Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, May 16, 2017

Polisi auawa Kinyerezi Dar

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni 

Dar es Salaam. Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala.

Taarifa zilizotufikia punde na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni zinasema aliuawa nyumbani kwake. Hata hivyo hakumtaja jina lake.

Taarifa zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni.

Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye.

“Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi  tutawapa taarifa baadaye,” alisema.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment