Writen by
sadataley
2:27 PM
-
0
Comments
Rais wa gambia
Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo
kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na
mfanyibiashara Adama Barrow.
Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.
Akiongezea: ''Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu.
Amewashtumu viongozi hao kwa kuingilia a ya ndani ya Gambia.
ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua bw Barrow kama rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.
Viongozi wa kieneo watahudhuria kuapishwa kwa Bw Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.
Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo manamo tarehe mosi mwezi Disemba ,lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha mungu.
Alisema kwamba matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.
No comments
Post a Comment