Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, December 10, 2016

Rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa aendeleza juhudi za usuruhishi huko Burundi.

Mkapa amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.




Image captionMkapa amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa rais wa Tanzania za kutatua mzozo ulio nchini humo.
Hii inajiri baada ya William Mkapa kuwaambia waandishi wa habari kuwa si jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Raia Pierre Nkurunzia.
Nchi ya Buurndi ilitumbukia kwenye mzoo baada ya bwana Nkurunziza kutangaza kuwa angewania muhula wa tatu.
Mamia ya watu wameuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.
Bwana Mkapa alipewa jukumu la kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni wanatafutwa na serikali kwa kupanga maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza hatua ambazo serikali inazitaja kuwa za kihalifu. 
Wengine waliilaumiwa wa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.
Chanzo: BBC Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment