Writen by
sadataley
6:27 PM
-
0
Comments
Chama tawala nchini Tanzania CCM kimemfukuza uanachama aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bernard Membe.
Membe
alikuwa akikabiliwa na tuhuma za maadili pamoja na viongozi wengine
waandamizi wengine wawili makatibu wakuu wa zamani Yusuf Makamba na
Abdulrahman Kinana, ambao wao hawajafukuzwa. Makamba amesamehewa, huku Kinana akionywa kwa karipio.
Akisoma taarifa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM hii leo, Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole amedai kuwa mwenendo wa Membe umekuwa si wa kuridhisha toka mwaka 2014.
"Kamati Kuu imeazimia kwa kauli moja kwamba Bernard Membe afukuzwe uanachama wa CCM. Uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonesha mwenendo wake kutoka mwaka 2014 ambako katika chama amewahi kupata adhabu nyingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha," ameeleza Polepole.
Kwa mujibu wa Polepole, uongozi wa chama hicho umeazimia kumsamehe Mzee Makamba kwa kuwa: "...amekuwa mtu muungwana na mnyenyekevu kwa mamlaka ya chama. Na ameomba asamehewe kwa barua."
"Mzee Kinana anapewa adhabu ya karipio kwa mujibu wa kanuni... Atakuwa katika hali ya matazamio kwa mda wa miezi 18 ili kumsaidia katika jitihada za kujirekebisha. Hatakuwa na haki ya kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama, japo ataruhusiwa kupiga kura kama atakuwa na dhamana hiyo," ameeleza Polepole.
'Membeatoa neno'
"Watanzania wenzangu nimepata habari ya kufukuzwa kwangu kutoka kwenye Chama changu cha CCM. Simu zinamiminika hadi nashindwa kuzijibu. Tulieni! Nitapata muda wa kuongea na wote muda si mrefu!"
BBC
No comments
Post a Comment