Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 28, 2016

Tunaitafakari Uingereza bado:Marekani

Kufuatia kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi. Msimamo huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni kufuatia kura ya maoni ijumaa wiki iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema hayo katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo. John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo. Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa dunia kwa ujumla
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment