Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, October 31, 2014

Rais wa Burkina Faso ameng'olewa mamlakani

   
Kuna hofu kuwa rais Compaore anataka kuendelea kushikilia madaraka

Msemaji wa jeshi amewaambia waandishi wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena.
Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpwito ya mwaka mmoja .
Lakini wanasiasa wa upinzani wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja.
Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miaka 27 tayari.
Kumeripotiwa maandamano mapya nchini Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Viongozi wa upinzani wanakutana kwenye mkji mkuu Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua.
Siku ya Alhamisi waandanamaji walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27 madarakani na wakateketeza bunge na kusaka kituo cha runinga cha serikali.
Rais Compaore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa atabaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
<span >Viongozi wa Upinzani Nchini Burkina Faso wamewaomba waandamanaji kutolegeza kamba bali kuendelea na maandamano huku wakimtaka Rais Blaise Campaore ang'atuke mamlakani mara moja.
Licha ya Rais Compaore wa Burkina Faso kuhutubia taifa siku moja baada ya vurugu kubwa na kutangaza kuvunja serikali waandamanaji hawataki kusikia kwamba apewe muda wa mwaka mmoja ndipo aondoke madarakani.
<span >Jana jioni kiongozi wa Jeshi J<span >eneral Honore Traore alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpwito itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja japo hakusema ninani atakayeiongoza.

Jen.Traore ajitangaza rais Burkina Faso

   
Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo
Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu.
Jenerali Traore ameshinikizwa na waandamanaji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa Bwana Compaore.
Bwana Compaore amesema kuwa amekubali kuondoka madarakani ili kutii matakwa ya waandamanaji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kutawala kwa miaka 27.
Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90.
Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanaji kuwa bwana Compaore hayuko tena madarakani huko Ouagadougou.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea mabarabarani kwa siku ya pili
Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari.
Siku ya Alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza muda wa uongozi wake baada ya kutawala kwa miaka 27 waliteketeza jengo la bunge na kuvamia kituo cha televisheni ya taifa.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi.

MAGAZETI YASEMAVYO LEO IJUMAA

 
3_51b6d.jpg
2_3ec90.jpg
4_21781.jpg
5_0fe9b.jpg
6_63609.jpg

20_b790e.jpg
21_a9509.jpg
22_3c520.jpg
23_52bf3.jpg
24_85b3a.jpg
25_1b2fd.jpg
26_b456f.jpg
27_65c72.jpg
28_a51ca.jpg

Kivumbi cha Ligi kuu England

   
Golikipa Simon Mignolet wa timu ya Liverpool ashindwa kuupangua mpira.
Kitimtim cha ligi kuu ya England kitaendelea tena kesho wakati ambapo mashabiki wa soka nchini humo na duniani kote watapata nafasi ya kuzishuhudia timu zao zikitafuta pointi tatu muhimu.
Newcastle Utd wataikaribisha Liverpool katika mchezo ambao utarushwa moja kwa moja kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC majira ya saa tisa unusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Arsenal wao wataikaribisha Burnley, huku Chelsea nayo wakiialika QPR. Everton watakuwa nyumbani kucheza Swansea City. Hull City wataikabili Southampton. Michezo mingine ni itakayochezwa siku hiyo ya kesho ni kati ya Leicester City watakapo kwaana na West Brom, Huku Stoke City watakapoikabili West Ham utd.
Siku ya jumapili ni mpambano wa kukata na shoka ambapo Manchester United wataavaana na Manchester City mechi ambayo pia itatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ,huku Tottenham watakapokwaana na Aston villa.

Rais wa Burkina Faso asema atajiuzulu

   
Rais Blaise Compaore
Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso amesema atajiuzulu baada ya miezi 12 ya serikali ya mpito.
Ameyasema hayo wakati akilihutubia taifa siku moja baada ya kutokea machafuko. Wakati ambao pia Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo ametangaza kuivunja serikali ya nchi hiyo.
Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia kituo binafsi cha Televisheni, Rais Compaore amesema ameuelewa ujumbe uliotolewa na waandamanaji na kwamba ataondoka madarakani baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito cha miezi miezi kumi na mbili.
Wapinzani na waandamanaji nchini humo, waliandamana na kufanya vurugu kupinga kubadilishwa kwa katiba itakayomwongezea muda wa utawala Rais wa nchi hiyo Blaise Compaore, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 27.
Wamemtaka rais huyo kujiuzulu mara moja.

Burkina Faso:Jeshi lachukua mamlaka

   
Bunge la Burkina Faso limetekezwa moto
Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.
Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.
Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Mmoja wa wabunge nchini Burkina Faso akitorokea kuokoa maisha yake.
Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.
Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .
Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Uharibifu katika majengo ya serikali Ougadougou
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.

Pinda ataka TZ isitegemee wafadhili

   
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda
Suala la baadhi ya wafadhili wa TZ kubana au kuchelewesha fedha walizoahidi kusaidi bajeti ya nchi linaendelea kuiumiza serikali.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mizengo Pinda, amesema umefika wakati sasa kwa Tanzania kujitegemea kwa mapato ya ndani kwa asilimia 100 badala ya kuegemea kwa wahisani ambao amedai wanakuwa na maslahi yao katika kusaidia.
Hivi karibuni wahisani wamesitisha kutoa fedha hizo kuishinikiza Tanzania kuchukua hatua dhidi ya upotevu wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya rushwa.
Kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ya Tanzania ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya ughaibuni ambako alihudhuria mikutano katika nchi mbali mbali akishughuli maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na uwekezaji.
Japokuwa Waziri Mkuu Pinda hafafanua kwanini serikali haichukui hatua za haraka kukamilisha uchunguzi wa upotevu wa takriban dola milioni 120 kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kugubikwa na rushwa kubwa, amesema wahisani hao wasingeisumbua Tanzania kama ingekuwa inajitegemea asilimia 100 kutokana na mapato ya ndani ya nchi.
“Ukishakuwa tu ni mtu ambaye unaonekana wewe bila wao tabu, ndiyo shida inaanzia hapo.Ndiyo maana wakati mwingine inabidi kusema bwana sisi tujitahidi, TRA huyu huyu twende naye akiweza kuongeza zaidi kidogo basi tutamshukuru sana.
“First and foremost tumtumie yeye na tuone hiki kidogo tunachokipata kutoka TRA tunavyoweza kukutumia vizuri zaidi kutupunguzia matatizo yetu. Kama zikija hizo nyingine well and good lakini si option ambayo unasema inakupa faraja kubwa sana. Kwasababu anything jambo lolote likitokea wanabana tu, halafu matokeo yake inakuwa ovyo sana katika shughuli zenu za maendeleo,” alieleza Bw Pinda.
Ingawa kauli yake haitapunguza maumivu ya wananchi wanaosubiri huduma na utekelezaji wa miradi ambayo ilishapangwa, pia ni vigumu kufanikisha jambo analolisema kwa muda mfupi.
Waziri Mkuu Pinda alipoongea na BBC hivi karibuni alikiri kwamba madai hayo ya utoroshaji wa fedha ni jambo linaloitia doa serikali ya Tanzania.
Swala hilo linaonyesha kuiumiza kichwa serikali wakati hasa kutokana na shughuli nyingi za maendeleo kuchelewa au kukwama, huku ikijikuta ikiwa haina njia nyingine ya haraka kurekebisha hali ya mambo.
Hata hivyo Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya Salum, akizungumza Dar Es Salaam amesema baadhi ya wahisani wamekwishatoa fedha na mazungumzo yanaendelea na waliobaki.
Ripoti ya uchunguzi unaofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi hiyo kwa miezi kadhaa inasubiriwa kwa hamu ili ibainike endapo kulikuwa na hila katika kuchomolewa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti maalum katika Benki Kuu ya Tanzania kusubiri usuluhishi wa swala la kibiashara umalizike.

Askofu Angowi ahimiza amani, ataka kura maoni


Askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Jesse Angowi akihubiri katika uzinduzi wa Halmashauri Kuu ya Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro jana. Picha na Daniel Mjema. 
Na Daniel Mjema, Mwananchi
Moshi. Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Jesse Angowi amesema kutounga mkono kufanyika kwa kura ya maoni Aprili, 2015 ni kukaribisha machafuko nchini.

Hayo aliyasema wilayani hapa jana katika uzinduzi wa Halmashauri Kuu ya Jimbo la Moshi.

Aliwashauri viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuridhia kufanyika kwa kura hiyo na kuwaacha wananchi waamue kupigia kura kile wanachokitaka na siyo kuwalazimisha.

“Amani ikikosekana hata makanisa hayawezi kuhubiri injili. Hivi sasa kuna viashiria vya kutoweka kwa amani kabla hata ya mchakato wa kupigia kura Katiba Inayopendekezwa haujaanza.

“Ni lazima tutii kauli ya Rais Kikwete kwamba kura ya maoni itafanyika Aprili mwakani, vinginevyo ni kukaribisha machafuko. Hakuna Mtanzania ambaye yupo tayari kwa hilo,” alisema Askofu Angowi na kuongoza kuwa kanisa hilo linamuunga mkono Rais ili kura hiyo ifanyike.
Alisema ni vyema viongozi wa dini wakabeba jukumu lao la kutoa elimu kwa waumini kuhusu kuheshimu maagizo ya viongozi wao.

Thursday, October 30, 2014

DRC: Beni yagubikwa na mikasa ya vita  

Wanajeshi wa jeshi la Congo walikiwa msituni.
Wanajeshi wa jeshi la Congo walikiwa msituni.
               
Vita na mizozo vimezuka tena kuanzia katika mwa mwezi kwa kumi katika mji wa Beni nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya congo huku mamia ya watu wakipoteza maisha na maelfu kukoseshwa makazi yao.
Kwa mujibu wa mtetezi wa haki za binadamu Paluku Ngahangombi aliyoko katika mji huo na kushuhudia visa mbalimbali vinavyofanywa na wanaosadikiwa kuwa ni waasi wa ADF – NALU kutoka Uganda, anasema hali ya usalama inazidi kuwa mbaya.
Licha ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuanza kulala nje usiku wakiwasha moto, wakiwa na silaha kama vile mapanga na visu kujilinda na uvamizi wa waasi lakini bado ghasia zimeshamiri.
Usiku wa kuamkia  Jumatano waasi walivamia kambi ya jeshi katika mji wa Beni kwenye mtaa mkubwa wa Owicha na kufyatuliana risasi na wanajeshi wa serikali hali iliyopelekea askari mmoja  kupoteza maisha, na waasi wengi kujeruhiwa lakini  waliweza kutoroka.
Wakazi wa mji huo wameilaumu serikali na Jeshi la umoja wa mataifa MONUSCO kushindwa kushirikiana vyema kurejesha hali ya utulivu .
Paluku Ngahangombi anasema kina mama na watoto ndio wahanga wakubwa katika mapigano na visa vinavyofanywa na waasi kwa sababu hawawezi kujikinga kwa haraka.  Drc imegubikwa na vita, mizozo na mivutano ya aina mbalimbali kwa miongo kadhaa sasa.

Ukistaajabu ya Musa!

    
waliobahatika kuwa shule ndo hao, wengine huanza shule ya awali wakiwa na miaka 11.
Wakati harakati mbali mbali za kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi za Afrika, baadhi ya nchi barani humo zinakabiliwa na changamoto hiyo kupita kiasi.
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kesi ya kwanza na ya aina yake imefanyika na hukumu yake kutolewa nchini Ivory Coast baada ya mwanamume mmoja kumuoa binti yake wa umri wa miaka 11.
Kutokana na kitendo cha mwanamume huyo kumuoa binti yake alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya dola za Kimarekani mia saba.
Mwendesha mashtaka Rosine Kone amesema kwamba kesi hiyo ya aina yake itatuma ujumbe mzito kwa raia wa nchi hiyo ili wanaume waache tamaa.
Nao Umoja wa Mataifa unasema kwamba ndoa za utotoni nchini Ivory Coast si suala la kushangaza, kwani mmoja kati ya mabinti watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka kumi na nane.

Chama Cha Nidaa chashinda Tunisia

   
Kiongozi wa Nidaa Tounes
Chama cha kidini nchini Tunisia Nidaa Tounes kimeshinda viti 85 katika uchaguzi wa ubunge nchini humo kulingana na matokeo.
Chama tawala cha Ennahda kimejishindia viti 69 katika bunge hilo la viti 217.
Matokeo rasmi yamethibitisha ubashiri wa awali na maafisa Ennahda wametoa wito kwa chama cha Nidaa kubuni serikali ya umoja.
Serikali ya mpito iliobuniwa ili kurejesha demokrasi nchini Tunisia baada ya mapinduzi ya mwaka 2011 imeungwa mkono na wengi.
Wafuasi wa Nidaa
Nidaa Tounes kimepata viti 85 kati ya viti 270 vya ubunge. Ennahda kilijipatia viti 69.
Uchaguzi huo ulikua wa kwanza chini ya katiba mpya na waandishi wa habari wamesema ni hatua kubwa kwa Tunisia katika kuafikia mfumo wa demokrasia baada ya miongo ya utawala wa kiimla.
Takriban raia millioni tano wa Tunisia walisajiliwa kushiriki katika shughuli hiyo.

Bunge la Burkina Faso lachomwa

   
Rais Blaise Campaore
Waandamanaji nchini Bukina Faso wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, kupinga hatua ya kuongeza muhula wa Rais Blaise Compaore ambaye ametawala nchi kwa miaka 27.
Runinga ya itaifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Burkina Faso
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.
DAR ES SALAAM ZANZIBAR KUUNGANISHWA KWA DARAJA

BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.

Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara na Unguja, kwa upande wa Zanzibar.

Umbali kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni kilometa 73.43, sawa na maili 45.62 hivyo kuwapo kwa mradi huo ni jambo linalowezekana, kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.

Kwa sasa, daraja refu kabisa duniani ni lile la Danyang–Kunshan lililopo China ambalo lina umbali wa kilometa 165, sawa na maili 102.4. Daraja hilo lilifunguliwa Juni mwaka 2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau wakati alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda ambaye alitaka kufahamu kama kuna matarajio ya kujenga daraja kubwa zaidi, ikiwezekana la kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Alisema wapo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ambapo mazungumzo hayo yakienda sawa, ujenzi wa daraja hilo huenda isiwe ndoto, bali ukweli.
"Hilo wazo lipo mheshimiwa na tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali, kwa hiyo hilo wazo lipo na sisi tulilifikiria," alisema Dk Dau.

Kamati hiyo ilifanya ziara katika miradi mikubwa mitatu ya shirika hilo ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi na 'Dege Eco village' ambao una nyumba zaidi ya 7,000.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mtanda alisema, kamati yake imeridhishwa na miradi hiyo ya NSSF ambayo inaendelea huku akitaka kuongezwa kwa kasi ili watanzania waanze kunufaika na miradi hiyo.

"Muangalie na hilo la ujenzi wa daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na mradi wa makazi bora na salama ambao utaweza kubadili taswira ya Jiji la Dar es salaam," alisema.
Alisema kamati yake isingependa kuona changamoto zozote ambazo zinaweza kukwamisha miradi hiyo na kwamba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaangalia namna ya kuunganisha miundombinu karibu na miradi hiyo.

"Lakini pia tumesikia kuwa serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi, tunashauri serikali kuilipa mifuko hii ili kuifanya kuwa na nguvu na kuweza kuleta maendeleo," alisisitiza Mtanda
PSPF YACHANGIA MABATI YA UJENZI WA MAABARA WILAYA YA KILOLO
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akizungumza mara baada ya kupokea msaada kutoka PSPF
Amelia Rweyimamu, Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam akizungumzia lengo la kushiriki ujenzi wa maabara
Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Iringa, Baraka Jumanne akifafanua jambo
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Wawakilishi wa PSPF, na Waaandishi wa habari wakizungumza wakati wa hafla

Na Mathias Canal, kilolo
Mfuko wa Penseni (PSPF) umechangia bati 200 zenye geji 28, kwa ajili ya kusaidia Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa, ili kukamilisha adhma ya ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari Wilayani humo.

Akizungumza baada ya kupokea bati hizo,Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita, alisema kuwa hakutarajia kupokea zawadi kama hiyo pamoja na kwamba alituma maombi PSPF, hivyo bati hizo zitatumika kwa kazi maalumu ya ujenzi wa maabara Wilayani humo kufuatia agizo lililotolewa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, la kujenga maabara ambapo hadi kufikia tarehe 30 Novemba ujenzi huo unatakiwa kuwa umekamilika.

Guninita alisema kuwa kukamilika kwa maabara hizo kutahamasisha watoto wengi kupenda masomo ya sayansi kwani watasoma kwa vitendo na uhakika zaidi, huku akizungumzia ufaulu mzuri wa kidato cha nne mwaka jana ambapo Halmashauri ya wilaya hiyo ilishika nafasi ya kwanza kimkoa huku ikiwa imeshika nafasi ya tisa kitaifa.

"Ninawashukuru PSPF kwa kujitolea bati hizi kwa ajili ya Wilaya yangu ya Kilolo, naamini hakutakuwa na kigugumizi katika utekelezaji wa agizo la Rais kwani wadau kama ninyi mnapojitolea sisi hatuna budi kushukuru na kufanyia kazi inayokusudiwa ya ujenzi ndani ya muda mwafaka". Alisema Guninita

Guninita aliongeza kuwa Wilaya ya Kilolo ina jumla ya shule 20 za Sekondari ambazo kwa asilimia kubwa ujenzi wa vyumba vya maabara umekamilika hivyo kwa sasa wamejikita katika ujenzi wa meza.

Kwa upande wake Amelia Rweyimamu ambaye ni Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam, akizungumza wakati wa kukabidhi bati hizo alisema kuwa PSPF inatambua umuhimu wa kuwepo kwa maabara hapa nchini hivyo ofisi yake imeona vyema kushiri katika ujenzi huo kwa kutoa bati hizo.

Rweyimamu alisema PSPF inatoa mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao la kifo, fao la mazishi, fao la wategemezi lisilo na kikomo, fao la kujitoa, fao la uzee, fao la kufukuzwa kazi, na fao la ujasiriamali.

Aidha aliongeza kuwa PSPF inatoa fao la elimu ambapo mfuko hudhamini mikopo katika bodi ya mikopo ya wanafunzi, lengo kubwa ikiwa ni kujenga uwezo wa kuhudumia wanafunzi wengi katika taaluma mbalimbali ikiwemo pia taaluma ya sayansi, Teknolojia na Afya.

Naye Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Iringa, Baraka Jumanne, alisema kuwa PSPF imetoa bati 200 kwa Wilaya ya Kilolo ambazo zina thamani ya shilingi milioni sita za kitanzania ili kusaidia ujenzi wa shule Wilayani humo.

Jumanne alisema maabara ya sayansi ni muhimu katika maendeleo ya wanafunzi kujifunza kwa nadharia na vitendo kutokana na umuhimu huo, kunahitajika ushirikiano kama ule ulioonyeshwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari za kata.

Hata hivyo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini, kujenga maabara kwa kila shule ya sekondari katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia sasa ambapo alitoa agizo hilo wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi mkoani Singida, waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji mdogo wa Itigi.
KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YAFANYA ZIARA KATIKA MIRADI MITATU YA NSSF JIJINI DAR
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mbunge jimbo la Lindi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Salum Barhan akifatilia kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni iliyokuwa ikitolewa na Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (hayupo pichani)
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akielekeza jambo wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyovu Mkoani Kigoma,Mh. Albert Obama akiuliza swali kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo kuhusiana na mradi huo wa Daraja la Kigamboni.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mhandisi Karim Mattaka (katikati) akiwaeleza Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii namna wanavyopanga nondo ili kuweka uhimara wa daraja la Kigamboni ambalo linatarajiwa kumalizika mapema mwakani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa nne kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo wakitembelea Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakiangalia namna maji yanavyotolewa chini kwa ajili ya kuweka nguzo za Daraja la Kigamboni.
Waheshimiwa wakijadiliana wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
 Ubao wa Maelezo ya Mrad wa Kijiji
Baadhi ya Nyumba za Mradi wa Kijichi.
Mh. Obama akiangalia Mandhali tulivu ya Kijichi.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo.
Majengo yanayoendelea kujengwa katika eneo la Mradi wa Kijichi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. 
Mh. Maua Daftari
Mh. Sugu.
Baadhi la Majengo ya Mradi wa Kisasa wa Dege eco Village yakiendele kujengwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda akizungumza na wanahabari walioambatana nao kwenye ziara hiyo.
Picha ya pamoja ya Wabunge Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) mara baada ya kumalizika kwa ziara.