Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, August 28, 2013

Marekani yaadhimisha miaka 50 ya maandamano ya Washington.

MLK
MLK (Martin Luther King)Wamarekani wanaadhimisha miaka 50 tangu maandamano kuelekea Washington na hotuba ya kihistoria “I Have a Dream” iliyotolewa na mchungaji Martin Luther mbele ya makumbusho ya rais Lincoln.
Tangu jumamosi maelfu ya Wamarekani wamekuwa wakiwasili katika mji mkuu wa Marekani kuhudhuria sherehe mbali mbali zilizoandaliwa ili kukumbuka siku hii muhimu ya Ougusti 28 iliyobadili kabisa ukurasa wa historia na haki za kiraia Marekana.
Siku ya Jumamosi maelfu na maelfu ya wamarekani waliwasili kutoka pembe mbali mbali za nchi hii ili kuiga maandamano yaliyofanyika miaka 50 kumkumbuka kiongiozi wa kutetea haki za kiraia aliyeuliwa  pamoja na kuwasilisha  ujumbe sawa na ulotolewa wakati ule kuhusiana na masuali mbali mbali ya kijamii.
Watayarishaji na waandamanaji wametoa wito kutaka kutekelezwa masuala mbali mbali, ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuanzia haki za wanawake na raia, hadi mageuzi ya uhamiaji, kukomeshwa ghasia za bunduki na kubuniwa nafasi za ajira.
Mbunge kutoka Georgia John Lewis kiongozi pekee aliyehutubia mkutano huo wa 1963 aliyehahi, alizungumzia siku ya jumamosi juu ya maisha magumu aliyokabiliana nayo akiwa Mmarekani mwenye asili ya kiafrika.
"Nilikamatwa mara 40 mnamo miaka ya 60 nilipigwa na kuachwa kwenye damu nikiwa nimezirai. Lakini sijachoka wala siko tayari kukachini na kusema nimeshindwa. Niko tayari kwa vita na vita vitaendelea."
 Kwa marekani wengi wenye asili ya kiafrika ingawa kuna rais mweusi White house wangali wanaamini ndoto haijakamilika. Kijana wake kiongozi aliyeuliwa, martin Luther King wa tatu anasema baadhi ya maswala babake alipigania yangali ni masuala yenye matatizo makubwa hii leo.
"Hii leo kukiwa na asili mia 12 ya wasokuwa na kazi miongoni mwa wamarekani wenye asili ya kiafrika na asili mia 38 ya watoto wote wasio wazungu nchini humu wanaishi chini ya kiwango cha umaskini , basi tunajua ndoto iko mbali na kukamilika."
Kutokana na hali hiyo hii leo maandamano yanafanyika kukumbuka malengo yaliyotolewa miaka 50 ilyopita, na kuhamasisha na kuzungumzia changamoto zilizopo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment