Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, June 22, 2016

Bemba ahukumiwa miaka 18 jela na ICC

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono. Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003. Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo. Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment