Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, January 3, 2023

‘Mchakato wa katiba kukwamuliwa na Mikutana ya hadhara ruksa Tanzania’- Rais Samia

Na Yusuph Mazimu, BBC Swahili

Samia

CHANZO CHA PICHA,MSEMAJI WA SERIKALI

Rais wa Tanzania, amesema Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya katiba, uliokwama kwa zaidi ya miaka 8, toka mwaka 2014.

Mbali na hilo Rais Samia ameondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, lililodumu kwa zaidi ya miaka 7, tangu mwaka 2015.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu Tanzania, Rais Samia amesema ‘Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya katiba, kwa jinsi tutakavokuja kuelewana huko mbele’, wengine wanasema tuanze na katiba ya warionba, wengine tuanze na katiba pendekezwa, lakini kuna mambo ya ulimwengu yamebadilika’, alisema.

Alisema itaundwa kamati maalumu kwa ajili kutoa ushauri wa namna ya kwenda kupata katiba ‘si muda mrefu, tutakwenda kuanza na kamati itakayokuja kutushauri, nataka kusema katiba hii ni ya watanzania si ya vyama vya siasa’, alisema.

Ukiacha Katiba mpya, kwa muda mrefu nchini humo kulikuwa na kilio hasa kutoka kwa wanasiasa na jamii za kimataifa kuhusu haki ya kufanya siasa hasa mikutano ya siasa kuruhusiwa, ambayo ipo kisheria.

'Hii ni haki kwa sheria zetu, ni haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara’, uwepo wangu leo mbele yenu ni kuja kutangaza, lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoka', alisema.

Mikutano hiyo ilizuiwa muda mfupi baada ya aliyekuwa rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kuingia madarakani kupitia uchaguzi mkuu wa 2015.

'Lakini ndugu zangu tuna wajibu, wajibu wetu serikali ni kulinda mikutano ya vyama vya siasa, wajibu wenu vyama vya siasa ni kufuata sheria na kanuni zinavyosema’, twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, tukafanye siasa za kupevuka, tukafanyeni siasa za kujenga sio za kubomoa, si kurudi nyuma hapa tulipofika, ‘sisi ndani ya CCM tunaamini katika kukosolewa na kujikosoa’, alisema.

Hata hivyo baada ya Rais Samia kuingia madarakani mwaka 2021, kufuatia kifo cha Magufuli, alionyesha dhamira ya kuleta maridhiano kwa kuunda kikosi kazi cha kukusanya maoni.

'Wakati mnanikabidhi kuongoza nchi hii, busara zilinituma, kwamba jinsi nilivyolipokea taifa hili, kuna haja ya kufanya taifa liwe kitu kitu kimoja, wote tuzungumze lugha moja, alisema Rais Samia na kuongeza ' Ili taifa lilwe moja, lazima tuwe na maridhiano, nikasema kwanza tuwe na mazungumzo kwenye vyama vya siasa'.

Kikosi kazi kilichoundwa kilileta maoni kwenye maeneo 9, ambapo makubwa matatu yaliyojitokeza ni kutaka kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya na marekebisho sheria mbalimbali.

Rais amesema tayari michakato ya marekebisho ya sheria imeanza na waziri husika atakuja kuleta taarifa ya muelekeo.

Wanasiasa, akiwemo kiongozi Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo akizungumza kuhusu uamuzi wa huo wa Rais kukwamua mchakato wa katiba na kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa alisema ‘ni hatua kubwa sie tuna furaha, amesimama kwenye maneno yake’.

Mbali na Makamu wa rais Phillip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mkutano huo wa rais na vyama vya siasa uliofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na Wenyeviti, makamu wenyeviti na makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu kutoka vyama vote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu Tanzania.

Vyama hivyo ni UPDP, NRA, TADEA, TPL, CHADEMA, CUF, NCCR, UDP na UMD.

Vingine ni chama tawala CCM, DEMOKRASIA MAKINI, DP, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT- Wazelendo.

BBC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment