda la IGAD la mataifa yaliyo katika upembe mwa Afrika, limeamua kuwa waangalizi wanapaswa kwenda nchini Sudan Kusini kuhakikisha kuwa mkataba wa kusitisha mapiganop unatekelezwa.
Uamuzi ulifikiwa katika mkutano wa Muungano wa Afrika unaondelea mjini Addisa Ababa Ethiopia.
Makabiliano makali yameendelea kuripotiwa nchini humo, licha ya mkataba wa amani kutiwa saini wiki jana kati ya waasi na serikali.
IGAD pia imetoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wote wa kigeni nchini humo.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesema kuwa Uganda haina mipango ya kuondoa wanajeshi wake ambao wamekuwa wakisaidia majeshi ya Sudan Kusini kupambana na waasi nchini humo.

35 wauawa CAR mapigano yakichacha

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema kuwa watu 35 wameuawa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
Rais mpya wa muda nchini CAR, Catherine Samba Panza
Msemaji wa kamati hiyo ya Red Cross mjini Bnagui ,Nadia Dibsy,amesema kuwa mji huo sasa unakumbwa na vita vibaya.
Vita inasemekana vimekithiri huku wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine 5,000 wa Muungano wa Afrika wakiwa nchini humo kujaribu kutuliza hali.Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, miili ilionekana ikiwa imekatakatwa kwa mapanga na kutapakaa kote.
Mgogoro wa kisiasa ulianza mwezi Machi mwaka jana kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea wakati huo ambapo waasi waisilamu walimsaidia aliyekua Rais Djotodia kuingia mamlakani kwa nguvu.
Tangu hapo vita vimekuwa vikichacha kati ya waasi waisilamu na wakristo.
Na sasa kwa kuwa waisilamu wameondoka mamlakani, wakristo nao wameanza kulipiza kisasi.

TZ: Wabunge wajipa 'mkono wa kwaheri'

Kumekuwa na ghadhabu nchini Tanzania kufuatia uamuzi wa wabunge kujiongeza maelfu ya dola kama marupurupu.
Kikao cha bunge la TZ
Pesa hizo wanasema ni mkono wa kwaheri.
Marupurupu hayo yatatolewa kwa kila mbunge wa bunge la Tanzania lenye wabunge 357 wakati watakapokamilisha muhula wao wa tano kama wabunge.
Kila mbunge nchini Tanzania, hupokea mshahara wa dola elfu saba kila mwezi.
Wakazi wa mji mkuu Dar es Salaam waliambia BBC kuwa wameshtushwa sana na marupurupu hayo hasa baada ya kuambiwa na serikali kuwa hakuna pesa za kutosha kwa matumizi ya huduma za jamii.

Bandari bubu tatu kutambuliwa rasmi

Tanga. Mkoa wa Tanga upo kwenye mchakato wa kurasimisha bandari bubu tatu ili zipandishwe hadhi na kufanya kazi chini uangalizi wake, tofauti na sasa zinatumika kupitisha biashara za magendo na wahamiaji haramu.
Akizungumza na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira juzi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa alisema bandari hizo bubu zinatumika vibaya, hivyo ni bora zikatambuliwa ili kuingiza mapato serikalini.
Gallawa alitaja bandari hizo kuwa ni Jasini iliyopo wilaya ya Mkinga, Kigombe wilayani Muheza na Kipumbwi iliyopo Pangani na kwamba, hizo ni kati ya 40 zilizopo Tanga.
Alisema baada ya kuzitembelea na kukagua shughuli zinazofanyika kila siku, Serikali imebaini bandari hizo bubu zinavusha bidhaa mbalimbali. Pia, zinatumika kama milango ya kuingia kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Mwenyeikiti wa kamati hiyo, James Lembeli alipongeza Mkoa kwa kuchukua hatua hiyo, kwani siku zilizopita zilikamatwa meno ya tembo nje ya nchi na kubainika kuwa zimepitia mkoani hapa.

Tanzania yajibu madai ya News of Rwanda.

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili.
Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili.

Mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Bw.Salva Rweyemamu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu
Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda “News of Rwanda”  ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo  iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya  Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema  wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo  na marais wa nchi hizo wameshazungumza  vizuri wakakubaliana  na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania .
Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa “Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale?

Mahakama Tanzania yawaachia huru waandishi habari.

Absalom Kibanda akizungumza na waandishi.
Absalom Kibanda akizungumza na waandishi.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru  Meneja Uendelezaji Biashara wa Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji  wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika(VOA ) Absalom Kibanda ambaye pia ni  Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri amesema maamuzi ya mahakama hiyo yamerejesha  matumaini mapya kwa tasnia ya habari kwa wanahabari na vyombo vya habari kwamba pamoja na sheria kandamizi wanayo  fursa ya kushinda  baadhi ya hila, baadhi ya mipango ya kudhulumu vyombo vya habari  nchini  Tanzania.

Akielezea maamuzi ya mahakama hiyo amesema kwamba mahakama iliamua kuwa  serikali ilifungua kesi hiyo katika misingi ya hisia kwani yalioandikwa ni masuala ya kawaida hakukuwa na nia ya uovu, waandishi walitumia uhuru wao wa kujieleza  na hakukuwa na matukio yeyote ya wazi kwamba baada ya ile makala kumekuwa na vitendo au matukio yaliotokana na uandishi wa makala hiyo.
Amesema maamuzi hayo yatalazimisha mabadiliko kwani ni sawa na kujifunza kwa viboko kwani kuna dhamira mbaya na chuki za wazi dhidi ya vyombo vya habari, ni fundisho  kwamba lazima walio madarakani, waandishi   na wananchi wa kawaida wanapaswa kujifunza  kwamba  hakuna aliye juu ya sheria.

 Amesema wana imani kupitia mchakato wa katiba mpya kuwa wataweza kupata fursa ya kuingiza masuala mengi yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari katiba katiba mpya ijayo nchini humo.

Akielezea zaidi kuhusu chuki dhidi yao amesema upande mmoja ni kwasababu ya waandishi wenyewe na kwa upande mwingine viongozi walioko madarakani hawapendi kukosolewa kutokana na tabia zao akitolea mfano  matumizi mabaya ya madaraka ya Polisi.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania azituhumu nchi za ukanda wa maziwa makuu kuchochea machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benrad Membe
waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benrad Membe

Na Ali Bilali
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania, Bernard Camilius Membe amesema kuwa mzozo unaoshuhudiwa mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC unachangiwa na nchi wanachama za ukanda wa maziwa makuu.

Akizungumza na mwandishi wetu wa idhaa ya rfikingereza pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU, waziri Membe anakiri kuwa kwa sehemu kubwa mzozo wa mashariki ya kongo unachochewa na zenyewe zinazoizunguka nchi ya DRC na kwamba ni wao wenyewe ndio wanaoweza kumaliza ama kuendeleza machafuko.
Tulipomuuliza iwapo anataarifa za kuchapishwa kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa inayozitaja nchi za rwanda na Uganda kuhusika na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa M23, waziri Membe anasema hana taarifa hizo lakini anasisitiza kuwa jambo la muhimu ni kuyashirikisha makundi hayo kwenye mazungumzo ya kisiasa.
Katika hatua nyingine mkuu wa tume ya umoja wa mataifa nchini DRC, MONUSCO, Martin Kobler amesema kuwa kuanzia mwezi ujao wanatarajia kuongeza ndege zisizo na rubani kufanya doria kwenye mpaka wa Rwanda na Uganda na nchi ya DRC.

Serikali ya Tanzania yakanusha taarifa za mazungumzo ya rais Kikwete na viongozi wa waasi wa FDLR

Rais wa Tanzania Jakaya mrisho Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya mrisho Kikwete

Na Ali Bilali
Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake nchini Rwanda imekanusha taarifa zilizocahpishwa na gazeti moja la serikali nchini humo likimtuhumu rais Jakaya Kikwete kuwa na mazungumzo ya siri na viongozi wa kundi la waasi wa FDLR.

kwenye taarifa iliotolewa na Ikulu ya rais jijini Dar es Salaam ikinukuu taarifa rasmi iliotolewa na kaimu balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Balozi Francis Mwaipaja, imekanusha vikali habari iliochapishwa na gazeti la serikali la news of Rwanda likidai kuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa na mazungumzo ya siri na viongozi wa kundi la FDLR la Rwanda.
Gazeti hilo hivi karibuni liliandika habari zinazodaikuwa kwa nayakati tofauti rais Kikwete amekuwa na mazungumzo jijini Dar Es Salaam na waanzilishi wa chama cha National Congress NRC, Dr Theogene Rudasingwa kamanda wa kundi la Democratic Forces of Liberation of Rwanda FDLR, luteni Kanali Wilson Irategeka, Kanali Hamadi pamoja na aliyekuwa waziri mkuu wa Rwanda Faustin Twagiramungu.
Kufuatia habari hiyo, Serikali ya Tanzania imemuandikia barua mhariri wa gazeti la News of Rwanda kumtaka aombe radhi pamoja na kuacha kuandika habari za uvumi ambazo kwa sehemu kubwa zimemuhusu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr, Jakaya Mrisho Kikwete.
Taarifa hiyo ambayo nakala yake rfikiswahili inayo, imekanusha kuwa mkutano kati ya rais Kikwete na viongozi hao ulifanyika tarehe 23 ya mwezi huu na kwamba tarehe hiyo rais Kikwete alikuwa safarini mjini Davos, Uswis kuhudhuria mkutano wa kiuchumi.
Wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania pia imekanusha kutoa pasi za kusafiria wala kuishi nchini humo kwa viongozi waliotajwa kuwa na mazungumzo na rais Kikwete.
Tangazo la Serikali ya Tanzania kukanusha taarifa hizi linakuja huku kukiwa imepita miezi kadhaa toka kuwepo kwa taarifa kuwa nchi hizo mbili zimekuwa kwenye mvutano kwa madai kuwa Tanzania inawasaidia waasi wanaompinga rais Paul Kagame.

Muhongo: Hatudanganyiki tena na wawekezaji madini

Profesa Muhongo alisema kwa sasa sekta ya madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa.PICHA|MAKTABA 
Na Leon Bahati, Mwananchi
Dar es Salaam. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo, amejigamba kuwa Tanzania haitadanganyika tena kwa wawekezaji wa sekta ya madini kutolipa kodi na kuifanya nchi kutofaidika na rasilimali zake.
Alisema hayo juzi katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya Serikali za Tanzania na Finland, kutiliana saini, makubaliano katika kutafiti na kukuza sekta ya madini.
“Kama ni kutuibia walifanya hivyo siku za nyuma, lakini kwa sasa hawawezi tena,” alijigamba Profesa Muhongo akidai historia inaonyesha kuwa nchi zote zenye rasilimali za madini, mwanzoni zilidanganyika.
Alikiri kuwa awali wawekezaji katika migodi walikuwa wakijitetea kuwa walikuwa wanapata hasara lakini kwa sasa, sheria inawalazimisha kulipa asilimia 30.
Kauli ya Profesa Muhongo ilitokana na waandishi kumbana, kuhusu Watanzania kutonufaika na sekta ya madini wakati ina faida kubwa.
Profesa Muhongo alisema kwa sasa sekta ya madini inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa.
Alisema malengo ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.
Mapema, wakurugenzi wa sekta ya madini katika Serikali za Tanzania na Finland, walitiliana saini ya kukuza na kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumzia makubaliano hayo, Profesa Muhongo alisema yanazingatia mambo matatu, ambayo ni pamoja na utafiti wa madini katika mikoa ya kusini.
Alisema kimsingi tayari wamegundua kuwa ukanda huo una makaa ya mawe, shaba, niko na platiniamu.
Alisema watakachokifanya ni kuainisha maeneo yenye madini na viwango halisi ili wakipatikana wawekezaji wa kuyachimba, waingie kwenye makubaliano ya uhakika.

Mzungumzo Syria kwenda 'mapumzikoni'

Wajumbe wa upinzani katika mazungumzo ya amani nchini Syria mjini Geneva
Awamu ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya Syria itakamilika hii leo mjini Geneva, bila ishara ya mafanikio lakini kuna 'matumaini' anasema mjumbe wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi.
Serikali ya Syria na waakilishi wa upinzani bado wana misimamo mikali juu ya maswala muhimu.
Lakini mpatanishi wa Umoja wa Mataifa anayeongoza mazungumzo hayo anasema anatumai awamu ya pili ya mazungumzo hayo itakayofanyika baada ya siku kumi zijazo italeta mafanikio kiasi .
Siku kumi baada ya umoja wa mataifa kuanzisha juhudi ya kumaliza vita wenyewe kwa wenyewe nchini Syria wajumbe kutoka pande mbili katika mgogoro huo bado wako kwenye meza moja ya mazungumzo.
Nwenyekiti wa mazungumzo hayo, Lakhdar Brahimi, anazingatia hilo kuwa ufanisi wa aina yake, huku akielezea kuwa kulikuwa na baadhi ya nyakati za hasira, lakini pia nyakati za matumaini.
Kisha akaelezea jinsi wajumbe wa pande zote mbili walipokubaliana kubaki kimya kwa dakika moja kukumbuka nyoyo za wale waliofariki katika mapigano nchini Syria.
Mazungumzo yamekuwa magumu lakini yenye matumaini kati ya serikali na upinzani.
"Tulikuwa na nyakati za hasi hali kadhalika nyakati zenye matumaini. Upinzani ulipendekeza tuwe na kimya cha dakika moja kuwaenzi waliokufa nchini Syria, bila kuzingatia kambi wanayotoka na ujumbe wa serikali mara moja ulikubali na kisha tukabaki kimya kwa dakika moja,'' amesema bwana Brahimi.
Lakini hapajakuwa na mafanikio makubwa katika mazungumzo kuhusu maswala muhimu yanayoikabili Syria kama vile ugavi wa madarakani na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingizwa katika maeneo yaliyozingirwa.
Hata mpangilio wa jinsi maswala haya yanapaswa kushughulikiwa umezua malumbano.
Bwana Brahimi ana matarajio kuwa likizo ya siku kumi kwa wajumbe kuanzia baada ya kikao cha mwisho leo Ijumaa, itatoa hewa safi kwa pande zote kuzingatia mbinu bora zaidi za kushugulikia maswala hayo na pia kuwapa fursa wafadhili wao-marekani na Urusi kutumia ushawishi wao.

Mawaziri wa mashauri ya kigeni, John Kerry wa Marekani na mwenzake wa Urusi Sergev Lavrov watakutana wikendi hii mjini Munich nchini Ujerumani.

AU kuzungumzia migogoro Afrika

Viongozi wa Afrika wameanza mkutano wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo agenda yao kuu itakuwa swala la mizozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini.
Mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa tume ya Umoja huo Nkosazana-Dlamini Zuma amewaambia viongozi 54 ambao ni wanachama wa Muungano wa Afrika, kwamba wanapaswa kushirikiana ili kuleta suluhu ya kudumu kwa migogoro Afrika.Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na mgogoro wa kisisa kwa miezi kumi sasa tangu waasi kuipindua serikali.
Katika taifa jirani ya Sudan Kusini, makundi hasimu yalitia saini ya mapatano juma lililopita baada ya mapigano makali yaliyodumu mwezi mmoja, lakini mapigano yangali yanatokota kati ya serikali na waasi.
Maelfu ya watu wameuwawa katika mzozo huo.
Mkutano huo pia utaangazia,tatizo la uhaba wa chakula na kilimo katika bara hilo. Licha ya uchumi kukuwa katika sehemu nyingi za Afrika,eneo la Sahel na upembe wa Afrika ni maeneo ambayo hukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula mara kwa mara.
Muungano wa Afrika umekosolewa kwa kujikokota katika kuchukua hatua kukabiliana na migogoro ya kisiasa Afrika ya Kati na Sudan Kusini.
Muungano huo umemteua Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kama mwenyekiti wake mpya.
Generali Abdel Aziz aliingia mamlakani nchini Mauritania mwaka 2009, baada ya kuongoza matukio mawili ya mapinduzi katika kipindi cha miaka minne.

Jambazi sugu asakwa Tanzania

Ramani ya TZ
Polisi Nchini Tanzania wanamsaka mtu mmoja mwenye silaha, ambaye amewauwa watu wanane kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watatu.
Kisa hicho cha mauaji kilifanyika Jumamosi usiku katika eneo la Mara kaskazini.
Walioshuhudia wanasema kuwa jamaa huyo alikuwa akitaka kupewa pesa na simu za mkononi toka kwa waathiriwa.
Kikosi maalum kinachojumuisha maafisa wa polisi wapatao 160 kimekabidhiwa majukumu ya kumsaka jambazi huyo kwa nia ya kumtia mbaroni.
Mwanahabari wa BBC Nchini Tanzania anasema kuwa sio kawaida kwa watu wa Mara wanaopakana na Ziwa Victoria kubeba bunduki katika harakati za kulinda mifugo wao.

Nec: Daftari la wapigakura litaboreshwa

Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva.PICHA|MAKTABA 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Dar es Salaam. Pamoja na kushindwa kutaja tarehe rasmi ya kuanza kuboresha daftari la kudumu la wapigakura, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema daftari hilo litaboreshwa kabla ya kuanza kwa upigaji wa kura ya maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya. Upigaji wa kura hiyo utafanyika ndani ya siku 70 baada ya kumalizika kwa Bunge Maalumu la Katiba linalotarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao mjini Dodoma. Litafanyika kwa kati ya siku 70 na 90.
Nec imetoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wananchi kwamba tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, daftari hilo halijawahi kuboreshwa, jambo ambalo litasababisha upigaji wa kura kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kutawaliwa na vurugu. Malalamiko hayo yanatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu waliotimiza umri wa kupiga kura lakini hawamo katika daftari hilo.
Pia waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura na wenye kasoro mbalimbali zinazowafanya wapoteze sifa.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva jana alitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa tume hiyo imeshapata fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kuendesha mchakato wa kufanya maboresho hayo.
“Tumeanza mchakato wa kuboresha daftari kwa kuanza kuhakiki vituo vya uandikishaji wa kupiga kura vitakavyoongezeka kwa lengo la kuvisogeza karibu zaidi na wananchi,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Inafafanua kwamba mpaka kufikia upigaji wa kura ya maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya na uchaguzi mkuu mwaka 2015, daftari hilo litakuwa limeshafanyiwa marekebisho.
“Nec inawataka wananchi kutokuwa na wasiwasi juu ya suala hili. Jukumu la kusimamia na kuendesha mchakato huu ni la tume hii hivyo vyombo vingine visijiingize katika shughuli zisizowahusu” inaeleza.
Katika taarifa hiyo Nec imevitaka vyama vyote 21 vya siasa nchini kuwahamasisha wananchi kushiriki katika kura ya maoni na Uchaguzi Mkuu ujao, siyo kuwayumbisha wananchi juu ya suala hilo.

K.K.K.T -DAYOSISI YA IRINGA YASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA MAZAZI WA MCHUNGAJI HIMID SAGGA MAZIKO KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 31.01.2014 ILULA IRINGA

Wednesday, January 29, 2014

DAYOSISI MPYA YA KKKT RUVUMA YAPATA ASKOFU. ASKOFU MTEULE NI AMON MWENDA NA MASAIDIZI NI LAURENT NG'UMBI. ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII KUPATA HARI ZAIDI

Viongozi wa waasi S.Kusini matatani

Maelfu waliachwa bila makao kutokana na vita Sudan Kusini
Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa itawafungulia mashitaka wahusika wakuu wa njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir.
Serikali ya Kiir, imesema kuwa njama hiyo ndiyo iliyosababisha mapigano kati ya serikali na waasi waliokuwa wanaongozwa na Riek Machar.
Baadhi wanahofia kuwa hatua hii huenda ikasababisha uhasama zaidi na kutishia mkataba wa amani kati ya waasi na serikali.
Pande zote mbili kwenye mgogoro wa Sudan Kusini zilitia saini mkataba wa kusitisha vita Ijumaa iliyopita, lakini vita vimepungua tu bali havijasitishwa.
Duru zinasema makabiliano yangali yanaendelea huku zaidi la watu 800,000 wakilazimika kutoroka makwao.
Mkuu wa misaada katika Umoja wa Mataifa,Valerie Amos, anakamilisha ziara yake ya siku tatu nchini humo ambako ameshuhudia vita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Wanaume wanne waliozuiliwa watafikishwa mahakamani na wengine watatu akiwemo Riek Machar, pamoja na mjumbe mmoja wa amani kutoka upande wa waasi,Taban Deng -- aliyetia saini mkataba wa amani watakabiliwa na sheria watakapokamatwa.
Rais Kiir alimtuhumu Machar pamoja na waliokuwa maafisa wa serikali kwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya serikali yake baada ya mapigano kuzuka mjini Juba mwezi Disemba mwaka jana.
Maafisa 11 wa zamani walikamatwa wakati yeye Machar aliyepinga kupanga njama ya mapinduzi kutoroka.
Makabiliano mapya yameripotiwa kutokea katika jimbo la Unity karibu na anakotoka bwana Machar.
Wafanyakazi wa misaada wamesema kuwa wanakabiliwa na wakati mgumu na kuwa wanahitaji msaada zaidi kuwasaidia waathiriwa wa mapigano hayo.

Jaribio la kumuua waziri Libya latibuka

Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim.
Libya imekuwa ikikumbwa na msukosuko wa kisiasa tangu Muamar Gadaffi kuuawa
Shirika la kitaifa la habari LANA na lile la AFP yamethibitisha tukio. Inaarifiwa kwamba gari alimokuwa Abdel Karim lilipigwa risasi alipokuwa akielekea katika mkutano katika makao makuu ya bunge.
Abdel-Karim anatarajiwa kuhutubia waandishi habari hivi punde.
Abdel Karim aliteuliwa na waziri mkuu nchini Libya kuwa kaimu waziri wa ndani baada ya waziri Mohamed Sheikh kujiuzulu mnamo Agosti mwaka jana.
Seddik Abdelkarim, alikuwa katika gari lake aliposhambuliwa na watu wasiojulikana waliomfyatulia risasi. Inaarifiwa hakuna aliyeuawa kwenye shambulizi hilo.
Libya imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kisiasa tangu waasi kuipindua serikali na kumuua aliyekuwa Rais Muamer Kadhafi mwaka 2011.
Waziri huyo alikuwa njiani kuelekea bungeni wakati gari lake liliposhambuliwa.
Shambulizi lenyewe limetokea chini ya wiki tatu baada ya mauaji ya naibu waziri wa viwanda Hassan al-Droui, aliyeuawa mjini Sirte

Tahadhari ya njaa yatolewa Kenya

Serikali ya Kenya imetoa tahadhari kuhusu tisho la nja kwa watu milioni 1.6 kutokana na uhaba wa chakula.
Mashirika mbali mbali yametoa tahadhari kuhusu uhaba wa chakula
Wizara ya kilimo imesema kuwa chakula kilichohifadhiwa kwa sasa kinaweza kudumu tu hadi mwezi Mei.
Wafanyabiashara wa sekta binafsi wametakiwa kuingilia kati na kununua chakula zaidi kutoka nje ili kuokoa hali.
Hii leo serikali imetoa tahadhari kuhusu uhaba wa chakula lakini wiki jana halmashauri ya serikali ya kukabiliana na ukame ilitoa tahadhari kwa serikali kuhusu tisho la ukame.
Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na ukame ni maeneo ya Mashariki ambako mvua haijanyesha kwa muda mrefu.
Mkuu wa halmashauri hiyo aliitaka serikali kuchukua hatua mwafaka ili kuzuia ukame na janga la njaa ambalo liliwahi kushuhudiwa nchini humo miaka kadhaa iliyopita.
Katika eneo la Turkana Kaskazini mwa Kenya ambako jamii za kuhamahama huishi, hali inasemekana kuwa mbaya zaidi.
Kuna ripoti za watu kukabiliwa na njaa pamoja na ukame. Mtoto mmoja aliripotiwa kufariki kutokana na njaa
Inaarifiwa watu kadhaaa wamelazwa hospitalini kutokana na utapia mlo huku familia moja ikilazimika hata kupika nyama ya Mbwa kutokana na ukosefu wa chakula.

NJIWA WA AMANI WA PAPA FRANCIS WASHAMBULIWA MBELE YA UMATI

Purukushani na kusakwa kukiwa kumeanza, kunguru akifukuza wa kwake, shakwe akisaka wa kwake. ©AP
Katika hali isiyotarajiwa, ndege aina ya njiwa ambao walirushwa kutoka kwenye dirisha ambalo Papa Francis alikuwa akihubiria siku ya Jumapili kama ishara ya kutakia amani mataifa ya ulimengu ikiwemo Ukraine, ambayo iko kwenye machafuko kaw siku kadhaa sasa, walijikuta katika hali ya taharuki mara baada ya kushambuliwa na ndege wenzao aina ya kunguru na shakwe (seagull), makao makuu ya kanisa Katoliki Duniani, Vatican.

Njiwa hao ambao walipeperushwa na watoto waliokuwa sanjari na Papa kwenye kibaraza cha dirisha hilo, hawakupewa muda wa ziada, bali kuanza kushambuliwa kwa minajili ya kutumika kama kitoweo na ndege wenzao.

Hata hivyo katika shambulio hilo kwa njiwa hao ambao ni ishara ya amani, ambalo lilianza mara baada ya Papa na watoto hao kuondoka dirishani, njiwa mmoja alijiokoa kwa kuingia kwenye dirisha la ghorofa la chini yake, ilhali njiwa mwingine ambaye alikuwa akifukuzwa na kunguru, hatma yake haikujulikana mara moja mara baada ya kupoteza manyoya kadhaa mkiani alipokuwa akidonolewa na kunguru mara kwa mara.

Hapa watoto wakiwaachia njiwa wapae ©AP

Njiwa wakijipanga kwa safari. ©AP

Mpambano wa ndege ulipoanza, ndege aina ya shawe (seagull) akimshambulia njiwa wa 'amani' ©AP

Njiwa akiwa amedakwa mkiani na shakwe ©AP



Kunguru akifukuzia windo ©AP
Vurugu angani, njiwa kichwa chini mkia juu ©AP



kudonolewa kukiendelea ©AP


Picha zote kwa hisani ya Associated Press.

Wakamatwa na pembe za Ndovu Togo

Polisi nchini Togo wamewakamata watu watatu baada ya kuwanasa na tani mbili za pembe za Ndovu wakizafirisha kwenda Vietnam
Afrika inakabiliana na changamoto ya kutokomeza biashara haramu ya pembe za Ndovu
Wawili kati ya washukiwa hao ni raia wa Togo na mwengine ni raia wa Vietnam.
Watetezi wa mazingira, Magharibi mwa Afrika wanasema kuwa eneo hilo, ni kitovu cha kusafirishia pembe za Ndovu kutoka Afrika ya Kati hadi Asia.
Licha ya marufuku ya biashara ya Pembe za Ndovu, karibu nusu karne iliyopita, idadi ya Ndovu wa Afrika inaendelea kupungua na huenda wakatokomea.
Idadi ya Ndovu hao imepungua kwa asilimia 60 katika miaka kumi iliyopita.
Pembe hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya Konteina pamoja na mbao ambazo zilikuwa zikisafirishwa kwenda Vietnam.
Watetezi wa mazingira wanasema kuwa kiwango cha pembe hizo kinaonyesha kama ni Ndovu 230 waliuawa.
Mataifa ya Afrika yanakabiliana na changamoto ya kukomesha biashara haramu ya Pembe
Siku ya Jumanne mahakama moja nchini Kenya ilitumia kwa mara ya kwanza sheria zake kali za kupambana na biashara haramu ya pembe za Ndovu kwa kumtoza mchina mmoja faini ya dola zaidi ya laki mbili.
Alikamatwa wiki jana akiwa na kilo tatu na nusu za pembe za ndovu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi