Writen by
sadataley
9:50 AM
-
0
Comments
mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza |
Dawa za kulevya |
..............................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
BAADA ya mapambano ya vita dhidi ya madawa ya kulevya kuendelea kuchukua kasi katika mkoa wa Dar es Salaam kwa watuhumiwa mbali mbali kukamatwa , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametangaza mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani hapa na kuwa tayari mapambano yameanza kuzaa matunda baada ya watuhumiwa 19 kukamatwa wakiwemo wafanyabiashara wa dawa za kulevya
Akizungumza na mwandishi maalum wa mtandao wa matukiodaimaBlog mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa hata kabla ya agizo la Rais Dkt John Magufuli juzi mkoa ulianza kupambana na madawa ya kulevya pamoja na matukio mbali mbali yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya kama unywaji pombe muda wa kazi oparesheni ambayo imefanywa kwa nguvu kubwa na jeshi la polisi .
“ Pamoja na kuwakamata watuhumiwa mbali mbali ila mkoa umeendelea kuandaa utaratibu wa kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya kwa kuwatafutia nafasi ya matibabu na kupitia hao wataweza kupata mtandao mzima wa wauzaji na waingizaji wa dawa za kulevya mkoani Iringa …..tunaendelea kutekeleza agizo la Rais kwa vitendo zaidi hatutalala wala kukubali vijana wetu kuendelea kuharibiwa akili kwa matumizi ya dawa za kulevya “
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi akizungumza na waandishi wa habari jana juu ya utekelezaji wa agizo hilo la mapambano dhidi ya dawa za kulevya alisema kuwa jeshi la polisi limeendelea na msako mkali wa dawa za kulevya kwa kuwakamata watuhumiwa 19 wa dawa za kulevya .
Kamanda Mjengi alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao watuhumiwa 14 ni mateja ambao wameathirika kwa utumiaji wa dawa za kulevya na watuhumiwa 5 ni wafanyabiashara wa dawa za kulevya .
“ Tulianza kuwakamata watumiaji wa dawa za kulevya ambao baadhi yao ni mateja (waathirika) na baada ya hapo mateja hao waliweza kuwataja wauzaji hao watano ambao tumewakamata na tunaendelea kuwahoji mtandao mzima wa uingizaji wa dawa za kulevya mkoani Iringa “
Hata hivyo alisema kwa sasa ni mapema kutaja majina ya watuhumiwa hao wa dawa za kulevya kwani bado wanaendelea na zoezi la kuwahoji ili kupata mtandao mzima wa wauzaji wa dawa za kulevya na kabla ya kuwafikisha mahakamani wote kwa pamoja .
Alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Iringa likiwemo eneo la Miyomboni , Mwembetogwa , Mlandege , Mshindo , Ipogolo ,kitanzini na Kihesa na kuwa zoezi la kuwakamata wote waliotajwa kwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ama uuzaji linaendelea .
Kuhusu aina ya dawa ambazo walikuwa wakiuza alisema watuhumiwa hao wote hakuna aliyekamatwa na dawa za kulevya na katika mahojiano wote wanadai kuwa walikuwa wakijihusisha na biashara hiyo zamani ila kwa sasa wameiacha kabisa .
Kamanda huyo alisema mbali ya kutokutwa na ushahidi bado hawataachiwa huru watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao .
Aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara ama matumizi ya dawa za kulevya kwani alisema oparesheni hiyo inayoendelea ni mkoa mzima wa Iringa
Chanzo Matukio Blog
No comments
Post a Comment