Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, May 6, 2017

Wabunge walia na bajeti ya afya, wataka iongezwe

WABUNGE wamepigia kelele bajeti kiduchu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wameitaka serikali iongeze ili kutosheleza mahitaji ya Wizara. Wabunge hao kwa nyakati tofauti walipigia kelele udogo wa bajeti hiyo wakati wakichangia bajeti hiyo iliyowasilishwa bungeni na Waziri Ummy Mwalimu.

Mbunge wa Bunda, Gitare Mwita (CCM) alisema fedha zinazotolewa kwa ajili ya huduma mbalimbali katika hospitali mbalimbali nchini zikiwamo za Muhimbili na Ocean Road ni ndogo hivyo, Serikali inatakiwa kuongeza fedha hizo.

Gitare alisema hata fedha zilizotengwa kwa ajili ya Hospitali ya Mafunzo ya Mloganzila Sh bilioni 4, inatakiwa kupewa fedha ili kuanza kufanya kazi ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa uhakika nchini.

Alisema Hospitali ya Benjamin Mkapa katika Chuo Kikuu cha Dodoma, inatakiwa kupewa fedha na kupewa watumishi ili kuboresha huduma za afya nchini. Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) alisema kama Serikali inataka kutoa huduma bora kwa wananchi, inapaswa kuwekeza katika afya kwa kuongeza fedha na kuwalipa watendaji wake.

“Bajeti inayotengewa wizara hii ni kidogo kiasi kwamba haitoshelezi katika kuweka miundombinu, kuajiri watendaji na kutoa huduma muhimu nyingine, kwani tunajua kwamba afya ya binadamu kuliko dhahabu,” alisema Mbatia.

Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF), alisema bajeti ya Wizara inayotolewa ni pungufu ya asilimia 50 inayotakiwa kupewa Wizara hiyo wakati kwenye Sera ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Mwaka 2007, Wizara inatakiwa kupanua huduma ya afya na kutoa huduma bora na kuwafikia watu wote.

Alisema serikali haiwezi kupanua huduma hizo kwani hadi sasa hakuna zahanati katika vijiji vyote, hakuna vituo vya afya katika kata na hakuna hospitali katika kila wilaya zote. Mtulia alisema Azimio la Abuja, Nigeria la 1989, linaitaka Wizara hiyo ya Afya ipewe asilimia 15 ya bajeti yote, na kwa mantiki hiyo, katika bajeti ya Sh trilioni 31, Wizara hiyo ilitakuwa kupewa asilimia 15 ambazo ni Sh trilioni 4.5.

“Badala yake wizara hiyo imepewa shilingi trilioni 1.1, ambazo ni kidogo na haziwezi pamoja na mambo mengine, kutekeleza malengo azma ya kuondoa vifo vya mama na mtoto na magonjwa mengine,” alisema Mtulia na kusema angalau ingetengewa asilimia tano ya bajeti nzima. Mbunge wa Viti Maalumu, Felista Bura (CCM), alisema bajeti ya Afya ni kidogo kiasi kwamba serikali inatakiwa kutenga fedha za kutosha kuangalia afya za wananchi wake; wakati Amina Makilagi (Viti Maalumu- CCM), alisema serikali inatakiwa kupeleka fedha za kutosha kwani hakuna uchumi wala maendeleo bila afya njema.
Chanzo:Muungwana Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment