Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, April 16, 2017

Maelfu waandamana kutaka Trump kutangaza kodi aliyolipa kwa serikali

 Makumi ya maelfu ya watu kote katika Marekani wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mbalimbali wakitaka Rais Donald Trump, kutangaza kodi aliyolipa kwa Serikali, jambo ambalo yeye binafsi amekataa kufanya.

Waandamanaji wengine walibeba sanamu kubwa za kuku, wakimaanisha kuwa Rais ni mwoga na amekataa kutoa takwimu za kodi yake.

Karibu watu 14 wametiwa mbaroni katika Berkeley, katika Carlifornia ambako wafuasi wa Rais Trump na wapinzani wake walikabiliana.

Ingawa hakuna sheria inamlazimu Bwana Trump kutangaza kodi yake, Marais wote wa Marekani wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda wa miongo minne iliyopita.

Maandamano hayo yalipangwa kwenda sambamba na siku ya mwisho ya raia kuwasilisha takwimu zao za kodi.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment