Writen by
sadataley
5:36 AM
-
0
Comments
Uchaguzi huo uliofanyika mwezi Februari unatarajiwa kupingwa na aliyekuwa mgombea Amama Mbambazi na chama chake akidai kuwa haukuwa wa huru na haki.
Jopo la majaji tisa wakiongozwa na jaji mkuu wa Uganda Bert Katurebe, wataanza kusikiliza rufaa iliyowasilishwa katika mahakama kuu kupinga ushindi wa Yoweri Museveni kama rais wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Februari.
Museveni ametayarisha mawakili 40 huku Mbabazi akiwa na mawakili 43. Mbabazi, anataka matokeo ya kura kufutiliwa mbali na uchaguzi kuandaliwa upya kwa msingi kwamba sheria zote za uchaguzi zilivunjwa na wizi wa kura kutekelezwa.
Wakati huo huo wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Uganda wamesema ni vyema mvutano na mzozo wa uchaguzi huo kutatuliwa mahakamani.Chanzo:VOA SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment