Writen by
sadataley
11:48 AM
-
0
Comments
Ndege ya abiria imeanguka leo asubuhi nchini Iran ikiwa na watu 66 wakiwemo wasafiri na wahudumu
Ndege hiyo ya Shirika la Aseman ilitoweka katika rada leo saa mbli asubuhi ikiwa inasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Mehrabad mjini Tehran kuelekea mji wa Yasuj ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Kohgiluyeh na Boyer-Ahmad kusini magharibi mwa Iran.
Ndege hiyo aina ya ATR 72 ilitoweka kwenye rada dakika 20 hivi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Tehran. Ndege hiyo imeanguka katika eneo la Semirom katika mkoa wa Isfahan kati mwa Iran na shughuli za uokoaji zinaendelea. Maelezo zaidi yatakujieni baadaye.
PARSTODAY
No comments
Post a Comment