Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, February 28, 2014

Uwanja wa ndege wa Crimea nchini Ukraine waendelea na shughuli zake licha ya taarifa za kutekwa na watu wenye silaha

Polisi wakiwa kwenye Uwanja wa ndege wa Crimea nchini Ukraine kuhakikisha usalama
Polisi wakiwa kwenye Uwanja wa ndege wa Crimea nchini Ukraine kuhakikisha usalama
www.startribune.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Uwanja wa mjini Crimea nchini Ukraine umeripotiwa kuendelea na shughuli zake za kawaida hii leo licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa uwanja huo ulikuwa umetekwa na watu wenye silaha.

Taarifa zinaeleza kuwa abiria wanaendelea kuingia katika uwanja huo wa ndege kama kawaida kwa ajili ya safari zao.
Hayo yanakuja wakati huu mataifa yenye nguvu yakionya kuhusu hatua ya kuingilia masuala ya Ukraine ambayo inakabiliwa na hali ya sintofahamu baada ya rais Victor Yanukovich kuondolewa madarakani.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel ametoa angalisho kwa mataifa kutoingilia mipaka ya Ukraine.
Kwa upande wake waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa nchi ya Urusi inapaswa itekeleze ahadi yake ya kutoingilia mipaka ya Ukraine.

Usalama na uchumi katika ajenda ya ziara ya rais wa Ufaransa nchini Nigeria

Marais wa Ufaransa na Nigeria, Francois Hollande na Goodluck Jonathan mjini Paris, februari 11 mwaka 2013.
Marais wa Ufaransa na Nigeria, Francois Hollande na Goodluck Jonathan mjini Paris, februari 11 mwaka 2013.
REUTERS/Philippe Wojazer

Na RFI
Rais wa ufaransa François Hollande ni mgeni wa heshma nchini Nigeria katika sherehe ya kumbukumbu ya miaka mia moja ya muungano wa taifa hilo. Ziara ya siku moja, ambayo ni ishara kubwa, kwa taifa ambalo sehemu yake kubwa linazungumza kingereza. Kando na sherehe hizo, mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, amani na maendeleo katika bara la Afrika unatazamiwa kuanza mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria.

Hii ni fursa ya rais wa Ufaransa ya kudumisha uhusiano, hasa katika masuala ya usalama, katika nchi ambayo inakabiliwa na vurugu za usalama zinazosababishwa na kundi la waislamu la Boko Haram.
Visa vya mashambulizi ya kujilipua, mauaji ya kuvizia, na utekaji nyara, vimekua vikishuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Nigeria, huku kundi la Boko Haram likiendelea na hujuma zake kaskazini mwa taifa hilo, baada tu ya jeshi kuanzsha operesheni tangu katikati mwa mwezi wa mei mwaka 2013 katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa.
Siku tatu ziliyopita, watu wenye silaha walifanya shambulizi dhidi ya shule moja la sekondari, na kuua wanafunzi 43 katika jimbo la Yobe. Mpaka sasa hakuna kundi lolote ambalo, limekiri kutekeleza shambulio hilo, lakini bado dhana ya mauaji hayo imekua ikielekezwa kwa kundi la Boko Haramu.
Mbali na sherehe ya kumbukumbu ya miaka mia moja ya muungano, Nigeria inaandaa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, amani na maendeleo katika bara la Afrika. Viongozi wengi wanasubiriwa kushiriki mkutano huu. François Hollande ni mmoja pekee wa marais kutoka mataifa ya magharibi, ambaye amealikwa katika mkutano huu.
Ziara hii ya rais François Hollande inakuja baada ya mwenyeji wake wa Nigeria, Goodluck Jonathan kufanya ziara mjini Paris mwezi desemba mwaka jana, ziara ambayo rais Goodluck Jonathan, aliomba Ufaransa kusaidia kuweka ushirikiano wa kimataifa kwa kukabiliana dhidi ya kundi la Boko Haram.
Juma liliyopita, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alitishia katika ukanda wa video kuanzisha mashambulizi katika jimbo muhimu la mafuta linalopatikana kusini mwa Nigeria, matamshi ambayo yaliwafanya viongozi wa taifa hilo, kutoa wito wa kuweko na ushirikiano wa kimataifa dhidi ya waasisi wa kundi hilo, ambao wako pembezuni mwa ziwa Tchad.

