Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, May 16, 2017

Watanzania 3 wapewa shavu na CAF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF}

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF} limewateua watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi katika kusimamia mchezo wa Kundi A hapo kesho utakaowakutanisha Ghana na Gabon kwenye uwanja wa Port Gentil michuano ya Afcon U-17.

Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine ambaye atakuwa Kamishna wa mchezo huo, Frank John Komba kupewa nafasi ya mwamuzi msaidizi pamoja na Dk. Paul Gaspel Marealle kushika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania  {TFF} imewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na CAF huku wakiwatakia kila la kheri atika kutimiza majukumu waliyopangiwa kesho na baadaye hasa ikizingatiwa kuwa fainali zijazo za vijana kama hizi, zitafanyika Tanzania mwaka 2019.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment