Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 25, 2017

WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE YA SEKONDARI ILULA WILAYA YA KILOLO WACHANGIA UKARABATI WA SHULE


Wawakilishi wa wanafunzi  waliosoma  shule ya  sekondari  Ilula  katika  wilaya ya Kilolo  mkoani  Iringa Mwalimu  Nguvu  Chengula  kushoto na mchungaji  Yekonia Koko  wakimkabidhi  fedha  kiasi cha  Tsh  milioni 1.3 mkuu wa shule ya  sekondari  Ilula mwalimu  Vincent  Shauri (katikati)  kulia ni makamu  mkuu wa  shule  hiyo  Joachim Mlay
Mkuu  wa  shule ya  Sekondari  Ilula  katikati  akiwaonyesha  choo  cha  kisasa 
kinachojengwa  shuleni hapo kwa  ajili ya matumizi ya  walimu
Mkuu  wa  shule ya  Sekondari  Ilula  Vicent Shauri  kulia  akionyesha  choo  hicho
Hiki  ndicho  choo cha  walimu  kinachojengwa  shule ya  sekondari  Ilula
   hizi 
ndizo  nguzo  za  umeme  zinazoelekea  bwenini  kweli  serikali  Kilolo 
kuna haja ya  kulitazama  hili  kabla ya  kuleta  majanga
Mkuu  wa shule ya  sekondari  Ilula akionyesha  nguzo za  umeme
Bweni  lililoezuliwa na kimbunga  likiwa bado  kuezekwa
 
Na  MatukiodaimaBlog
 
WANAFUNZI  waliosoma   shule
ya  sekondari  Ilula  wilayani  Kilolo  mkoa wa  Iringa wametoa  msaada 
wa  fedha  kiasi cha  Tsh milioni 1.3  kwa ajili ya  kuchangia
ukarabati  wa shule   hiyo baada ya  kukumbwa na maafa ya kuezuliwa na 
kimbuka  vyumba  vya  madarasa na bweni la  wanafunzi.
 
Wakikabidhi 
maasada huo    mchungaji  Yekonia Koko na Mwalimu  Nguvu  Chengula
jana  kwa niaba ya  umoja  wa  wanafunzi  waliosoma  katika   shule  
hiyo  walisema kuwa  wameguswa na  changamoto  mbali mbali  zilizopo 
katika shule  hiyo  hasa  baada ya  kupatwa na maafa ya  vyumba  vya 
madarasa  na bweni kuezuliwa na  kimbunga  na  kupelekea  wanafunzi 
kuendelea  kulala darasani  kwa  zaidi  ya  mwezi mmoja  sasa.
 
Hivyo 
walisema  kupitia  umoja   wao wanafunzi  waliosoma katika   shule 
hiyo  wamelazimika  kuchangishana   fedha  ili  kusaidia  uboreshaji 
wa  shule   hiyo kama sehemu ya  mchango  wao kwa  shule  hiyo  pia  
njia  moja wapo ya uhamasishaji wa  wananchi kuendelea  kuchangia 
maendeleo ya  elimu badala ya  kuiachia  serikali .
 
Alisema Chengula
 kuwa baada ya  serikali  kufuta ada  katika  shule ya  msingi na 
sekondari  wananchi  wanao wajibu wa  kushiriki kuchangia maendeleo ya 
shule  hiyo  kama  ujenzi na ukarabati  wa  shule kwani  pasipo 
kufanya    hivyo shule  nyingi  zitabaki magofu kutokana na baadhi ya
wananchi   kuwa na dhana  potofu  kuwa hawapaswi  kuchangia  maendeleo 
ya  elimu .
 
Chengula
 ambae ni mkurugenzi  wa  shule ya  Sun Academy mjini  Iringa alisema 
kuwa ili  jamii  iweze  kunufaika na ubora  wa  elimu  inayotolewa 
nchini ni  lazima  mazingira ya  ufundishaji  na mashule  kuboreshwa  
na njia  pekee ya  kuboresha  ni pamoja na wananchi kuendelea  kutoa 
ushirikiano kwa uongozi wa  shule ikiwa ni  pamoja na kuwa na harambee 
za mara kwa mara kwa ajili ya  kuboresha majengo ya  shule .
 

Shule   hii hii  imetoa  wanafunzi  wengi  sana ambao baadhi yao  kwa  
sana  wanafanya kazi katika maeneo mbali mbali na baadhi yao 
wameanzisha shule  zao binafsi kama ilivyo kwangu mimi ………ila
shule  hizi  ambazo zimetuwezesha  hadi kufika  hapa  zina  changamoto
nyingi  zikiwemo  za uchakavu wa majengo  jukumu  letu ni  kurudisha
shukrani kwa  shule  tulizosoma kwa kuchangia maendeleo  ya  shule 
hizi  ili  wanafunzi  wasome katika mazingira  mazuri  zaidi”
 
Hata 
hivyo alisema  inasikitisha kuona  wanafunzi  wanaendelea  kulala 
darasani  kutokana na bweni lao  kuezuliwa na kimbunga na kuwa kuna haja
ya  serikali ya  wilaya ya  Kilolo na  wadau  kufanya  jitihada za
kuboresha  miundo  mbinu ya  bweni hilo  ili  kuwawezesha  wanafunzi 
kurejea katika  bweni  badala ya  kuendelea  kulala darasani.
 
Kuhusu 
wanafunzi  waliosoma  katika  shule  hiyo na  sasa wanafanya kazi 
katika taasisi  na wengine kuwa na  taasisi zao  aliwataka   kukutana 
na  kuangalia  uwezekano wa  kupeana majukumu ya  kuchangia  uboreshaji
wa  shule   hiyo  kama ambavyo  wachache   wao  walivyoanza kuchangia
kwa  ajili ya uboreshaji wa  shule   hiyo.
 
Wakati 
mchungaji Koko  alieleza  kusikitishwa  kwake na miundo  mbinu  mibovu
ya  umeme iliyopo katika shule  hiyo na  kuwa  pasipo  shirika la umeme
nchini (Tanesco)  wilaya ya  Kilolo na  mkoa  wa Iringa kuchukua 
jitihada za haraka upo uwezekano  wa  shule  hiyo  kukumbwa na maafa 
siku za  mbeleni .
 
Kwani 
alisema inasikitisha  kuona nguzo  ambazo zimepeleka  umeme  katika
mabweni ya  wanafunzi  kuwa za kienyeji  ambazo zimewekwa na uongozi wa 
shule  hiyo na umeme  unaotumika  shuleni hapo  kuwa umeme wa kiwango 
cha  chini  zaidi baada ya  kuwekewa umeme wa njia mbili badala ya njia 
tatu  ambao  umewezesha  shule  hiyo  kuwa na uhakika  wa umeme.
 
Mkuu 
wa  shule  hiyo  Vecent Shauri   mbali ya  kuwashukuru  wanafunzi hao 
waliopata  kusoma katika  shule  hiyo  kwa  kusaidia  kiasi hicho  cha 
fedha kwa  ajili ya  ukarabati wa  shule   hiyo  bado  alisema tayari 
uongozi wa  shule   hiyo  ulijaza  fomu TANESCO  kuomba  kufikishiwa 
umeme wa uhakika na kuwa ni nguzo tatu  pekee  zinahitajika  ila hadi 
sasa zaidi ya  miaka  mwaka mmoja  hawajafika  kusogeza umeme katika 
shule  hiyo.
 
Akitoa 
taarifa  ya uchakavu  wa  majengo ya  shule  hiyo alisema  kuwa
jitihada mbali mbali  zimefanyika hasa  baada ya shule   hiyo  kuezuliwa
na kimbunga na kuwa  jitihada  za  wadau  mbali mbali  zimefanyika 
kukabati  vyumba vya madarasa  vilivyoezuliwa japo  alisema  hadi  sasa
bweni moja  bado  kukarabatiwa hivyo  wanafunzi wanaendelea  kulala
darasani.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment