Writen by
sadataley
3:10 PM
-
0
Comments
Mgombea urais Donald Trump ameshambuliwa sana na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama cha Republican, muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe wa chama hicho kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono.
Bw Trump, anayeongoza kwenye kura za maoni kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz.
Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Bw Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si udhaifu.
Baadhi ya wanachama wakuu wa Republican wanasema Bw Trump hafai na kwamba hawezi kushinda urais dhidi ya chama cha Democratic.
Mdahalo huo ulioandaliwa na kituo cha Fox News ulianza kwa Bw Trump kuulizwa kuhusu shutuma za awali kutoka kwa Mitt Romney, aliyewania urais 2012, aliyesema mfanyabiashara huyo ni mchokozi, mlafi na aliyejaa chuki.
Bw Trump amempuuzilia mbali Romney na kumtaja kuwa “mgombea aliyefeli”. Lakini mara moja alijipata akishambuliwa na Bw Rubio.
Seneta huyo wa Florida alisema hatasalimisha vuguvugu la wahafidhina kwa mtu anayedhani “nuclear triad” (mkusanyiko wa silaha za nyuklia) ni bendi ya rock kutoka miaka ya 1980.
Miongoni mwa mengine:
Bw Trump ameahidi kurejesha viwanda vyake vya kutengeneza nguo kutoka Marekani hadi Uchina.
Seneta wa Texas Bw Cruz amesema Bw Trump ni sehemu ya mfumo fisadi wa Washington, uliofadhili kampeni ya Hillary Clinton 2008
Gavana wa Ohio John Kasich amesema yeye ndiye “mtu aliyekomaa” jukwaani aliye na nafasi bora zaidi dhidi ya mgombea wa Democratic Hillary Clinton
Akitumia michoro mikubwa kwenye skrini, mtangazaji wa Fox Chris Wallace amemuuliza Bw Trump kuhusu ukweli wa mpango wake wa akiba
Bw Trump ametetea mbinu ya kutumia maji kupata habari kutoka kwa “wanyama walio Mashariki ya Kati” na kuuawa kwa familia za magaidi
Lakini amekataa pendekezo la kuruhusu New York Times waachilie huru kanda za sauti yake zilizonaswa bila yeye kujua.
Katika moja ya matukio ya kushangaza, Bw Trump ametetea ukubwa wa mikono yake kisha akafanya mzaha kuhusu kiungo kingine chake.
Amewatusi pia wenzake, akimweleza Rubio kama mtu mdogo” na Ted kama “muongo”.
Trump asema Cruz hafai kuwa rais Marekani
Mfanyabiashara huyo kutoka New York amelazimika kufafanua kuhusu kesi ya kusambaratika kwa chuo kikuu chake cha Trump University.
Amesema atashinda kesi hiyo lakini Bw Rubio amesema mfanyabiashara huyo anajaribu kuhadaa watu wampigie kura, sawa na alivyowahadaa wamkabidhi pesa zao.
Bw Trump pia ameulizwa na jopo la Fox News kuhusu kubadilika kwa msimamo wake kuhusu wahamiaji wa Syria, vita Afghanistan na Rais George W Bush.
Amejibu: "Mimi ni mtu thabiti sana. Lakini sijawahi kumuona mtu aliyefanikiwa ambaye hakubadili msimamo wak wakati mwingine.”
Bw Trump, ameshinda majimbo 10 kati ya 15 yaliyofanya mchujo chama cha Republican.
Wagombea wakuu sasa wamesalia wane baada ya Ben Carson kujitoa.
Awali walikuwa 17.
Mdahalo huo, wa Fox News, ulikuwa wa kwanza kwa Trump kukabiliana moja kwa moja wa wapinzani wake tangu ashinde majimbo saba Jumanne Kuu.
Aidha, ulimkutanisha na mtangazaji Megyn Kelly, ambaye alishutumu sana mdahalo wa kwanza na baadaye akasusia mdahalo kwa sababu yake.
Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda majimbo 10 naye Bernie Sanders majimbo matano.
Wawili hao watakutana katika mdahalo Flint, Michigan, mnamo Jumapili. Chanzo:BBC SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment