Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, September 29, 2014

‘Katiba itaibeba CCM Zanzibar’


 
Na Sharon Sauwa na Daniel Mjema, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mohamed Aboud Mohamed amesema Katiba inayopendekezwa, itaibeba CCM katika uchaguzi mkuu ujao visiwani humo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu bungeni jana, Aboud alisema katiba hiyo itawasaidia katika kujibu kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwani imejibu asilimia 90 ya kero hizo.

“Kwa asilimia zaidi ya 90 kero za muda mrefu za wananchi wa Zanzibar zimejibiwa. Kwa hiyo wananchi watajua kuwa tumeshughulika na kero zao kwa kuzipatia ufumbuzi,”alisema.

Aboud alisema watakwenda kwa wananchi wa Zanzibar wakiwa kifua mbele kufafanulia kero ambazo zimetafutiwa ufumbuzi na wajumbe wa Bunge la Katiba, wengi wao wakitokana na CCM.

“Mimi ninaamini kuwa wananchi wakipelekewa Rasimu ya Katiba hii inayopendekezwa na wakaiona kuwa imekidhi matakwa yao wataiunga mkono,”alisema Aboud katika mahojiano hayo.
Aeleza kuhusu urais 2015

Waziri huyo ambaye aliwahi kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar mara mbili (mwaka 2000 baada ya Dk Salmin Amour kumaliza muda wake na mwaka 2010 wakati Amani Abeid Karume alipokuwa akiondoka madarakani), alisema hatagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

“Sina nia wala dhamira ya kugombea tena urais. Mimi dhamira yangu kubwa ilikuwa ni kuiunganisha Zanzibar kazi ambayo Rais aliopo (Dk Ali Mohamed Shein) ameifanya vizuri,”alisema
Aboud alisema sifa ya Rais ni uadilifu na kuwaunganisha Wazanzibari na Watanzania kwa jumla, sifa ambazo zote amekuwa nazo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Shein. Hata hivyo, alisema kazi yoyote inayofanywa na mwanadamu inakuwa na upungufu, haiwezi kuwa kamili.

“Mimi nina uhakika matarajio ya Wazanzibari yamepata majibu katika Rasimu hii ya Katiba. Na ninaamini kuwa wataipokea vizuri. Lazima tufahamu kuwa Katiba ni mchakato,” alisema.

Aboud alisema kama kuna jambo ambalo hawakulipata katika mchakato wa sasa wa Katiba unaomalizika Oktoba 4 au hawakufikia mwafaka , kesho wanaweza kupata nafasi ya kulizungumzaAlipoulizwa kero zilizopatiwa ufumbuzi katika Katiba hiyo, Aboud aliitaja kero ya mafuta na gesi ambapo sasa Zanzibar itakuwa na uwezo wa kushughulikia.
Kwa habri zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Katiba-itaibeba-CCM-Zanzibar-/-/1597296/2467614/-/13sjm6b/-/index.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment