Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, April 16, 2017

Mchungaji ahimiza kuitumia Pasaka kuimarisha amani nchini

Dar es Salaam. Watanzania leo wanaadhimisha sikukuu ya kufufuka kwa Yesu, maarufu kama Pasaka huku viongozi wa dini na wasomi wakihimiza amani, upatanisho na msamaha.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Kigogo (KKT), Richard Hinanja alisema sikukuu hii ni ishara ya ushindi dhidi ya dhambi, hivyo ni muhimu kuiadhimisha kwa hali ya utulivu.

“Sherehe zetu zionyeshe kumtukuza Mungu na kushinda mauti na pia tusisherehekee tu bali itumike kujitafakari na kuondoa chuki na uhasama miongoni mwa familia na ndugu zetu,” alisema.

Aliwataka wananchi kutumia siku hiyo kwa kushirikishana juu ya habari za Mungu na kuachana na starehe au vurugu ili matendo yawe ni mfano bora kwa kizazi kilichopo.

Wasomi nao walitoa ujumbe wao katika siku hii muhimu kwa Wakristo wakisisitiza Watanzania kuliombea taifa.

Profesa Gaudance Mpangala wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha alisema kuna tatizo katika taifa kutokana na matukio ya kutekana na mauaji.

“Katika nchi yenye amani haiwezekani watu wanauawa, watu wanatekana. Kuna tatizo katika taifa, viongozi wa dini na Wakristo kwa ujumla waliombee taifa,” alisema.

Pia, aliwataka viongozi wa dini kutoa ushauri kwa viongozi wa Siasa na Serikali ili waweze kusikiliza malalamiko ya wananchi na kutatua matatizo kwa njia ya ushirikiano.

Hata hivyo, sikukuu hiyo inakuja huku kukiwa na sintofahamu juu ya hali ya usalama nchini iliyoambatana na kutokea kwa matukio ya mauaji na utekaji wa watu.

Jeshi la Polisi limekwisha kutoa tahadhari na kuwataka wananchi kuliunga mkono kwa kutoa taarifa za uhalifu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment