Writen by
sadataley
8:04 AM
-
0
Comments
Na Daniel Mjema, Mwananchi
Moshi. Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Jesse Angowi amesema kutounga mkono kufanyika kwa kura ya maoni Aprili, 2015 ni kukaribisha machafuko nchini.
Hayo aliyasema wilayani hapa jana katika uzinduzi wa Halmashauri Kuu ya Jimbo la Moshi.
Aliwashauri viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuridhia kufanyika kwa kura hiyo na kuwaacha wananchi waamue kupigia kura kile wanachokitaka na siyo kuwalazimisha.
“Amani ikikosekana hata makanisa hayawezi kuhubiri injili. Hivi sasa kuna viashiria vya kutoweka kwa amani kabla hata ya mchakato wa kupigia kura Katiba Inayopendekezwa haujaanza.
“Ni lazima tutii kauli ya Rais Kikwete kwamba kura ya maoni itafanyika Aprili mwakani, vinginevyo ni kukaribisha machafuko. Hakuna Mtanzania ambaye yupo tayari kwa hilo,” alisema Askofu Angowi na kuongoza kuwa kanisa hilo linamuunga mkono Rais ili kura hiyo ifanyike.
Alisema ni vyema viongozi wa dini wakabeba jukumu lao la kutoa elimu kwa waumini kuhusu kuheshimu maagizo ya viongozi wao.
No comments
Post a Comment