Writen by
sadataley
2:14 PM
-
0
Comments
Na Goodluck Eliona na Editha Majura, MwananchiDar es Salaam. Serikali imepoteza zaidi ya Sh362.9 bilioni kutokana na baadhi ya kashfa kubwa za ufisadi na operesheni mbalimbali zilizoligharimu taifa tangu uhuru.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini taifa kukumbwa
na kashfa mbalimbali za upotevu wa fedha au kuanzisha mipango ambayo
utekelezaji wake ulisababisha maumivu kwa wananchi na hakuna awamu ya
uongozi wa Serikali iliyokwepa hali hiyo.
Kuanzia awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere
aliyeiongoza nchi toka mwaka 1961 ilipopata uhuru hadi 1986, Rais Ali
Hassan Mwinyi (1986-1995), Rais Benjamin Mkapa (1995-2005) na Rais
Jakaya Kikwete (2005-hadi sasa), kumeibuka kashfa mbalimbali, saba
zikiwa kubwa na kulitikisa taifa.
Kashfa na operesheni saba kubwa zilizotikisa taifa
ni pamoja na Operesheni Uhujumu Uchumi, ufisadi katika Mfuko wa
Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support –
CIS) na Kashfa ya Rada.
Nyingine ni ufisadi Akaunti ya EPA, kashfa ya
Richmond, Operesheni Tokomeza Ujangili na ile ya uchotaji mabilioni
katika akaunti ya Escrow.
Operesheni Uhujumu Uchumi
Mwaka 1984 Serikali ilianzisha Operesheni Uhujumu
Uchumi, iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Sokoine ili
kutaifisha mali ambazo baadhi ya watu walidaiwa kujipatia kwa njia isiyo
halali.
Operesheni hiyo ilishuhudia baadhi ya watuhumiwa
wakimwaga fedha mitaani na majalalani, huku wengine wakitupa mali
kuhofia kutiwa kwenye mkono wa sheria.
Hata hivyo, katika operesheni hiyo baadhi ya
watendaji wa Serikali ambao hawakuwa waaminifu, waliitumia nafasi hiyo
vibaya kutaifisha mali za baadhi ya watu, ambao hawakuwa wahujumu
uchumi.
Zoezi hilo lilisababisha wananchi kadhaa hasa
vijijini kuwekwa ndani na wengine kuachwa maskini baada ya kunyang’anywa
mali zao ikiwamo mifugo na mashine za kusaga nafaka, kwa kudaiwa kuwa
walizipata kwa njia isiyo halali.
Mfuko wa Commodity Import Support (CIS)
Miaka 24 baadaye yaani mwaka 2008, liliibuka
sakata jingine lililokuwa na harufu kubwa ya ufisadi wa mabilioni katika
Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import
Support – CIS).
Kwa hari zaidi ingia www.mwananchi.com
Kwa hari zaidi ingia www.mwananchi.com
No comments
Post a Comment