Uganda yapuuza vitisho vya mataifa ya Magharibi baada ya kupitisha sheria kali dhidi ya ushoga

Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo
Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo
www.redpepper.co.ug

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Serikali ya Uganda imepuuzilia mbali kauli za vitisho na hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa na mataifa ya magharibi kusitisha misaada yao kwa nchi hiyo kutokana na kupitisha sheria kali inayokataza vitendo vya ushoga, ikisema inaweza kujiendesha hata bila kutegemea mataifa ya Ulaya.

Msemaji wa Serikali ya Uganda, Ofwono Opondo, amewaambia waandishi wa habari mjini Kampala kuwa nchi yao haitishwi na mataifa ya magharibi kwa kukatisha misaada yao kwa sababu ya kukataa ushoga na kuongeza kuwa nchi yake itaendelea kujiendesha hata bila ya misaada yao.
Kauli ya Uganda inakuja kufuatia benki ya dunia kutangaza kusitisha msaada wa fedha kwa nchi ya Uganda uliokuwa unafikia kiasi cha dola milioni 90 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini humo.
Nchi za magharibi zimeendelea kutishia kusitisha misaada yao kwa nchi ya Uganda baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya kupiga marufuku wanaoendeleza mapenzi ya jinzia moja huku wadadisi wa maswala ya kiuchumi wakisema huenda nchi hiyo ikakumbwa na wakati mgumu.

RAIS KIKWETE ALIPOUNGANA NA JUMUIYA YA CHUO KIKUU KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA BALOZI KAZAURA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo . Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadick.
  























Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine  kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo siku  ya tarehe  27.02, 2014.






















 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho  kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo.
























Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu  kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo 
 PICHA NA IKULU

MWIGULU ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM KALENGA


 











Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 











Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 











Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 








 


Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
 











 Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.                                 
 Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga.
 Katibu wa CCM  mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu
 Mjumbe Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana,  akitema cheche jukwaani, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA MAREKANI, IKULU DAR ES SALAAM.


                                                                                                                                                           


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.



















Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya sanamu ndogo ya mji wa Vallejo toka kwa  Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.



















Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na  Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis na ujumbe wake walipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.

PICHA NA IKULU

TFF yasitisha mkataba wa kocha wake

Timu ya Taifa ya Tanzania
Hatimaye Shirikisho la Kabumbu nchini Tanzania TFF limetangaza kuvunja mkataba wake na Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen kwa kile kilichoelezwa maafikiano ya pamoja baina ya kocha huyo,TFF, na Serikali.
Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la soka Tanzania amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida hasa baada ya wadau mbali mbali kuona kuwa huu ni wakati wa kufanya mabadiliko ya lazima katika benchi la ufundi la Taifa Stars ambayo inajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa Fainali za kombe la mataifa Afrika hapo mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.
Kwa Upande wake Kocha Kim Poulsen amesema na rekodi yake inaonyesha kuimarika kwa soka la Tanzania katika kipindi cha takriban miaka miwili aliyokuwa akikinoa kikosi cha Taifa Stars lakini kusitishwa mkataba ni jambo la kawaida kwa kocha yeyote baada ya kipindi fulani kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na ndiyo sehemu ya maisha.Kuhusu gharama za kuvunja mkataba na Kocha huyo Bwana Malinzi amesema serikali haitagharamia uvunjaji huo wa mkataba na kocha huyo na badala yake wapo wadau waliojitokeza kugharamia kutokana na kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko katika kipindi hiki kwa faida ya soka la Tanzania.
“Kama kocha unapoona ndiyo umefanya kazi yako,unapaswa kuangalia mbele zaidi baada ya kufanya kazi yako si lazima uendelee kuwa hapo, mnakaa na kujadiliana na kuachana kwa amani kisha unapaswa kusonga mbele,ninaondoka nikiwa najivunia kipindi nilichofundisha soka hapa,na ninawatakia kila la kheri Tanzania na Taifa Stars kwa ujumla.”alisema Poulsen.
Kuhusu Kocha mpya wa Taifa Stars Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa TFF amesema hadi sasa wapo makocha watatu raia wa Uholanzi ni wawili na Mjerumani mmoja wanaosailiwa kwa ajili ya kumrithi Kim Poulsen,lakini moja ya vigezo Malinzi amesema kuwa ni lazima kocha huyo awe amewahi kuipeleka kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika moja ya nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.
Katika hatua nyingine kocha Salum Madadi ameteuliwa kukaimu nafasi iliyoachwa wazi na Kim Poulsen ambapo kocha huyo akisaidiwa na Hafidh Badru kutoka Zanzibar watasimamia Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyoko kwenye kalenda ya FIFA baadaye mwezi ujao.

Kenya: Wajumbe wa ODM wazua vurugu

Bwana Odinga anatarajiwa na wengi kuwa atagombea kiti cha urais 2017
Vurugu zimezuka katika uchaguzi wa kuwachagua maafisa wapya wa chama kikuu cha upinzani cha ODM nchini Kenya, chake aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Raila Odinga.
Polisi waliwasili katika ukumbi wa uwanja wa michezo wa kimataifa wa Kasarani viungani mwa jiji la Nairobi kurejesha utulivu baada ya baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliodaiwa kuwa walinda usalama kurusha vita pamoja na masanduku ya kupigia kura wakijaribu kuvuruga uchaguzi huo.
Chama cha ODM ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Kenya kikiwa na idadi kubwa ya wabunge katika bunge la kitaifa pamoja na Senate. Chama hicho kimemudu mgao mkubwa zaidi wa pesa za kufadhili shughuli za vyama vya kisiasa kutoka kwa serikali ya Kenya.Ugomvi ulizuka baada ya kuzuka madai kuwa kulikuwa na orodha ya wajumbe bandia iliyokuwa ikisambazwa pamoja na makaratasi bandia ya kupigia kura. Mbunge maalum Isaac Mwaura ambaye anaishi na ulemavu wa ngozi-Albino-alionekana akisukwasukwa na wajumbe baada ya kuzua zahama kuhusu madai hayo ya udanganyifu katika zoezi hilo la upigaji kura.
Kutokana na raslimali za chama hicho uchaguzi wa leo umeonekana kuzua msisimko mkali pamoja na patashika baina ya wanasiasa mashuhuru ambao wanagombania vyeo mbali mbali.
Bwana Odinga ambaye alishindwa na rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliokumbwa na madai ya udanganyifu mwezi Machi mwaka uliopita anatetea kiti chake kama kiongozi wa chama, dalili kwamba huenda akagombea tena kiti cha urais mwaka 2017.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura Bwana Odinga alizungumzia maswala mbali mbali yanayohusiana na usalama nchini Kenya pamoja na kuiponda serikali ya mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta kwa kushindwa kuleta suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wakenya.

K.K.K.T DAYOSISI YA IRNGA YAONDOKEWA NA MTENDAKAZI WAKE. NI MHASIBU WA SHULE YA SEKONDARI BOMALANG'OMBE


Mtikila, Makaidi, Kingunge ‘waliteka’ Bunge la Katiba

Mchungaji Mtikila, ambaye jana alizungumza kwa utulivu wakati akitoa hoja zake za kuunga mkono kanuni inayotaka kufanya maamuzi kwa kupiga kura kwa siri. 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Wajumbe watatu wa Bunge Maalumu la Katiba wamekuwa kivutio katika ndani na nje ya Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru.
Mchungaji Mtikila, ambaye jana alizungumza kwa utulivu wakati akitoa hoja zake za kuunga mkono kanuni inayotaka kufanya maamuzi kwa kupiga kura kwa siri,  mara nyingi huzungukwa na waandishi wa habari na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, wakimsikiliza kwa makini hoja zake. Kikubwa kinachomfanya Mtikila kuwa maarufu ni ile hoja yake ya kutaka kurejea kwa Tanganyika na kuvunjwa kwa Muungano.
Kila anaposimama, Mchungaji Mtikila lazima azungumzie suala la Tanganyika na hata jana aliposimama kuchangia mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, idadi kubwa ya wajumbe walikuwa makini wakimsikiliza.
Wengine walidiriki hata kupiga meza kuashiria kuwa kitakachozungumzwa na mjumbe huyo, kitakuwa na utata.
Dk. Makaidi amejipatia umaarufu mjini hapa kutokana na kumteua mkewe, Modesta Ponera kuwa mmoja wajumbe wawili wa Bunge hilo.
Uteuzi wake na mkewe uliibua sintofahamu baada ya Naibu Katibu wa NLD-Zanzibar, Khamis Haji Mussa, kudai kuwa Makaidi aliwasilisha majina mwili, la kwake na mkewe kwa ajili ya uteuzi.  Hata hivyo, Dk Makaidi kila anapoulizwa kuhusu tuhuma hizo anasema licha ya kuwa Ponera ni mke wake, pia ni mwanachama wa NLD na kwamba ana haki ya kuteuliwa.
Anasema majina ya chama hicho yaliyopelekwa kwa ajili ya uteuzi, yalifuata taratibu zote.
Wa mwisho ni Mzee Kingunge ambaye uteuzi wake ulizua mjadala mkali kutokana na kuteuliwa kupitia kundi la taasisi zisizokuwa  za Serikali.
Baada ya kutakiwa kueleza taasisi aliyotokea, alisema amepitia Kundi la Waganga wa Tiba ya Jadi.
 Karibu kila mjumbe anayekutana na Kingunge hupenda kumsalimia kwani tangu aachane na masuala ya siasa, amekuwa haonekani katika maeneo ya mikusanyiko ya watu mara kwa mara.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz

Mwigulu amwaga ahadi kibao Kalenga

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa (mwenye skafu shingoni) akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Ifunda jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Na Hakimu Mwafongo na Zainabu Maeda, Mwananchi
Iringa. Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba jana alizindua kampeni za chama hicho katika Jimbo la Kalenga mkoani hapa kwa kumwaga ahadi za kuwapatia wananchi maji, umeme na mawasiliano ambayo ni changamoto katika jimbo hilo.
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia uzinduzi huo uliofanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ifunda.
Aliwataka Wanakalenga kuacha kupotoshwa na maneno ya wagombea wengine kwa sababu hawana ridhaa, sifa ya kuwa viongozi wa jimbo hilo na wala hawana uwezo wa kuwaletea maendeleo.
Alisema endapo watamchagua mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa watashirikiana naye kupitia Ilani ya chama hicho kuhakikisha changamoto zote za jimbo hilo zinafanyiwa kazi na mengine mapya yanaongezeka kwa kipindi hiki cha miezi 22 iliyobaki hadi mwaka 2015.
“Nazungumza hili nikiwa kama Naibu Katibu Mkuu wa chama ila msisahau mimi pia ni Naibu Waziri wa Fedha. Nakuagiza Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa andika matatizo yanayolikabili jimbo hili, chama kipeleke serikalini na wananchi watatuliwe kero zao,” alisema Mwigulu.
“Mpeni ridhaa mgombea wa CCM kwa kushirikiana na viongozi wa chama akiwamo Rais wetu ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, tutahakikisha tunayaendeleza mambo yaliyoachwa na marehemu mbunge wetu na kuyamaliza kabisa,” alisema na kuongeza:
“Wagombea wengine wanawadanganya, hawana nia nzuri na ninyi, msijaribu kuwapa upinzani kwani mtapata shida, mtumeni kijana Mgimwa awapelekee changamoto zenu zipatiwe ufumbuzi, mkichagua mgombea mwingine mnajichelewesha wenyewe.”
“Mchagueni mbunge atakayeenda bungeni kutetea bajeti. Wabunge walio wengi wakiwa bungeni kipindi cha kupitisha bajeti wanakataa kuunga mkono bajeti kwa sababu hawana mema na nyie, hawataki maendeleo ya wananchi ili waseme Serikali ya CCM haitekelezi.”
Alisema kati ya shughuli alizokuwa akizitekeleza aliyekuwa mbunge wa Kalenga, marehemu Dk William Mgimwa ni ujenzi wa barabara, hivyo kuwataka wananchi wamchague mgombea wa CCM ili waweze kushirikiana nao ili kuhakikisha kero inamalizika.
Mgimwa
Akizungumza katika mkutano huo, Mgimwa aliwaomba Wanakalenga kumchagua ili aweze kuungana na wabunge wengine kuwaletea maendeleo.
Alisema yupo tayari kuendeleza yote yaliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM na yaliyoachwa na baba yake, marehemu Dk Mgimwa, huku akiweka kipaumbele chake kuwa ni elimu hasa shule za msingi na sekondari, afya na ujenzi wa zahanati katika kila kijiji.

Wabunge wawili CCM wajilipua

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ester Bulaya akichangia hoja juu kuhusu Kanuni za Bunge, Dodoma jana. Bulaya, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), aliunga mkono hoja ya kura za siri.  Picha na Emmanuel Herman 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dodoma/Dar. Wajumbe watatu wa Bunge la Katiba ambao ni wabunge wa CCM wametofautiana na msimamo wa chama chao kwa kuunga mkono kura ya siri itumike kuamua ibara za Rasimu ya Katiba.
Hilo lilitokea jana katika mjadala mkali baina ya wajumbe kuhusu ama matumizi ya kura za siri yatumike au kura za wazi.
Katika mjadala huo ulioonyesha mgawanyiko wa wazi, wajumbe wengi wanaotokana CCM na ambao wamekuwa wakipigania kura za wazi, walionekana kuwazidi kwa wingi wale wanaotaka kura za siri.
Wajumbe wa CCM ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganom– Esther Bulaya na Profesa Juma Kapuya walijitoa mhanga na kueleza bayana kuwa hawako tayari kuona demokrasia ikikandamizwa kwa kulazimishwa kupiga kura za wazi. Akishangiliwa kwa nguvu, Bulaya alisisitiza kuwa hayuko tayari kulazimishwa kupiga kura ya wazi huku akijua kuwa utaratibu huo unamnyima uhuru wake.
“Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi maamuzi magumu kama haya yalifanyika?” Alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu.
Bulaya alisema hakuna sheria inayomtaka mtu kushurutishwa kufanya uamuzi na kwamba kumtaka atoe sauti ya juu katika kura za wazi, ni kumlazimisha kufanya kinyume na matakwa yake.
Alisema kamwe hawezi kuuza uzalendo wake kwa kupiga kura za wazi na kwamba atapimwa kwa utashi wake kuhusu kile anachokiamini. Kwa upande wake, Profesa Kapuya alisema namna nzuri ya kumpa uhuru mpiga kura, ni kutomshurutisha ili afuate matakwa ya wengine.
Alisema kura za siri ndizo zitakazowaimarisha wajumbe na kwamba kinyume chake, kura za wazi zitawagawa na hatimaye kutoka bungeni wakiwa vipande vipande.
Kwa upande wake, Anna Kilango Malecela aliunga mkono ‘kiaina’ kura ya siri akisema alimsikiliza Profesa Ibrahim Lipumba kwa karibu saa nzima kupitia Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC), akamshawishi kutokana na hoja alizozitoa.
Alisema kwa kuwa suala hilo limezua mvutano mkubwa katika bunge hilo, ni bora likaamuliwa kwa kupigiwa kura ya siri.
Wajumbe wengine
Mjumbe wa Bunge hilo, Sheikh Mussa Kundecha aliunga mkono utaratibu wa kura ya siri akisema ndiyo pekee unaoweza kuwaunganisha wajumbe.
Mchungaji Christopher Mtikila alitumia dakika tano kutoa somo kwa wajumbe wa Bunge hilo, kuhusu umuhimu wa kupiga kura ya siri badala ya kura ya wazi.
“Mwenyekiti, wewe tumekuchagua kwa kura ya siri siyo kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni democratic civility (ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
Mjumbe mwingine, Philemon Ndesamburo aliwataka wajumbe kuacha ushabiki wa kisiasa na kwamba lazima wazingatie kwamba wanatengeneza Katiba itakayodumu kwa miaka 50 au miaka 100 ijayo. Hata hivyo, wajumbe, Sixtus Mapunda na Stephen Wassira wote wa CCM, walisema kura za wazi ndiyo suluhisho la kutoa uamuzi juu ya nani anasema nini na kwa wakati gani.
Dk. Zainabu Gama alisema baadhi ya watu wanaotaka kura za siri wametumwa au wamekula rushwa ndiyo maana hawataki kura za wazi.
Wassira alikiri kuwa CCM imeingia na msimamo ndani ya Bunge, lakini alisema hata wajumbe wengine pia wana misimamo yao.
Waunda umoja kuikabili CCM
Katika hali inayoonyesha dhahiri kwamba wajumbe wa Bunge hilo wamegawanyika, vyama vya upinzani na wajumbe wa makundi mengine wameunda umoja wenye lengo la kuhakikisha kuwa Rasimu ya Katiba inapita.
Rasimu hiyo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni wakati wowote kuanzia sasa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Umoja huo umepewa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao sasa unajipanga, kuhakikisha unadhoofisha misimamo ya CCM ya kutaka kuikwamisha.
“Umoja huu pia unawashirikisha baadhi ya wajumbe kutoka CCM wenye msimamo wa kutaka mawazo ya wananchi yapewe nafasi katika Katiba tunayoiandaa,” alisema mmoja wa wajumbe.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia gazeti hili jana kuwa tayari taratibu zimefanyika kwa wajumbe wa Ukawa kukutana na kuweka mikakati.
“Ukawa inaundwa na wajumbe kutoka makundi yote ya uwakilishi katika Bunge la Katiba ambao lengo lao ni kuhakikisha kuwa Katiba inayopatikana ni ile inayozingatia maoni ya wananchi,” alisema Profesa Lipumba.
Mjumbe mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema wameamua kuunda umoja huo ili kupata nguvu ya pamoja na kwamba hatua hiyo imekuja baada ya kugundua kuwa CCM imeandaa waraka wake unaopingana na maoni ya wananchi.
Wajumbe 43 ‘wachomoa’
Wajumbe 43 kati ya 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushiriki katika Bunge Maalumu la Katiba hawajaripoti bungeni hadi kufikia jana.
Hadi jana ikiwa ni siku ya kumi na moja, wajumbe hao walikuwa hawajasajiliwa na kati ya hao ni sita tu waliotoa udhuru katika Ofisi ya Katibu wa Bunge.
Taarifa zilisema wajumbe wengi ambao hawajafika waliteuliwa kupitia makundi ya wakulima, wafugaji na yenye malengo yanayofanana.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema: “Ni kweli kabisa kuhusu hizo taarifa, unajua tangu Bunge limeanza mpaka hii leo (jana) wajumbe 43 hawajaripoti na maana yake ni kwamba hawajasajiliwa. Hao sita wameeleza wazi kuwa wanauguliwa na ndiyo ambao taarifa zao zipo ofisini, ila hao wengine sijui wako wapi kwa sasa.”
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema: “Tunajua kuna wengine hawajapata ruhusa kazini, wengine wana shughuli maalumu na wengine wameamua kutokuja tu.”
Habari hii imeandikwa na Sharon Sauwa, Daniel Mjema, Fidelis Butahe na Habel Chidawali (Dodoma) na Leon Bahati (Dar).

Benki ya Dunia 'yabana' msaada kwa UG

Wafadhili wakatiza misaada Uganda
Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheriua mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .
Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.

Uhaba wa chakula. Sababu? Wewe

Uharibifu wa chakula
Ni kiasi gani cha chakula unachokitupa ambacho pengine ungekila?
Basi Ripoti mpya kutoka benki ya dunia inasema kuwa robo ya chakula chote kinachokuzwa duniani hupotea ama kutupwa, na sasa inawataka raia kufikiri kwa makini kile kuhusu uharibifu huu wa chakula.
Lakini katika jangwa la Sahara chakula kingi hupotea wakati wa uzalishaji.Inasema kuwa katika maeneo kama vile Marekani na Uchina ,watumiaji wa chakula ndio wa kulaumiwa pakubwa kwa kupoteza chakula hicho.
Benki ya dunia inasema kuwa kati ya asilimia 25 na 35 ya chakula chote kinachokuzwa duniani hutupwa.
katika mataifa yanye utajiri wa viwanda ,lawama kubwa zaidi huwaendea watumiaji wa chakula hicho ambao hukiwacha chakula kuoza katika jokovu.
Raia wa marekani kazkazini ni miongoni mwa wale walio na lawama kubwa kwa kuwa asilimia 61 ya chakula chao huharibika wakati wa matumizi.
Mwandishi wa ripoti hiyo Jose Cuesta anasema kuwa kile kinachohitajika ni kubadili tamaduni.
Lakini katika jangwa la Sahara chakula kingi huharibika wakati wa uzalishaji .
Benki kuu duniani inasema kuwa kiwango cha chakula kinachotupwa kinaweza kutofautisha kati ya chakula bora na uhaba wa chakula katika mataifa mengi.

Imeonya kuwa iwapo mbinu za uzalishaji hazitaimarishwa na tabia za kula kubadilishwa ,dunia huenda ikakumbwa na uhaba wa chakula kwa idadi kuu ya watu inayozidi kuongezeka.