Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, June 30, 2016

Mwandishi wa ''The Concubine'' afariki

Mwandishi maarufu wa Nigeria Elechi Amadi amefariki akiwa na umri wa miaka 82. Amadi ambaye aliandika vitabu maarufu kama vile The Concubine,Isiburu,Sunset in Biafra,Peppersoup na The Road to Ibadan alifariki siku ya Jumatano mwendo wa saa tisa,wiki moja moja baada ya kuripotiwa kuugua. Duru zimearifu kuwa marehemu alitarajiwa kuhudhuria hafla ya kusoma vitabu katika bandari ya Hacourt lakini hakuweza kutokana na kuugua kwake. Akiwa mzaliwa wa eneo la Aluu katika jimbo la Riverstate mwaka 1934,Elecchi Amadi alisoma katika taasis ya Umuahia,Oyo na chuo kikuu cha Ibadan ambapo alipata shahada yake katika somo la fizikia na hesabati. Pia aliwahi kufanya kazi kama mpimaji wa mashamba.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment