Writen by
sadataley
6:32 AM
-
0
Comments
Mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi, Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, unatarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki hii, Arusha Tanzania.
Mwenyekiti wa sasa wa jumuia hiyo ya EAC, Rais John Magufuli wa Tanzania, tayari amewasili mjini humo kuongoza kikao hicho, ambacho ni cha kawaida.
Suala la Burundi na kukubaliwa kwa nchi ya Somalia kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa.
Hata hivyo, kabla ya kikao hicho, Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi za jumuiya hiyo.
Aidha siku ya Alhamisi Machi tatu, Rais huyo wa Tanzania pia na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Holili, Taveta na Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika mashariki, inayotekelezwa na nchi wanachama.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment