Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, September 18, 2015

Tamko la Viongozi wa Dini Kuhusu Uhuru,Haki na Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Sisi, viongozi wa Dini pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi (NEC, TAKUKURU, Polisi pamoja na Msajili wa vyama vya siasa) tuliokutana leo tarehe 17/9/2015, tumepata nafasi ya kujadili kwa kina suala la uhuru,haki na amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 25/10/2015 na wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa uhuru,haki na amani vinalindwa kipindi hiki. Suala la uhuru haki na amani ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla na halina mjadala.Kila mmoja achukuwe nafasi yake kulinda uhuru,haki na amani na kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vya siasa. Viongozi wa dini wamepata nafasi ya kujadili na vyombo hivi masuala ya msingi kama kuhakikisha kuwa maadili ya uchaguzi yanazingatiwa kwa wote, muda wa kutangaza matokeo ya kura unazingatiwa , haki ya wananchi kupata matokeo haraka ili kuepuka fujo wakati wa kusubiri na kutangazwa kwa matokeo. Jeshi la polisi kutokutumia nguvu kupita kiasi, wajibu wa Msajili kuhakikisha vyama vyote vinapata fursa sawa na pia tumejadili suala la kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya jukwaa la siasa. Viongozi wa dini tumekubaliana kwa pamoja kuepuka kutumia nyumba za ibada kuonyesha ushabiki wa aina yoyote kwa chama chochote cha siasa. Baada ya kujadili kwa kina masuala hayo viongozi wa dini wanatoa wito ufuatao; 1. Vyombo vya habari vifanye kazi kwa ueledi bila upendeleo na pia kuhakikisha kuwa inatoa taarifa ya kutosha kuelimisha umma. 2. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo iweke utaratibu maalum wa kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha pamoja na watu wote waliojiandikisha/watakaojiandikisha waweze kupiga kura. 3. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo siku ya kupiga kura isiwe siku ya ibada. 4. NEC iendelee kutoa elimu ya uraia kuhusu haki ya raia kupiga kura na haki yao ya kukaa mita mia moja kusubiri matokeo yatangazwe kwa utulivu kama ambavyo NEC imehakikishia viongozi wa dini kuwa kila kituo itabandika matokeo yote (Urais,Ubunge na Udiwani) 5. Pamoja na kutimiza wajibu wake wa msingi wa kulinda raia na mali zao Jeshi la polisi wakati huu wa uchaguzi liendelee kutimiza wajibu wake wa kusimamia amani na taratibu kwa haki bila upendeleo. 6. Wagombea,wafuasi na wanaowanadi, wanaaswa waache mara moja lugha za matusi,vitisho,kejeli na kukashifiana vinavyoweza kuchochea fujo na kuleta uvunjifu wa amani wajikite kunadi sera za vyama vyao. 7.Tunawahimiza wananchi kuwa makini katika kufuatilia kampeni na sera mbalimbali za wagombea, kuzipima kwa hali ya juu sera hizo, kutokuuza kadi zao za kupigia kura, kutokununuliwa na kujitokeza kwa wingi kutumia uhuru na haki yao ya kuchagua viongozi wanao wataka kwa hiari na amani. 8. Viongozi wa dini wanawahimiza Watanzania wote kuendelea kuombea nchi hii kuendelea kuwa taifa lililojengwa katika misingi ya uhuru , haki na amani. 9. Viongozi wa dini tutabaki kuwa manabii na wahubiri wa uhuru,haki na amani wakati huu , wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi Sisi viongozi wa dini Tunawashukuru Inspekta generali wa polisi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ufafanuzi makini na wa kina juu ya nafasi na utayari wao wa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha uhuru, haki na amani vinaendelea nchini. Maelezo yao na mafafanuzi yao tumeyasikia na tutaendeleza kwa kuwa hiki ni kikao cha mwanzo na tutaendelea kuwa na vikao vingine pamoja nao kuelekea uchaguzi mkuu ili kufuatilia utekelezaji na kuendeleza makubaliano yetu katika kuhakikisha uhuru,haki na amani. Chanzo:Zanzibar News

Thursday, September 17, 2015

Jumba refu zaidi Afrika mashariki lafunguliwa TZ

Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania. PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147. Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini. Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu. Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika. Chanzo:BBC

Refugee crisis: Churches in other LWF regions express solidarity with European Churches

Prayers for safety, advocacy for additional support The Lutheran World Federation (LWF) member churches outside Europe are expressing their solidarity with churches receiving refugees in the region through ongoing prayers, additional financial support and advocacy to governments. In a 9 September alert to its members the Evangelical Lutheran Church in America, emphasized the church’s calling and commitment to meet basic humanitarian needs and uphold the rights of people fleeing war and crisis. “We are also in communication with our church companions in Germany, as they receive tens of thousands of refugees,” Rev. Daniel Rift, director of ELCA World Hunger and Disaster Appeal wrote to the church’s members. The ELCA has been supporting the Evangelical Lutheran Church in Hungary and the Slovak Evangelical Church of the Augsburg Confession in Serbia, both of which have been welcoming refugees entering through their borders, and providing them with food and other materials. Earlier this month, ELCA Presiding Bishop Elizabeth Eaton called upon congregation members to be in prayerful solidarity as the “horrendous consequences of a refugee crisis in the Middle East” crossed overflowed into Europe. In Canada, the Evangelical Lutheran Church in Canada (ELCIC) and its humanitarian agency, Canadian Lutheran World Relief (CLWR) issued an appeal, 15 September, asking their members for prayers and support to assist Syrian refugees who have been “displaced by brutal violence in their country.” “We pray for their safety and access to shelter and basic necessities. I urge our members to assist with financial contributions to the appeal and help support our sisters and brothers,” ELCIC National Bishop Susan C. Johnson said. The ELCIC and CLWR said donations made between 12 September and 31 December 2015 will be matched dollar-for-dollar by the Canadian government through its Syria Emergency Relief Fund. In Argentina, Rev. Gustavo Gómez, president of the United Evangelical Lutheran Church, has expressed deep concern for the increasing number of persons seeking to survive and thus moving towards Europe. Receiving refugees “is a call to engage in commitment,” said Gómez whose church has received migrants in the past. He described the act of welcoming others as “renewal in service and active love” as there is room to be enriched by the arrival of different cultures. Other churches in the region have offered prayers. Source:www.lutheranworld.org/news/refugee-crisis

Wanasiasa 7 wafurushwa serikalini DRC

Wanasiasa saba waandamizi wamefurushwa kutoka kwa serikali ya muungano katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kumuandikia rais wakimtaka kutokwamilia madaraka, kulingana na maafisa. Katika barua kwa Joseph Kabila,viongozi wa G7,kundi lenye vyama ndani ya muungano huo lilitaka hatua kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kufikia mwezi Novemba. Mda wa kikatiba wa rais Kabila unakamilika mwaka ujao,lakini amekataa kuthibitisha kwamba hatowania muhula mwengine. Upinzani pia unahofia kwamba uchaguzi huo utacheleweshwa. Ulifanya mkutano wa kisiasa katika mji mkuu wa Kinshasa hapo siku ya jumanne ili kumtaka rais Kabila ajiuzulu mwaka ujao. Msemaji wa serikali Lambert Mende alikana kwamba bwana Kabila alitaka kukiuka katiba kulingana na chombo cha habari cha Reuters. Chanzo:BBC

Tuesday, September 15, 2015

Ligi ya mabingwa Ulaya kutimua vumbi leo

Msimu wa michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2015-2016 kuanza leo Msimu mpya wa michuano ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa msimu wa 2015-2016 utaanza leo kwa nyasi za Viwanja vinane kuwaka moto. Katika kundi A, PSG itawaalika timu ya Malmo Ff kutoka Sweden huku Real Madrid, wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk, mchezo utakaopigwa kwenye Dimba la Santiago Bernabéu. Katika kundi B PSV Eindhoven, ya Uholanzi watakua wenyeji wa Manchester United, toka Uingereza huku mchezaji wa zamani kwa kikosi hicho Memphis Depay, akirejea kucheza na timu yake hiyo ya zamani. Mchezo wingine wa kundi hili VfL Wolfsburg, ya Ujerumani watashuka dimbani kuwakabili CSKA Moscow, kutoka Urusi. Michezo mingine itayopigwa leo hi ya michuano hii. Kundi C Galatasaray na Atletico Madrid Benfica na FC Astana KUNDI D Man City na Juventus Sevilla na Borussia Monchengladbach

Monday, September 14, 2015

Kwa nini mataifa ya kiarabu hayawachukui wakimbizi wa Syria

Picha za wakimbizi wa Syria waliokwama katika mipaka na vile vile katika vituo vya treni bila kutaja picha ya mvulana mdogo wa miaka mitatu Alan Kurdi aliyekuwa amesombwa na maji katika ufukwe wa bahari wa Uturuki zimezua hisia kwa juhudi zaidi kuchukuliwa ili kuwasaidia wale wanaotoroka vita. Hasira zaidi zimelenga mataifa ya uarabuni kama vile Saudi Arabia,Bahrain,Kuwait,Qatar,Oman na UAE ambao wamefunga milango yao kwa wakimbizi hao. Kufuatia ukosoaji huo,ni muhimu kukumbuka kwamba mataifa hayo ya Uarabuni hayajataka kuwasaidia wakimbizi wa Syria. Ukarimu wa watu binafsi umewasaidia pakubwa wakimbizi hao. Kampuni za kibinfasi za wahisani zimechangisha maelefu ya madola na wakati wafanyikazi wa viwanda vya kitaifa kwa mfano kile cha mafuta cha Qatar,walipoulizwa iwapo wako tayari kutenga kiwango fulani cha fedha kila mwezi ili kuwasaidia wakimbizi hao wa Syria ,wengi wao walikubali. Mataifa ya Uarabuni yametoa takriban dola milioni 900 kupitia kampuni za wahisani pamoja na michango ya watu binafsi. Hatahivyo,huku vita vya Syria vikiendelea ,imekuwa vigumu kuwatafutia raslimali wakimbizi hao wanaoishi katika kambi. Image copyrightReuters Image caption Wakimbizi wa Syria Ulimwengu umelazimika kutafuta suluhu nyengine ili kukabiliana na idadi kubwa ya wakimbizi hao,kwa kuwa raia hao wa Syria wamechoshwa na vita na kuishi katika kambi bila matumaini ya kijamii na fedha wamelazimika kuondoka maeneo hayo ya vita ili kutafuta maisha bora ya baadaye. Kwa ufupi,utoaji wa chakula na maji kwa watu wanaoishi katika kambi ilikuwa suluhu kwa tatizo la jana. Swala tata zaidi ni kuwatafutia mamia ya maelfu ya watu mahala pa kuishi,na ni hapo ambapo mataifa ya Uarabuni yameshindwa kutafuta jibu. Huku mataifa hayo ya Uarabuni yakiwa yamewaruhusu baadhi ya raia wa Syria, Saudi Arabia inasema kuwa imechukua zaidi ya raia laki tano tangu mwaka 2011,wakiwa wafanyikazi wahamiaji lakini hakujakuwa na sera yoyote kwa mataifa hayo kuwatafutia hifadhi wakimbizi wanaowasili kwa wingi bila wadhamini ama hata vibali vya kufanya kazi. Ili kujaribu kuelezea hili,utahitaji kuingia ndani zaidi ili kubaini hofu ya mataifa hayo ya Uarabuni kuhusu uthabiti wa kisiasa katika mipaka yao pamoja na maswala makubwa ya vitambulisho na dhana kuhusu umuhimu wa kuwa raia wa Uarabuni. Mnamo mwaka 2012,wakati vita vya Bashar Al Asaad vilipoanza na kubainisha ushindani mkubwa kati ya mataifa ya Uarabuni yenye wasunni na washirika wao wa Iran,hofu ilianza kuyatawala mataifa hayo kwamba raia wa Syria wanaomtii rais Assad watalazimika kuingia mataifa hayo ya Uarabuni ili kulipiza kisasi. Ukaguzi wa wakimbizi wa Syria wanaoelekea katika mataifa hayo ya Uarabuni ulianza na ilikuwa vigumu kwa raia wa Syria kupokea vibali vya kufanya kazi ama hata kuvipiga chapa mpya ili kuendelea kufanya kazi. Sera hiyo haijabadilishwa nchini Qatar,Saudi Arabia ama hata UAE kwa hofu ya uwezekano wa raia walio watiifu kwa rais Assad kulipiza kisasi. Uvumi umeendelea kuwepo katika mataifa hayo ya kiarabu kwa kipindi cha miaka mitatu kuhusu seli za magaidi wanaokamatwa na kuzuiliwa ijapokuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa mpango wa wafuasi wa Assad ambao umeripotiwa. Mataifa mengi ya Uarabuni wanahofu kwamba raia wanaomtii Bashar al Asaas huenda wakalipiza kisasi Idadi ya maelfu ya raia wa Syria wanaotaka kuingia katika mataifa hayo huenda ikaathiri uchumi unaotegemewa na mataifa hayo ili kuweza kufanya kazi. Kwa mfano,idadi ya raia wa UAE na Qatar iko chini kwa asilimia 10 ya raia wa mataifa hayo. Idadi kubwa ya raia ni wafanyikazi wanaofanya kazi katika eneo moja hadi jingine. Wageni huruhusiwa pekee iwapo wake zao ama waume zao wana kazi kamili,hauwezi kusalia katika mataifa hayo ya Uarabuni bila kazi na wakati kandarasi zao zinapokamilika basi wahamiaji wote hulazimika kurudi makwao. Hivi ndivyo mataifa hayo ya Urabuni yanavyofanya kazi.Kwa hivyo wazo la maelfu ya wageni wanaoingia bila kazi ama bila siku rasmi ya kurudi makwao huyaweka mataifa hayo kati hali isiyo nzuri. Chanzo:BBC Swahili

Waziri mkuu Australia apokonywa uongozi

Australia inaelekea kupata waziri mkuu mpya baada ya Tony Abbott kuondolewa uongozini katika chama cha Liberal na waziri mmoja wa chama chake. Kwenye uchaguzi wa kiongozi wa chama uliofanywa haraka, Bw Abbott, ambaye umaarufu wake umekuwa ukididimia kwa mujibu wa kura za maoni, alipata kura 44 huku waziri wake Bw Malcolm Turnbull akipata kura 54. Wabunge wa chama hicho hata hivyo walimpigia kura Julie Bishop kusalia kama naibu kiongozi wa chama hicho. Bw Turnbull anatarajiwa kuapishwa baada ya Bw Abbott kumwandikia gavana mkuu na kujiuzulu. Mapema Jumatatu, kwenye kikao na wanahabari Canberra, Bw Turnbull alisema iwapo Bw Abbott angesalia kiongozi wa chama hicho, serikali ya muungano ingeshindwa kwenye uchaguzi mkuu ujao. Alisema ilikuwa vigumu kwake kufanya uamuzi huo, lakini kwamba ni “wazi kuwa serikali haijafanikiwa katika kutoa uongozi wa kiuchumi unaohitajika” na kwamba Australia inahitaji mtindo mpya wa uongozi. Bw Turnbull atakuwa waziri mkuu wa nne wa Australia tangu 2013. Waziri mkuu wa chama cha Leba Julia Gillard aliondolewa uongozini na Kevin Rudd kwenye kura ya uongozi wa chama Juni 2013, miezi kadha kabla ya uchaguzi mkuu ambao chama cha Liberal, chake Tony Abbott, kilishinda. Bi Gillard mwenyewe alikuwa amemuondoa Rudd kama waziri mkuu 2010. Chanzo:BBC Swahili

Friday, September 11, 2015

Mvua yasimamisha mechi za US Open

Michuano ya US Open kwa upande wa kinadada imesimamishwa kwa muda baada ya mvua kali kunyesha hali iliyosababisha ugumu wa mchezo huo. Serena Williams atapaswa kusubiri mpaka ijumaa ya leo kuendelea na ratiba ya kalenda ya Grand slam ya nusu fainali kwa wanawake ambapo atacheza dhidi ya Roberta Vinci. Hali hiyo ya mvua haikuzuia mchezo wa wanaume na uliendelea kama ulivyopangwa ambapo matumaini ya bara la Afrika kuendelea kuwepo katika michuano hiyo yalifikia tamati baada ya Kevin Anderson wa Afrika Kusini kushindwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa na Stan Wawrinka seti 6-4 6-4 6-0. BBC SWAHII

Bendera ya Palestina kupepea ofisi za UN

Baraza kuu la Umoja wa mataifa limepiga kura muswada kuipa fursa ya kipekee na kutoa baraka zake kuiruhusu bendera ya Palestina kupepea mbele ya majengo ya Umoja wa Mataifa . Chini ya azimio hilo ambalo yalilopitishwa, bendera za mataifa mawili ambayo si mataifa kamili ambayo ni watazamaji wa umoja huo Palestina na Holy See ,sasa watakuwa na ruhusa ya kupeperusha bendera sambamba na nchi wanachama. Muwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansour,amesema kwamba tukio hilo ni hatua kubwa kuimarisha heshima ya nchi yake . Lakini Israel imesema hatua hayo imeshusha hadhi ya umoja huo na kusisitiza kwamba njia pekee kwa Palestina kupata hazi ya kuwa taifa huru ni kupitia meza ya mazungumzo ya ana kwa ana. Chanzo:BBC Swahili

Thursday, September 10, 2015

MCHUNGAJI ALIYEKATAA KUTOA CHETI CHA NDOA KWA MASHOGA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Hatimaye mchungaji aliyewekwa lupango kwa kosa la kukataa kuwapa kibali cha ndoa wapenzi wa jinsia moja huko Kentucky nchini Marekani, ameachiwa huru na mahakama hapo jana na kuahidi kurejea katika utumishi wake wiki hii. Mchungaji Kim Davis alimwaga machozi mbele ya kundi kubwa la wafuasi waliokuwa wakiunga mkono msimamo wake, ambapo aliwashukuru kwa upendo wao waliouonyesha, sambamba na kuwaambia kuwa anarudisha utukufu kwa Mungu kwa umoja na ukakamavu waliouonyesha, na kuongeza kwamba wanamtumikia Mungu aliye hai na kwamba anawajua kila mmoja kwa nafasi zao, kwakuwa yeye ni Mkuu. Mchungaji Davis alionyesha msimamo wa kuwa tayari kwenda jela maisha kuliko kuhalalisha ndoa ya watu wa jinsia moja kwakuwa ni kinyume na imani pamoja na dini yake. Akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kama kukaa kwake jela kuna mafanikio yeyote, mchungaji huyo alijibu kwa tabasamu huku akitingisha kichwa akimaanisha mafanikio yapo. Kwa upande wa mwanasheria wa mchungaji huyo Mat Staver amesema mteja wake atarejea kazini wiki hii na kwamba hata jiuzulu nafasi yake. Hata hivyo mchungaji Davis hakuweka wazi kuhusu kesi yake, huku maswali kuhusu tukio hilo yakiwa hayajibiwa lini ataanza rasmi kazi na ni kitu gani atakifanya atakaporejea kazini kwake. Mchungaji Kim Davis aliwekwa jela na jaji David Bunning ikiwa siku tano tangu jaji huyo kumuhukumu mchungaji huyo kwenda jela, ambapo aliachiwa sambamba na kupewa masharti ambayo mchungaji huyo hayuko tayari kuyakubali. Aidha taarifa zinasema, jaji huyo aliridhishwa na hatua ya kumwachia mchungaji huyo kwasababu wafanyakazi wenzake walitoa kibali cha ndoa kwa wapenzi hao ilihali mchungaji Kim Davis akiwa jela. Chanzo: www.gospelkitaa.co.tz

Tuesday, September 1, 2015

Tanzania yaanza rasmi sheria ya uhalifu wa mtandao

Serikali ya Tanzania ilitoa tamko maalum la kuanza utekelezaji rasmi wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ambayo imekuwa gumzo kubwa tokea kupitishwa sheria hizo huku wengi wakiiona kwamba itanyima uhuru wa kutoa na kupata habari Tamko la kuanza utekelezaji rasmi wa sheria hizo mbili yaani ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 lilitolewa na Wizara ya Mawasilaiano, Sayansi na Teknolojia kupitia waziri wake, Profesa Makame Mbarawa. Sheria hizo zinaanza kutumika rasmi kuanzia Jumanne yaani Septemba mosi mwaka huu. Profesa Mbarawa alisema licha ya kuwepo mafanikio katika matumizi ya mitandao, changamoto zilizojitokeza zilifanya serikali kutunga sheria hizo mbili. ​Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alisema hakuna ukweli wowote kwamba sheria hizi mbili zimeletwa ili kudhibiti uhuru wa mawasiliano kwa watanzania hususan wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu ujao na kwamba wamejipanga ili kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda kwa haki. Kuanza kwa utekelezaji wa sheria hizi mbili za makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 kunatokana na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha hatua hiyo hapo April mosi mwaka huu. CHanzo:VOA

Papa Francis alegeza msimamo wa Katoliki

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameitikia shinikizo kutoka kwa wanawake wengi waumini wa kanisa hilo na kulegeza msimamo wa kanisa hilo kuhusu uavyaji mimba mwaka ujao wa jubilee. Huwa ni marufuku kwa waumini wa kanisa Katoliki kuavya mimba, kitendo ambacho huchukuliwa kuwa kosa kubwa katika kanisa hilo. Papa Francis amesema atawaruhusu mapadri kuwasamehe wanawake wanaoavya mimba na pia madaktari wanaowasaidia kutoa mimba. Kinyume na watangulizi wake, Papa Francis, huchukulia fadhila na huruma kuwa nguzo kuu zinazozidi nyingine zote. Waandamanaji nchini Marekani wakitaka serikali kuhalalisha uaviaji mimba Papa huyo mzaliwa wa Argentina, alisema anafahamu shinikizo ambazo baadhi ya wanawake hukumbana nazo ndipo waavye mimba lakini akasema pia amekutana na wanawake wengi wanaobeba moyoni kovu la alichosema ni uamuzi wa kusikitisha na mchungu. Ametangaza mwaka wa jubilee, ambao kawaida huhusishwa na msamaha, uadhimishwe na wakatoliki kote duniani kuanzia mwezi Desemba. Maneno hasa aliyotumia Papa Francis yanaashiria kuwa anafahamu kuna wengi wa wanaojidai kutetea utamaduni wa kanisa hilo ambao hawatafurahishwa na uamuzi wake. "Nimeamua," Papa Francis alisema. "Bila kujali pingamizi, kuwaruhusu mapadri kutoa msamaha wa dhambi wa kuavya mimba kwa wale wanafanya hivyo na wanaotafuta msamaha wakati wa mwaka wa jubilee." Chanzo:BBC Swahili