Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, August 5, 2016

Mkutano wa Vijana wa Mandela Washington Fellowship wamalizika Marekani.

Mkutano wa vijana viongozi kutoka barani Afrika unaojulikana kama Mandela washington Fellowship ulimalizika alhamisi katika hoteli ya Omnishoreham Washigton Dc. Mkutano huo uliwakutanisha pamoja vijana 1000 kutoka mataifa 49 ya barani Afrika kabla ya kufika Washington vijana hawa walikwenda katika vyuo mbali mbali hapa Marekani kwa wiki 6 kupata mafunzo na kubadilishana uzoefu wa miradi na kazi mbali mbali wanazofanya. Na baada ya hapo ndipo walikutana na rais Barack Obama katika hitimisho la mafunzo yao . Rais Barack Obama alizungumza na vijana hao akieleza kuwa Marekani pia inajifunza kutoka barani Afrika. Emmanuel Odama mchungaji kijana na mshiriki wa program hii kutoka nchini Uganda ndiye aliyemkaribisha rais Obama huku akisisitiza umuhimu wa vijana wa Afrika kuendelea kufanya kazi kwa bidi kwenye maeneo yao. Rais Obama pia alimtambua mmoja wa washiriki kutoka Tanzania Geline Fuko kwa kazi anayofanya ambapo ameweza kuasaidia kuanzisha mtandao wa kituo cha taarifa za katiba, akiwa mtafiti wa masuala ya katiba anafanya kazi na kituo cha sheria na haki za biinaadamu nchini humo ambapo mtandao huo unawawezesha watanzania kuweza kupata nakala ya katiba na taarifa zake ili kuwaruhusu watanzania kupata nafasi ya kufahamu zaidi haki na wajibu wao na kuifahamu serikali yao bila malipo yoyote. Wakati huo huo mmoja wa washiriki kutoka Tanzania Simon Titus Malugu ametunukiwa tuzo ya USADF kwa uvumbuzi wake wa mashine ya kutotoa vifaranga vya kuku. Na mmoja wa washiriki kutoka nchini Kenya Alantei Leng’eti ambaye ni mwanaharakati wa haki za wanawake ameeleza amepata mengi katika mkutano huu na ataendelea na juhudi zake akirudi nyumbani ili kuzuia ukeketaji ambao unaanzia kwa watoto tangu wakiwa na umri wa miaka 8, ambao pia hawapewi nafasi ya kwenda shule kwasababu ya mila potofu analenga kupinga mila hizo na pia kuunga mkono mila zilzio bora hasa kudumisha utamaduni wa mmasai.

ANC yatarajia matokeo mabaya ya uchaguzi

Huku matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa kimaeneo yakitarajiwa kutolewa leo, imebainika wazi kuwa chama cha ANC kimeibuka na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi kuwahi kushuhudiwa. Chama cha Democratic Alliance kimeibuka na ushindi mkubwa na muhimu katika baraza la manispaa ya Nelson Mandela Bay. Chama cha ANC kinajitahidi kuchukua udhibiti wa miji ya pretoria na Johannesburg. Hata hivyo, ANC inasalia kuwa chama maarufu katika siasa za Afrika Kusini, kwa kuzoa aslimia 54 ya kura hizo. Chama cha Democratic Alliance, kimekuwa kikiungwa mkono na wazungu pamoja na chotara, japo wapiga kura weusi wameanza kukiunga mkono, kwa kukatishwa tamaa na mwendo wa kobe wa uimarishaji wa uchumi wa chama tawala cha ANC, na sakata nyingi zinazomkabili rais Jacob Zuma.

Marekani yakana kuilipa kikombozi Iran

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, amekanusha vikali madai kwamba Marekani ililipa kikombozi cha dola milioni moja kuwakomboa wafungwa wa taifa hilo waliozuiliwa nchini Iran. Amesema malipo hayo yalikuwa ya kutatua mgogoro kuhusu mpango wa ununuzi wa bidhaa za kijeshi. Wanasiasa wa chama cha Republican wameshambulia serikali kutokana na malipo hayo. Malipo hayo yalitolewa wakati wa kutia saini mkataba wa kinyuklia, na ubadilishanaji wa wafungwa ambapo wafungwa wanne wa Marekani waliachiliwa.

Olimpiki kusahaulisha shida za Wabrazil?

Rais wa serikali ya Mpito ya Brazili amesema anaamini kwamba Wabrazil watarudisha tena furaha yao, michezo ya Olimpiki ikianza rasmi leo mjini Rio De Janeiro. Michel Temer amesema Brazil kuwa mwenyeji wa michezo hiyo ya Olympiki, licha ya misukosuko ya uchumi na kisiasa inayowakabili ni kuthibitisha uwezo wa nchi hiyo, kukabiliana na vikwazo. Ulinzi umeimarishwa mjini Rio, kuweza kuzuia ghasia zinazoweza kuzushwa na waandamanaji wenye hasira juu ya gharama za mashindano hayo. Shamra shamra za ufunguzi wa michezo hiyo katika uwanja wa Maracana zimepunguzwa kutokana na kupunguzwa kwa bajeti iliyokuwa imewekwa. Image copyright Getty Images Lakini hata hivyo Waandaaji wake wameahidi kuwepo kwa sherehe zitakazovutia zaidi za kiutamaduni na nyingine tofauti.