Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, June 30, 2016

Ibuprofen inaweza kupunguza makali ya Ebola

Dawa ya maumivu Ibuprofen na dawa ya kutibu saratani Toremifene zinaweza kukata makali ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ,watafiti wamesema. Wanasayansi walitumia Kifaa cha Diamond Light Source kuvifanya uchanganuzi virusi vya ebola kwa kina. Walibaini kwamba dawa hizo mbili zinaweza kushirikiana kukabiliana na Ebola wakati virusi hivyo vinapojiandaa kuambukiza seli za mwili wa bindamu. Hatahivyo ,watafiti hao wameonya kwamba huo ni mwanzo na kwamba dawa zaidi zilizo na uwezo mkubwa zinafaa kutafutwa. Synchrotron hiyo huchochea kasi ya elektroni hadi kuzalisha mwanga mkali sana. Hii inaweza kutumika kwa kuchambua mradi wa kutengeza vitu wa atomiki katika mpango mkubwa zaidi kuliko darubini za kawaida. Lengo la utafiti huo ni protini kwenye uso wa virusi vya Ebola ambayo inaviruhusu kuambukiza seli. ''Hili ndio lengo kuu katika uso wa virusi hivyo,hili ndio huwajibika kujiweka katika seli ,ni protini muhimu kuelewa'',alisema mtafiti Prof Dave Stuart, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment