Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 21, 2017

Serikali ya DRC yakataa kuchunguza video ya picha za mauaji


Rais wa Jamhuri ya Congo Joseph Kabila

Serikali ya Demokrasia ya Congo imekataa wito wa kimataifa wa kulitaka taifa hilo kufanyia uchunguzi picha ya video inayowaonyesha raia wa nchi hiyo wakiwaua mwanamke na mwanaume.

Msemaji wa serikali amesema kuwa ilikuwa ni wajibu wa wanaolituhumu jeshi kuweza kutoa uthibitisho wa tuhuma hizo.

Video hiyo iliyozagaa mwishoni mwa wiki inaonekana kuwa ilichukuliwa katika mji wa Kasai jimbo la kati nchini humo,ikionyesha wanajeshi wakikabiliana na wapiganaji.

Marekani imelaumu kuhusiana na video hiyo na kusema ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Mkuu wa idara ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa Zeid Ra'ad al Hussein anasema serikali inapaswa kuangalia kile ambacho tuhuma dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment