Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, June 30, 2016

Mercy without works is dead, Pope Francis says

Vatican City,In his Jubilee general audience for the month of June, Pope Francis focused his speech on the works of mercy and how to put them into action. He also gave thanks for his recent visit to Armenia, and spoke of his coming trips to Georgia and Azerbaijan. “Mercy without works is dead,” the Pope said June 30, quoting St. James. What brings mercy to life, he said, is “it’s constant dynamism for going to meet the needy and the necessities of the many spiritually and materially disadvantaged.” He encouraged pilgrims to make “a serious examination of conscience,” telling them “not to ever forget that mercy is not an abstract word, but a style of life.” “It’s one thing to speak of mercy, but it’s another to live mercy,” he said, noting that a person can either be merciful or unmerciful, but either way “it’s a lifestyle I choose.” The Pope spoke to the thousands of pilgrims gathered in St. Peter’s Square for his eighth Jubilee general audience. Typically held on Saturdays once a month for the duration of the Holy Year of Mercy, the Jubilee audience for June was moved to Thursday, since the Pope will take a break from all public meetings and audiences for the month of July. In his address, Francis noted how not a day goes by that we don’t encounter the many needs of society’s poorest and “most tested.” At times “we pass in front of dramatic situations of poverty and it seems as if they don’t touch us,” he said. “Everything continues as if there was nothing, in an indifference which eventually renders us hypocrites and, without realizing it, leads to a form of spiritual lethargy that numbs the spirit and renders life sterile.” People who pass through life without ever becoming aware of the needs of others are people who don’t really live, nor do they know what it means to serve others, he said. “Remember well: whoever doesn’t live to serve, doesn’t need to live!” the Pope said, explaining that with Jesus, there are no “escape routes.” He pointed to the Gospel passage from Matthew 25 read aloud at the beginning of the audience in which Jesus tells his disciples that when the sheep and the goats are separated at the end of time, the Lord will tell the sheep to come, because they fed him, gave him something to drink and clothed him when he was hungry, thirsty and naked. “You cannot beat around the bush in front of a person who is hungry: we need to feed them. Jesus tells us this!” Pope Francis said, adding that the works of mercy are not merely theoretical subjects, “but concrete testimonies.” He encouraged pilgrims to “give space to the imagination of charity” in finding new ways to meet the needs of the spiritually and materially poor in an increasingly globalized world. Christians, he said, must remain vigilant when faced with the poverty produced by “the culture of well-being.” Doing so, he said, will not only keep their gaze from weakening, but will also allow them to keep their focus on what’s essential. Looking at the essential, Francis said, means see Jesus “in the hungry, in the prisoner, in the sick, in the naked, and those who don’t have work and have to provide for a family…in those who are only sad, who are mistaken and need advice.” “These are the works Jesus asks of us: to look at Jesus in them, in these people, because Jesus looks at me, at all of us, like this.” Pope Francis then turned his focus to his recent trip to Armenia, “the first Christian nation,” where he traveled June 24-26 for an official visit. Armenians, he said, are “a people who, in the course of their long history, have witnesses to the Christian faith with martyrdom,” and expressed his gratitude for having been welcomed “as a pilgrim of fraternity and peace.” The Pope noted how he will also visit the Caucasus nations of Georgia and Azerbaijan Sept. 30 – Oct. 2, and said he accepted the invitation to do so for two reasons. The first, he said, is to “value the ancient Christian roots present in these lands – always a spirit of dialogue and with other religions and cultures,” while the second is to “encourage hope and pathways of peace.” “History teaches us that the path of peace requires great tenacity and continued steps, beginning with the small ones and gradually making them grow, going toward one another. Because of this my wish is that each person give their contribution for reconciliation,” he said. Francis closed his address by extending his “embrace” to the bishops, priests, religious and faithful of Armenia, and praying that the Virgin Mary would “help them to remain solid in the faith, open to encounter and generous in the works of mercy.”

Mwandishi wa ''The Concubine'' afariki

Mwandishi maarufu wa Nigeria Elechi Amadi amefariki akiwa na umri wa miaka 82. Amadi ambaye aliandika vitabu maarufu kama vile The Concubine,Isiburu,Sunset in Biafra,Peppersoup na The Road to Ibadan alifariki siku ya Jumatano mwendo wa saa tisa,wiki moja moja baada ya kuripotiwa kuugua. Duru zimearifu kuwa marehemu alitarajiwa kuhudhuria hafla ya kusoma vitabu katika bandari ya Hacourt lakini hakuweza kutokana na kuugua kwake. Akiwa mzaliwa wa eneo la Aluu katika jimbo la Riverstate mwaka 1934,Elecchi Amadi alisoma katika taasis ya Umuahia,Oyo na chuo kikuu cha Ibadan ambapo alipata shahada yake katika somo la fizikia na hesabati. Pia aliwahi kufanya kazi kama mpimaji wa mashamba.

Ibuprofen inaweza kupunguza makali ya Ebola

Dawa ya maumivu Ibuprofen na dawa ya kutibu saratani Toremifene zinaweza kukata makali ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ,watafiti wamesema. Wanasayansi walitumia Kifaa cha Diamond Light Source kuvifanya uchanganuzi virusi vya ebola kwa kina. Walibaini kwamba dawa hizo mbili zinaweza kushirikiana kukabiliana na Ebola wakati virusi hivyo vinapojiandaa kuambukiza seli za mwili wa bindamu. Hatahivyo ,watafiti hao wameonya kwamba huo ni mwanzo na kwamba dawa zaidi zilizo na uwezo mkubwa zinafaa kutafutwa. Synchrotron hiyo huchochea kasi ya elektroni hadi kuzalisha mwanga mkali sana. Hii inaweza kutumika kwa kuchambua mradi wa kutengeza vitu wa atomiki katika mpango mkubwa zaidi kuliko darubini za kawaida. Lengo la utafiti huo ni protini kwenye uso wa virusi vya Ebola ambayo inaviruhusu kuambukiza seli. ''Hili ndio lengo kuu katika uso wa virusi hivyo,hili ndio huwajibika kujiweka katika seli ,ni protini muhimu kuelewa'',alisema mtafiti Prof Dave Stuart, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.

Tuesday, June 28, 2016

Tunaitafakari Uingereza bado:Marekani

Kufuatia kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi. Msimamo huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni kufuatia kura ya maoni ijumaa wiki iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema hayo katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo. John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo. Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa dunia kwa ujumla

Mila zatawala usakaji wa waliokufa maji Kenya

Mili miwili ya wanamuziki 10 waliokufa maji katika ziwa Victoria baada ya dau lao kuzama imepatikana. kulingana na gazeti la The Standard,mili hiyo hatahivyo itasalia kuwepo katika ufukwe wa bahari hadi pale miili minane iliosalia ipatikane kulingana na tamaduni za eneo hilo. Kuomboleza kumepigwa marufuku kwa muda kutokana na hofu kwamba huenda kukaleta bahati mbaya na kuathiri juhudu za kuitafuta miili hiyo. Wingu la kusikitisha bado limetanda katika ufukwe huo huku miili ya wanachama hao wa bendi ya Boyieta Ohangla ambao maisha yao yalisitishwa mara moja na mawimbi makali katika ziwa Victoria ilipatikana huku operesheni ya kuisaka miili mingine ikiendelea. Jamaa za wanachama hao walilazimika kuzuia machozi ili kuitizama miili ya wapendwa wao. Kulingana na Odida Buoga mwenye umri wa miaka 70 ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wazee wa Kiluo hakuna mtu anayepaswa kulia kabla ya miili hiyo haijapatikana. ''Ni utamaduni wetu kwamba mtu anapofariki jamii yake ni lazima ipige kambi katika ufuo wa ziwa hadi pale mwili unapopatikana'',mzee buoga aliliambia gazeti la The Standard nchini Kenya. Ameelezea kwamba watu hawafai kulia kwa hofu kwamba kilio hicho huenda kikazuia miili ama mwili huo kupatikana. Anasema kwamba wakati msakaji wa mwili anapopata mwili huo ndani ya maji ama katika ufuo ,hulazimika kuufunga kamba mwili huo na kuuvuta hadi ufuoni na baadaye kuwajuza watu wa familia yake. Kulingana na gazeti la The Standard,iwapo mtu atashindwa kufanya hivyo basi inasemekana kwamba huenda akaandamwa na mazingaombwe. Mzee huyo anasema kuwa mtu yeyote atakayepata mwili atalazimika kuandamana na mwili huo hadi nyumbani kwa familia ya mfu huo ili achinjiwe kuku kwa lengo la kujitakasa. ''Kuku ama mbuzi unayepewa sio wa kufugwa bali ni kumchinja na baadaye umfanye kitoweo ili kujitakasa''.Anasema kuwa mmiliki wa boti iliyozama pia naye anapewa kuku ili kujitakasa. Iwapo hilo halitofanyika basi boti hiyo huonekana kama yenye bahati mbaya na hivyobasi haiwezi kutumika tena. Kwa lengo la kuomboleza na familia ya marehemu wavuvi huwa hawaruhusiwi kufanya uvuvi,badala yake hutumia boti zao kuisaka miili. Maafisa wa polisi pia walizuiliwa kuchukua miili hiyo hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti na badala yake wameagizwa kusubiri hadi miili yote itakapopatikana.

Aliyeibuka wa kwanza katika mtihani India afungwa jela

Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili. Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi. Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali. Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai. Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto. Gazeti la Hindu lilimnukuu afisa mkuu wa polisi Manu Maharaj akisema kuwa bi Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto. Wakati huohuo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye alishindwa kusema kwamba H20 ni maji.

Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzani.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi. Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika. Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania. Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia. Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035. Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika. Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo. Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen. ''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.

Monday, June 27, 2016

Kundi la IS lakiri kushambulia Kambi Jordan

Kundi la wanamgambo wa Isalmic State siku ya jumapili lilikiri kutekeleza shambulio la kujitoa muhanga lililoua wanajeshi saba wa Jordan katika mpaka wa Syria.Taarifa hiyo ilitolewa kwenye tovuti ya shirika la habari la Amaq. likinukuu chanzo ambacho hakikutajwa kwa jina, lilisema kuwa shambulio la jumanne dhidi ya kambi ya Jordan na Marekani mjini Rokban nchini Jordan lilitekelezwa na mpiganaji wa Islamic State. Mlipuko, ambao pia uliwajeruhi wanajeshi 13 ulitokea katika eneo ambalo maelfu ya raia wa Syria wamepiga kambi.

Mabaki yanayokisiwa kuwa ya ndege ya Malaysia yapatikana TZ

Maafisa wa uchukuzi nchini Tanzania wanachunguza iwapo mabaki ya ndege yaliyopatikana ufuoni ni ya ndege ya Malaysia iliyotoweka miaka miwili iliyopita. Picha za mabaki hayo yaliyopatikana visiwa vya Pemba zimekuwa zikisambaa sana mtandaoni. Maafisa wa Tanzania wamewasiliana na maafisa wa Malaysia ambao wanapanga kutuma wachunguzi, Hilo litawezekana tu wakati watengenezaji wa ndege hiyo watafika na kuchunguza mabaki hayo. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uchukuzi wa Ndege Tanzania Redemptus Bugomola ameambia BBC kwamba bado ni mapema mno kubaini iwapo mabaki hayo ni ya ndege ya MH370. Shirika la habari nchini Malaysia Bernama lilimnukuu waziri uchukuzi nchini humo Liow Tiong Lai, akisema kuwa mabaki ya ndege hiyo yatafanyiwa uchunguzi kubainia ikiwa yana uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea ya MH370. "Mabaki hayo ya ndege ni makubwa ... lakini ni baada tu ya kubaini kwamba ni ya ndege aina ya Boeing 777 ndipo tutatuma wachunguzi huko kwenda kuchunguza iwapo kweli ni ya MH370 au la," amesema Liow. Ndege hiyo ya Boeing 777 nambari MH370 ilitoweka 2014 ikiwa na watu 239 muda mfupi baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur ikielekea Beijing. Vipande vya ndege hiyo vilipatikana katika visiwa vya Reunion Julai mwaka 2015. Hivi majuzi, mabaki ya ndege sawa na hiyo yalipatikana Madagascar lakini baada ya uchunguzi ikabainishwa kwamba hayakuwa ya ndege hiyo ya MH370.

Msiwahukumu wa mapenzi ya jinsia moja :Papa Francis

Papa Francis amewataka Wakatoliki Duniani kuwaomba radhi watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kwa madai kuwa si haki kuwahukumu na kuwachukulia kinyume kwani kanisa halina mamlaka ya kuwahukumu. Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege wakati akirejea kutoka Armenia,Papa Francis kanisa pia linapswa kuwaomba makundi mengine ambayo yametengwa kama vile wanawake,masikini na watoto ambao wapo katika ajira hatarishi. Hata hivyo baadhi ya wakatoliki wenye msimamo mkali wamepinga hatua yake ya kuwazungumzia watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Thursday, June 23, 2016

Ethiopia yatupa mipira ya kondomu milioni 69

Ethiopia inatarajiwa kutupa mipira ya kondomu milioni 69, iliyonunuliwa kwa kima cha dola milioni mbili kutoka na ubora wa chini wa mipira hiyo. Hii ilitangazwa na mfuko wa serikali unaohusika na madawa nchini humo. Hatua sasa zinachukuliwa kuhakisha kuwa fedha zilizotumika na zilizotolewa na shirika moja la kimataifa linalofadhiliwa na Umoja wa Mataifa zimerejeshwa.

Wabunge wakaa chini shinikizo la silaha

Wabunge wa chama cha Democrats huko Marekani wamegoma kukaa kwenye viti vya bunge la Congress la nchi hiyo na kukaa kwenye sakafu kushinikiza kutungwa kwa sheria kali kuhusu umiliki wa bunduki. Wanataka Bunge hilo kuendelea na vikao vyake vilivyopangwa hadi wiki ijayo ili wapigie kura sheria hiyo kufuatia mauaji yaliyotokea katika klabu ya usiku huko Florida. Hata hivyo Spika wa Bunge hilo Paul Ryan, kutoka chama cha Republican ametupilia mbali hatua hiyo ya kukaa sakafuni kusema hiyo ni mbinu ya kujitangaza kisiasa.Mbunge mmoja wa Democrat Jared Huffman kutoka California amempinga spika huyo na kumtaka afanye kazi na wabunge wa Democrats. "Spika Ryan, toka nje ya ofisi yako. Njoo uzungumze na sisi. Sikiliza sauti ya raia wa Marekani. Jiondoe kwenye mlengo wa kulia kwa ajili ya maslahi maalum yasiogemea upande wowote wa itakadi na kusikiliza sauti ya raia wa Marekani. Kama hatuna mswada, kama hatutapiga kura hatutakuwa na mapumziko.Naye mbunge mmoja John Lewis amesema maisha ya maelfu ya watu wasio na hatia yamepotea, lakini bunge hilo halijafanya chochote. ""Muda wa kunyamaza kimya na uvumilivu umekwisha. Tunataka uongozi wa bunge waje na mswada wa sheria wenye maana hapa bungeni wa kudhibiti bunduki. Tunataka kupiga kura. Turuhusu tupige kura. Tumekuja hapa kufanya kazi yetu. Tumekuja hapa kufanya kazi Raia wa marekani wanataka hatua zichukuliwe."

Wednesday, June 22, 2016

Ashtakiwa kumtusi Magufuli katika WhatsApp

Raia mmoja wa Tanzania amefunguliwa mashtaka kutokana na ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo anadaiwa kumtusi Rais John Pombe Magufuli. Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni. Ni mtu wa pili kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa tuhuma za kumtusi rais. Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanza kutekelezwa mwaka uliopta. Kyaruzi anadaiwa kuandika: "'Kwani rais Magufuli hana washauri? hashauriki? Ama ni mjinga tu? Ni Mpumbavu sana. Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?.

Bemba ahukumiwa miaka 18 jela na ICC

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono. Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003. Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo. Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.

Marekani na kura ya Uingereza

Mkuu wa kitengo cha shirikisho la uhifadhi nchini Marekani ,Janet Yellen, ametupilia mbali hoja ya Marekani kuingia kwenye kipindi cha mpito na kuyumba kwa uchumi wake endapo Uingereza itajiondoa katika umoja wa ulaya. Wakati akijibu maswali kutoka katika kamati ya Senate Yellen amesema kipindi cha mpito na kuyumba kwa uchumi wa nchi yake hakutokani ama haitakuwa chanzo cha kura hiyo, hakuna ajuaye nini kitatokea. Ameeleza imani yake kwa wawekezaji kwamba watafanya maamuzi sahihi na kuamua kwa busara katika masoko ya fedha, ambako italeta taswira bei shirikishi na viwango vya juu vya riba kwa wakopaji walio wengi.