Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, February 8, 2017

MAJALIWA ATAKA UWAJIBIKAJI KWA MABALOZI

kasim1
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasim2 kasim3 kasim4
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasim5
kasim7 kasim8
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Amesema  mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi  hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil, China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.
Mabalozi hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo (Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela (Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC), Balozi Mbelwa Kairuki (China).
“Serikali inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.
Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kulinda maslahi ya Taifa katika nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kuhakikisha wanawatambua Watanzania wanaoishi katika mataifa hayo na kushirikiana nao katika kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Balozi Mella ambaye alizungumza kwa niaba ya mabozi wenzake alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watakwenda kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment